AMOUR MZUNGU AMTISHIA NYAU MARWA
Zungu (kushoto) wakati akipima ubavu na Kiza Kinene (kulia)
BONDIA machachari mwenye makazi yake kisiwani Unguja Amour Said”Zungu”  amejitapa kumpiga vibaya na kumstaafisha ngumi bondia mkongwe aliyewahi kuchukua medali na mataji kadhaa katika ngumi za ridhaa na kuwa bingwa katika ngumi zakulipwa Joseph Marwa katika  pambano litakalofanyika katika ukumbi wa  CCM Mwinjuma-mwananyamala April  7.
Zungu alisema kuwa kwa namna alivyojiandaa atamnyuka Marwa maarufu kama Smart Man'.
"Marwa umri umekwenda, japo alikuwa mwalimu wangu, lakini lazima nimnyuke," alisema.
Mabolndia hao watapigana katika pambano la raundi nane na watasindikizwa na mabondia wanaokuja vema katika mchezo huo nchini kwa sasa kama Issa Omar na Shaaban Madilu watakaocheza raundi kumi za ubingwa wa taifa wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO),Ambao upo wazi kugombaniwa na mabondia hao.