STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 16, 2013

Kijogoo: Mwanasoka aliyehamishia makali yake katika uigizaji

Kijogoo katika pozi tofauti
KUVUTIWA kwake na msanii Mohammed Mwikongi 'Frank' kulimfanya Boniface Gilliard 'Kijogoo' au 'Kikoti' kusahau soka, mchezo aliokuwa akiupenda na kuucheza utotoni.
Muigizaji huyo wa kundi la Jakaya Arts linalotamba na michezo yake kupitia kituo cha runinga cha ITV, anasema alikuwa 'kichaa wa soka' akishiriki michezo ya Shule za Msingi na Sekondari na kucheza Ligi Daraja la Nne katika timu ya Burudani kabla ya Frank aliyekuwa Kaole Sanaa kumhamisha na kuwa muigizaji.
"Kipaji cha uigizaji ni cha kuzaliwa nacho, ila Frank ndiye aliyenifanya nibadili  mawazo yangu katika sanaa, ninashukuru ndoto nilizokuwa nazo tangu nijitose kwenye fani hiyo zimeanza kuonekana japo sijaridhika," anasema Kijogoo.
Msanii huyo anasema enzi akicheza soka alimudu nafasi za ushambuliaji kuanza namba 7, 8, 9 na 10 na baadhi ya rafiki zake wanashangaa kukuona kwenye sanaa kwa umahiri aliokuwa nao katika mchezo huo, japo anaendelea ila siyo kama zamani.
Kijogoo anasema aliingia jumla katika uigizaji mwaka 2010 kupitia kundi la Jakaya Arts, igizo lake la kwanza likiwa ni 'Riziki' kabla ya kufuatiwa na 'Barafu la Moto', 'Mapito', 'Donda la Kichwa', 'Ulimbo' na igizo lililoisha hivi karibuni la 'Chekecheo anaoutaja kama mchezo bomba kwake.

Mbali na tamthilia, Kijogoo ambaye ni kocha wa timu ya soka ya kikundi hicho cha Jakaya, anaigiza pia filamu baadhi ya kazi alizocheza ni 'Mahaba Niue', 'Like Father Like Son', 'XXL', 'Best Player' na nyingine.
"Kwa kweli nashukuru sanaa imesaidia kunitambulisha mbele ya jamii, naingiza kipato kinachonisaidia kuendesha maisha yangu pia na mengine ambayo sikutegemea," anasema na kuongeza;
"Hata hivyo sijaridhika hadi nije kutamba kimataifa na kumiliki kampuni yangu binafsi ya kuzalisha filamu na kuwasaidia chipukizi, ambao wamekuwa wakipuuzwa pale wanapohitaji msaada," anasema.


UHASIBU
Kijogoo shabiki mkubwa wa Yanga na Arsenal akiwazimia nyota wa timu hizo, Haruna Niyonzima na Mesut Ozil, mbali na usanii na uanasoka kitaaluma ni Mhasibu aliyesomea fani hiyo Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mkali huyo anayependa kula pilau na kunywa vinywaji mchanganyiko, anasema anafurahi kuhitimu masomo yake hayo akitarajia kutunikiwa shahada yake hivi karibuni na kudai ametimiza ndoto zake za utotoni za kuwa mhasibu.
"Nilikuwa na ndoto za kuja kuwa Mhasibu na ninashukuru ndoto hizo zimetimia baada ya kuhitimu masomo yangu na ninamshukuru kaka yangu Rabson Gilliard aliyenisomesha na kunikazania masomo kwani wazazi wetu wote walishafariki na yeye kubeba jukumu la kutusaidia wadogo zake," anasema.
Msanii huyo anakiri hakuna tukio linalomtoa machozi mpaka leo kama hilo la kuwapoteza wazazi wake wote japo kwa nyakati tofauti kutokana na ukweli wazazi ni kila kitu na nguzo ya maisha ya binadamu yeyote, japo anamshukuru Mungu kwani ni yeye aliyeumba na ni yeye anayetwaa.
Kijogoo anayemzimia kwa sasa Jacob Stephen kwa umahiri wake wa kuigiza nchini, anasema sanaa ya Tanzania imepiga hatua kubwa lakini imekuwa haina manufaa kwa wasanii kutokana na vikwazo mbalimbali ikiwemo wizi na unyonyaji.
Pia anasema fani hiyo ni ngumu tofauti na wengi wanavyoichukulia na hasa msanii anapokuwa mchanga kwa kushindwa kupewa sapoti kwa waliomtangulia.
Kuhusu skendo zinazofanywa na wasanii wachache, Kijogoo anasema hiyo inatokana na ushamba na ujinga walionao baadhi yao kwa kudhani kujihusisha na skendo kutawasaidia kupata umaarufu wa haraka ilihali wanajiharibia mbele ya jamii na kusababisha sanaa nzima kuonekana kama ya wahuni, kitu ambacho sicho.
"Mimi nawaona ni kama wajinga kwa sababu mtu mwenye akili zake hawezi kukubali kila siku kuandikwa kwa mambo ya upuuzi, umaarufu unakuja kwa mtu kuchapa kazi kwa ufanisi, hivyo wasanii wajitambue wao ni kioo cha jamii na kubadilika kwani wanajiharibia pengine tunakosa hata matangazo kwa matendo maovu yanayofanywa na wachache wetu," anasema.

ALIPOTOKA
Boniface Gilliard alizaliwa Machi 16, 1985 jijini Dar es Salaam akiwa ni mtoto wa nane kati ya 9 wa famili yao na alisoma Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani kabla ya kujiunga na masomo ya Sekondari katika Shule ya Kambangwa  jijini Dar es Salaam na kumalizia Ifunda-Iringa kabla ya kujiunga Chuo cha IFM.
Msanii huyo anayechizishwa na nguo za rangi ya maziwa (cream), anasema wakati akisoma alishiriki kwenye sanaa na michezo akiigiza, kuimba na kucheza soka akishiriki michuano ya UMISHUMTA na ile ya UMISSETA huku akicheza pia Ligi Daraja la Nne wilayani Kinondoni.
Alikuja kuachana na soka alipotua Jakaya Arts na kuhamishia akili zake katika sanaa akishiriki michezo na filamu mbalimbali.
Kijogoo anayefurahishwa na tukio la kuzaliwa kwa mwanae wa pekee aliyenaye sasa Nabri anaiomba serikali iwasaidie wasanii kuondokana na wizi wanaofanyiwa katika jasho lao pamoja na kuwathamini kama inavyowathamini wanapokuwa wakiwatumia katika shughuli zao ikiwamo kampeni na uhamasishaji wa mambo mbalimbali.

"Wasanii unajua tumegeuzwa kama karai la kujengea, hatuthamini mpaka nyumba inapohitaji kukarabatiwa, tuthaminike na kusaidiwa vipindi vyote na siyo wakati wa shughuli maalum tu za kiserikali au kisiasa," anasema.
Msanii huyo anayemshukuru kaka yake na ndugu zake kwa ujumla, kundi zima la Jakaya Arts na rafiki zake wote ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakimpa sapoti.
Kijogoo anasema anapenda kutumia muda wake wa ziada kuangalia soka, muvi na kubadilishana mawazo na watu wengine sambamba na kufanya mazoezi.

Hizi ndizo nasaha za Jonas Mkude kwa viongozi, makocha

Jonas Mkude

KIUNGO chipukizi wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amewataka viongozi wa soka na makocha kuthamini na kuwajali wachezaji ili wacheze kwa ufanisi uwanjani na kupata matokeo mazuri.
Mkude, ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, aliiambia MICHARAZO katika mahojiano maalum kuwa wachezaji vijana hukatishwa tamaa na baadhi ya mambo yanayofanywa na viongozi wao na makocha mara niyngine.
"Ili soka liweze kusonga mbele, ni lazima viongozi na makocha wabadilike na kuwajali na kuwathamini wachezaji na kuwasaidia pale wanapoonekana kukosea kuliko kuwakatisha tamaa," alisema Mkude bila kufafanua.
Aidha Mkude alisema upo ulazima wa kuwekeza katika soka la vijana kwa ajili ya kutafuta mafanikio kimataifa.
"Soka la vijana ndiyo ukombozi wa kandanda la Tanzania," alisema Mkude na kueleza zaidi kuwa "hata mataifa ya nje yamefika yalipo kwa kuwekeza katika soka la vijana kitu ambacho nasi tunapaswa kuiga kufikia mafanikio ya kweli," alisema.
Mkude aliyesajiliwa na Simba mwaka 2010 akitokea Mwanza United alisema anaamini Tanzania itaacha kuwa msindikizaji katika anga ya kimataifa kama nguvu kubwa zitawekwa kwa vijana na kupewa maandalizi mazuri.

Elias Maguli achekelea kuingia Stars na 'mguu' mzuri

https://fbcdn-sphotos-d-a.akamaihd.net/hphotos-ak-frc3/1461574_230784413749326_1852912229_n.jpg
MSHAMBULIAJI nyota wa Ruvu Shooting aliyeitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu B ya taifa, Elias Maguli, amesema anamshukuru Mungu kwa kuanza na mguu mzuri baada ya kufunga bao lililoizamisha Taifa Stars zilipoumana katikati ya wiki katika mechi ya kujipima nguvu.
Maguli ndiye mfungaji namba mbili kwa kupachika mabao mengi kwenye ligi kuu ya Bara iliyofika nusu msimu baada ya kupachika mabao tisa, moja nyuma ya Amisi Tambwe wa Simba na timu ya taifa ya Burundi.
Maguli alifunga bao hilo kwenye uwanja wa Karume kwa kumalizia pasi ya yosso wa Mtibwa Sugar, Juma Luizio ambao wote wamejumuishwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 32 wa Taifa Stars inayojiandaa kucheza Kombe la Chalenji.
Mchezaji huyo alisema anamshukuru Mungu kwa kumuongoza katika kila anachofanya na amefurahi kuingia na mguu mzuri Stars.
"Namshukuru Mungu kwa kila jambo (pamoja) na bahati hii niliyoingia nayo katika timu ya taifa ninayochezea kwa mara ya kwanza," alisema Maguli.
Maguli alisema atajibidiisha zaidi ili aendelee kudumu katika timu hiyo.
Stars iliyoanza kambi rasmi ya maandalizi ya Chalenji katikati ya wiki, itacheza pambano la kirafiki dhidi ya Harambee Stars ya Kenya Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa.
Baada ya pambano hilo wachezaji kutoka Zanzibar wataondoka katika timu hiyo kwenda kuungana na wenzao wa Zanzibar Heroes na waliobaki wataunda Kilimanjaro Stars itakayocheza Kombe la Chalenji kuanzia mwishoni mwa mwezi huu nchini Kenya.


Cheki Dogo la Sir Juma Nature videoni

Bonyeza hapa kupata uhondo http://youtu.be/aGkgTM11ePg 

Mwili wa Dk Mvungi kuagwa leo Karimjee pichani mwili huo ulipowasilia usiku wa jana toka Afrika Kusini

 
JENEZA LA MWILI WA MAREHEMU DK SENGONDO MVUNGI MARA BAADA YA KUWASILI  KWENYE  UWANJA WA NDEGE WA MWL NYERERE JANA SAA 1:15
VIONGOZI WA SERIKALI WALIOFIKA KUPOKEA MWILI WA MAREHEMU MVUNGI
VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA NDUGU WA MAREHEMU DK MVUNGI WAKIUOMBEA
BAADHI YA VIONGOZI WA NCCR WALIOFIKA KUPOKEA MWILI WA MAREHEMU DK MVUNGI
VIJANA WA NCCR WAKIBEBA MWILI WA MAREHEMU DK MVUNGI MARA BAADA YA KUWASILI JANA
VIJANA WA NCCR WAKIBEBA MWILI WA MAREHEMU DK MVUNGI MARA BAADA YA KUWASILI JANA UKIINGIZWA KWENYE GARI 
MWILI WA MAREHEMU DK MVUNGI ULIWASILI JANA UKITOKEA AFRIKA YA KUSINI BAADA YA KUPELEKWA KWA AJILI YA KUTIBIWA BAADA YA KUPIGWA MAPANGA NA MAJAMBAZI LEO JUMAMOSI MWILI WAKE UTAPELEKWA KATIKA VIWAJA VYA KARIMJEE KUANZIA SAA 3 ASUBUHI  KWA AJILI YA KUAGWA NA KUSOMEWA  MISA ITAKAYOSOMWA PAPO HAPO. VIONGOZI NA WANANCHI WOTE WATAUAGA MWILI WA MAREHEMU NA BAADAE MWILI HUO UTAPELEKWA NYUMBANI KWAKE NA KESHO JUMAPILI UTASAFIRISHWA KUPELEKWA KIJIJINI KWAKE  KISANGARA JUU, WILAYANI MWANGA KWA AJILI YA KUZIKWA

Kaseba, Segu wapigwa kwa KO Australia

 http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2012/06/Kaseba.jpg
BINGWA wa taifa wa ngumi za kulipwa nchini, Japhet Kaseba usiku wa kuamkia leo amekumbana na kipigo cha KO ya raundi ya pili toka kwa mwenyeji wake, Jeremy van Diemen katika pambano la kimataifa la uzito wa Light Heavy lililochezwa nchini Australia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa, Mtanzania hatua huyo hakuweza kuhimili makali ya mpinzani wake na kukubali kipigo cha KO ya raundi ya pili tu ya mchezo huo uliokuwa uwe wa raundi sita uliochezwa kwenye ukumbi wa Metro City.
Inaelezwa Kaseba anayefahamika kama Champion, alionyesha upinzani katika raundi ya kwanza tu, kabla ya kushindwa kuhimili ngumi nzito za mpinzani wake ambaye katika mapambano saba aliyocheza sasa ameshinda matano manne kati ya hayo ni ya KO).
Kabla ya Kaseba kudundwa, bondia mtanzania mwingine,m Jonas Segu naye alikumbana na kipigo kama hicho cha KO baada ya kunyukwa na Luke Sharp katika pambano la utangulizi uzito wa kati.
Segu alishindwa kuendelea na pambano katika raundi ya 5 raundi moja kabla ya kuhitimisha pambano hilo na kuendeleza unyonge wa mabondia wa Tanzania wanapoenda kucheza nje ya nchi kwa kupigwa kila mara.
Mabondia hao wawili wanatarajiwa kurejea nchini kesho kinyonge.

