STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, December 7, 2013

Mario Balotelli aiokoa Milan ugenini, Juve dah!

 http://cdn.bleacherreport.net/images_root/slides/photos/003/451/372/hi-res-452749825-mario-balotelli-of-milan-celebrates-his-teams-second_crop_650x440.jpg?1385904879
SUPER Mario Balotelli aliyenukuliwa kwamba ataacha utukutu wake, ameifungia timu yake ya AC Milan mabao mawili na kupata sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Livorno katika mfululizo wa Ligi ya Italia (Seria A) muda mfupi uliopita.
Balotelli alianza kwa kuwashtua wenyeji kwa kufunga bao la kuongoza dakika ya saba tu ya mchezo huo kwa kujunganisha krosi pasi ya Kaka kabla ya wenyeji kusawazisha kupitia kwa Luca Siligardi dakika ya 26 na kwenda mapumziko timu hizi zikiwa nguvu sawa ya kufungana 1-1.
Kipindi cha pili wenyeji walijipatia bao la pili lililotupiwa kambani na Paulinho katika dakika ya 58 kabla ya Balotelli kusawazisha dakika saba kabla ya pambano hilo kumalizika na kuipa pointi moja muhimu Milan ambayo msimu hii imekuwa na wakati mgumu Seria A.
katika mechi nyingine iliyochezwa jana, vinara na watetezi wa ligi hiyo Juventus ilipata ushindi muhimu wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Bologna kwa mabao ya Arturo  Vidal na  Giorgio Chiellini na kufikisha pointi 40 na kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo huo.

PSG yazinduka na kufanya 'mauaji' Ufaransa

Zlatan Ibrahimovic
Kitu! Zlatan Ibrahimovic akifunga moja ya mabao yake jioni hii katika ligi ya Ufaransa

BAADA ya 'kutenguliwa' udhu majuzi na timu ya Evian TG, mabingwa watetezi wa Ufaransa, PSG jioni hii imemaliza hasira zake kwa Sochaux kwa kuishindilia mabao 5-0 katika mfululizo wa mechi za Ligi ya nchi hiyo.
PSG ilipata ushindi huo ikiwa uwanja wake wa nyumbani kwa mabao ya Thiago Silva aliyefunga dakika ya  14 akimalizia kazi ya Zlatan Ibrahimovic kabla ya Ezequeil Lavezzi kufunga bao la pili dakika ya 47 na Edinson Cavani kutupia bao la tatu dakika ya 62 akimaliza pasi murua ya Ibrahimovic.
Zlatan aliongeza mabao mengine mawili katika dakika ya 87 na dakika ya 90+1 na kuifanya PSG iendelea kukalia kiti cha uongozi cha ligi hiyo ikiwa na pointi 40.

Mzee Madiba kupumzishwa kaburini Jumapili ijayo

RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza mazishi ya Nelson Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 mwaka huu kijijini kwake Qunu, katika jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini.

Rais Zuma ametangaza siku 5 za maombolezo kitaifa na bendera zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo. Na ameitangaza siku ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.


Tayari msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria umekamata dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu Bill Clinton na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya viongozi ambao wamethibitisha kushiriki.

Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa wa FNB Desemba 10, 2013 jijini Johanesburg.

Mwili wake utawekwa katika jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia Desemba 11 hadi 13, kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa kijijini Qunu kwa mazishi.

Bayern Munich yazidi kutakata Ujerumani, Ribery arejea na mawili


http://cache.images.globalsportsmedia.com/news/soccer/2013/12/5/402988header.jpg

MABINGWA watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich wameendeleza rekodi yao ya kutopotezaq mchezo baada ya jioni hii kutoa kipigo cha 'mbwa mwizi' cha mabao 7-0 dhidi ya Werder Bremen na kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Mabavarian hao ambao pia ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, walijipatia mabao yake kupitia kwa  beki wa wenyeji Bremen, Assani Lukimya kujifunga kabla ya Daniel Van Buyten, Frank Ribery aliyefunga mara mbili, Mario Mandzukic, Thomas Muller na Mario Gotze.
Katika mechi nyingine za ligi ambayo Bayern wanaendelea kuongoza wakiwa na pointi 41, saba zaidi ya timu inayopifuata katika nafasi ya pili, jana Nurnberg ilizamishwa sare ya 1-1 na Mainz 05, Borussia Monchengladbach kuilaza Schalke 04 kwa mabao 2-1, Stuttgart kuilamba Hannover 96  mabao 4-2, huku  Hamburger SV ikilala 1-0 nyumbani mbele ya Augsburg nayo Eintracht Frankfurt kukubali kipigo nyumbani dhidi ya Hoffenheim iliyoshinda mabao 2-1.

