STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 28, 2013

David Moyes mambo magumu, Man United yanyukwa tena, City ikifa kwa Aston Villa EPL

http://i.huffpost.com/gen/1138374/thumbs/o-WAYNE-ROONEY-DAVID-MOYES-570.jpg?7
Wanafarijiana, Rooney na kocha wake, David Moyes

KOCHA David Moyes ameendelea kuwa na wakati mgumu kwenye Ligi Kuu ya England baada ya leo kulazwa mabao 2-1 nyumbani na timu ya West Bromwich Albion, huku majirani zao Manchester City wakigaragazwa ugenini kwa kipigio cha mabao 3-2 toka kwa Aston Villa.
Moyes aliyemrithi mikoba Sir Alex Ferguson koicha mwenye mafanikio makubwa kisoka katikka klabu hiyo na barani Ulaya, alijikuta vijana wake wakipokea kipigo cha pili mfululizo katika ligi hiyo baada ya wiki iliyopita kulala kwa Manchester City.
Wageni walitangulia kupata bao katika dakika ya 54 kupitia kwa Morgan Amalfitano kabla ya Wayne Rooney kusawazisha dakika chache baadaye na bao lililowakatisha tamaa Mashetani Wekundu lilitupiwa kambani na Saido Berahino dakika ya 67.
Nayo Manchester City baada ya kuwafunga mdomo mahasimu wao wa jiji la Manchester, leo haikuwa na chao mbele ya Astoni Villa kwa kulazwa mabao 3-2, huku Cardiff City wakipata ushindi ugenini dhidi ya Fulham na West Ham United ikilala bao 1-0 ugenini dhidi ya Hull City, na Southampton ikipata ushindi wa pili mfululizo kwa kuilaza Crystal Palace mabao 2-0.

Megan Young ndiye Miss World, Tanzania kama kawa yaanguka

Miss World 2013, Megan Young.
Mshindi wa Pili Miss World 2013, Marine Lorphelin.
Mshindi wa Tatu 2013, Carranzar Naa Okailey Shooter.
KISURA toka Philippines, Megan Young ameibuka kidedea katika shindano la Miss World 2013 baada ya kunyakua taji hilo, huku Tanzania ikiendelea kuwa wasindikizaji.
Wakati mwakilishi wa Tanzania akishindwa kufurukuta, Mghana Carranzar Naa Okailey Shooter aliitoa kimasomaso Afrika bada ya kushika nafasi ya tatu miongoni mwa warembo 130 waliochuana katika shindano hilo.,
Megan amerithi taji hilo kutoka kwa mrembo wa China, Yu Wenxia aliyefanya hivyo mwaka jana.
Katika shindano hilo lililofanyika mjini Jakarta, Indonesia na kumalizika muda mfupi uliopita, mrembo kutoka Ufaransa, Marine Lorphelin alishika nafasi ya tatu.
Tanzania kama kawaida yake, haikuweza kabisa kufua dafu baada ya mshiriki wake, Brigitte Lyimo kushindwa kufurukuta katika mtanange huo mkali na unaobeba hisia kubwa miongoni mwa wadau wake duniani kote.
Dalili za Miss Ghana kung'ara katika shindano hilo zilizidi kuongezeka hasa kutokana na umahiri wake katika kujibu swali na kujiamini.

Yanga yazinduka, Kagera yaipumulia Simba,


HATIMAYE mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ikimchezesha kwa mara ya kwanza kiungo mshambuliaji wake nyota, Mrisho Ngassa, imezinduka leo kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuidonoa Ruvu Shooting ya Pwani kwa bao 1-0.
Ushindi huo wa pili kwa mabingwa hao watetezi kwa msimu huu, umewafanya wafikishe pointi 9 na kuchupa hadi nafasi ya nne toka nafasi ya tisa iliyokuwa ikikamata ikiwa inalingana na JKT Ruvu ambayo kesho itashuka dimbani kupepetana na Simba, Azam na Ruvu Shooting wakitofautiana uwaiano wa mabao yao tu.
Yanga ambayo imetoka kuchezea kipigo cha mabao 3-2 toka kwa Azam na kuambulia sare tatu mfululizo,leo ilionyesha dhamira ya kuibuka na ushindi kwa kuishambulia kama nyuki wapinzani wao ambapo hata hivyo umahiri wa kipa Abdul Seif uliwakatisha tamaa na kufanya hadi mapumziko mambo yawe 0-0.
Bao lililowapa faraja Yanga jioni yua leo lilifungwa dakika ya 62 na Hamis Kiiza 'Diego' kwa 'tiktak' akimaliza pasi ndefu iliyotumwa na Ngassa aliyepokea pasi murua ya Mbuyi Twitte.
Hata hivyo ni mpaka alipoingia Athuman Idd Chuji katika kipindi hicho cha pili na kubadilisha mchezo ndiyo Yanga ilipoonyesha uhai, baada ya dakika 45 za awali kubanwa vilivyo na Ruvu japo ilishambulia mara kadhaa na kukatishwa tamaa na kipa aliyekuwa Abdul Seif aliyekuwa akidaka michomo na kufanya mbwembwe uwanjani.
Katika michezo mingine ya leo Kagera Sugar imefanikiwa kuitungua Rhino Rangers nyumbani kwao Tabora kwa bao 1-0 na kukwea hadi nafasi ya pili ikilingana pointi na Simba zote zikiwa na 11 zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Bao wa washindi hao lilifungwa na Themi Felix, huku ikishuhudiwa wenyeji wakicheza pungufu baada ya Nudrin Bakar kulimwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Kagera.
Nayo Coastal Union ilishindwa kulinda bao lao lililotupia na Haruna Moshi 'Boban' na kulazimishwa sare ya bao 1-1 ugenini na wenyeji wao Mbeya City. hata hivyo Boban alilimwa kadi nyekundu katika mchezo huo baada ya kumkutana mwamuzi wa pembeni na kuifanya Coastal kumaliza pungufu ya wachezaji wawili baada ya mchezaji wake mwingine kutolewa na mchezaji wa Mbeya City walipotaka kupigana uwanjani.
Katika mchezo mwingine uliyechezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga, wenyeji Mgambo JKT walishindwa kutambiana na Oljoro JKT ya Arusha baada ya kutoka suluhu ya kutiofungana.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mechi za leo
                                   P  W  D  L   F   A  GD  PTS
1.  Simba                     5   3   2   0  13  4    9   11
2.  Kagera Sugar          6   3  2   1   7   3    4   11
3. Coastal Union          6   2  4   0   6   3   3   10
4. Yanga                      6   2  3   1  11  7   4   9
5. JKT Ruvu                5   3   0   2   6   2   4    9
6.  Azam                     5    2  3   0   8   5   3    9
7.  Ruvu Shooting        6   3  0   3   6   4   3    9
8.  Mbeya City           6   1  5   0   6   5   1    8
9.  Rhino Rangers       7   1  4   2   7  8    -1   7
10.Mtibwa Sugar        5   1  3   1   3  4   -1   6
11.Oljoro                    6   1   2   3   3   6  -3   5
12.Mgambo               6   1   2   3   2  10 -8   5
13.Prisons                  5   0   3   2   2    8  -6   3
14.Ashanti                  6   0   1   5   2  13 -11  1

Miili 71 yapatikana jengo la Westgate, kilichosema na Al Shaabab chadhihirisha ni kweli

* Lilidai liliua watu 137 kupinga idadi iliyotangazwa na serikali ya Kenya

  MIILI takriban 71 yadaiwa kupatikana katika jengo lililotekwa
- Wengine wakutwa wamenyofolewa macho, wameng'olewa meno kwa plaizi na hata wengine wakiwa hawana vidole!
- Miili ya watoto yadaiwa kukutwa kwenye friji za vyakula ikiwa na visu bado!
Westgate Mall, Nairobi: Eyes gouged out, bodies hanging from hooks, and fingers removed with pliers 'Eyes gouged out, bodies hanging from hooks, and fingers removed with pliers': Horrific claims of torture emerge as soldiers reveal gory Kenyan mall massacre details

Kenyan soldiers claim to find scenes of torture by mall terrorists
  • They say children found dead in food fridges with knives still in bodies
  • Men were said to have been castrated and had fingers removed

Soldiers told of the horrific torture meted out by terrorists in the Nairobi mall massacre yesterday with claims hostages were dismembered, had their eyes gouged out and were left hanging from hooks in the ceiling.

Men were said to have been castrated and had fingers removed with pliers before being blinded and hanged. 

 Children were found dead in the food court fridges with knives still embedded in their bodies, it was claimed.

Most of the defeated terrorists, meanwhile, were reportedly discovered ‘burnt to ashes’, set alight by the last extremist standing to try to protect their identities.


The horrifying details came yesterday as the first pictures emerged from within the wreckage of the building, showing piles of bodies left strewn across the floor. A third of the mall was destroyed in the battle between terrorists and Kenyan troops.


Lying in the rubble are feared to be the bodies of as many as 71 civilians who have been declared missing by the Kenyan Red Cross.


With detectives, including the FBI and the Metropolitan Police, still unable to reach the wrecked part of the mall for fear of setting off explosives, it could take up to a week to determine exactly who is still inside.

Yesterday, soldiers and doctors who were among the first people into the mall after it was reclaimed on Tuesday, spoke of the horrifying scenes inside. 


‘You find people with hooks hanging from the roof,’ said one Kenyan doctor, who asked not to be named.

‘They removed eyes, ears, nose. They get your hand and sharpen it like a pencil then they tell you to write your name with the blood. They drive knives inside a child’s body. 'Actually if you look at all the bodies, unless those ones that were escaping, fingers are cut by pliers, the noses are ripped by pliers. Here it was pain.’

A soldier, who took pictures at a bread counter and at the ArtCaffe, said he was so traumatised by what he saw he has had to seek counselling.

Bomb disposal experts with sniffer dogs were yesterday painstakingly combing the part of the building still standing for explosives before clearing forensic officers, police and troops to search for bodies.


Images also emerged yesterday revealing the true extent of the destruction caused to the centre during the four-day battle between Kenyan forces and Islamic militants.


The first pictures taken inside the site show a gaping hole in the mall's roof after three storeys collapsed when Kenyan soldiers fired rocket-propelled grenades inside the complex, knocking out a support column, a government official said. 


Children's buggies are left abandoned just metres from the yawning pit, as cars hang precariously over the edge. 


Beneath many more vehicles lie on top of each other, smashed to pieces.The collapse happened on Monday when government troops launched a massive assault on the mall where up to 150 people are thought to have been killed.


During the firefight, hostages reportedly had their throats slashed from ear to ear and were thrown screaming from third-floor balconies as the siege came to a bloody end. 


Forensics teams, still sifting through the mountains of rubble, fear many more bodies are yet to be found.


Shell-shocked Kenyan troops said the inside of the Israeli-run mall resembled a ‘scene from a horror movie’ with blood spattered everywhere and dead bodies strewn across the floor.


SOURCE: http://www.dailymail.co.uk

Hivi ndivyo marehemu Venance George alivyoagwa Morogoro

Mke wa mkuu wa waandishi wa habari kampuni ya Mwananchi Communication LTD mkoa wa Morogoro, Venance George (40) Sauda Mgombelwa akilia mara baada ya kuaga mwili wa mume wake wakati wa misa kabla ya kuanza safari ya kwenda kijiji cha Bukoti Geita kwa mazishi, Venance alifariki dunia Septemba 26 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ambako alilazwa.

 
 Venance George enzi za uhai wake.

 Mwandishi wa kampuni ya IPPMEDIA mkoa wa Morogoro Devotha Minja akiwa mwenye huzuni huku akiwa amemkumbatia Hamida Shariff wa gazeti la Mwananchi Morogoro jana wakati wa kuaga mwili wa bosi wake.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera kushoto akimpa pole baba wa Venance George, Mzee George Mhakingilwa wakati wa misa ya kuaga mwili wa marehemu Venance, Kulia ni Mke wa Marehemu Sauda Mgombelwa.

Bendera akifafanua jambo huku George Mhangilwa (katikati) na Boninvetura Mtalimbo kulia wakisikiza jambo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kusafirisha mwili wa marehemu Venance George kwenda kijiji cha Bukoti Geita kwa ajili ya mazishi.

 Jeneza lenye mwili wa mwaandishi Venance George likiingizwa katika basi ndogo aina ya coaster tayari kw kuanza safari.
 
 Mtoto wa kiume wa Venance George, Erasto akiwa amekaa katika gari hilo.

 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akisali na kutoa heshima za mwisho kwa Mwananchi Venance George wakati wa zoezi la kuaga.

 Mratibu wa Morogoro Press Club Morogoro, Thadei Hafigwa akiweka shada la maua katika jeneza lenye mwili wa marehemu Venance George na kutoa heshima za mwisho.

Mratibu wa mazishi ya Venance George, Bonveture Mtalimbo akizungumza jambo.

 
 Waandishi wa magazeti ya HabariLeo John Nditi kulia na Peter Kimath JamboLeo wakitoa heshima za mwishi.  Mwandishi wa gazeti la Uhuru na Mzalendo mkoa wa Morogoro Latifa Ganzel kulia na Ester Mwimbula wa Mwananci nao wakitoa heshima za mwisho.

 Dastan Shekidele kulia naye akitoa heshima za mwisho katika tukio la kuaga mwili wa marehemu.

Katekesta wa kanisa la romani katoliki jimbo la Morogoro Ernest Mathey akinyunyuzia maji ya baraka katika jeneze lenye mwili wa Venance George nyumbani kwake mtaa wa Tubuyu kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro.

 Kutoka kushoto, Devotha Minja (ITV) Hamida Shariff (Mwananchi) Mwenyekiti wa Morogoro Press Club, Idda Mushi, Latifa Ganzel (Uhuru na Mzalendo) na Lilian Lucas (Mwananchi) wakifuatilia jambo wakati wa misa ya ibada ya marehemu Venance George (40) iliyofanyika nyumbani kwake mtaa wa Tubuyu kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro jana.

 Mtoto wa kwanza wa Veanace George, Ivon Veanace George akiwa mwenye huzuni wakati wa ibada hiyo.

 kutoka kushoto mstari wa nyuma, Lilian Justice (Majira) Amina Saidi (Star Tv) na Merina Robert (Mtanzania na Clouds Fm) kila mmoja akiwa ameweka pozi la majonzi wakati wa tukio hilo.
 Mwandishi wa Tanzania Daima, Joseph Malembeka kulia akisaidiana na mwenzake kumpa msaada mwanamke ambaye aliishiwa nguvu wakati wa tukio la kuaga.

 Mwenyekiti wa Morogoro Press Club Idda Mushi akitoa neno juu ya msiba huo.

 Mwenyekiti wa CCM wilaya Morogoro Fikiri Juma akizungumza jambo

 Katibu wa mbunge wa jimbo la Morogoro kupitia CCM, Abdullaziz Abood, Mourice Massala naye akizungumza jambo

Huyu ndiye Andrew Mpasa ambaye ni Meneja Mauzo gazeti la Mwananchi Morogoro akihakikisha kila jambo lina kwenda sawa katika msiba huo.
 Timu ya watumishi wa Mwananchi Communication LTD katika msiba huo.



HISTORIA FUPI YA MAREHEMU VENANCE GEORGE.

Marehemu Venance George Mhangilwa alizaliwa mnamo 8/12/1973 Bukoti wilaya ya Geita.



ELIMU:

-Marehemu alisoma katika shule ya msingi Bugogo kuanzia mwaka 1981 mpaka mwaka 1987 alipohitimu elimu yake ya msingi.
-Mnamo mwaka 1988 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Forest Hill iliyopo Morogoro na kuhitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1994.


-Mwaka 1995 alijiunga katika chuo cha uandishi wa habari na kuhitimu mwaka 1996.



AJIRA:

Marehemu alianza kazi ya uandishi wa habari katika kampuni ya,

 -Uhuru Publication Limited, 1996-1998.

-Kuna Entarprises Company Limited, 1998-1999.

-Village Travel And Transport Project (VTTP), 2001-2003.

-Swiss-Contact Tanzania Limited, 2001-2003

-Mwananchi Communication Limited, 2003 mpaka mauti yalipomkuta.

Pia alijiendeleza kimasomo katika chuo kikuu huria cha Tanzania ambapo alitakiwa kuhitimu shahada yake ya mawasiliano ya umma mwezi wa 12 mwaka huu 2013.



MWISHO:

-Marehemu alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu na kifua hali iliyopelekea kwenda kulazwa katika hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es salaam na kupata nafuu, Baada ya kurudi nyumbani hali ilbadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa katika hospitali ya Holly Cross Mission iliyopo mkoani Morogoro na baadaYe kuhamishiwa katika hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro.
Marehemu alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani , baada ya siku kadhaa hali ilibadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi umauti ulipomkuta mnamo tarehe 26/09/2013 saa 9:15.

