STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 16, 2013

CCM, CHADEMA VITA TUPU IRINGA, MORO

MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wilayani Kilolo, Lunyiliko Nyaulingo amelazwa katika Hospitali ya mkoa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mgololo amelazwa Hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wanaodaiwa ni wanachama wa CCM katika kampeni za mwisho za kuwania nafasi ya udiwani.

Sambamba na hiyo Katibu wa CCM kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo, Wilhad Ngogo (40) na Yohana Mchafu anayedaiwa kuwa ni mwanachama wa CCM wanashikiliwa na Polisi kwa kuhusika na matukio hayo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema watu hao walikamatwa jana kufuatia 
vurugu zilizojitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya mwisho katika wilaya hizo mbili.

Alisema kufuatia mzozo huo wanachama wa CHADEMA walizuia barabara ya Iringa-Mbeya kwa kuweka magogo ili kuzuia magari kupita na kuwa Polisi wanamtafuta Rabart Sam maarufu kwa jina la Kideri kwa kuongoza vurugu hizo.

Kamanda Mungi alisema wanafanya uchunguzi wa kina juu ya matukio hayo na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wote wa vyama vya siasa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuepusha vurugu ambazo zinaweza kutokea.

Leo Uchaguzi wa udiwani katika kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo na Mbalamaziwa wilayani Mufindi ulifanyika ambapo Zuberi Nyomolelo (CCM) na Ezekiel Mlyuka (CHADEME) walipambana kwa kata ya Mbalamaziwa na kwa upande wa Ng’ang’ange Kilolo Nafred Chahe (CHADEMA) na Namgalesi Msuva (CCM) walipambana.

Tukio hilo limejiri wakati huko Morogoro nako inaelezwa wanaodaiwa vijana walinzi wa CCM kuwakata mapanga viongozi wa CHADEMA, huku watanzania wakiendelea kuomboleza tukio la mlipuko wa bomu jijini Arusha lililopoteza uhai wa watu wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Katibu  Mwenezi wa tawi la Minepa, Jimbo la Ulanga Magharibi, Severin Matanila aliyekaa aliyejeruhiwa katika tukio la Morogoro, huku viongozi wenzake, Mwenyekiti wa Jimbo, Kibam Ally Mohammed na Katibu wake, Lucas Lihambalimo (aliyeipa kamera mgongo) wakiwa pembeni yake 
via Mjengwa

Pambano la Golden Bush na Mburahati Veterani katika picha

Wachezaji wa Golden Bush na Mburahati wakichuana leo kwenye uwanja wa Chuo Kikuu
Onesmo Waziri 'Ticotico' (4) akimcheza rafu mchezaji wa Mburahati Veterani
'Mido' Shija Katina akimtoka mchezaji wa Mburahati
Karume wa Mburahati (kushoto) akimtoka Nico Nyagawa, huku Faraji akiwa makini
Game imeisha wachezaji wakipongezana
Wachezaji Golden Bush wakiwa kwenye mapumziko
Nani alikuambia Ivo Mapunda anajua kudaka tu, hapa alikuwa akikipiga kama mshambuliaji wa Golden Bush
Wisdom Ndhlovu akihamisha mpira mbele ya Karume wa Mburahati
Ivo Mapunda akiwajibika uwanjani

wachezaji wa akiba wa Mburahati wakiishuhudia timu yao ikilazwa mabao 3-2 na Golden Bush
Ally 'Neymar' wa Mburahati (kushoto) na Machota wakipongezana baada ya mchezo. Wote wawili walizifungia timu zao bao

Refa Madaraka Sdeleman (jezi ya njano) akitoka uwanjani na wachezaji baada ya kupuliza kipyenga cha mwisho
Msijali kwa kipigo. Refa Madaraka Seleman kama anamwambia mchezaji wa Mburahati baada ya kumalizika kwa pambano
Hongereni! Kipa wa Mburahati akiwaambia wachezaji wa Golden Bush, Kapeta na Machota
Heka heka uwanjani

Hivi ndivyo Mbunge Nasari alivyofanyiziwa Arusha

Joshua Nassari
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshambuliwa na vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Arusha aliyejulikana kwa jina la Kalanga na  kulazimika kulazwa katika hopitali ya Selian Mkoani Arusha katika fujo zilizotokea katika kituo cha kupigia kura cha Zaburi, kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Akizungumza kutoka eneo la tukio, Mratibu wa wanawake wa Chadema Mkoa wa Arusha Sesilia Ndossi alisema “muda wa saa 5 asubuhi tulienda katika kituo cha kupiga kura cha Zaburi, kumsindikiza Mbunge wa Arumeru ambaye katika Uchaguzi huo yeye alikuwa Wakala.

'lakini tulipofika hapo tulimkuta raia mmoja mwenye asili ya kisomali akiwaita watu na kuwaambia pigia CCM, ndipo Nassari akamuuliza kwanini unapiga kampeni kituoni, huyo Baba alihamaki, akamrukia Nassari wakamchangia na Diwani mmoja aliyeitwa Kalanga, wakamsukuma akaanguka damu ikaanza kumtoka puani, tukalazimika kuingilia kati na kuondoka na Nassari akaenda mahali tulipokuwa tunalala akabadili mavazi akaenda kutibiwa Minjingu,  hata tulipofika huko waliendelea kutufuata wakaja na gari imejaa vijana wa kimasai wakimtafuta Nassari, hivi tulilazimika kukodi gari ambayo hawaifahamu ndipo tukamwondoa kumpeleka Arusha hospitali ya Selian kwa matibabu zaidi'.
Taarifa zaidi kutoka Makuyuni zinasema walipomkosa Nassari walimpiga dereva wake Gadi Palangyo  na Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Monduli, Thomas Kilongola, hadi walipokuja kuokolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Makuyuni. Hadi tunaandika habari hii Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia suala hili baada ya simu yake kuita bila mafanikio.

HABARI MSETO

Waliofariki kwa bomu Arusha waanza kutambuliwa

DSC07407
Wahanga wa mlipuko wa jana jijini Arusha
 WATU wawili ambao ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , waliofariki jana baada ya kulipukiwa na bomu katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Udiwani kata ya Kaloleni,jijini Arusha, mmoja ametambuliwa na mwingine bado hajafahamika.
Mganga, mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Arusha, Dakta Josiah Mlay, amemtaja marehemu huyo kuwa ni Judith Mushi, (46) mkazi wa Sokon one jijini Arusha, na mwingine ni kijana wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 15-16 ambae hajafahamika ambae alifia hospital ya AICC.

Dakta Mlay, amesema katika tukio hilo hospital hiyo imepokea majeruhi 10 kati ya 15 na wote ni wanaume isipokuwa majweruhi mmoja wa kike aitwae Sharifa Jumainne ,ambae hali yake ni mbaya.

Amesema kuwa katika uchunguzi wa awali imegundulika kuna kupande cha chuma kwenye mapafu ambacho kinatokana na mlipuko wa bomu

Aidha amesema kuwa majeruhi mwingine aliyepata majeraha ya kichwa amehamishiwa kwenye hospital ya Seliani ya Arusha kwa uchunguzi zaidi akisubiriwa kupelekwa hospital ya rufani ya KCMC ya mjini Moshi.

Dakta Mlay, amesema hali za majeruhi wengine waliolazwa hospital ya mkoa wa Arusha ya mount Meru, zinaendelea vizuri.

