STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 9, 2013

Ronaldo apiga hat trick nyingine, Real Madrid ikishinda 51

Different level: Cristiano Ronaldo scored a hat-trick as Real Madrid comfortable saw off Real Sociedad
Cristiano Ronaldo
CRISTIANO Ronaldo jioni hii amefunga hat trick yake ya 19 katika Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) wakati Real Madrid ikiishindilia Real Sociedad kwa mabao 5-1 katika mfululizo wa ligi hiyo.
Ronaldo alifunga mabao hayo katika mechi iliyochezwa uwanja wa Santiago Bernabeu, siku chache baada ya kuisaidia timu yake ya Real Madrid kutoka sare ya 2-2 na Juventus katika Ligi ya Mabingwa.
Mkali huyo toka Ureno alifunga mabao katika dakika ya 12 kumaliza kazi nzuri ya mshambuliaji mwenzake Karim Benzema , kisha akammegea pande Benzema kufunga bao la pili la real Madrid kabla ya mwenyewe kufungwa kwa penati dakika ya 26.
Bao lake la tatu alililofunga kwenye kipindi cha pili katika dakika ya 76, wakati huo tayari Sami Khadira alishafunga bao jingine la Madrid katika dakika ya 36 kwa pasi murua ya Gareth Bale.
Wageni walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa  Griezmann dakika ya 61 kwa pasi murua ya Carlos Vela.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo Getafe ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Elche. Michezo mingine miwili inatarajiw akuchezwa usiku huu katika ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment