STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 20, 2014

DU NOMA KWELI! KASISI AFARIKI KWA 'HAWARA' KENYA

 
KASISI mmoja mashuhuri wa kanisa moja nchini Kenya alizimia na kufariki dunia katika hali ya kutatanisha akiwa ndani ya nyumba ya mwanamke ambaye sie mke wake.
Tukio hili lilishuhudiwa katika mtaa wa Buruburu mjini Nairobi Kenya.
Mwili wa kasisi huyo kwa jina Geoffrey Maingi wa kanisa la Redeemed Gospel church mjini Nairobi, ulipatikana ndani ya chumba cha mwanamke huyo,baada ya kufarikini kutokana na sababu ambazo hazijulikani mnamo siku ya Jumanne. Polisi walisema kuwa kasisi Maingi mwenye umri wa miaka 70, aliingia katika nyumba ya muumini mmoja wa kanisa lake kwa kile ambacho muumini huyo mwanamke alisema ilikuwa maombi maalum wakati alipofariki.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 ambaye alitalakiana na mumewe mwaka jana kutokana na ugomvi wa kinyumbani, aliambia polisi kuwa Maingi alikuwa amemtembelea kwa maombi kabla ya kuzirai na kufariki.
Kadhalika alisema kuwa kasisi huyo amekuwa akija nyumbani kwake kwa maombi,kwani mbali na kuwa kiongozi wake wa kanisa pia ni rafiki yake wa karibu.
Alihojiwa na kuachiliwa ingawa uchunguzi ungali unaendelea.
Kifo cha mzee huyo kilivutia hisia kutoka kwa majirani waliokuwa wanadai kuwa kasisi huyo alifariki kutokana na kutumia tembe za kuongeza nguvu mwili.
BBC

ALLY CHOKI AWAPA VIDONGE WAPINZANI WAKE

* Awaambia washindane jukwaani siyo maneno ya mitaani
* Asema Extra Bongo wapo kikazi zaidi kuliko 'kutafutana'
Ally Choki (kushoto) akizungumza na wanahabari, huku Juma Kasesa Msemaji wa bendi akiwa makini kumsikiliza
Jenerali Banzastone (kushoto) akifafanua jambo huku dansa kiongozi wa Extra Bongo akisikiliza kwa makini wakati wa mkutano wa wana Extra Bongo na wanahabari, kwenye ukumbi wa Heikein Mbagala Kuu.
Wanahabari wakiwa makini katika mkutano huo wa leo
Madansa wa kiume wa Extra Bongo wakionyesha manjonjo yao kwa wanahabari

Ally Choki mwenye mic, akiwachezesha madansa wa kike katika mkutano wa wanahabari juu ya kambi ya maandalizi ya uzinduzi wao utakaofanyika Jumamosi pale Dar Live

MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo 'Wana Kimbembe', Ally Choki 'Mzee wa Farasi' a.k.a Kamarade amewashukia wapinzani wake kimuziki kwa kuwaambia yeye hataki kushindana kwa maneno ya mitaani bali anataka wapimane ubavu jukwaani kupitia kazi zao za muziki.
Choki alitoa kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na wanahabari kwa kudai kuwa kumekuwa na mashambulizi ya maneno toka kwa wapinzani wake kimuziki na kuiandama bendi yao, lakini alisema yeye hana muda wa kuwajibu kwa sababu yeye kazi ya ni muziki.
Mtunzi na muimbaji huyo aliyewahi kutamba na bendi kadhaa zikiwamo Extra Kimwa, The Bantu Group, TOT-Plus, African Stars 'Twanga Pepeta' na Mchinga Generation 'Timbatimba', alisema washindani wake nawataka wakutane kwenye jukwaa la muziki na siyo blabla naa maneno yasiyo na tija.
"Wapo wanaotuandama na kutushambulia kwa maneno na kuiandama bendi yetu ila sisi hatuna muda wa kujibishana nao, sisi tunataka tushindane na kupimana jukwaani siyo maneno ya mitaani," alisema Choki.
Aliongeza kuwa kutokana na kwamba yeye huwa habahatishi katika zinduzi za bendi au albamu mashabiki watarajie makubwa siku ya Jumamosi ambapo Extra Bongo watazindua albamu ya 'Mtenda Akitendewa'.
"Mashabiki waje waone mtumishi wao nitawafanyia nini, ila tumejipanga kuwapa burudani ya uhakika ambayo hawajawahi kuipata kwa siku za karibuni, kwani kutakuwa na manjonjo mengi kama kawaida yangu ila siwezi kuwaambia nitaingiaje ukumbini siku hiyo, ila kuna bonge la Surprise nimeandaa," alisema Choki.
Extra Bongo watazindua albamu hiyo ambayo ni ya pili kwa bendi yao baada ya awali kutamba na 'Mjini Mipango', kwenye ukumbi wa Dar Live a.k.a Uwanja wa Taifa wa Burudani ambapo mashabiki watapata audio na video siku hiyo ya uzinduzi ili kukata kiu yao ya burudani.

