Watu wawili wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la Super Feo kugongana na Land Rover, eneo la Mikumi, mkoani Morogoro jana. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea ajali hiyo.
Taarifa kutoka Morogoro zinasema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa jioni jana wakati basi lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea jijini Dar na kugongana uso uso na gari ndogo na kusababisha vifo na majeruhi hao, ambapo wanane wanaelezwa wamelazwa katika hospitali moja iliyopo Mikumi na wengine kuruhusiwa baada ya kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment