STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 13, 2014

'HATUITAKI KATIBA MPYA PENDEKEZWA'

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema hakiikubali Katiba inayopendekezwa kwa kuwa haina maslahi ya wananchi wa Zanzibar.
Badala yake chama hicho kimewataka Wazanzibari waikatae Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba (BMK).
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Demokrasia vya Kibanda Maiti, mjini Zanzibar.
“Wananchi, Katiba haikubaliki kwa Wazanzibari, mimi mwenzenu siikubali, sijui nyinyi wenzangu?” alihoji Maalim Seif na wananchi kuitikia kuwa nao hawaikubali.
Alisema kuwa miongoni mwa mambo yanayoipokonya Zanzibar hadhi yake ni Katiba inayopendekezwa kumpokonya Rais wa Zanzibar mamlaka ya kugawa mikoa, tofauti na Katiba ya Zanzibar ya sasa. 
Alisema kwa maana hiyo Rais wa Muungano anachukua mamlaka ya Rais wa Zanzibar na anaweza kuteuliwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wa Zanzibar. 
“Kwa mabadiliko hayo ya rasimu ya Chenge, Rais wa Muungano anaweza kututeulia Sheha wa Shehia ya Mtoni Zanzibar kutoka Bukoba,” alisema Maalim Seif huku akishangiliwa na wanachama na wafuasi wa CUF.
Maalim Seif alisema Katiba ya Zanzibar na marekebisho yake ya mwaka 2010 iko sahihi kabisa na inazingatia matakwa ya Makubaliano ya Muungano.
Alisema hayuko tayari kuona rasimu hiyo inakubalika na kwamba Wazanzibari hawataki kuiona.
Alisema hakubaliani na kauli za baadhi ya watu waliosema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inaridhishwa na mchakato wa Katiba mpya.
“Nataka kuwambia hakuna kikao chochote cha SMZ kilichokaa na kusema tunaijadili rasimu, kama kuna mtu anataka kusema eti Smz imeridhishwa aseme mwenyewe binafsi na siyo Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Maalim Seif.
Maalim Seif aliisifu Rasimu ya Jaji Joseph Warioba ambayo ndiyo ilizingatia matakwa ya Watanzania walio wengi na kwamba pamoja na awali Wazanzibari kupendekeza muundo wa Muungano wa mkataba, lakini kwa busara ya tume hiyo waliikubali muundo wa serikali tatu.
Maalim Seif alisema anahutubia mkutano huo akiwa na furaha kubwa kutokana na umma ulioteremka katika viwanja vya Kibandamaiti, na hiyo ni sababu tosha na ujumbe kuwa hawaitaki Katiba inayopendekezwa.
“Ndugu yangu, rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete ufahamu kuwa umma huu uliohudhuria Kibandamaiti ni ujumbe tosha kuwa Katiba hiyo hawaitaki, na mwambia Rais Kikwete kuwa Katiba hii hatuikubali,” alisema Maalim Seif. 
Maalim Seif alisema Katiba bora ni ile inayozingatia maoni ya wananchi. 
“Lakini Rais (Rais Jakaya Kikwete), Katiba yenu mmeweka upande maoni ya wananchi, mmejifungia wenyewe, mmeipitisha wenyewe na mmeichezea ngoma wenyewe”, alisema. 
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui, alisema wajumbe saba wa Bunge Maalum la Katiba waliopiga kura ya Hapana hadharani kukataa rasimu hiyo ni mashujaa wa Zanzibar na Wazanzibari wote wanapaswa kuwapa heshima kubwa.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Salum Bimani, alisema wananchi wa Zanzibar wameshaamua na hawatarejea nyuma zaidi ya kuiondoa CCM mwaka 2015 na kuipa Zanzibar mamlaka kamili.
Bimani alisema msiwape kura viongozi wa CCM ambao wanauza nchi ya Zanzibar huku wakicheza ngoma.
“Kwa Shilingi 300,000 watu hawa wanadiriki kuuza nchi, hawa waliopiga kura za ndiyo ni madalali wa Zanzibar, hata wale waliopiga kura za siri pia ni madalali,” alisema Bimani.
Alisema wanasheria wawili wameitetea Zanzibar na wakafikwa na masahiba mazito.
Aliwataka wanasheria hao kuwa Jaji Walfgong Dourado na Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyefutwa kazi, Masoud Othman Masoud.
Bimani alisema Wazanzibari wapo pamoja nao katika kuhakikisha Zanzibar inabaki na wale wenye nia mbaya wajue kwamba Zanzibar wataitapika watake wasitake. 
Mansour alisema naendelea kuwa muumini wa Maridhiano ya Zanzibar. Katiba hii ni yao wenyewe si ya Wazanzibari.
“Baada ya kuona umma huu uliohudhuria katika mkutano huu tunapaswa kumhofia Mwenyezi Mungu,” alisema.
“Naendelea kumuunga mkono Maalim Seif Sharif Hamad, ni kiongozi asiyekuwa mnafiki anajitambua na hatawaliwi na utawala wa Dodoma, anatawaliwa na Wazanzibari wenyewe na matakwa na matumaini yao,” alisema na kuwataka Wazanzibari wasiwe na hofu kwani hawawezi kufungwa wote wako wengi sana, wakati umefika. 
“Tumeungana kwa hiari yetu, tukakubali kwa hiari yetu, sisi si watumwa wa mtu yoyote, tumefungwa tumefukuzwa makazini kwa sababu ya nchi hii, hatuwezi kurudi nyuma,” alisema.
Alieleza kuwa watu wasishangae kumuona Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Mzee Nassoro Moyo, amesimama kwenye jukwa anatetea nchi yake.
Mzee Moyo alisema Wazanzibari hawakubalini kuona watu wanataka kuichukua nchi yao ovyo ovyo.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza kuhutubia na Maalim Seif tangu BMK limalize kazi yake na kuwasilisha rasimu kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, ulihudhuriwa na maelefu ya wananchi huku baadhi yao wakibeba mabango.
Baadhi ya mabango hayo yalibeba ujumbe usemao “Wapige mabomu rasimu yao hatuitaki, Hongera Othman Masoud, Katiba ya vijisenti (Chenge) hatuitaki”. 
Katika hatua nyingine, Maalim Seif alikanusha taarifa kwenye mitandao kuwa hatajiuzulu wadhifa huo na ataendelea kukiongoza CUF kushika madaraka na kushika Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika uchaguzi mkuu wa mwakani, akiwa kwenye nafasi hiyo.
Maalim alisema taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa baada ya kufukuzwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Masoud Othman Masoud, naye amejiuzulu Umakamu wa Kwanza ni uzushi mtupu.
CHANZO: NIPASHE

CAF yaichomolea Morocco AFCON 2015

http://static.goal.com/243400/243477_heroa.jpgSHIRIKISHO la Soka Afrika, CAF, limeichomolea Morocco wenyeji wa Fainali za Afrika za mwakani, ambao waliomba kuahirishwa kwa michuano hiyo kwa hofu ya ugonjwa wa EBOLA.
CAF wamesisitiza kuwa fainali hizo za mataifa ya Afrika 2015 itaendelea kama ilivyopanga licha ya hofu ya wenyeji dhidi ya ugonjwa huo hatari.
Morocco waliomba shindano hilo liahirishwa kufuatia mripuko wa ugonjwa huo ambao umeua watu zaidi ya 4,000 baada ya maafisa wa afya nchini humo kuonya kuendelea kwa fainali hizo kwa madai yanaweza kuendeleza uambukizaji zaidi.
Mshauri wa Waziri wa Michezo wa Morocco, Mohammed Ouzzine, alieleza taifa hilo la magharibi mwa bara hilo lina wasiwasi kuandaa shindano hilo linalochukua wiki tatu.
“Matakwa ya Morocco na wakaazi wake pamoja na wale wa bara Afrika yanadunisha linguine lolote. Morocco wamewasilisha ombi hilo kufuatia ushauri muhimu kutoka maafisa wa afya.
“Hatuwezi hatarisha maisha ya watu kwa kuendelea kuandaa shindano hili kwani msingi wa tahadhari unafaa kufuatwa,” mshauri Hamid Faridi aliambia stesheni ya redio, Atlantic Jumamosi.
Kwa majibu, Caf walitoa taarifa wakitofautiana na wenyeji hao huku Afrika Kusini wakilengwa kama waandalizi wa dharura ikiwa Morocco watajiondoa.
“Caf wanadhibitisha hakuna badiliko kwenye ratiba ya shindano hili. Tungependa kukumbusha kwamba tangu dimba la kwanza la 1975, shindano hili halijawahi chelewa au kuhairishwa,” taarifa ya utawala huo wa kandanda ilisema.
Mataifa ya Afrika magharibi, Guinea, Liberia na Sierra Leone yameadhirika zaidi na mkurupuko wa sasa wa Ebola. Guinea na Sierra Leone bado wanawania tiketi za Morocco 2015.
Afrika Kusini waliokoa jahazi la shindano hilo 1996 na mwaka jana.