Man Utd bado gonjwa, Chelsea hoi, Liverpool haishikiki England

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/71601000/jpg/_71601162_71601161.jpg
Hawaamini macho yao kama wanaweza kulowa nyumbani mara mbili mfululizo
Cabaye akishangilia bao lililoizamisha Man Utd
Tough task: West Ham's defence could not keep Suarez in check for the full 90 minutes
Suarez akichuana na mchezaji wa West Ham ambapo Liverpool imeshinda mabao 4-1, Suarez akifunga moja na jingine kumbabatiza beki wa wapinzani wao.

Mmorocco Ossuman Assaidi akishangilia bao lake lililoizamisha Chelsea 'jioni'

MABINGWA watetezi wa Ligi ya England, Manchester United imeendelea kuwa 'urojo' baada ya jioni jii kupigwa tena bao 1-0 na Newcastle United ikiwa nyumbani Old Trafford, huku Chelsea ya Jose Mourinho wakionja kipigo wakiwa ugenini dhidi ya Stoke City.
Manchester inayonolewa na David Moyes ilikumba na kipigio hicho cha pili mfululizo baada ya majuzi kunyukwa kama hivcyo na Everton na kuzidi kuwapa wakatiu mgumu mashabiki wa timu hiyo ambao waliozoea kushinda enzi za Sir Alex Ferguson.
Bao lililizamisha Mashetani Wekundu, lilifungwa na Yohan Cabaye dakika ya 61 na kumfanya Moyes kukuna kichwa namna ya kuepukana na vipigo mfululizo ambavyo zimeifanya timu yake kusalia na pointi zake 22 na kung'ang'ania nafasi ya 9.
Katika mechi nyingine, Chelsea ilijikuta ikinyolewa mabao 3-2 na Stoke City, huku Liverpool ikiendelea kufanya mauaji ya shalubela baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya West Ham United kwenye uwanja wa Anfield.
Licha ya kutangulia kupata bao kupitia kwa Andre Schürrle katika dakika ya 9, Chelsea ilishindwa kuendeleza ubabe baada ya Peter Crouch kulisawazisha dakikia tatu kabla ya mapumziko na Stephen Ireland kuongeza la pili.
Schurrle alisawazisha bao hilo dakika ya 53 ikiwa dakika tatu kabla ya wenyeji kupata bao lake na kuonekana kama matokeo yangeisha kwa sare ya 2-2 kabla ya Oussuma Assaidi kufunga bao dakika ya 90 na kuzimisha vijana wa darajani.
Liverpool waliyopata ushindi mnono wa mabao 5-1 juzi dhidi ya Norwich City iliendelea kufanya mauaji kwa kuicharaza West Ham mabao 4-1 yaliyowekwa kimiani na Guy Demel, Mamadou Sakho, kabla ya Martin Skrtel kujifunga na kuwapa wageni bao la kufutia machozi.
Hata hivyo  Luis Suarez alifunga bao la tatu na  wageni nao wakajifunga kupitia kwa Obrein na kuifanya Liverpool kuijongelea Arsenal kileleni kwa sasa.
Katika mechi nyingine, Cardiff City ikiwa ugenini ilikumbana na kipigo cha mabao 2-0 toka kwa Crystal Palace, huku Norwich City ikapata ushindi ugenini dhidi ya wenyeji wao West Brom wa mabao 2-0 na timu za Manchester City ililazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Southampton.
Kwa sasa timu za Sunderland na Tottenham Hotspur zinaendelea kuonyeshana kazi, Spurs wakiwa ugenini.

Tanzanite yashindwa kutamba nyumbani mbele ya Wasauzi
TIMU ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 Tanzania 'Tanzanite' imefungwa mabao 4-1 na Afrika Kusini 'Basetsana' kwenye mchezo wa raundi ya pili ya  kutafuta nafasi ya kufunzu kombe la dunia mwakani nchini Canada kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Afrika Kusini ilianza vyema mchezo huo kwa  kuwazidi  ujanja Tanzanite katika kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya kuzitumia vizuri nafasi walizopata kwa kufunga bao la kwanza dakika ya nne ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wake Amogelang Motay.
Bao hilo liliamsha mashambulizi  makali kwa Tanzanite waliokuwa wakitafuta nafasi ya kusawazisha ambapo dakika ya 13 walifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Theresa Yohana alimpiga shuti la mita kama 30 na kuingia golini moja kwa moja.

