STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 9, 2014

Francis Cheka kuzipiga na Pascal Ndomba

Francis Cheka
Pascal Ndomba
BINGWA wa zamani wa Dunia wa WBF, Francis Cheka anatarajiwa kupanda ulingoni siku ya Novemba Mosi kupigana na bondia Pascal Ndomba katika pambano lisilo la ubingwa litakalofanyika mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) Chaurembo Palasa, pambano hilo la uzito wa juu litachezwa kwenye uwanja wa Sabasaba mjini humo.
Palasa alisema TPBC imetoa baraka zote kwa pambano hilo litakalokuwa la raundi 10.
Rais huyo alisema mchezo huo na mingine ya utangulizi siku hiyo imeandaliwa na kampuni ya Cheka Promotion na mabondia watakawasindikiza wanatarajiwa kutangazwa baadaye.
Hilo litakuwa ni pambano la kwanza kwa mabondia hao kukutana na pia la kwanza kwa Cheka tangu bondia huyo alipopanda ulingoni mara ya mwisho  Aprili 19 mwaka huu alipopigana na bondia toka Iran Sajad Mehrabi  na kutoka naye sare kwenye ukumbi wa PTA.
Cheka ndiye bondia asiyepigika nchini kwa sasa akiwa amewatandika karibuni wapinzani wake wote tangu mwaka 2008 hajapigwa, ingawa anapotoka nje ya nchi amekuwa 'urojo'.

Newz Alert! Kaburi ya aliyekufa ajali ya mkoani Mara lafukuliwa

KABURI la mmoja kati ya watu waliopoteza maisha katika ajali mbaya iliyohusisha mabasi ya Mwanza Coach na J4 katika eneo la Sabasaba, Musoma, Mara limekutwa likiwa limefukuliwa na watu wasiojulikana leo asubuhi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichofika katika eneo la makaburi ya Musoma Basi, ndugu wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Juma Sai walienda asubuhi kuangalia kaburi ikiwa ni siku ya tatu tangu wafanye mazishi, ndipo walipokuta kaburi limefukuliwa na mbao zilizotumika kuhifadhi mwili kwa imani ya dini ya kiislamu zikiwa zimewekwa pembeni.

“Mwili wa marehemu bado uko ndani, watu wengi wako hapa na polisi wameimarisha hali ya usalama. Madaktari wameshafika hapa na wanafanya uchunguzi kuona kama kuna kiungo chochote kilichotolewa kwenye mwili wa marehemu. Inasikitisha sana.” Kimeeleza chanzo chetu cha kuaminika.

Ijumaa iliyopita, kulitokea ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, mabasi ya kampuni ya Mwanza Coasch na J4 pamoja na gari dogo aina ya Landcruiser. Watu zaidi ya 40 walifariki na wengine 79 kujeruhiwa.

Udaku Specially

Maskini, Kisura huyu kumbe alijinyonga

Ripoti: Mwimbaji wa kike wa Marekani aliyekutwa amekufa nyumbani kwake alijinyonga
POLISI wa Los Angeles wameeleza kuwa mwimbaji wa kike wa Marekani, Simone Battle aliyekutwa amekufa nyumbani kwake wiki iliyopita alijiua kwa kujinyonga.
Sababu ya kifo chake imetajwa siku mbili baada ya polisi kuanza uchunguzi kufuatia tukio hilo lililotokea kusini mwa Hollywood.
Simone Battle aliwahi kuwa mshiriki wa shindano la kuimba la X Factor na kufika katika hatua ya fainali, pia alikuwa member wa kundi la G.R.L.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda kutua nchini kesho

http://media.web.britannica.com/eb-media/05/61705-004-8486B3D5.jpg 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, anatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatano asubuhi, tarehe 10 Septemba, 2014 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Katika ziara hiyo nchini, Mhe.Museveni atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam. Rais Museveni ataondoka baadaye siku hiyo hiyo kurejea nyumbani.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Didier Zakora atundika daluga kuichezea Tembo wa Ivory Coast

