STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, May 20, 2016

Breaking News...! Rais Magufuli amtumbua Waziri Kitwanga, kisa...!

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kwa kosa la kuingia Bungeni kujibu maswali akiwa bwii kwa kilaji. 
Taarifa ya Ofisi ya Rais Ikulu imefunguka kama inavyosomeka hapo chini;


Mabingwa wa England watua salama Bangkok kufanya ziara

http://3.bp.blogspot.com/-X9BbzIKslIA/VPfU84zfvoI/AAAAAAAACs4/BrkAkbrWN1M/s1600/asian%2Bfc%2Bowners%2B5%2Bvichai%2Bsrivaddanaprabha.jpg
Tajiri wa Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha (kulia) akichekelea taji la EPL
MABINGWA wa soka wa England, Leicester City wapo Bangkok, Thailand kwa ajili ya ziara ya kimichezo ikishangilia taji lao la kwanza tangu kuasisiwa kwao zaidi ya karne moja na ushei.
Wakali hao wakiongozwa na Kocha wao, Claudio Ranieri walitua jana katika nchi hiyo ambayo ni asili ya mmiliki wao Vichai Srivaddhanaprabha, ambaye ana furaha kwa mafanikio ya vijana wake, ambao hawakupewa nafasi ya kufunika msimu huu ikizingatiwa msimu uliopita waliponea chupuchupu kushuka daraja.
Kocha Claudio Ranieri

Nahodha wa Leicester City Wes Morgan
Mlinda mlango wa Leicester 

Kaka kashindikana Marekani kwa mkwanja mnene

http://www.trbimg.com/img-55a537e5/turbine/os-orlando-city-kaka-mls-all-star-dream-come-true-20150714
Kaka
AMA kweli wa mbili havai moja. Kiungo wa kimataifa wa Brazil, Kaka ndiye mchezaji anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu ya Marekani-MLS, akimfunika mpaka nyota wa kimataifa wa Italia Sebastian Giovinco na nahodha wa Marekani Michael Bradley.
Kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa jana Alhamisi, Kaka ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or anayeichezea klabu ya Orlando City ya Florida anakunja mkwanja mnene wa Dola 7,167,500 akifuatiwa na Giovinco anayechukua Dola 7,115,556 huku Bradley yeye akichukua dola milioni 6.5.
Nyota wengine wenye majina makubwa waliojiunga na MLS katika miaka ya karibuni ndio wanafuatia akiwemo Steven Gerrard anayecheza Los Angeles Galaxy anashika nafasi ya nne kwa kupokea kiasi cha dola 6,132,500.
Nyota wa zamani wa Chelsea na Manchester City, anayeichezea New York City FC Frank Lampard anayekunja Dola Milioni 6, Andrea Pirlo Dola Milioni 5.9 na David Villa anatia kibindoni Dola Milioni 5.6.