Kilimanjaro Stars yapangwa mchekea Chalenji Cup 2013BARAZA la Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) linatarajia kutangaza ratiba rasmi ya michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika nchini Kenya. tayari makundi ya michuano hiyo yametangazwa.
Tanzania Bara inayowakilishwa na Kilimanjaro Stars yenyewe imepangiwa kundi mchekea la B pamoja na timu za Zambia ambao ni waalikwa, Burundi na Somalia.
Wawakilishi wengine wa Tanzania, Zanzibar Heroes ya Zanzibar yenyewe imepangwa kundi A na wenyeji Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini, wakati kundi la kifo ni kile la C lenye timu za Uganda ambao ni mabingwa watetezi , Rwanda, Sudan na Eritrea.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kuanzia Novemba 27 jijini Nairobi kuwania taji hilo ambalo kwa miaka mingi limetawaliwa na Waganda.
MAKUNDI YALIVYO CHALENJI 2013:
KUNDI A- Kenya, Ethiopia, Zanzibar, South Sudan

KUNDI B- Tanzania, Zambia, Burundi and Somalia

KUNDI C- Uganda, Rwanda, Sudan and Eritrea.

Canal Top wa Akudo Impact adaiwa kunaswa na 'unga' China

http://4.bp.blogspot.com/_PnI9d8LAaQQ/Sii7NjLnEMI/AAAAAAAADzM/_iCaASaqwXU/s400/DSC02167+%5B800x600%5D.JPG
Canal Top (wa kwanza kulia) alipokuwa akiwajibika Akudo

RAPA mahiri aliyewahi kutamba na bendi ya Akudo Impact, Canal Top amenaswa nchini kwa tuhuma za kukutwa na Dawa za Kulevya.
Inaelezwa kuwa rapa huyo alinaswa nchini hivi karibuni baada ya kuingiza dawa hizo nchini humo.
Hata hivyo taarifa rasmi zinaendelea kufuatiliwa kujua undani wa tukio hilo kama ni kweli mwanamuziki huyo kutoka DR Congo amenaswa kweli na Unga au kwa mambo mengine, japo mashushushu waliopo nchini humo wamedai ni 'sembe' zilizomkamatisha.
Bongoclan

Ureno yaichinja Sweden, Ugiriki yanusa Brazil, Ufaransa Mmh!

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/71150000/jpg/_71150286_71150285.jpg
Ronaldo akipongezwa baada ya kuifungia Ureno baoa pekee jana dhidi ya Sweden
Clash of the titans: Portugal's Cristiano Ronaldo (left) and Sweden's Zlatan Ibrahimovic shake hands before kick off
Ronaldo na Ibrahimovic walipokuwa wakilisimiana kabla ya pambano, wote ni manahodha wa nchi zao
CRISTIANO Ronaldo amethibitisha yeye ni bora kuliko Zlatan Ibrahimovic baada ya usiku wa jana kuiongoza Ureno kupata ushindi kiduchu nyumbani kwao dhidi ya Sweden katika pambano la mkondo wa kwanza wa mtoano wa kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia kwa timu za Ulaya.
Pambano la pambano la timu hizo mbili, lakini pia kulikuwa na maneno ya chini chini kuwapambanisha wakali hao wawili na Ronaldo alionyesha anaweza kumzima Ibrahimovic anayecheza PSG kwa kufunga bao pekee lililoipa ushindi Ureno, japo bado nchi hiyo haina uhakika wa kwenda Brazil mwakani.
Bao hiulo la Ronaldo alilifunga kwa kichwa dakika ya 82 kuunganisha krosi ya Miguel Veloso na kuifanya Ureno kusubiri matokeo ya mechi ya mkondo wa pili itakayochezwa mapema wiki ijayo ugenini dhidi ya wenyeji wao Sweden ambao wana rekodi nzuri kwenye dimba lao la nyumbani.
Katika mechi nyingine za 'kapu' Ukraine iliizima Ufaransa kwa mabao 2-0 na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele, huku Ugiriki ikiwa nyumbani ikaifyatua Romania mabao 3-1, huku Iclenad na Croatia zikitoshana nguvu kwa kwenda suluhu ya bila kufungana.
Mechi za mkondo wa pili zitakazoamua hatma ya wawakilishi wa mwisho wa Bara Ulaya zitachezwa siku ya Jumanne.