http://images.supersport.com/2014/5/Didier-Zokora-100615-Gestures-R300.jpg 
http://futboler.tv/wp-content/uploads/2014/05/fft99_mf1310873.jpegKIUNGO nyota wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Zokora ametangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya kuitumikia timu ya taifa kwa zaidi ya miaka 10. Maestro kama anavyofahamika kwa mashabiki wa soka nchini mwake, alisema anadhani ni muda muafaka kuwapisha wengine kuitumikia timu hiyo.
"Baada ya miaka 15 ya kucheza soka ya kiwango cha juu, nafikiri ni wakati wa mimi kufikia tamati ya soka soka ya kimataifa" amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 katika mashindano maalum yaliyoandaliwa kwa heshima yake mjini Abidjan kitongoji cha Williamsville."Ni wakati wa kutoa nafasi kwa vijana wadogo. Katika mechi na Sierra Leone, nimeona wachezaji wadogo ambao wanaweza kuchukua nafasi," aliongeza.
Zokora alianza kuichezea timu hiyo tangu mwaka 2000 na amekuwa na rekodi ya kucheza mechi 121.
Amecheza fainali tano za Kombe la Mataifa ya Afrika mfululizo 2006, 2008, 2010, 2012 na 2013, mbali na  Kombe la Dunia mara tatu mfululizo 2006, 2010 na 2014.
Kiungo huyo mkabaji, kwa sasa anachezea klabu ya Akhisar Belediyespor ya Uturuki, baada ya kuchezea klabu nyingine za Racing Genk ya Ubelgiji, Saint-Etienne ya Ufaransa, Tottenham Hotspur ya England, Sevilla ya Hispania na Trabzonspor ya Uturuki pia.
Ni matunda ya akademi ya ASEC Mimosas ya mwaka 1998 ambao walishinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga Dynamos ya Zimbabwe kwenye fainali, michuano ambayo pia Yanga SC ilishiriki.
Zokora ambaye majina yake kamili ni
Déguy Alain Didier Zokora alizaliwa Desemba 14, 1980) ni gwiji mwingine wa Ivory Coast kustaafu kwa sasa baada ya Nahodha wa zamani, Didier Drogba anayechezea Chelsea.

Diamond, Yami Alade kuangusha ya pamoja Coke Studio Africa

STAA wa Mdogomdogo na My Number One, Diamond Platnumz amerejea tena kwenye msimu wa pili wa kipindi cha Coke Studio Africa na awamu hii atatangeneza 'pea' na mkali wa Johnny, Yemi Alade kutoka nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mtandao, Diamond ni msanii wa nne mwaka huu kutoka Tanzania aliyeshiriki kwenye kipindi hicho kinachorekodiwa jijini Nairobi, Kenya.
Wengine waliowahi kushiriki ni pamoja na Vanessa Mdee aliyerekodi na Burna Boy wa Nigeria, Joh Makini aliyerekodi na Chidinma wa Nigeria na Shaa aliyerekodi na Jacky Chandiru wa Uganda.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Yemi aliyekuja nchini hivi karibuni aliweka picha yake akiwa na Diamond katika na kudokeza anavyojisikia furaha kufanya kazi na mshindi huyo wa tuzo saba kwa mpigo wa Kili Music Awards-2014.
#wonderment! With the infamous ubertalented six-abbs superstar Diamond….@diamondplatnumz
#iAmHumbled #thankYouCokeStudio, ForThe Opportunity God bless AFrica.. #cokeastudioafrica
@cokestudioafrica @dresomes Nosa @chocolatecity
Diamond has been singing your song all morning@audumaikori.
Naye Diamond katika picha akiwa na mrembo huyo
ameandika:
Na dem ake Johny @yemialade , ushaelewa nini kinaendelea si eti????….. (jus me and Johny’s
Girlfriend…You allready know what it is ryt???… Cc@yemialade

Hispania yaifumua Macedonia 5-1 bila Diego Costa, David Silva nouma

Silva na Paco Alcacer wakipongezana baada ya kinda hilo (9) kufunga bao
Breaking away: Cesc Fabregas escapes a challenge from Macedonian midfielder Stefan Spirovski as Spain exerted their authority in the midfield areas
Utanivunja nyonga bure! Mtaalam Cesc Fabregas akimpeleka mtu chini
MABINGWA watetezi wa Kombe la Mataifa ya Ulaya, Hispania ikiwa bila mshambuliaji wao nyota Diego Costa anayesumbuliwa na majeraha ya nyama za Paja, usiku wa kuamkia leo ilitoa onyo kwa wapinzani wake baada ya kuifumua Macedonia kwa mabao 5-1 katika mechi za kuwania fainali hizo za Uero 2016.
Mchezaji aliyechukua nafasi ya Costa, Paco Alcacer , 21 aliitenda haki kwa kuifungia Hispania bao la pili katika dakika ya 17 akimalizia krosi pasi safi ya Cesc Fabregas.
Bao la kwanza la wababe hao wa zamani wa Dunia, lilitumbukizwa wavuni na Sergio Ramos  kwa panalti dakika ya 16 baada ya David Silva kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Macedonia walijipatuia bao lao la kufutia machozi katika dakika ya 28 baada ya Juanfran kufanya madhambi na Agim Ibraimi akafunga kwa kumtungua Iker Casillas.
Sergio Busquets aliiandikia Hispania bao la tatu sekunde chache kabla ya kwenda mapumziko, huku mabao mengine ya ushindi huo mnono kwa Hispania yakiwekwa kimiani na David Silva katika dakika ya 50 na Pedro aliyepigilia msumari dakika za lala salama.