Wakati huo huo tume ya taifa ya uchaguzi jimbo la Arusha, imeahirisha uchaguzi huo hadi June 30 mwaka huu kutokana na tukio hilo la mripuko wa bomu lililojeruhi watu .
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, amewatembelea majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospital mbalimbali za mkoani Arusha zikiwemo mount Meru, Seliani, na AICC .
Katika hatua ingine viongozi mbalimbali w a chadema wametembelea katika eneo la tukio akiwemo mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Freeman Mbowe na wabunge wa jimbo la Arumeru pamoja na Arusha mjini.
 
Chanzo:Libeneke

Steps yatoa tuzo kwa wasanii vinara 2012

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps, Diresh Solanki akimpa tuzo msanii bora wa kiume katika tasnia ya filamu nchini Jacob Stevin JB wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com
Pazia ra Tuzo za Steps Bongo Movie Awards ukiwa umefunguliwa na waziri wa Sayansi na Teknolojia Makame Mbawala

Mzee Majuto akipokea Tuzo ya msanii bora wa uchekeshaji


Msanii Stiv Nyerere akipokea Tuzo

Msanii Nice Mohamedi 'Mtunis' akipokea tuzo ya Mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Steps Entatainment tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com

MAMA SHILOLE AKIWA JUKWAANI

Mtoto Jenifa akichukua tuzo yake

Add caption

Msanii Niva akichukua TUZO ya msanii bora Chipkizi kulia yupo msanii mwenzake Rado

Photo: Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com

Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete wa tatu kushoto akiwapongeza baadhi ya wasanii wa marehemu Kanumba baada ya kuwakabizi tuzo

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akimkabizi tuzo ya mwongozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 Vicent Kigosi 'Ray ' wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akifafanua jambo baada ya kumkabizi tuzo Vicent Kigos 'Ray' ya mwogozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com

Wafanyakazi wa Kampuni ya Steps wakipokea tuzo

Baazi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabiziwa tuzo zao za kwanza kwa mwaka 2012 zilizozaminiwa na kampuni ya steps Picha na www.burudan.blogspot.com

MPIGA PICHA mOHAMED aralakia  ZA KAVA MBALIMBALI ZA KAMPUNI YA STEPS AKIPOKEA TUZO

:KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo

Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampunu hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo

Baadhi ya washindi ambao walipatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Stevin Mangendela 'Stive Nyerere', Issa Mussa 'Cloud 112' Mohamed Nurdini 'Chek budi' Nice Mohamed 'Mtunisi' Iren Paul akinyakuwa msanii bora chipkizi wa kike

Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Stevin 'JB' huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Iren Uwoya

na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda 'Jimmy Masta'

Wakati katika kipengere cha muhongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi' Ray' na kampuni yake ya RJ Filamu

mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri rakini kwa sasa awapo duniani moja ni kwa Stevin Kanumba,Saidi Kilowoko 'Sajuki' John Stefano,
Hussein Ramadhani Mkiety,'Sharo Milionea'

Katika utoaji wa tuzo huzo kulikua na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi

Kanye West, Kardashian wapata mtoto wa kike

Kardashian alipokuwa mjamzito akiwa na Kanye West

MASTAA wawili wapenzi nchini Marekani Kanye West na Kim Kardashian wamechekelea mahusiano yao kuzaa matunda baada ya wawili hao kufanikiwa kupata mtoto wa kike asubuhi ya jana.
Kardashian alijifungua mtoto huyo kwenye hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center, Los Angeles, mtandao wa OMG umethibitisha, na ikielezwa kuwa wakati mrembo huyo alijifungua Kanye West alikuwa pembeni kushuhudia tukio hilo ambalo limekuja mwezi mmoja na tarehe ilioyotangazwa awali kwamba mtoto huyo angezaliwa Julai 11.

"Kim aliugua Ijumaa usiku na hatimaye kupata mtoto mapema jumamosi," chanzo cha hospitali kimeileza Us Weekly. “Inafurahisha, wote wako katika hali nzuri!"

Kanye West, 36, na Kim 32, huo ni uzao wao wa kwanza kwa kila mmoja ambao walianza kuwa wapenzi tangu mapema mwaka jana kabla ya Desemba, 2012 kutangaza uchumba wao kujaliwa mimba hiyo.

