STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 9, 2013

WATU WAMETOKA MBALI, RAIS MPYA WA KENYA ALIPOKUWA 'KINDA'

RAIS Mpya wa Kenya, Uhuru Kenya aliyeapishwa leo nchini humo, huenda akiiona picha hii itamkumbusha mbali. Hapa ni alipokuwa mdogo akiwa ameshikwa mkono na baba yake Jomo Kenyatta wakati huo akiwa rais wa taifa hilo.Nyuma ya Kenya mwenye suti nyeusi ni aliyekuja kuwa Rais wa Pili wa Kenya, Daniel Arap Moi. Jamani watu tunatoka mbali nyie acheni!

Yanga, kocha Toto waadhibiwa na TFF kwa 'ukora'

Kikosi cha Yanga
Kocha wa Toto, Athuman Bilal 'Bilo'

Na Boniface Wambura
KLABU ya Yanga na Kocha Msaidizi wa timu ya Toto Africans, Athuman Bilali wamepigwa faini ya sh. 500,000 kila mmoja kutokana na makosa mbalimbali katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea nchini.

Adhabu hizo zimetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Jumapili (Aprili 7 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za waamuzi na makamishna kwa michezo namba 108 hadi 171.

Yanga imepigwa faini hiyo baada ya kupata kadi tano za njano katika mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Februari 7 mwaka huu. Vilevile Kagera Sugar imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) dhidi ya African Lyon iliyochezwa mjini Bukoba, Februari 23 mwaka huu.

Naye Kocha Bilali amepigwa faini hiyo na kufungiwa mechi tatu za ligi hiyo kwa kumshambulia kwa maneno kocha wa timu pinzani, hali iliyosababisha mwamuzi amtoe kwenye benchi la wachezaji. Alifanya tukio hilo kwenye mechi kati ya Toto Africans na Tanzania Prisons iliyochezwa Aprili 3 mwaka huu jijini Mwanza.

African Lyon na Simba zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa kushindwa kuchezesha timu zao za U20 kwenye mechi za utangulizi wakati zilipocheza na Oljoro JKT na Coastal Union, Machi mwaka huu kwenye viwanja vya Azam Complex na Uwanja wa Taifa.

Suala la Meneja wa Coastal Union, Akida Manchai kumshambulia kwa maneno yasiyo ya kiungwana Makamu Mwenyekiti wake Steven Mnguto baada ya kwenye mechi kati ya African Lyon na Coastal Union iliyochezwa Machi 30 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex limepelekwa Kamati ya Nidhamu kwa ajili ya hatua za kinidhamu.

Adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom.

Kivumbi cha Ligi Kuu kutimka tena kesho


Na Boniface Wambura
TIMU ya Polisi Morogoro inapambana na Ruvu Shooting katika moja kati ya mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa kesho (Aprili 10 mwaka huu). Matokeo ya mechi hiyo yanatarajia kutoa mwanga kama Polisi inaweza kubaki kwenye ligi hiyo msimu ujao.

Timu hiyo itakuwa nyumbani Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro katika mechi hiyo itakayochezeshwa na Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga akisaidiwa na Godfrey Kihwili na Ephrony Ndissa wa Arusha.

Polisi Morogoro inayonolewa na Adolf Rishard inakamata nafasi ya mwisho ikiwa na pointi 18 tu na imebakiza mechi tatu dhidi ya Simba, Kagera Sugar na Coastal Union.

Mechi nyingine za kesho ni kati ya Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 20 dhidi ya Mgambo Shooting. Mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mgambo ina pointi 24 na iko katika nafasi ya tisa.

Mwamuzi Said Ndege wa Dar es Salaam atachezesha mechi kati ya wenyeji Mtibwa Sugar na Toto Africans itakayofanyika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro. Toto Africans ya Kocha John Tegete ina pointi 21 ikiwa nafasi ya 11 wakati Mtibwa Sugar iko nafasi ya tano na pointi zake 32.

Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Aprili 11 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Azam na African Lyon itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex.

TFF yazipongeza zilizopanda daraja



Na Boniface Wambura
KAMATI ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezipongeza timu za Ashanti United ya Dar es Salaam, Mbeya City ya Mbeya na Rhino Rangers ya Tabora kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao (2013/20114).

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wallace Karia amezitaka timu hizo kufanya maandalizi ya kutosha ili ziweze kushindana katika VPL ikiwemo kutimiza masharti ya kuwa klabu za Ligi Kuu.

Moja ya masharti ya klabu zenye hadhi ya Ligi Kuu ni kuwa na timu ya pili (U20) ambayo itakuwa na inacheza mechi za utangulizi kwenye uwanja wa nyumbani kila timu ya wakubwa inapocheza.

Mbali ya kuthibitisha timu hizo tatu kupanda daraja, pia Kamati ya Ligi imethibitisha rasmi timu tatu zilizoshuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa katika mkoa husika. Timu zilizoshuka kutoka Daraja la Kwanza (FDL) ni Small Kids ya Rukwa kutoka kundi A.

Kundi B timu iliyoshuka ni Moro United ya Dar es Salaam wakati Morani FC ya Manyara yenyewe imeporomoka kutoka kundi C.


NI VITA NYINGINE ULAYA, DROGBA ANA KIBARUA KIZITO, DORTMUND KUVUNA NINI NYUMBANI?