Nyie jichanganyeni muisome namba kwa TFF

http://4.bp.blogspot.com/-CIyoW3Xt1Ww/U531sm4lXlI/AAAAAAAFq1s/q0UL2cH3jy4/s1600/2.jpg
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
NA ALFRED LUCAS, TFF
WAKATI pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara likitarajiwa kufungwa Jumapili Mei 22, 2016 kwa michezo minane, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa onyo kali kwa timu zote kutojiingiza kwenye mtego wa aina yoyote wa kupanga matokeo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameziasa timu zote za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kucheza mechi hizo kwa kufuata taratibu, kanuni za Ligi Kuu kadhalika sheria 17 zinazoongoza mchezo huo ambao unapendwa na mamilioni ya watu Tanzania na dunia nzima.
“Nimefanya tathmini yangu na kubaini kwamba, inawezekana kukawa na mipango ya kupanga matokeo. Nichukue nafasi hii kuzionya timu zote kutojiingiza hulo. TFF iko makini, tena makini sana na ina watu wake kila mkoa ambako michezo hiyo itafanyika, sasa basi naziasa timu kufuata taratibu, kanuni na sheria,” alisema Malinzi.
Mbali ya Malinzi, pia Bod ya Ligi nayo imetoa onyo ikisema michezo yote haina budi kuanza saa 10.00 jioni hata kama kutakuwa na hali ya mvua katika viwanja husika lengo likiwa ni kukabiliana na upangaji wa matokeo.
Baada ya michezo 29 kwa kila timu, tayari Coastal Union ya Tanga ikiwa imeaga rasmi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania 2015/16 na kwamba kuna timu tano ambazo baadhi yake (timu mbili) zikipata matokeo mabaya zitaungana na Wagosi wa Kaya kushuka daraja msimu wa 2015/16. Coastal Union yenye pointi 22 na hata ikishinda mchezo wa mwisho, haiwezi kuzifikia timu zilizo juu yake.
Timu ambazo ziko kwenye hatari ya kushuka ni African Sports ya Tanga yenye pointi 26 (nafasi ya 15); Mgambo pia ya Tanga iliyojikusanyia pointi 27 (nafasi ya 14); Kagera Sugar ya Kagera iliyovuna pointi 28 (nafasi ya 13); JKT Ruvu ya Pwani iliyopata pointi 29 (nafasi ya 12) na Toto Africans ya Mwanza yenye pointi 30 (nafasi ya 11).
Kwa hali ya mambo ilivyo, licha ya kwamba Toto inaweza kujihesabu ina nafuu ikilinganishwa na timu nyingine, ukweli unabaki kuwa kwa timu zenye pointi 27 hadi 29 zinaweza kuishusha kama Wanakishamapanda hao watapoteza mchezo wa mwisho au kupata sare huku wapinzani wao wakishinda.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Toto Africans itakuwa mwenyeji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuikaribisha Stand United, wakati JKT Ruvu mgeni wa Simba ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wenyewe Kagera Sugar watamaliza na Mwadui FC watakuwa kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga wakati Mgambo wataalikwa Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ilihali African Sports ‘Wanakimanumanu’ wataifuata Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro.
Mechi nyingine ya kukunja jamvi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom zitakuwa kati ya Mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu, Yanga itakayokuwa mgeni wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji wakati Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara.
Mchezo mwingine wenye presha utakuwa ni kwa Tanzania Prisons yenye pointi 48 ambayo licha ya kucheza na Coastal Union ambayo imeshuka daraja kwenye Uwanja wa Mkwakwani, itakuwa inafukuziwa na Mtibwa Sugar kuwa na nafasi ya nne. Mtibwa Sugar ina pointi 47.
Tanzania Prisons itacheza na timu ambayo haina nafasi katika Ligi Kuu msimu huu. Presha kubwa ni kwa Simba na Azam ambazo zina tofauti ya pointi moja katika msimamo wa ligi hiyo iliyoshirikisha timu 16.
Azam FC ina pointi 63 ikishika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Yanga huku Simba inayoshika nafasi ya tatu ina pointi 62. Mvutano wa Tanzania Prisons, Mtibwa ni wa nafasi ya tatu na nne hasa ukirejea kwenye zawadi za Vodacom ka timu vinara kama ilivyo kwa Azam na Simba.
Yanga ambayo imetwaa ubingwa, tayari imepewa taji na medali kwa wachezaji 24, viongozi saba wa benchi la ufundi na viongozi wanne wa Kamati ya Utendaji Jumamosi iliyopita na inachusubiri ni fedha Sh 81,345,723 wakati Azam na Simba zinawania zawadi ya mshindi wa Pili Sh 40,672,861 na Mshindi wa Tatu Sh 29,052,044 huku Prisons na Mtibwa Sugar zikichuana kupata zawadi ya Mshindi wa Nne ambayo ni Sh 23,241,635.
Pia timu zote zinawania zawadi ya Mchezaji Bora ambayo ni Sh 5,742,940 kiwango kinachofanana na atakachopewa Mfungaji Bora wa Ligi na Kipa Bora wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Vodacom wakati Mwamuzi Bora atazawadiwa Sh 8,614,610 kiwango kinachofanana atakachopewa Kocha Bora wakati timu yenye nidhamu itavuna Sh 17,228,820.