Tenga amteua Mganda kuwa Makamu wake wa Rais CECAFA

Barua ya uteuzi wa Mulindwa kuwa Makamu wa Rais wa CECAFA

Linah, Amin, Muumin, Mashujaa kuwasindikiza Extra Bongo

* Watazindua albamu yao ya Mtenda Akitendewa
* Choki kubatizwa jina gani Dar Live?
* Super Nyamwela, Banza waapa kufanya kufuru Jumamosi

Ally Choki (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya uzinduzi wa albamu yao siku ya Jumamosi. Wengine pichani toka kushoto ni Banzastone, Super Nyamwela na msemaji wa bendi ya Extra Bongo, Juma Kasesa

Choki akifafanua jambo kwa waandishi
Super Nyamwela akitoa tambo zake

Sisi ndiyo sisi wengine kama mafisi tu!

Oyaa msiniangushe! Super Nyamwela akiwaelekeza madansa wake kabla ya kuwaonyesha wanahabari jinsi ya kucheza Kimbembe

Mduduuu mduduuuu!

Hii siyo ya kukosa Dar Live Jumamosi

Asha Sharapova (kushoto nyumba) akionyesha kuzoea mazingira ya Extra Bongo

Unatikisa namna hiii...yaaani hiviii! Wanenguaji wa Extra Bongo wakionyesha manjonjo yao

Munachezaga namuna hii bana!

Watatukomaje Jumamosi Dar Live?

Nyamwela akiwaongoza wenzake kuonyesha Kimbembe kwa wanahabarti mapema leo

Yebaaaaa Kimbembe Kimbembe!

