STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 9, 2013

Zlatan atupia tatu PSG ikiizamisha Nice

Zlatan Ibrahimovic
 MSHAMBULIAJI nyota wa PSG, Zlatan Ibrahimovic ameendelea kudhihirisha kuwa ni bonge la strika baada ya usiku huu kutupia mabao matatu wavuni wakati mabingwa hao watetezi wakiizamisha Nice kwa mabao 3-1 katika Ligi ya Ufaransa.
Ibrahimovic, nyota wa Sweden, aliyafunga mabao hayo katika dakika ya 39, 57 kwa mkwaju wa penati na jingine la dakika ya 76 na kuifanya PSG izidi kujikita kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 31 wakizidi kuwaacha wapinzani wao wa karibuni, Monaco waliotoka sare ya 1-1 jana, pamoja na Lille itakayoshuka dimbanio hivi punde zikiwa na pointi 26 kila moja.
Baoa la kufutia machozi la Nice iliyokuwa ugenini lilifungwa na Nemanja Pejcinovic katika dakika ya 70.

No comments:

Post a Comment