STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 17, 2014

MARIA SHILA NDIYE REDDS MISS KINONDONI 2014

Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila (katikati) akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa ndiye mshindi wa taji hilo na kuwaongoza warembo wengine 15 waliokuwa wakiwania taji hilo. 
Wengine mshindi wa pili Camila Cindy John (kulia) na mshindi wa tatu Queenlatifa Hasim. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia jana. (Picha: FK Blog).

Maafa! Jiwe laporomoka na kuua wanne Mwanza

http://radio-tanzania.de/wp-content/uploads/Bismarck-Rock.jpg
WATU wanne wa familia mbili tofauti wa  barabara ya Nyerere ‘A’ katika eneo la Mabatini wilayani  Nyamagana jijini Mwanza, wamefariki baada ya kuporomokewa na  jiwe kubwa lililoviringika kutoka mlimani kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi.
Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi waliofariki ni pamoja na Sayi Otieno na mkewe Quenter Kweko walifariki papo hapo baada ya kukandamizwa na jiwe kubwa lilivunja nyumba waliyokuwa wakiishi eneo hilo, huku mtoto wao mwenye miaka 4 akinusurika kifo.
Baada ya jiwe hilo kuleta madhara katika nyumba hiyo, pia likalisukuma jiwe jingine ambalo liliporomoka na kuipiga nyumba ya Joseph William na kuwaua watoto wake wawili papo hapo waliotajwa Keflin Masalu (14) na Emaueli William (12) anayesoma darasa la tano huku Jophrey Joseph (14) wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mbugani akinusurika.

Polisi na uongozi wa serikali ya Mwanza imewataka wakazi waliojenga kwenye milima ya mawe na kuhatarisha maisha yao kuhama katika maeneo hayo kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha ili kuepuka maafa zaidi.

Stoke City wamnyakua Victor Moses wa Chelsea

http://images.dailystar-uk.co.uk/dynamic/58/photos/178000/620x/6178.jpgWINGA wa Chelsea, Victor Moses amejiunga na Stoke City kwa mkopo wa muda mrefu kocha Jose Mourinho akijaribu kupounguza kikosi chake kuelekea msimu mpya.
Moses anaachana na kocha huyo Mreno na kwenda kujiunga na timu ya Mark Hughes Uwanja wa Britannia.
Mnigeria huyo alicheza kwa mkopo msimu uliopita Liverpool, lakini akawa anasotea namba kwenye kikosi cha kikosi cha Brendan Rodgers.

Tanzania wenyeji wa Wushu, nchi 8 kuja kuchuana




Mkurugenzi wa Mipango na Ufundi wa TWA, Karama Masoud 'Kalapina'
NCHI nane zikiwamo za China, Kenya, Iran na wenyeji Tanzania inatarajiwa kuchuana katika michuano ya kimataifa ya mchezo wa Wushu itakayofanyika kati ya Agosti 30-31 jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wushu Tanzania (TWA), Sempai Golla Kapipi aliliambia MICHARAZO kuwa, michuano hiyo itafanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na Tanzania kuanzia saa 4 asubuhi.
Sempai Kapipi alisema wenyeji Tanzania itawakilishwa na klabu 23 na wachezaji wengine mmoja mmoja dhidi ya wawakilishi wa nchi za Kenya, Uganda, Iran, China, Libya, Nigeria na Zimbabwe.
"Nchi zilizothibitisha mpaka sasa kushiriki michuano hiyo ni majirani zetu wa Kenya na Uganda, Iran, China, Zimbabwe, Nigeria na Libya na wenyeji Tanzania itakayowakilishwa na klabu 23," alisema.
Katibu huyo alifafanua kuwa katika michuano hiyo kutakuwa na mitindo miwili itakayoonyeshwa kupitia mchezo huo maarufu kama Kungfu ya Sanda na Tai-ru itakayohusisha mapigano ya mapanga.
Sempai Kapipi alisema kuwa wapo katika mipango ya kuwaalika wanamichezo wa judo, karate na ngumi ili kuonyesha manjonjo yao.
Hii ni mara ya pili kwa chama hicho kuandaa michuano mikubwa ya mchezo huo baada ya awali kuandaa michuano ya taifa iliyohusisha klabu pekee za Tanzania iliyofanyika Ufukwe wa Coco mwaka 2011.
Naye Mkurugenzi wa mashindano wa chama hicho, Karama Masoud 'Karapina' alisema maandalizi yanaendelea vyema na wawakilishi wa nje ya nchi na klabu za mikoa mbalimbali wataanza kuwasili wiki ijayo.
"Kila kitu kimekaa vema na tutaanza kupokea wageni ndani ya wiki ijayo, hadi siku ya kuanza kwa michuano tunaamini wawakilishi wote watakuwa wameshawasili jijini Dar es Salaam," alisema Kalipina.