Polisi yatuma timu maalum kuchunguza tukio la mlipuko wa bomu Arusha

JESHI la Polisi Tanzania, limetangaza kutuma timu maalum ya uchunguzi kwenda Arusha kwa ajili ya kuchunguza tukio la mlipuko unaosadikiwa kuwa bomu ambao umesababisha vifo vya watu wasio na hatia uliotokea jana jioni kwenye mkutano wa kufungia kampeni wa chama cha CHADEMA.
Taarifa ya jeshi hilo inayoeleza kila kitu kuhusu kikosi kazi hicho kilichotumwa Arusha hiyo hapo chini isome mwenyewe.


http://3.bp.blogspot.com/-XK38jMSnmvE/Ub248DhoAKI/AAAAAAAAIXo/2F2B0KsG37c/s1600/taarifa.jpg

Safari ya Tanzania kwenda Brazili yafikia mwisho yalala 4-2 kwa Ivory Coast Taifa

Thomas Ulimwengu akimtoka Bamba Seleman katika pambano lililoisha jioni hii (Picha:Bin Zubeiry)

SAFARI ya Tanzania katika mbio za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014, zimefikia ukingoni baada ya jioni hii timu ya taifa, Taifa Stars kukubali kipigo cha mabao 4-2 mbele ya Ivory Coast katika pambano kali la kundi C.
Stars ilikuwa ikihitaji ushindi ili kuweka hai matumaini yake ya kuingia hatua ya mtoano wa Top 10, pamoja na kuonyesha kiwango kikubwa, ilishindwa kufurukuta kwa vinara hao wa ubora wa soka Afrika na kulala.
Ushindi huo uliopatikana kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam umeifanya Ivory Coast kufuzu hatua hiyo ya mtoano wa timu bora 10 kwa kufikisha pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ya kundi hilo.
Stars ilianza pambano hilo kwa bao lilitupiwa kambani na kiungo Amri Kiemba dakika ya kwanza ya mchezo kabla ya Ivory Coast kusawazisha dakika ya 13 kupitia Lacina  Troure.
Kiungo mahiri wa Manchester City Yaya Toure aliifungia Ivory Coast bao la pili kwa mpira wa adhabu ndogo katika dakika ya 23 ambalo lilirudishwa na Thomas Ulimwengu dakika ya 34 akiunganisha krosi ya Shomar Kapombe iliyoguswa na Amri Kiemba.
Dakika moja kabla ya mapumziko, Yaya Toure aliiandikia tena Ivory Coast bao la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya beki Erasto Nyoni kumwangusha Gervinho na kufanya hadi mapumziko matokeo kuwa mabao 3-2.
Kipindi cha pili, Tanzania ilionyesha kama ingeweza kurudisha bao kwa kasi iliyoingia nayo na kufanya kosa kosa kadhaa kabla ya mtokea benchi, Wilfred Bony kuiandikia wageni bao la nne dakika ya 74.
Bao hilo liliwakatisha tamaa mashabiki waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa na kuanza kutoka uwanjani kwa kuamini safari ya timu yao imefikia mwisho licha ya kusaliwa na mechi ya kukamilisha ratiba dhidi ya 'vibonde' Gambia ambao jana walilala mabao 2-0 mbele ya Morocco.

Ntiro, Nyagawa waibeba Golden Bush Veterani wakiilaza Mburahati Veterani 3-2

Onesmo Waziri 'Ticotico' akimiliki mpira langoni mwa Mburahati, huku Salum Swedi (11) akiwa tayari kutoa msaada.