Benteke aamua kukomaa kwa Klopp, la sivyo anasepa

http://www.thisisanfield.com/wp-content/uploads/P160320-087-Southampton_Liverpool-562x456.jpgLAZIMA kieleweke. Straika wa kimataifa wa Liverpool, Christian Benteke amesema ni lazima afanye mazungumzo na klabu hiyo kujadili mustakabali wake baada ya kumaliza msimu wake wa kwanza ambao haukuwa mzuri hata kidogo. Benteke amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda klabu kadhaa katika kipindi cha kiangazi ikiwemo West Ham United baada ya kushindwa kung’aa akiwa Anfield akifunga mabao 10 katika mechi 42 za mashindano yote aliyocheza toka anunuliwe kwa kitita cha Pauni Milioni 32.5 kutoka Aston Villa.
Kocha Mkuu wa LIverpool, Jurgen Klopp hakuwa akimpa nafasi kubwa kama aliyokuwa nayo wakati akiichezea Aston Villa, kiasi cha Brendan Rodgers kumsajili kabla ya kutimuliwa baada ya timu kuyumba.
Kukiwa hakuna uwezekano wa kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao baada ya kufungwa mabao 3-1 na Sevilla katika Fainali ya michuano ya Europa League juzi Jumatano, Benteke amesema yeye sambamba na wachezaji wengine wana matumaini ya kuzungumza na Kocha Klopp kuhusu mipango ya msimu ujao. Akihojiwa Benteke amesema anafahamu kuwa bado anatakiwa kuzoea mazingira na kwasababu msimu umemalizika anadhani sasa ni wakati wa kukaa chini ya Klopp na kujaribu kutafuta suluhisho kwa ajili ya msimu ujao.
Liverpool imemaliza msimu huu wa EPL katika nafasi ya nane ikikusanya pointi 60 katika mechi 38, ikiwa ni pungufu ya pointi 21 na zile za mabingwa Leicester City.

Kafunika! Ozil ndiye baba lao kwa Wapiga Mitutu wa Arsenal

https://d.ibtimes.co.uk/en/full/1432414/arsenal-mesut-ozil.jpg
Fundi Ozil akiwajibika uwanjani. Picha:ibtimes
KIUNGO Fundi wa kimataifa wa Ujerumani, Mesut Ozil amechaguliwa na mashabiki kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu yaArsenal kutokana na kiwango cha juu alichoonyesha msimu huu. 
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ameshinda tuzo hiyo akiwafunika Alexis Sanchez aliyeshika nafasi ya pili na Hector Bellerin aliyeshika nafasi ya tatu. 
Ozil amekuwa katika kiwango kizuri akifunga mabao nane na kutengeneza nafasi nyingine 19 msimu huu ambazo zimechagiza kwa kiasi kikubwa Arsenal kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Leicester City. Assist hizo zimemfanya Ozil kumaliza kama kinara katika Ligi Zote Tano za Ulaya na kiwango hicho pia kilimfanya Ozil kuteuliwa katika orodha ya tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA ambayo ilinyakuliwa na Riyad Mahrez wa Leicester.

Eeh! Chelsea yamtamani tena Lukaku

http://static.standard.co.uk/s3fs-public/thumbnails/image/2014/04/12/13/Romelu%20Lukaku.jpg
Lukaku
SIKIA hii. Klabu ya Chelsea inadaiwa kutaka kumrejesha tena mshambuliaji wao wa zamani Romelu Lukaku kutoka Everton.
Chelsea walimuuza Lukaku kwa kitita cha Pauni Milioni 28 kwenda Everton mwaka 2014, baada ya kuitumikia timu hiyo kwa mkopo na tangu wakati huo nyota huyo wa Ubelgiji, amefunga mabao 61 katika mechi 127 alizocheza. 
Chelsea iliyoshindwa kutetea taji lao la Ligi Kuu ya England (EPL) kwa msimu huu baada ya kuzidiwa ujanja na Leicester City, kwa sasa inadaiwa kutaka kumrejesha tena Lukaku, ingawa inadaiwa Everton watataka kulipwa ada ya Pauni Milioni 61 kiasi ambacho kinadaiwa kitaweza kulipwa. 
Chelsea pia inawawinda nyota wa Napoli na kinara wa mabao wa Serie A kwa msimu huu, Gonzalo Higuain na mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.
Mabingwa hao wa zamani walikuwa na msimu mbovu kiasi cha kumtimua aliyekuwa Kocha wao, Jose Mourinho, lakini bado ikamaliza nafasi ya 10.