Danny Welbeck aibeba England michuano ya kuwania Euro 2016

At the double: Danny Welbeck wraps up victory for EnglandMSHAMBULIAJI mpya wa Arsenal, Danny Welbeck usiku wa kuamkia leo amethibitihs aubora wake baada ya kuipa England ushindi wa 2-0 dhidi ya Uswisi ugenini katika mechi ya kuwania kufuzu Euro 2016. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, alifunga mabao hayo katika dakika za 59 na 90 na kumfanya kocha Roy Hodgson aondoke na furaha uwanjani.
Welbeck aliyekuwa hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu alinyakuliwa na Arsene Wenger mwishoni mwa msimu wa usajili kwa mkopo.

Lulu Kayage atamba kumtandika mtu Sept 27

 Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini akimwelekeza bondia Lulu Kayage jinsi ya kukupa ngumi wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu mpambano utakaofanyika September 27 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam picha na SUPER D BLOG
 Bondia Lulu Kayage kulia akielekezwa jinsi ya kupiga makomde mazito na Kocha Habibu Kinyogoli 'Masta' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu Septermber 27 katika ukumbi wa frends Corner Manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
Bondia Juma Biglee kushoto akioneshana umwamba na Lulu Kayage wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Amana Dar es salaam Lulu anajiandaa na mpambano wake na Fatuma Yazidu utakaofanyika Septermber 27 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage kushoto akipambana na Juma Biglee wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu september 27 Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage kushoto akifanya mazoezi ya kuimalisha misuli ya tumbo wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu september 27 katika ukumbi wa frends corene manzese Dar es salaam kushoto ni Titus Jonson Picha na SUPER D BLOG
Na Mwandishi Wetu

 

lulu kayage
BONDIA Lulu Kayage yupo katika mazoezi makali kwa ajili ya kupambana na bondia Fatuma Yazidu Septermber 27 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam

akizungumza wakati akiwa mazoezini katika kambi ya ilala amana Dar es salaam amemtahadhalisha mpinzani wake kufanya mazoezi ya kutosha kwani yeye kwa sasa yupo fiti kupita kiasi na akuna bondia wa kike kwa Tanzania hii mwenye uzito wake anaeweza kumsumbua kwa sasa kwani ana uzoefu mkubwa na wakutosha

aliongeza kwa kusema kuwa jinsi anavyosimamiwa mazoezi na jopo la makocha wake wanao ongozwa na kocha mkongwe nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na Kondo Nassoro ambao wanamuhimiza kila wakati kufanya mazoezi ya kutosha na ndio wana muongeza moyo zaidi kwa ajili ya kufanya mazoezi

Lulu aliongeza kuwa mchezo wa masumbwi nchini wasichana wanaojitokeza ni wachache sana hivyo kukosa msisimko wa kila wakati kucheza wasichana kwa wasichana hivyo kuomba wasichana mbalimbali wajitokeze kufanya mazoezi na kucheza mchezo kwa  ajili ya afya pia ni kwa ajili ya ajira kumbuka mchezo wa ngumi ni ajira kama una uwezo wa kufanya vizuri

siku hiyo pia kutakuwa na mpambano mkali utakao wakutanisha Nassibu Ramadhani na Mohamed Matumla mwingine ni Sadiki Momba na Adam Ngange, Issa Omari na Juma Fundi
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

Marco Reus bado majanga matupu Dortmund kumkosa wiki nne

KLABU ya Borussia Dortmund imethibitisha kuwa Marco Reus anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nne baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwakani dhidi ya Scotland.
Mshambuliaji alikosa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil kutokana na majeruhi ya kifundo cha mguu aliyopata mwishoni mwa msimu uliopita na sasa inaonekana tatizo limejirudia kwa kujitonesha. 
Hata hivyo Dortmund katika taarifa yake wamedai kuwa majeruhi hayo aliyopata Reus, 25 siyo makubwa sana kama yale yaliyopita. 
Reus sasa anakabiliwa na changamoto ya kuwa fiti kwa ajili mechi za kufuzu za Ujerumani zinazofuata ambazo zitakuwa dhidi ya Poland na Jamhuri ya Ireland katikati ya Octoba mwaka huu.