Mashambulizi yaliendelea pande zote mbili, ambapo dakika ya 17 mchezaji wa Afrika Kusini Shiwe Nogwanya aliipatia timu yake bao la pili lililodumu hadi mapumziko.

Baada ya mapumziko timu zote zilikuwa zikifanya mashambulizi  lakini Afrika Kusini waliendeleza mashambulizi yao upande wa Tanzanite na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa mchezaji wake Mosili Makhoali dakika ya 61.
Uzoefu wa Afrika Kusini ulionekana dhahiri kwani waliliandama lango la Tanzanite kila mara lakini golikipa Najiat Abbas alikuweza kupangua mashuti kadhaa na mengine kuishia nje lakini uzembe wa mabeki uliweza kusababisha kufungwa bao la nne dakika ya 78 kupitia kwa Mosil Makhoali.

Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, Waziri wa habari, vijana michezo na Utamaduni, Fenella Mukangara aliwataka wachezaji kutolia kwani mwanamke jasiri anapanga nini afanye baada ya alichotangulia kukifanya hivyo kwa pamoja na benchi la ufundi wakae watathimini walipokosea ili wafanye marekebisho kwa ajili ya mchezo wa marudiano

Kili Stars hiyoo nusu fainali ya Chalenji, Ivo Shujaa

Mashujaa wetu Kilimanjaro Stars waliotinga nusu fainali za Chalenji
TIMU ya Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Chalenji baada ya kuwavua taji waliokuwa watetezi wa michuano hiyo Uganda The Cranes kwa mikwaju ya penati 3-2 baada ya kumaliza muda wa kawaida wakifungana mabao 2-2, Shujaa akiwa Ivo Mapunda aliyedaka penati mbili.
Kwa ushindi huo Stars sasa itavaana na wenyeji wao Kenya, Harambee Stars ambayo jioni hii nayo imepoata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rwanda 'Amavubhi' katika robo fainali ya pili.
Katika pambano la Kili Stars dhidi ya Uganda, lililochezwa kwenye uwanja wa Manispaa ya Mombasa, Kenya, Uganda ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza likifungwa na Daniel Sserunkuma katika dakika ya 16 akimalizia krosi ya Hamis Kiiza, kabla ya Mrisho Ngassa kusawazisha dakika mbili baadaye.
Baada ya bao hilo Stars walizidi kucharuka na kuliandama lango la The Cranes kabla ya Ngassa kuwanyamazisha waganda kwa kufunga bao la pili dakika ya 39, matokeo yaliyodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili Kili Stars inayofundishwa na Kim Poulsen, raia wa Denmark, ilipata pigo baada ya kiungo wake Salum Abubakar 'Sure Boy' kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kucheza rafu, ambapo nafasi hiyo iliwapa nguvu Uganda kupata bao la kusawazisha kupitia Martin Mpuga matokeo yaliyodumu hadi mwisho.
Ndipo ikafuata changamoto ya penati na Tanzania kufanikiwa kupata mikwaju mitatu kupitia kwa Amri Kiemba, Athuman Idd 'Chuji' na nahodha Kelvin Yondani, huku Uganda wakipata  kupitia kwa Emmaneul Okwi na Hamis Kiiza.
Waliokosa kwa Kili Stars ni Erasto Nyoni na Mbwana Samatta aliyekuwa nyota wa mchezo huo wa leo, huku Godfrey Walusimbi, Khalis Alucho na Sserunkuma walikosa baada ya kipa Ivo Mapunda kuonyesha ushujaa kwa kuokoa mikwaju yao na kuivusha Kili Stars nusu fainali na ikilipa kisasi kwa Uganda.
Kenya nayo ilifuatia baadaye uwanjani na kupata ushindi wa bao 1-0 na hivyo kujikuta uso kwa uso na Kili Stars ambayo mwaka uliopita ilishika nafasi ya nne kwa kufungwa na ndugu zao Zanzibar Heroes ambato safari hii wametoilewa hatua ya makundi.