Suarez bado haamini kama kamfunika Messi

http://worldsoccertalk.com/wp-content/uploads/2015/06/Suarez.jpg
Suarez
http://images.latinpost.com/data/images/full/84962/messi-neymar-suarez.jpg
Suarez, Messi na Neymar Jr wakiwa uwanjani pamoja
STRAIKA nyota wa mabingwa wa Hispania, Barcelona, Luis Suarez amesema hakutegemea kama angeweza kuchukua nafasi ya Lionel Messi ya kuwa kinara wa mashambulizi ya klabu hiyo kwa msimu huu.
Suarez amekuwa akiimarika tangu alipojiunga na Barcelona akitokea Liverpool na amefanikiwa kuibeba timu hiyo kutwaa taji la La Liga mara mbili, huku mwenyewe akimaliza kama mfungaji kinara. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay, amefunga mabao 40 katika mechi 35 za ligi alizocheza msimu huu na kumzidi mshambuliaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo katika tuzo ya Pichichi kwa kufunga hat-trick katika mchezo wao mwisho wa msimu. 
Kwasasa Messi ambaye ni mshindi wa tuzo tano za Ballon d’Or amerudi nyuma na kushambulia akitokea upande wa kushoto ili kumpisha Suarez nafasi ya katikati. 
Akihojiwa na waandishi wa habari, Suarez amesema hakutegemea kucheza nafasi hiyo kwani ndio ilikuwa ikitumiwa na Messi lakini wamekuwa wakielewana vyema ndani na nje ya uwanja.

Serengeti Boys yazidi kukimbiza ughaibuni


https://3.bp.blogspot.com/-12PSnskvyOM/Vv_tgsReZVI/AAAAAAAAMtA/RIXVS17wciIdSGWXMjCGJe0v4urmJyfcA/s640/IMG-20160402-WA0208.jpghttps://pbs.twimg.com/media/CiAFIanWMAAW1Rr.jpg 
NA TARIQ JUNIOR
TIMU ya taifa ya Vijana U17 'Serengeti Boy' imeweka mguu mmoja ndani kutinga fainali ya michuano maalum ya kimataifa ya vijana 'AIFF Youth Cup 2016' baada ya jana kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea Kusini.
Serengeti inayonolewa na Bakar Shime imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo mwa michuano hiyo ikiwa na pointi 5 baada ya kushuka uwanjani mara tatu, huku Korea ikiwafuata nyuma yao ikiwa na pointi nne ikicheza mechi mbili tu.
Timu hiyo ya Tanzania itamaliza mechi zake keshop Jumamosi kwa kuvaana na Malaysia ili kujua hatma yake ya kucheza fainali ambayo itahusisha timu kinara na mshindi wa pili, huku zitakazoshika nafasi ya tatu na nne zitacheza mechi ya kuwania ushindi wa nafasi ya tatu.

YANGA YATUA KIBABE, ILA INA KAZI NGUMU

WAWAKILISHI pekee wa Tanzania na Ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Yanga mchana huu wametua jijini Dar es Salaam kutoka Angola walikoenda kuweka rekodi Afrika kwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Yanga iliikubali kipigo cha bao 1-0 mbele ya wenyeji wao GD Segrada Esperanca ya Angola, lakini hazina ya ushindi wa mabao 2-0 iliyoshinda katika mechi yao ya awali nyumbani jijini Dar es Salaam iliwavusha kwa jumla ya mabao 2-1.

Mashujaa hao wa Tanzania walitua saa 8 mchana na kupokewa na umati mkubwa wa mashabiki, huku Kocha Hans Pluijm akiwapongeza vijana wake kupambana kiume ugenini na hatimaye kupenya.

ILIVYO SASA

Kwa sasa Yanga na mashabiki wao na wadau wachache wa soka ambao uweka mbali ushabiki wao na kuvaa joho la uzalendo, wanashangilia mafanikio hayo ya Yanga kwani ni heshima kwa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla.
Achana na kitita cha fedha ambacho Yanga kitavuna kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi, lakini vijana hao wa Jangwani wamepata nafasi nyingine ya kufukia mashimo yote ya nyuma.
Kama hujui ni kwamba Yanga itapewa kiasi cha dola 150, 000 (zaidi ya Sh. 300 Milioni) kwa kufuzu hatua hiyo, huku ikiipa Shirikisho ya Soka (TFF) dola 15,000 (zaidi ya Sh. 30 Milioni 30).
Lakini dau hilo litapanda zaidi kwa Yanga hadi kufikia adi dola 239,000 (Sh. 500 Milioni) na TFF kuvuna dola 20,000 (zaidi ya 40 Milioni, iwapo itamaliza nafasi ya tatu katika kundi itakalopangwa.
Yanga ikiingia fainali itapata dola 432,000( Sh. 879 Milioni) TFF ikivuna dola 30,000 na kama itatwaa ubingwa basi Yanga itapewa dola 625, 000 zaidi ya Sh. Bilioni 1.2, wakati TFF itapata dola 35, 000 (Sh. Milioni 700).