Arsenal yaanza vyema England, Spurs yatusua ugenini




ARSENAL imeianza vyema Ligi Kuu ya England baada ya kuitandika Crystal Palace ilitimtimua kocha wake, Tony Pulis kwa mabao 2-1.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa mwisho kwa pazia la ufunguzi la ligi hiyo usiku wa jana ilishuhudiwa wageni wakitangulia kupata bao kupitia Hangeland dakika 35, kabla ya Koscienly kusawazisha dakika 45. Kipindi cha pili Arsenal walitengeneza nafasi nyingi lakini wakashindwa kuzitumia vizuri na mpaka dakika 90 bado ilikuwa 1-1, dakika 5 za nyongeza Aaron Ramsey akaifungia Gunners goli la ushindi.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Tottenham Hotspur ikiwa ugenini imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya West Ham licha ya kiucheza pungufu kwa muda mrefu baada ya beki wake mmoja kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29.
Bao pekee liliwekwa kimiani na Eric Dier katika dakika za ziada katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Boleyn Ground.

Stoke City ikiwa nyumbani kwake nayo ilijikuta ikilala kwa Aston Villa kwa kufungwa 1-0, bao likiwekwa kimiani na Andreas Weimann dakika ya 50.
Leicester City ilikaribishwa tena kwenye Ligi Kuu kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton, huku QPR ikilala nyumbani bao 1-0 dhidi ya Hull City, bao hilo likiwekwa kimiani na James Chester katika dakika ya 52.

Van Gaal aanza kwa kichapo nyumbani EPL


KOCHA mpya wa Manchester United , Mholanzi, Louis van Gaal amekaribishwa na kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Swansea City ndani ya dimba la Old Trafford.
Hii ni mara ya kwanza kwa Man United kupoteza mechi ya ufunguzi wa msimu katika uwanja wake wa Old Trafford.
Swansea City walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 28 kupitia kwa Ki Sung-yueng.
Mshambuliaji na nahodha wa Man United, Wayne Mark Rooney aliisawazishia timu yake bao hilo katika dakika ya 53 baada ya kupiga tikitaka mpira wa kona uliochongwa na Juan Mata.
Gylfi Sigurdsson ndiye aliibuka shujaa wa kuifungia bao la ushindi Swansea katika dakika ya 72 na kukalia usukani wa ligi kuu kwa saa kadhaa.
Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo pointi za muhimu alizozungumza Van Gaal ni:
-Sio kwamba safu ya ulinzi ndio inatakiwa kuboreshwa bali ni timu nzima.
-Amesema hatapaniki kwasababu ya Man United kupoteza.
-Atawapa nafasi zaidi wachezaji kumpatia ushindi.
Kikosi cha Manchester United: De Gea, Jones, Smalling, Blackett, Lingard (Januzaj), Fletcher, Herrera, Young, Mata, Rooney (c), Hernandez (Nani)
Wachezaji wa akiba: Amos, James, M Keane, Fellaini, Kagawa
Kikosi cha Swansea: Fabiański; Rangel, Williams, Amat, Taylor, Ki, Shelvey, Dyer, Sigurðsson, Routledge, Bony (Gomis)
Wachezaji wa akiba: Tremmel, Bartley, Richards, Tiendalli, Montero, Sheehan.

Azam watangulia Robo Fainali Kagame


MABINGWA wa soka nchini Azam wamefanikiwa kutinga hatua ya Robo fainali ya michuano ya Kagame baada ya kuibamiza Adama ya Ethiopia kwa mabao 4-1 katika mechi iliyocheza mjini Kigali, Rwanda.
Mechi hiyo iliyokuwa ya kukamilisha ratiba kwa Azam katika hatua ya makundi lilichezwa kwenye uwanja wa Nyamirambo na  maboa ya washindi yaliwekwa kimiani na nahodha, John Bocco 'Adebayor', Mcha Khamis 'Vialli', Didier Kavumbagu na Kipre Tchetche.
Ushindi huo umeifanya Azam kuongoza kundi lake kwa kuwa na pointi 8 baada ya sare mbili na ushindi wa mechi mbili na sasa itashuka dimbani Jumatano kuumana na El Merreikh ya Sudan.
Azam waliingia kwenye michuano hiyo kama zali baada ya waliokuwa wawakilishi wa Tanzania, Yanga kuenguliwa kwa kitendo cha kutaka kupelekea kikosi cha pili katika michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za klabu kwa timu za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Hii ni mara ya pili kwa Azma kuicheza michuano hiyo, mwaka 2012 iliishiriki wakati Tanzania ikiwa wenyeji na ilifanikiwa kufika fainali na kufungwa mabao 2-0 na Yanga iliyokuwa imetwaa kwa mara ya pili mfululizo.