STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, March 13, 2013

Silaha 23 za Kim Poulsen kwa Morocco hizi hapa

Kipa wa Mtibwa Husseni Sharrif 'Casillas' akiwajibika uwanjani
Na Boniface Wambura

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia kambini Jumamosi  jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco, akimjumuisha kipa wa Mtibwa Hussei Sharrif 'Casillas'.

Mechi hiyo ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

SEMINA ELEKEZI COPA COCA COLA KUFANYIKA MACHI 19


Na Boniface Wambura

SEMINA elekezi kwa ajili ya michuano ya Copa Coca-Cola 2013 itafanyika Machi 19 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Washiriki wa semina hiyo wanatakiwa kuripoti Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) siku moja kabla (Machi 18 mwaka huu).

Washiriki hao ni makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia waratibu wa mikoa wa mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).

Barua za mwaliko kwa ajili ya semina hiyo tayari zimetumwa kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa.

FIFA yaionya Tanzania kuingiza siasa TFF

Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Velcke
BERNE, (Reuters)
TANZANIA has been warned by soccer's governing body FIFA over alleged government interference in the country's football federation.

"We can confirm that FIFA secretary general Jerome Valcke has sent a letter to the president of the Tanzanian Football Federation, Leodegar Tenga, concerning alleged governmental interference in the internal affairs of the TFF," said FIFA in a statement sent to Reuters.

"FIFA is in contact with the TFF president who is optimistic that the matter can be sorted out between TFF, FIFA and the Tanzanian authorities.

"Furthermore, we can confirm that FIFA is also planning to send a mission to assess the situation with regard to the electoral process as soon as the current matter of alleged interference has been clarified."

Tanzanian media said that the government has declared the TFF's new statutes illegal and told it to use the old ones for upcoming elections.

FIFA statutes state that its member associations must remain independent of their respective national governments and routinely suspends those who break the rules.

Suspension for Tanzania would mean that they would be excluded from the World Cup qualifiers and their clubs would be kicked out of African competitions.

Tanzania, who have never qualified for the World Cup, are second in African qualifying Group C with three points from two games, one behind leaders Ivory Coast.

BARCELONA YAFANYA MAANGAMIZI ULAYA

 

'Mchawi Mweupe' Lionel Messi akishangilia moja ya mabao yake mawili usiku wa jana.

NI Maangamizi! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya vinara wa Ligi Kuu ya Hispania, Barcelona usiku wa kuamkia leo kuifumua bila huruma AC Milan ya Italia na kutinga robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya bila kutarajiwa.
Mabao mawili ya 'Mchawi Mweupe' Lionel Messi na mengi ya David Villa na Jordi Alba, imeifanya Barca kutinga hatua hiyo kwa kuitupa nje AC Milan kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya mechi ya awali kuchezea kipigo cha mabao 2-0 ugenini.
Messi aliendelea kuimarisha rekodi yake ya mabao katika michuano ya msimu huu kwa kufunga bao la kwanza dakika ya tano akimalizia kazi nzuri ya Xavi, kabla ya kuiongeza jingine dakika tano kabla ya mapumziko kwa shuti kali kwa pasi murua ya Iniesta na kuifanya Barca iende mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili, AC Milan wakiingia wakitafuta mbinu za kuweza kudhibiti mashambulizi ya wenyeji wao, lakini wakajikuta wakitungulia bao la tatu kupitia kwa Villa aliyemegewa pande tamu na Xavi na kufunga dakika ya 55.
Bao lililoikata maini AC Milan ambayo kupitia nyota wake Robinho, Kevin Prince Boateng, Sule Muntari walijaribu kufurukuta bila mafanikio, lilitumbukizwa kimiani na Alba dakika za nyongeza pambano hilo na kuifanya Barca kuweka historia kwa timu iliyonyukwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza kusonga mbele katika michuano hiyo ya Ulaya.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa usiku wa jana, wenyeji Schalke 04 walijikuta wakinyukwa nyumbani na wageni wao Galatasaray kwa mabao 3-2 na kung'oka kwenye michuano hiyo.

Kikosi cha Galatasaray kilichokuwa na Didier Drogba kilishtukizwa kwa kufungwa bao la dakika ya 18 kupitia Roman Neustadter kabla ya Hamit Altintop kusawazisha katika dakika ya 37 na Burak Yilmaz kuiongezea wageni bao la pili katika dakika ya 42.
Michael Bastos aliipatia Schalke bao la kusawazisha katika kipindi cha pili kwenye dakika ya 63 na wengi kuamini mechi hiyo ingeisha kwa sare hivyo ambapo jumla ya matokeo yalikuwa yakisomeka 3-3 kutokana na sare ya baoa 1-1 waliyopata timu hizo katika mechi ya ya kwanza, Galatasaray walipata bao la tatu.
Bao hilo lililwekwa kiminia kwenye dakika za nyongeza za pambano hilo kupitia kwa Umut Bulut na kuivusha timu yake hadi robo fainali ya michuano hiyo mkubwa kwa ngazi za klabu barani Ulaya.