PEKE YAO
Yanga ndio wawakilishi hao wa pekee wa Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) imeweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza Tanzania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini ikiwekwa mikononi mwa Waarabu.
Yanga imeweka rekodi hiyo ikiwa ni miaka 18 tangu ilipoweka rekodi nyingine ya kuwa klabu ya kwanza ya Tanzania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998 kabla ya watani zao Simba kufuata nyayo zao mwaka 2003.
Hata hivyo ushiriki wake wa hatua kama hiyo katika Ligi ya Mabingwa mwaka 1998 ulikuwa wa aibu, ikizingatiwa Simba ilipotinga hatua kama hiyo miaka mitano baadaye ilitakata na kuifunika Yanga, hata kama haikuvuka kutinga nusu fainali.

LIGI YA MABINGWA
Yanga katika safari yake ya kutinga hatua ya makundi kwa mara ya kwanza mwaka 1998, haikuwa na kibarua kigumu kwani ilianza kuumana na Rayon Sports ya Rwanda katika raundi ya kwanza.
Yanga ilianzia ugenini kwa kulazimisha sare ya mabao 2-2 kabla ya kupata nyingine ya bao 1-1 nyumbani na kutinga raundi ya pili ambapo walipangiwa na Coffee Ethiopia walioing'oa kibabe kwa jumla ya mabao 8-3.
Yanga ililazimishwa sare ya 2-2 ugenini kabla ya kushinda nyumbani kwa mabao 6-1 na hatimaye kutinga kwenye makundi ambapo hata hivyo kocha aliyeisaidia timu hiyo kutinga hapo, Tito Mwaluvanda alifurushwa na timu kupewa Raoul Shungu.

MAKUNDI
Katika makundi, Yanga iliwekwa kundi B na timu za ASEC Mimosas ya Ivory Coast waliokuja kuwa mabingwa, Mining Rangers ya Afrika Kusini na Raja Casablanca ya Morocco.
Ilianza kwa sare ya 1-1 na Maning Rangers kabla ya kwenda kukandikwa mabao 6-0 na Raja kisha kupokea kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Asec na waliporudiana nao Waivory walishinda mabao 3-0 jijini Dar es Salaam.
Yanga iliendelea kutoa takrima kwa wapinzani wake kwa kunyukwa mabao 4-0 huko Afrika Kusini na Mining na kuja kutoka sare ya mabao 3-3 na Raja. Mwishowe Yanga ilimaliza mkiani ikiwa na pointi mbili tu, ikiwa timu iliyofungwa mabao mengi(19) na kufunga machache (5) na kuziacha Asec na Mining zikisonga mbele kwa nusu fainali.

SIMBA YAFUNIKA
Baada ya timu za Tanzania kusota kwa miaka mitano, Simba ilifuata nyayo za Yanga mwaka 2003 kwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa tena kwa kuivua ubingwa, watetezi Zamalek ya Misri kwa mikwaju ya penalti.
Matokeo ya mwisho yalisomeka bao 1-1 kwani kila timu ilishinda mchezo wa nyumbani na Simba wakafanya kweli kwenye mikwaju ya penalti na kutinga makundi.
Tofauti na Yanga, Simba ilionyesha uhai kwelikweli kwa kushinda mechi mbili na kuambulia sare moja na kumaliza nafasi ya tatu ikiziacha timu zilizofuzu kucheza fainali Asec Mimosas na Ismailia ya Misri zikionyeshana ubabe mwishoni.
Simba ilianzia ugenini na kukandikwa mabao 3-0 na Enyimba kabla ya kuja kuituliza Asec jijini Dar kwa bao 1-0 na kuidindia Ismailia kwa sare isiyo na mabao na walipoenda Misri kurudiana na wapinzani hao hao walikubali kipigo cha 2-1.
Waliporudi nyumbani waliikaribisha Enyimba kwa kipigo cha mabao 2-1 na kwenda kupoteza ugenini kwa mabao 4-3 dhidi ya Asec na kujikuta ikimaliza nafasi ya tatu ikiwa ni timu ya pili iliyofungwa mabao machache (10) nyuma ya Ismailia (7).