-Marehemu ameacha mjane na watoto wawili wa kike na wa kiume.



SHUKRANI:

-Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote waliokuwa pamoja na sisi tangu marehemu alipoanza kuugua mpaka leo hii , shukrani ziwafikie wafanyakazi wenzake, ndugu, jamaa na marafiki wa karibu. Maelezo haya kwa mujibu wa Mratibu wa mazishia, Bonveture Mtalimbo.
Source:Juma Mtanda

HILI NDILO TAMKO LA SERIKALI IKIYAFUNGIA MAGAZETI YA MTANZANIA NA MWANANCHI

                                                   TAMKO LA SERIKALI
Serikali imeyafungia  kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba,2013  kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala  za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013”  kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri  haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI”  habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa  mkali mwenye hasira.Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la  ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam  mbwa ni najisi hapaswi kuingia  katika maeneo ya ibada.
Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti hili limeonywa mara nyingi  lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa  kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za  fani ya Habari.
Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.
Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta  kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika  na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na  waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.
Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama  wavione kuwa haviwasaidii.
Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania  kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 septemba,2013,.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.
Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.
Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia .Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani  nchini.
Imetolewa na

MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013

Chelsea chupuchupu, Torres alimwa kadi nyekundu

 Tottenham Hotspur v Chelsea: live
BAO la nahodha John Terry, liliisaidia Chalsea kuepuka kipigo cha ugenini dhidi ya wenyeji wao, Tottenham Hotspur katika mfululizo ya Ligi Kuu ya England (EPL) mechi iliyoisha hivi punde.
Vijana wa kocha Jose Mourinho walijikuta wakishutukizwa kwa bao la mapema lililofungwa na Gylfi Sigurdsson katika dakika ya 19 na kushuhudiwa wenyeji wakitawala sehemu kubwa ya kipindi hicho.
Hata hivyo mabadiliko yaliyofanywa katika kipindi cha pili kwa kuingizwa dimbani kwa Juan Mata kuliifanya Chelsea kutakata na kushambulia lanmgo la Spurs kwa muda mrefu ikifanya kosa kosa za hapa na pale kabla ya terry kufunga bao dakika ya 65 kwa kasi kubwa iliyofanywa na Mata.
Hata hivyo makali ya Chelsea yalipunguzwa baada ya mshambuliaji wao nyota, Fernando Torres kutolewa nje ya uwanja baada ya kuonyesha kadi ya pili ya njano dakika 10 kabla ya kumalizika kwa pambano hilo.
Kabla ya hapo 'El Nino' alishaonyeshwa kadi ya njano dakika sita baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na kuifanya Chelsea kucheza pungufu, japo waligangamala la kumaliza mchezo huo kwa sare ya 1-1 na kuifanya ifikishe pointi 11 na kuendelea kusalia nafasi ya tatu nyuma ya Arsenal yenye pointi 12 na vinara Tottenham ambao huenda wakaongoza kwa muda kwa sababu timu nyingine zipo dimbani kwa sasa japo Arsenal wenyewe watajitupa uwanjani baadaye na kama itashinda itarejea kileleni mwa msimamo.

Serikali yayafungia magazeti za MWANANCHI na MTANZANIA, kisa...

Moja ya magazeti yaliyofungiwa na serikali
 HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni Michezo na Vijana, imeyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kutokana na kile kilichoelezwa kukaidi maonyo ya kuacha kuandika habari za kichochezi.
Taarifa hiyo imesema kuwa Mwananchi limefungiwa kwa muda wa wiki mbili na lile la Mtanzania limefungiwa kwa siku 90 sawa na miezi mitatu.
Kufungiwa kwa magazeti hayo ni muendelezo wa adhabu ambazo serikali imekuwa ikivichukulia vyombo vya habari kutokana taarifa zao wanazochapisha au kutangaza zinazokinzana nayo kama ilivyowahi kulikuta gazeti la Mwanahalisi ambalo mpaka sasa bado lipo kifungoni.
Wengine waliowahi kukumbana na rungu la serikali ni gazeti la Majira na vituo vya redio Imani Fm na nyingine ya kidini ya mkoani Kagera.