STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 29, 2012

Ubalozi wa UAE watoa mkono wa Idd kwa nyama ya mbuzi wa Sh Mil 40

UBALOZI wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania,  kupitia asasi yake ya Red Crescent imetumia kiasi cha Dola za Kimarekani 27,000 ambazo ni zaidi ya Sh Milioni 40 kwa ajili ya kununua Mbuzi waliochinjwa na kugaiwa waumini wa Kiislam wa mikoa minne kama 'mkono wa Idd'.
Nyama hiyo ya mbuzi iligaiwa kwa waumini wa misikiti ya wilaya zote za Dar es Salaam ambapo mkoa huo pekee walichinjwa mbuzi 250, wilaya nyingine ni Same-Kilimanjaro, Mafia-Pwani na Lushoto -Tanga.
Akizungumza kwa niaba ya Balozi wa UAE nchini Tanzania, Mallalla Mubarak Al Ameir na msaidizi wake, Mohammed Obaid Salem AlZaabi, baada ya ugawaji wa jijini Dar, Mhasibu wa ubalozi huo, Abdallah Ahmedina, alisema mgao huo ni sehemu ya taratibu za ubalozi wao kila wakati wa sikukuu za Idd.
Mhasibu huyo, alisema ni kawaida kwa ubalozi wao kila mwaka kutoa sadaka hiyo kwa waumini wa kiislam kwa nia ya kuwafariji na kuifurahia sikukuu hiyo iliyosherehekewa mwishoni mwa wiki duniani kote.
Aliongeza kwa kuwaomba waislam na wtu wengine wenye uwezo kujenga utamaduni wa kuwasaidia wasiojiweza kila mara hili kusaidia kujenga upendo na furaha baina yao.
"Ni jambo zuri kama asasi na watu wengine wenye uwezo kufanya mazoea ya kuwakumbuka watu wa kipato cha duni kwa kuwasaidia kwa hali na mali kwani hujenga upendo na furaha kwao na familia zao," alisema.
Alisema mbali na ugawaji wa nyama, pia ubalozi wao umekuwa ukiwalisha futari waumini kipindi cha mwezi wa Ramadhani pamoja na kuwapa zakatul fitri kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid el Fitr ya kila mwaka.

Mwisho

SHIKAMOO PESA NEW HIT CLUB BANGER RELEASED-KINGKAPITA FT.TASHMY NAME IS ERICK artist name KINGKAPITA before was known as RICHBOI from Tanzania dar es salaam,HIPHOP artist wit HIT banger HERE WE GO wen with WAKACHA - JUx,gigga FLO,NAS 3 ,ACHAAAaa with ma boy NAS 3 and MTOTO MLITO by nas 3 as ma crew members.

Hii sasa ni new hit club banger SHIKAMOO PESA niliomshirikisha TASH mzee wa CHAPIA mulemule kuoka arachuga,NYimbo imerekodiwa katika STUDIO za ROCCANA BASEMENT chini ya producer jimmy jizze na mastering kumaliziwa HOME TOWN record chini ya master Traveller
naomba support yenu sana wadau!!

ASANTENI MUNGU BARIKI KAZI YA MIKONO YANGU,MUNGU BARIKI MUSIK WA TANZANIA
HULKSHARE LINK:: 

Shabani Kilumbelumbe kuzichapa na Mnamibia

Bondia chipukizi Mtanzania, Shabani Kilumbelumbe Novemba 13, anatarajiwa kupanda ulingoni jijini Windhoek-Namibia kuzipiga na Emmanuel Naidjala 'The Prince' wa Namibia katika pambano la raundi 12 kugombea ubingwa wa WBO-AFRICA .
Pambano hilo ni la uzito wa bantam-kgs 53.5 na litafanyika katika ukumbi wa Windhoek Country Club Resort.

Promota wa pambano hili ni Nestory Thobias wa Nestory Sunshine Boxing ya Namibia.

TPBO tayari imeshapata barua ya mwaliko kutoka Chama cha Ngumi na Mieleka cha Namibia na mktaba wa bondia pia umeletwa kwa TPBOkupitia wakala wa pambano hili  Julius Odhiambo wa Kenya .

Tayari Meneja wa Kilumbelumbe Mwalimu Hatibu ameshapewa taarifa kuhusu bondia wake kukabiliwa na pambano hili chini namibia.

TPBO imemtaka meneja huyo kumuandaa bondia hiyo kwa ajili ya pambano hilo ili aweze kuipeperusha vema bendera ya taifa.