MIAKA YA MATESO
Tangu Simba na Yanga ziliposhiriki hatua ya makundi Afrika, klabu hizo na wawakilishi wengine wa Tanzania walikuwa kama watalii tu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho hadi mwaka huu Yanga ilipofanya kweli.
Yanga ilianzia michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa kuing'oa Cercle de Joachim ya Mauritius katika raundi ya awali kisha kuiondosha APR ya Rwanda katika raundi ya kwanza na kupangiwa wababe wa Misrim, Al Ahly iliyowatupa nje kwa mabao 3-2.
Ndipo ikakutana uso kwa uso na GDS Esperanca ya Angola na kuwafunga mabao 2-1.
Pamoja na kusaka fedha zinazotolewa kwa klabu zinazocheza hatua ya Nane Bora, bado Yanga inapaswa kupambana kuweza kuweka heshima na kufunika ikiwezekana mafanikio ya watani zao Simba mwaka 2003.
Hakuna ubishi Yanga haina rekodi ya kujivunia katika michuano ya Afrika ukiondoa mara tatu zilizocheza robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika (1969 na 1970) na Kombe la Washindi mwaka 1995.

WAARABU TENA
Yanga imekuwa na gundu dhidi ya timu za Kiarabu na katika klabu nane zilizotinga hatua hiyo ya makundi kabla ya ratiba na makundi mawili kupangwa Jumanne ijayo (mei 24), lazima iwe mikononi mwa klabu hizo za Afrika Kaskazini.
Klabu tano za Waarabu zilizopenya ni MO Béjaïa (Algeria), Al Ahli Tripoli (Libya), FUS Rabat na Kawkab Marrakech (zote za Morocco) na Etoile du Sahel (Tunisia) ambazo zimeungana na Yanga, TP Mazembe ya DR Congo na Medeama ya Ghana.
Ikiwa na kikosi imara chenye kuundwa na wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu kisoka, huku wakiwa na Kocha mjanja, Hans Pluijm na wasaidizi wake, Juma Mwambusi na Juma Pondamali, Yanga inaweza kufanya mambo kama ikiamua.HESABU KALI
Lazima ipigie hesabu mechi zake za nyumbani, ili kujitengenezea mazingira ya kushika nafasi mbili za juu za kutinga nusu fainali na kuogelea kwenye mamilioni ya fedha za CAF, hata wenzao hutumia mechi za nyumbani kujinufaisha nao wasizubae.
Yanga isijiamini kupita kiasi na kuzichukulia poa timu itakazocheza nao kwa sababu ya mafanikio iliyopata kwa hivi karibuni, itambue kuwa kazi ndio kwanza imeanza.
Ni nafasi kwa kina Deus Kaseke, Simon Msuva, Mwinyi Haji, Deo Munishi, Ally Mustafa, Juma Abdul, Paul Nonga, Matheo Simon na wengine wakiwamo wageni kujiuza kupitia michuano hiyo, sambamba na kurejesha heshima ya Yanga kimataifa.

MICHARAZO MITUPU inawatakia kila la heri katika kufanikisha mipango yao ya kujenga heshima Afrika.

DIAMOND KAMA KAWA, KAMA DAWA ANGA LA KIMATAIFA

Diamond

Diamond
http://az616578.vo.msecnd.net/files/2016/03/26/635946329720736579-1505588360_Rihanna-pink-art.jpg
Rihanna naye yupo katika tuzo hizo

NYOTA wa kimataifa wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platinumz, ameendelea kuthibitisha kuwa HASHIKIKI baada ya kuteuliwa kuwania tuzo za BET 2016 zitakazofanyika nchini Marekani.
Diamond amekula shavu hilo akiwa msanii pekee wa Afrika Mashariki na Kati katika kipengele cha Msanii Bora wa Kimataifa kutoka Afrika akichuana na wakali wengine wa bara hilo akiwa AKA wa Afrika Kusini, Wizkid na Yemi Alade wa Nigeria.
Wasanii wengine wanaochuana na Diamond katika tuzo hizo zitakazofanyika Juni 26 katika ukumbi wa Microsoft Theater, mjini Los Angeles Marekani ni pamoja na Black Coffee na Cassper Nyovest wote wa Afrika Kusini,  Mzvee wa Ghana na Serge
Beynaud wa Ivory Coast.

