STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, August 3, 2013

Hamis Kiiza mshambuliaji wa 7 Jangwani

MSAHAMBULIAJI WA YANGA HAMIS KIIZA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI KUENDELEA KUKIPIGA YANGA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Hamis Kiiza hatimaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani na kufanya idadi ya washambuliaji katika kikosi hicho cha Jangwani kufikia saba mpaka sasa. 
Kiiza alisaini mkataba huo katika hoteli ya Protea, Dar es Salaam na kufanya idadi ya wachezaji wa kimataifa kufikia wanne akiwamo Haruna Niyonzima wa Rwanda, Mbuyu Twitte wa DR Congo na Didier Kavumbagu kutoka Burundi.

Kusainishwa kwa Mganda huo kumemaliza sintofahamu ya muda mrefu juu ya mustakabali wa mchezaji huyo aliyeibeba Yanga tangu alipotua klabuni hapo na kufanya safu ya mbele ya jangwani iwe na wafumania nyavu saba.
 
Wakali wengine ni Jerryson Tegete, Kavumbagu, Hussein Javu, Said Bahanuzi Shaban Kondo (aliyesajiliwa toka Msumbiji) na Realintus Lusajo (kutoka Machava- Moshi).

Barcelona waitafuna Santos ya Neymar 8-0

Headlines News :



Masupastaa: Lionel Messi na Neymar wakifurahi kabla ya mechi
ndiyo mwanzo wa mataji?

BARCELONA imeiangushia kipigo kizito cha 8-0 Santos ya Brazil kwenye uwanja wa Nou Camp na kutwaa taji la Joan Gamper katika mwendelezo wa mechi za maandalizi ya msimu mpya.

Neymar aliyesajiliwa kwa pauni 48 alianzia benchi dhidi ya timu yake ya zamani sambamba na mchezaji anayewaniwa na Manchester United Cesc Fabregas ingawa kiungo huyo wa zamani wa Arsenal alifunga mabao mawili katika kipindi cha pili.

Alexis Sanchez, Pedro na Lionel Messi kila mmoja alifunga bao moja katika kipindi cha kwanza, wakati bao la kujifunga mwenyewe la Leo na magoli mengine kutoka kwa Adriano, Jean Marie na mawili ya Fabregas yalihitimisha karamu hiyo ya magoli.

Supastaa wa samba Neymar ambaye alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye jezi ya Barcelona katika mchezo wa sare ya 2-2 huko Poland, alionekana akitaniana na mchezaji bora wa dunia Messi kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza mbele ya mashabiki wa Barcelona kwenye uwanja wa Nou Camp.

Messi alikuwa wa kwanza kufunga katika dakika ya 8 na muda mfupi baadae krosi ya nguvu ya Dani Alves ikamlazimisha beki Leo kujifunga.

Uchawi wa Messi ukahamia kwenye kusaidia kufunga mabao baada kumtengenezea winga wa Chile, Sanchez aliyekwamisha wavuni bao la tatu kabla ya Pedro kumalizia pasi ya Jordi Alba na kuhesabu goli la nne.

Kuingia kwa Neymar kulipokewa kwa shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki waliojazana Nou Camp ingawa mtu mmoja aliyevalia nguo zenye nembo ya timu pinzani ya Santos, Internacional alivamia uwanja huku akimfuata Neymar kabla hajazuiliwa na kuondolewa uwanjani.

CREDIT: SAIDI MDOE, SALUTI 5
                      Vurugu: Neymar akiokolewa dhidi ya shabili mwenye hasira

 Maelekezo: Kocha mpya Tata Martino (kulia) akimpa maelekezo Neyma
Magoli yake ya mwisho? Fabregas alitokea benchi na kufunga mabao mawili
 
Credit:Salute5

NMB yatoa msaada wa mashuka Hospitali ChakeChake Pemba


 Meneja wa Tawi la Benki ya NMB Chake Chake, Pemba, Hamidu Mughamba, (kulia) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa, Mhe. Hanuna Ibrahim, sehemu ya mashuka yaliyotolewa na Benki hiyo kama msaaada kwa hospitali za Wilaya ya Chake Chake.
 
NMB imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia mahitaji mbalimbali yanayoizunguka jamii.Kwa kutambua hilo hivi karibuni  maofisa wa NMB tawi la Chake chake walitoa mashuka ya hospitali yenye thamani ya shilingi million tano kwenye hospitali mbali mbali ikiwamo hospitali ya wilaya ya Wete, Chakechake, Mkoani na Micheweni. Mashuka haya  yatasaidia kupunguza hitaji kubwa la mashuka lililokua likizikumba hospitali hizi.

 Maofisa wa Benki ya NMB pamoja na Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Chake Chake, Pemba, wakiyatizama baadhi ya mashuka  yaliyokabidhiwa na Benki ya NMB.
Maofisa wa Benki ya NMB pamoja na Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Chake Chake, Pemba, wakiyatizama baadhi ya mashuka  yaliyokabidhiwa na Benki ya NMB.

CHADEMA YALAANI POLISI KUMDHALILISHA MWANDISHI CHANNEL 10

  https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEik9fmVEvTrvMxg4Kro3HAJDvaFvMsjDK6g3-Y9yKXaH8nGcFmuichIzChQ0dwIaLC6e5QLxYYfA4OT2b8OCVz-tlb0WfPCGooGPnPM4n7MJupnlQ-1DtdyE2JxlbPCmgw4FolZQBJrKCc/s1600/528890_103622173103898_656595116_n.jpg

CHADEMA, kupitia Kurugenzi ya Habari na Uenezi, inatoa kauli ya awali, kulaani kitendo cha kupigwa, kuchaniwa nguo, kujeruhiwa, kunyang'anywa vifaa na kufungwa pingu kwa mwanahabari wa Channel ten, Eliah Ruzika, kilichofanywa na askari wa Jeshi la Polisi eneo la Tazara, Dar es Salaam, wakati mwandishi huyo akitimiza majukumu yake kwenye mkutano wa wafanyakazi wa Tazara.

Huu ni mwendelezo wa unyanyasaji wa raia wasiokuwa na hatia, huku wengine wakiwa katika majukumu ya kazi zao, unaofanywa na Jeshi la Polisi.

Ni mwendelezo wa askari wa jeshi hilo kunyanyasa na kuingilia wanahabari katika utekelezaji wa majukumu yao, vitendo ambavyo vimekuwa vikifanyika kwa muda mrefu sasa, hata kusababisha mauaji, bila wahusika kuchukua au kuchukuliwa hatua za kisheria, kuzuia na kukomesha kabisa udhalimu huu.

Bila shaka pia ni utekelezaji wa kauli mbovu kabisa na inayokiuka vigezo vyote vya uongozi bora, siasa safi, misingi ya demokrasia na haki za binadamu, iliyotolewa bungeni hivi karibuni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. 

Kauli iliyoruhusu kuvunjwa kwa haki na hivyo kusababisha uvunjifu wa amani kama inavyotokea sasa. 

Kuminya au kujaribu kuminya utendaji kazi wa vyombo vya habari na wanahabari, ni hatua ya juu sana kuelekea kuminya haki na uhuru wa kufikiri na kutoa maoni, kwa mtu mmoja mmoja, kundi au makundi ya watu katika jamii. 

Kuminya uhuru na haki ya habari na kutoa maoni, huku ukitegemea polisi kutawala (kwa kuigeuza nchi police state) ni moja ya dalili za mwisho mwisho ya watawala waliochoka, wanaotakiwa kupisha madarakani.

Kurugenzi ya Habari CHADEMA

Kazimoto asaini mwaka Al Markhiya

Mwinyi Kazimoto
ALIYEKUWA kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto jana amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kwa ajili kuitumikia klabu ya Al Markhiya SC ya Doha, Qatar.
Habari za uhakika kutoka Qatar zinaeleza kwamba, Kazimoto amesaini mkataba baada ya kufaulu majaribio yake, sambamba na kukubaliana na uongozi ofa aliyopewa.
Imeelezwa kwamba, hatua ya Kazimoto kusaini mkataba huo imekuja baada ya uongozi wa timu hiyo kuongeza dau la kumnunua baada ya awali kugomea kwa madai kuwa halilingani na thamani waliyomnunulia.
Chanzo hicho kimeeleza kwamba, Al Markhiya iliwaangukia Simba kwa dau waliloafikiana kutokana na ukweli kwamba kwa sasa ipo katika hali mbaya ya kifedha na hasa ikizingatiwa kuwa wanahitaji kusajili wachezaji watakaoipandisdha tena daraja.
“Unajua timu imeshuka daraja hivi karibuni sasa wanajiimarisha kwa kusajili wachezaji wazuri na fedha waliyonayo haitoshelezi hivyo wameiomba Simba ipokee hicho walichonacho,”kilieleza chanzo hicho.
Juzi uongozi wa Simba kupitia kwa msemaji wake Ezekiel Kamwaga ulisema umeitupilia mbali ofa iliyotumwa na klabu hiyo kwa madai kuwa ni ya kipuuzi, huku ikidai pia Kazimoto ana maswali kwanza ya kujibu kwa Watanzania na mashabiki wa Simba kwa ujumla.
Simba pia ilidai inakusudia kuketi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kumjadili nyota huyo kwa kitendo chake cha kutoroka nchini.

Kazimoto ambaye alisajiliwa na Simba mwaka juzi kutokea JKT Ruvu, alitoroka nchini akiwa na timu timu ya Taifa iliyokuwa ikijiandaa na mechi yake ya kufuzu fainali za Afrika zinazoshirikisha nyota wanaocheza ligi za ndani (CHAN) dhidi ya Uganda ‘The Cranes’.
 
Sports Lady

Mtanzania mwingine anaswa na 'Unga'' Zimbabwe


WIMBI la kukamatwa kwa watanzania nje ya nchi wakiwa na dawa za kulevya likiendelea kuzua mjadala nchini, Mwanamke mwingine wa Kitanzania anadaiwa kunaswa Zimbabwe akiwa na 'unga' unaokadiriwa kuwa na thamani yaDola za 45,000 akitokea India.
Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Jacklyne Mollel (34) anayeishi Afrika Kusini, inadaiwa alinaswa kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Harare Julai 27 akiwa na dawa hizo zenye uzito wa kilo 15 alipowasili na ndege ya Emirates akitokea India.
Taarifa zaidi zinasema mtanzania huyo ameshafikishwa mahakamani akikabiliwa na kesi hiyo ya kuingiza dawa hizo aina ya Ephedrine zikiwa na uzito wa Kilo 15 na kusomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Donald Ndirowei juzi jijini humo.

ISOME TAARIFA NZIMA ILIYORIPOTIWA NCHINI HUMO JUU YA MKASA HUO

A 34–year–old Tanzanian woman was last week arrested at the Harare International Airport after she was found in possession of an illicit drug with a street value of $45 000 upon arrival from India.
SENIOR REPORTER
Mollel Jackline Richard, who stays in South Africa, was not asked to plead when she appeared before Harare magistrate Donald Ndirowei yesterday.
She was remanded in custody to July 27.
Richard was allegedly found in possession of 15kg of ephedrine which stimulates the heart and nervous system. It is often found in herbal and diet pills.
The State alleged that Richard arrived at Harare International Airport aboard an Emirates flight from India.
The alleged drug pusher produced her passport at the immigration desk at the airport where an alert officer tipped CID Drugs detectives that Richard had a visa for India which is a known source for illicit drugs.
The court heard that Richard was taken for interviewing and during a search conducted on her by detectives they recovered 30 khaki envelopes containing a whitish substance which was wrapped with fabric sheets inside a maroon bag.
Tests were conducted on the substance and revealed that it was ephedrine. The drug was then taken for recording and weighing.