Hapo chachaaa!
WASANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Linah na Amin kutoka THT pamoja na muimbaji nyota wa muziki wa dansi Prince Muwinjuma Muumin ni baadhi ya watakaowasindikiza wanamuziki wa bendi ya  Extra Bongo 'Wana Kimbembe' katika uzinduzi wa albamu yao ya ya pili iitwayo 'Mtenda Akitendwa' utakaofanyika siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alisema uzinduzi juo unaotarajiwa kunogeshwa na utambulisho wa wasanii wapya wawili walionyakuliwa na bendi hiyo toka African Stars 'Twanga Pepeta', mnenguaji Asha Sharapova na rapa na muimbaji Greyson Semsekwa utafanyika kwenye ukumbi wa Dar Live-Mbagala nje kidogo ya jiji utasindikizwa na wasanii kadhaa nyota.
Choki alisema ukiondoa nyota hao wa THT, wengine watakaowasindikiza katika onyesho hilo linalotarajiwa kuibua jina jipya la Choki baada ya yale ya 'Mzee wa Farasi' au 'Mzee wa Tingatinga' kudumu kwa muda mrefu ni pamoja na pamoja na Malkia wa Mipasho nchini Hal hanisa Khadija Omar Kopa, Prince Mwinjuma Muumin, bendi ya Mashujaa na kundi la Makhirikhiri la Tanzania.
"Kambi ya maandalizi ya onyesho letu la uzinduzi wa albamu yetu ya pili ya 'Mtenda Akitendewa' inaendelea vyema na kwa taarifa tu kila kitu kimekaa vyema kwa onyesho hilo la Jumamosi ambalo tutasindikizwa na wasanii mbalimbali kama akina Linah, Amin, Khadija Kopa, Mwinjuma Muumin na Makhirikhiri wa Tanzania," alisema Choki.
Aliongeza kuwa siku ya uzinduzi huo tutawatambulisha wasanii wao wapya pamoja na kutambulisha mtindo mpya wa bendi hiyo wa 'Kimbembe'.
Awali Extra Bongo ilikuwa ikitamba na mtindo wa Kizigo na mwaka huu mpya wameingia na staili mpya ya 'Kimbembe' ambao ulitambulihswa kwa wanahabari katika shoo fupi ya kuonyesha maandalizi ya bendi hiyo yanavyozidi kunoga chini ya udhamini wa Global Publishers.
Mkurugenzi huyo ambaye ni mtunzi na muimbaji wa bendi hiyo alisema siku ya uzinduzi wataachia kwa pamoja audio na video ya albamu hiyo ya pili ya bendi hiyo baada ya ile ya 'Mjini Mipango', na kuonheza kuwa, audio itakuwa na nyimbo saba ikiwemo bonasi ya shoo ya sebene na video itakuwa na nyimbo sita tu.
Alizitaja nyimbo hizo za albamu hiyo ni 'Mtenda Akitendewa', iliyobeba jina 'Mama Shuu', 'Neema', 'Falsafa', 'Fisadi wa Mapenzi' na 'Bakutuka'.
Naye mwealimu na kiongozi wa safu ya uenguaji ya bendi hiyo, Mussa Hassan 'Super Nyamwela' alisema kuwa inafahamika wazi kuwa kwa Tanzania hakuna shoo kali na matata kama ya Extra Bongo hivyo asingependa kusema maneno mengi zaidi ya kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kupata burudani Dar Live ambapo alisema watafanya 'kufuru' kwa namna walivyopania kuendelea kufika nchini.
"Hili halina ubishi sisi ndiyp funika bovu nchini katika safu za uenguaji hivyo wapenzi wetu waje wapata kile ambacho hawajawahiu kukishuhudia kwani tumewaandalia mambo mapya kabisa," alisema Nyamwela.
Ramadhani Masanja 'Banzastone' kwa upande wake alisema Extra Bongo wanajua kazi zao na wanajua kitu gani mashabiki na wapenzi wa muziki wanataka na hivyo kusema Jumamosi itakuwa haitoshi kwa namna watakavyofunika mbaya.
"Waje wapate uhondo kwani tumejipanga mbaya, Extra Bongo hawana mpinzani na tumepania kuendelea kukimbiza mwanzo mwisho," alisema Banza.

Ruvu Stars waja Dar kurekodi nyimbo zao mpya

Rogert Hegga
BENDI mpya wa muziki wa dansi ya Ruvu Stars, inatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kurekodi nyimbo zao tatu mpya.
Mmoja wa viongozi na muimbaji wa bendi hiyo yenye maskani yake Mlandizi, Pwani Rogert Hegga 'Catapillar', alisema wataingia studio kuanzia leo kwa ajili ya kurekodi nyimbo hizo za kuwatambulisha.
Hegga alizitaja nyimbo kuwa ni pamoja na 'Network Love' utunzi wa  Mhina Panduka 'Baba Danny' a.k.a Toto Tundu, 'Jua Kali' wa Kuziwa Kalala na 'Spirit' ambao ni utunzi wake (Hegga).
"Tunatarajia kutua jiji kesho  kwa ajili ya kuja kuingia studio kurekodi nyimbo zetu tatu mpya ambazo ndizo zitakazotutambulisha kwa mashabiki," alisema Hegga.
Mtunzi na muimbaji huyo wa zamani wa bendi kadhaa maarufu nchini ikiwamo ya African Stars, Mchinga Sound, G8 Wana Timbatimba na Extra Bongo, alisema mashabiki wasubiri kupata uhondo kwao baada ya kumalizika kwa kazi hiyo yua kurekodi.
"Mashabiki wajiandae tu kupata burudani, nyimbo hizi zitaleta mapinduzi makubwa katika muziki wa dansi kwani zimeenda shule na studio tunayorekodia itazidisha manjonjo zaidi," alisema.
Alipoulizwa jina la studio hiyo, Hegga alisema wasingependa kuweka hadharani kwa sasa mpaka wakimaliza kurekodi.