Orodha kamili ya wanaowania tuzo hizo na vipengele vyake ni kama ifuatavyo;

Best International Act Africa

AKA (SOUTH AFRICA)
BLACK COFFEE (SOUTH AFRICA)
CASSPER NYOVEST (SOUTH AFRICA)
DIAMOND PLATNUMZ (TANZANIA)
MZVEE (Ghana)
SERGE BEYNAUD (COTE D’IVOIRE)
WIZKID (NIGERIA)
YEMI ALADE (NIGERIA)


Best Female R&B/Pop Artist
ADELE
ANDRA DAY
BEYONCÉ
K. MICHELLE
RIHANNA

Best Male R&B/Pop Artist
BRYSON TILLER
CHRIS BROWN
JEREMIH
THE WEEKND
TYRESE

Best Group
2 CHAINZ & LIL WAYNE
DRAKE & FUTURE
PUFF DADDY & THE FAMILY
RAE SREMMURD
THE INTERNET

Best Collaboration
BIG SEAN FT. CHRIS BROWN & TY DOLLA $IGN – PLAY NO GAMES
BIG SEAN FT. KANYE WEST & JOHN LEGEND – ONE MAN CAN CHANGE THE WORLD
FUTURE FT. DRAKE – WHERE YA AT
NICKI MINAJ FT. BEYONCÉ – FEELING MYSELF
RIHANNA FT. DRAKE – WORK

Best Male Hip Hop Artist
DRAKE
FETTY WAP
FUTURE
J. COLE
KANYE WEST
KENDRICK LAMAR

Best Female Hip Hop Artist
DEJ LOAF
LIL KIM
MISSY ELLIOTT
NICKI MINAJ
REMY MA

Video of the Year
BEYONCÉ – FORMATION
BRYSON TILLER – DON’T
DRAKE – HOTLINE BLING
KENDRICK LAMAR – ALRIGHT
RIHANNA FT. DRAKE – WORK

Video Director of the Year
BENNY BOOM
CHRIS BROWN
COLIN TILLEY & THE LITTLE HOMIES
DIRECTOR X
HYPE WILLIAMS

Best New Artist
ALESSIA CARA
ANDRA DAY
BRYSON TILLER
KEHLANI
TORY LANEZ

Dr. Bobby Jones Best Gospel/Inspirational Award

ANTHONY BROWN & GROUP THERAPY
ERICA CAMPBELL
KIRK FRANKLIN
LECRAE
TAMELA MANN
TASHA COBBS

Best Actress
GABRIELLE UNION
KERRY WASHINGTON
TARAJI P. HENSON
TRACEE ELLIS ROSS
VIOLA DAVIS

Best Actor
ANTHONY ANDERSON
COURTNEY B. VANCE
IDRIS ELBA
MICHAEL B. JORDAN
O’SHEA JACKSON JR.

YoungStars Award
AMANDLA STENBERG
QUVENZHANÉ WALLIS
SILENTÓ
WILLOW SMITH
YARA SHAHIDI

Best Movie
BEASTS OF NO NATION
CONCUSSION
CREED
DOPE
STRAIGHT OUTTA COMPTON

Sportswoman of the Year
CHEYENNE WOODS
GABRIELLE DOUGLAS
SERENA WILLIAMS
SKYLAR DIGGINS
VENUS WILLIAMS

Sportsman of the Year
CAM NEWTON
KOBE BRYANT
LEBRON JAMES
ODELL BECKHAM JR.
STEPHEN CURRY

Coca-Cola Viewers’ Choice Award
BEYONCÉ – FORMATION
BRYSON TILLER – DON’T
CHRIS BROWN – BACK TO SLEEP
DRAKE – HOTLINE BLING
FUTURE FT. DRAKE – WHERE YA AT
RIHANNA FT. DRAKE – WORK

Centric Award
ANDRA DAY – RISE UP
BEYONCÉ – FORMATION
K. MICHELLE – NOT A LITTLE BIT
RIHANNA – BBHMM
THE INTERNET – UNDER CONTROL


Best International Act UK
KANO
KREPT & KONAN
LIANNE LA HAVAS
SKEPTA
STORMZY
TINIE TEMPAH