STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 16, 2011

Sunzu asaini mkataba wa miaka miwiliMSHAMBULIAJI wa Kimataifa kutoka Zambia, Felix Mumba Sunzu amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea klabu ya soka ya Simba kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu, aliuambia mtandao wa MICHARAZO jana usiku kwamba wameshamalizana na Sunzu na kwamba mchezaji huyo atarejea kwao wakati wakifanya taratibu za uhamisho wake wa kimataifa toka Al Hilal.
"Kila kitu kipo ok, baada ya mkutano mrefu baina yenu amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kuwepo Simba," alisema Kaburu.
Kaburu hakupenda kueleza kwa undani mambo mengine waliyokubaliana na mchezaji huyo.
Kadhalika, Kaburu alikanusha taarifa kwamba wamemnyakua mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete akidai wanaheshimu mkataba uliopo baina ya Yanga na mchezaji huyo.
"Hizo ni taarifa za mtaani, ila si kweli, mtu ambaye tumemalizana nae ni Sunzu, huyo Tegete wala hatuna mpango nae," alisema.
Pia alisema sio kweli kama beki wao king'ang'anizi, Kelvin Yondan, amewakacha na kwenda Yanga kwa maelezo bado wana mkataba naye, pia kisheria Yanga wanapaswa waonane nao kama ni kweli walimtaka mchezaji huyo.
"taratibu zipo wazi, pia Yondan ana mkataba wa kuichezea Simba sasa ataendaje Yanga, hizi ni nyepesi nyepesi tu ila mchezaji huyo bado yupo Simba, alisema Kaburu.
Katiak hatua nyingine ni kwamba wachezaji wawili, Mohammed Banka na Athuman Idd 'Chuji' huenda wakaichezea Villa Squad kwa mkopo baada ya kuridhiana na Simba juu ya wachezaji hao wanaomudu nafasi ya kiungo.
Viongozi wa Villa waliuambia mtandao huu walikuwa wakimalizana na Simba, lakini hawakuweka kila kitu bayana wakidai watazungumza leo.