Hekaheka langoni mwa Mburahati baada ya Machota (2) kukaribia kufunga bao

Peter Kalumbeta (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka Shija Katina wa Golden Bush

Mohammed wa Mburahati akichuana na Shomari

Nico Nyagawa 'akikusanya kijiji' kwa kuwatoka wachezaji wa Mburahati Veterani
Faraji wa Golden Bush (kulia) akikokota mpira huku akifuatwa na beki wa Mburahati huku Abuu Ntiro akiwa tayari kumsaidia wakati timu zao zilipoumana asubuhi ya leo.
Wachezaji wa Golden Bush Veterani wakati wa mapumziko
 
Kudra Omar wakati wa mapumziko
Nico Nyagawa akitafakari wakati wa mapumziko
Onesmo Waziri 'Ticotico' akichuana na wachezaji wa Mburahati huku Nahodha wake Yahya Issa akiwa makini kumsaidia

Yahya Issa akiambaa na mpira mbele ya mchezaji wa Mburahati
Salum Swedi (11) akiambaa na mpira huku akichungwa na beki wa Mburahati Veterani

Mshambuliaji nyota wa zamani Atufugwegwe Mwakalukwa (kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wa Mburahati nje ya uwanja
Benchi la timu ya Mburahati Veterani wakiwa hawaamini kama Golden Bush wamewashika leo kwenye uwanja wa Chuo Kikuu

Mchezaji wa Mburahati akiambaa na mpira huku mwenzake akiwa makini kumsaidia

Peter Kalumbeta wa Mburahati (kulia) akimtoka beki wa Golden Bush
WAKATI vijana wao jana kulala mabao 2-0 mbele ya Simba, timu ya Golden Bush Veterani leo asubuhi wamejifariji baada ya kuinyuka Mburahati Veterani kwa magoli 3-2 katika mchezo wa kirafiki.
Vijana wa Golden Bush walilala kwa Simba katika pambano lililochezwa jana jioni kwenye uwanja wa Kinesi, lakini wazee wao walifanya kweli viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Golden Bush Veterani ambayo wiki kadhaa ilikuwa 'baba huruma' kwa kuchezea vipigo kwa wapinzani wao, walianza kuandika bao katika kipindi cha kwanza kupitia Abuu Ntiro.
Licha ya Golden Bush iliyosheheni nyota waliowahi  kutamba nchini kama ivo Mapunda, Salum Swedi 'Kussi', Nico Nyagawa, Yahya Issa, Kudra Omar, Wisdom Ndlhovu, Steven Marashi na wengine kusakama lango la Mburahati matokeo yalibaki bao 1-0 hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ya wachezaji na kwa kiasi fulani ilibadili kasi na Mburahati ilifanikiwa kusawazisha bao kupitia shuti kali lililopigwa na Peter Kalumbeta.
Hata  bao hilo lilidumu kwa dakika moja tu kwani Nico Nyagawa alifunga bao la pili la Golden Bush akimalizia kazi nzuri ya Shoamri aliyepanda mbele.
Winga msumbufu wa Mburahati Ally 'Neymar' alifunga bao la kusawazisha kwa timu yake baada ya kuwatoka mabeki wa Golden Bush na kupiga shuti lililomshinda kipa Steven Marashi.
Dakika za lala salama baada ya kulilia kuingizwa dimbani, Machota alionyesha hakulilia bure kucheza mechi hiyo kwani aliiandikia Golden Bush bao la tatu na la ushindi kwa kichwa akimalizia krosi safi ya De Natale.
Mbuharati alikaribia kupata bao la kusawazisha kama sio uzembe uliofanywa na winga wao wa kulia, Karume kushindwa kutumbukiza wavuni mpira akiwa yeye la lango kufuatia kroshi ya 'Neymar'.
Mpaka filimbi ya mwamuzi Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' ikilia kuashiria mwisho wa pambano hilo Golden Bush waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-2 mbele ya wapinzani wao, Mburahati iliyowakosa baadhi ya nyota wao kama Abdul na Juma Chilumba na Atufugwegwe Mwakalukwa katika mchezo huo.