Maskini! Ajali yaua Diwani wa CCM Iringa

GARI aina ya Toyota Coaster iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka Ludewa Mjini kuelekea Lupingu baada ya kupata ajali iliyoondoa uhai wa Diwani wa Viti Maalum CCM Kata ya Lupingu, Prisca Kayombo (Zaruta).
Diwani wa Viti Maalum CCM Kata ya Lupingu, Prisca Kayombo (Zaruta) wa tatu kushoto enzi za uhai wake akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (wa kwanza kushoto), Katibu wake Stan Gowele (wa pili kushoto) na wananchi wengine wa Ludewa wakijiandaa kunyanyua nguzo ya umeme wiki mbili zilizopita.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wakiwashushwa katika Hospitali ya Wilaya Ludewa, mkoani Iringa leo.
Majeruhi wakiwa katika Hospitali ya Wilaya Ludewa.
Wananchi wa Kata ya Ludewa wakiwa hospitalini hapo kuwaona majeruhi wa ajali.

DIWANI wa Viti Maalum CCM Kata ya Lupingu, Prisca Kayombo (Zaruta) amekufa papo hapo huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya katika ajali mbaya ya gari iliyotokea leo asubuhi huko Ludewa mkoani Iringa.

Mashuhuda wa ajali hiyo walidai kuwa chanzo chake ni gari hilo ambalo walikuwa wakisafiria kutoka Lupingu - Ludewa kufeli breki na hivyo kupinduka .

Inadaiwa baada ya gari hilo aina ya Toyota Coaster inayojulikana kwa jina la DMX kufeli breki dereva aliwataka abiria kutulia ndani ya gari hilo ila diwani huyo hakuweza kufanya hivyo na kuamua kuchukua maamuzi magumu ya kutaka kuruka katika gari hilo ambapo wakati akiruka alimsukuma utingo wa basi hilo na hivyo wote wawili utingo na diwani kufunikwa na gari hilo na kupelekea kifo cha diwani huku utingo akiwa mahututi baada ya kubanwa na gari hilo.

"Diwani amepoteza maisha wakati akiwa njiani kuelekea kujumuika na wananchi wake katika shughuli ya maendeleo ya kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kuelekea kijijini kwake Lupingu" Alisema mmoja wa abiria.

Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe ameeleza kusikitishwa na kifo cha diwani huyo kutokana na mchango wake mkubwa aliouonyesha enzi wa uhai wakati kwa kushiriki vema na wananchi wa kata yake katika zoezi la kufyeka na kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kwenda Lupingu.

Alisema kuwa anakumbuka ni wiki mbili pekee zimepita toka diwani huyo alipoungana nae katika uchimbaji wa mashimo ya nguzo za umeme kwenda kijiji cha Ntumbati na kuwa hata wakati ajali hiyo inamkuta bado alikuwa katika harakati za kuwatumikia wananchi wake.

"Ludewa tumempoteza diwani mchapa kazi na aliyependa kujituma muda wote na hata wakati mwingine diwani huyo alikuwa akifanya kazi ngumu kama mwanaume kwa kubeba nguzo za umeme kwa kushirikiana na mimi na wananchi wake.....kwa kweli kifo chake ni pigo kubwa ndani ya CCM na kwa wananchi wa kata nzima ya Lupingu"

Kwani kati ya madiwani waliokuwa bega kwa bega na wananchi wao na mbunge ni pamoja na diwani huyo ambaye alikuwa mstari wa mbele kuona Kata ya Lupingu inapata umeme wa uhakika baada ya miaka zaidi ya 50 ya Uhuru bila umeme .

Mbunge Filikunjombe alisema atamkumbuka diwani huyo kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo na vile alivyofanya kazi na wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa, Juma Madaha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha kifo cha diwani huyo na kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2 asubuhi .

(PICHA / STORI: FRANCIS GODWIN, IRINGA)