ARSENAL MAJANGA, MAJERUHI WAZIDI KUONGEZEKA

http://img.bleacherreport.net/img/images/photos/003/042/640/hi-res-a01b8eaefd6aaec9613b24d358507950_crop_north.jpg?w=630&h=420&q=75KLABU ya Arsenal imezidi kupata pigo baada ya nyota wake kadhaa kupata majeraha, kufuatia kuumia kwa beki Laurent Koscielny aliyelazimika kujiondoa kwenye mazoezi ya timu yake ya kitaifa ya Ufaransa.
Beki huyo wa kati amejitoa Les Blues kutokana na maumivu ya ukano wa kisigino.

Meneja Arsene Wenger amepigwa na pigo moja baada ya lingine ikiwa ni mechi saba tu ndani ya msimu mpya huku ambapo sasa Koscielny anajiunga na nyota wenzake Danny Welbeck, Mathieu Debuchy, Mikel Arteta, Olivier Giroud, David Ospina, Aaron Ramsey na Yaya Sanogo kwenye zahanati.

Siku mbili baada ya Ujerumani kutangaza kiungo nyota Mesut Ozil atalazimika kutocheza kati ya wiki 10 na 12, Wenger ameongezewa tumbo joto na habari kuwa beki Koscielny amejiondoa kutoka mechi za Ufaransa dhidi ya Ureno na Armenia kwenye msururu wa kufuzu Kombe la Euro la 2016, huku Danny Welbeck naye akiiumia wakati England ikishinda 1-0.
Shirikisho la Ufaransa limeandika kwenye anwani yao ya mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa Koscielny anauguza uvimbe wa ukano wake wa kisigino.

Kocha Nigeria aweweseka kipigo cha Sudan, aomba radhi

http://mobifootball.com/wp-content/uploads/2013/08/B13FEGB0345.jpgKOCHA wa timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Keshi bado yuko katika mshangao kufuatia kipigo walichopata kutoka kwa Sudan katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika. 
Super Eagles walishindwa kucheza kwa kiwango chao cha juu na kujikuta wakichapwa bao 1-0 katika Uwanja wa Manispaa jijini Khartoum katika mechi za kuwania Fainali za Kombe la Afrika mwakani. 
Keshi amesema kikosi chake kingeweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo kama nafasi walizotengeneza zingetumika ipasavyo lakini haraka aliwaomba radhi mashabiki wa Nigeria kwa kupoteza mchezo huo. 
Kocha huyo amesema inabidi aombe radhi kwani mashabiki wa Nigeria walikuwa na imani kubwa na timu yao kuibuka na ushindi. 
Mbali na Keshi lakini pia golikipa na nahodha wa Super Eagles Vincent Enyeama naye aliwaomba radhi mashabiki kwa kipigo hicho na niaba ya wachezaji wenzake na kuahidi kufanya vyema katika michezo yao inayofuata.

Dk Ndumbaro yamkuta, afungiwa miaka 7 katika soka

BAADA ya tetezi zilizokuwa zikizagaa kwamba huenda Mwanasheria wa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara, Dk Damas Ndumbaro yupo kitanzini na huenda akaadhibiwa kwa kauli alizotoa hivi karibuni kuhusiana na makato ya 5% zilizotakiwa na Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, hatimaye imethibitika kuwa kweli.
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia Dk Ndumbaro kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa miaka saba na faini ya kiasi cha fedha.
Ndumbaro ambaye aliingia katika mzozo mkubwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi wiki iliyopita baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom, wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam TV.
Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa shirikisho, Malinzi.
Kikao cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha faini kwa sababu, Ndumbaro ambaye alizungumza kama wakili wa klabu za ligi kuu kupitia,.
TFF imedai Ndumbaro amekanwa na klabu ingawa taarifa zinaeleza si kweli kwa kuwa viongozi wa klabu 12 walisaini kumpitisha kuwa wakili wao.