STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, January 27, 2014

Huzuni! Muigizaji huyu wa Futuhi afariki dunia




HABARI zilizotufikia zinasema muigizaji, Mzee Dude amefariki dunia leo jioni baada ya jana kupatwa ghafla na maradhi na kukimbizwa hospitalini.

Man City vs Chelsea, Arsenal vs Liverpool FA Cup



DROO ya Raundi ya 5 ya FA CUP imefanyika leo ambapo bahati imezikutanisha vigogo vilivyopo kwenye Top 5 ya Ligi ya England, ambapo Manchester City itaavana na Chelsea na Arsenal itakutana na  Liverpool.
Mechi zingine zitakazohusisha timu za Ligi Kuu ya England ni kati ya Sunderland v Southampton na Everton v Swansea.
Mechi hizi zitachezwa wikiendi ya Februari 15 na 16 na Washindi kutinga Robo Fainali.
Droo hiyo ilifanyika huko Wembley Stadium Jijini London na kuendeshwa na Andros Townsend, Mchezaji Chipukizi wa Tottenham, pamoja na Baba yake Mzazi, Troy, ambae ni Mwanaharakati maarufu kwenye Soka.
RATIBA KAMILI:
Manchester City v Chelsea
Sheffield United AU Fulham v Nottingham Forest AUr Preston NE
Arsenal v Liverpool
Brighton v Hull
Cardiff City v Wigan
Sheffield Wednesday v Charlton
Sunderland v Southampton
Everton v Swansea

Simba, Yanga zaingiza Mil 139

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjIcondyKwoFCu6HZwULhEbB0KogLLWJzzr8fQ-G3EXLUiql5BUq8DuVwMHQTPxQBQs-fIgqEWxFG11jAd3BpggLzNc3a1e1Uj25TLwKl4zksNZE5EuSQTATHsdycqlpMe4-v2tMSksPTb0/s1600/DSC_0616.JPG
Na Boniface Wambura
MECHI za Ligi Kuu ya Vodacom zilizohusisha timu za Simba na Yanga na kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi zimeingiza jumla ya sh. 139,850,000.
Yanga iliyoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ashanti United pambano lake liliingiza sh. 86,035,000 kutokana na watazamaji 14,261. Mechi ya Simba ambayo ilishinda bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers kutoka Tabora iliingiza sh. 53,815,00 kwa watazamaji 9,629.
Mgawanyo kwa mechi ya Yanga ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 13,123,983.05, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu ilipata sh. 20,650,211.50.
Uwanja sh. 10,500,107.54, gharama za mechi sh. 6,300,064.53, Bodi ya Ligi sh. 6,300,064.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,150,032.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,450,025.09.
Mechi ya Simba mgawo ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 8,209,067.80, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu ilipata sh. 12,595,211.50.
Uwanja sh. 6,404,344.83, gharama za mechi sh. 3,842,606.90, Bodi ya Ligi sh. 3,842,606.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,921,303.45 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,494,347.13.
Vilevile tiketi zinapatikana kupitia maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo katika maeneo mbalimbali nchini. Watakaonunua kupitia maduka hayo watapata tiketi na kwenda moja kwa moja uwanjani.
Wakati huo huo: Mauzo ya tiketi za elektroniki kwa mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa keshokutwa (Januari 27 mwaka huu) tayari yameanza, hivyo wanatakiwa kununua mapema.
Mechi hizo ni kati ya Coastal Union na Yanga itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na ile ya Azam dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Kwa washabiki wa Dar es Salaam watakaokwenda Tanga kushuhudia mechi kati ya Coastal Union na Yanga wanashauriwa kuanza safari wakiwa na tiketi zao mikononi, hasa kwa wale watakaonunua kupitia maduka ya Fahari Huduma.
Tiketi pia zinaweza kununuliwa kupitia mtandao wa M-Pesa kwa kupiga namba *150*03*02#. Kwa wanaotumia CRDB simbanking wanaingia kawaida kwa *150*03.
Vilevile tunawakumbusha washabiki kuwa kwa viwanja ambavyo tayari vina mfumo wa tiketi za elektroniki hakuna tiketi zitakazouzwa uwanjani, hivyo wanaokwenda kwenye mechi wanatakiwa kuwa na tiketi zao mikononi.