Ronaldo wa Real Madrid

Didier Drogba wa Galatarasay
ISTANBUL, Uturuki
DIDIER Drogba na wachezaji wenzake wa Galatasaray wana mtihani mgumu leo wakati watakapojaribu kupindua matokeo ya kipigo cha 3-0 dhidi ya Real Madrid katika mechi yao ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Drogba, ambaye alishinda taji hilo msimu uliopita akiwa na Chelsea, ataingia akiwa na kumbukumbu nzuri ya kiwango cha juu alichoonyesha katika mechi yao ya ligi Jumamosi dhidi ya Mersin Idman Yurdu ambapo alifunga magoli mawili ya kipindi cha pili katika ushindi wa 3-1.
Hata hivyo, furaha ya ushindi huo wa Galatasaray iliingia doa wakati kocha Fatih Terim alipocharukia maamuzi ya refa yaliyosababisha yeye na wasaidizi wake wawili kutolewa kwa kadi nyekundu, na hivyo kutia wingu maandalizi ya mechi yao ya marudiano mjini Istanbul leo.
Mjini Madrid wiki iliyopita, Galatasaray walifundishwa "somo zuri" na klabu hiyo ya  Hispania, kwa mujibu wa Drogba.
"Sisi hatupo katika matawi yao lakini nadhani ni tatizo la ukosefu wa uzoefu zaidi kuliko jambo jingine lolote," Drogba aliiambia beIN Sport. "Tunajifunza, sisi ni timu changa. Kuna mambo tunayohitaji kuyaboresha.
"Ni somo zuri, na tunapaswa kuonyesha kwamba tumejifunza vyema katika mechi ya marudiano. Tulitaka kuwabana Madrid lakini  tungeweza kufanya jambo hilo kwa njia tofauti, kwa umakini zaidi na ungangari zaidi. Tungeweza kuwasababishia matatizo mengi kwa sababu tulipata nafasi lakini hivyo ndivyo ilivyo," alisema.
Pigo mojawapo kubwa kwa Galatasaray ni kukosekana kwa mshambuliaji muhimu Burak Yilmaz, ambaye ambaye amefungiwa kutokana na kupewa kadi ya pili ya njano mjini Madrid.
Vyombo vya habari vya Uturuki viliripoti Ijumaa kwamba klabu hiyo ya Istanbul iliwasilisha rufaa kwa UEFA ili kadi hiyo itenguliwe.
Galatasaray pia watamkosa beki wao wa kati Dany Nounkeu baada ya kuonyeshwa kadi ya njano ya pili mjini Madrid.

GOLI LA RONALDO
Real walitoa kipigo kikali cha 5-1 nyumbani dhidi ya timu ya katikati ya msimamo ya Levante Jumamosi wakati kocha Jose Mourinho alipowaanzishia benchi nyota wengi, akiwamo mshambuliaji Cristiano Ronaldo.
Ronaldo aliiangia akitokea benchi wakati wa mapumziko huku Real ikiongoza 2-1 na akafunga goli lake la 29 katika La Liga msimu huu kabla ya kumpikia jingine mtokea benchi mwenzake Mesut Ozil.
Beki wa kati Sergio Ramos na kiungo Xabi Alonso wote walicheza kwa dakika 90 kwa kuwa wamefungiwa mechi ya leo wakitumikia adhabu ya kadi.
"Itakuwa hivyo kwa sababu hivi sasa tuko katika kiwango chetu cha juu zaidi kwa msimu huu," Ronaldo, kinara wa mabao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu akiwa na magoli tisa, aliwaambia waandishi wa habari. "Tuna kikosi kilichokamilika ambapo wachezaji wote ni wazima na hilo ni habari njema."
Kuhusu mechi ya leo mjini Istanbul, alisema: "Ni mechi ngumu na kusonga mbele kwetu kwenye raundi nyingine bado hakujawa na uhakika. Magoli matatu ni uongozi mrefu lakini ni lazima twende pale na tucheze na tupate japo goli moja.
"Ni lazima tufanya mambo hatua kwa hatua, mechi baada ya mechi, lakini nadhani tuna nafasi ya kufika fainali."

Pambano jingine litakalochezwa kwenye mfululizo wa mechi za ligi hiyo Borussia Dortmund itawaalika Malaga ya Hispania nchini Ujerumani kurudiana nao baada ya mechi iliyopita kuisha bila timu hizo kufungana. 
Wajerumani hao ambao wameshatemeshwa ubingwa wa ligi yao ya nyumbani Bundesliga baada ya vinara Bayern Munich kutwaa taji mwishoni mwa wiki itahitaji ushindi kurejea mafanikio ya 1997.

MASHETANI WEKUNDU WAFA NYUMBANI, KUN AGUERO AWAZIMA

Robin Van Persie akijaribu kukukuruka langoni mwa Manchester City jana usiku 

Sergio Kun Aguero akishangilia bao lililoizamisha Manchester United kwao jana usiku
VINARA wa Ligi Kuu ya England, Manchester United 'Red Devils' usiku wa kuamkia leo walikiona cha moto baada ya kunyukwa mabao 2-1 na wapinzani wao wa jadi, Manchester City kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford.
Ushindi huo ambao ulishuhudia mabingwa watetezi wa ligi hiyo wakifunga mabao yote katika mechi hiyo, imeifanya Man City kupungua pengo la pointi  kati yake ya wapinzani hao wao kutoka 15 hadi 12.
Bao lililowazima Mashetani Wekundu ambao wanajiandaa kusherehekea ubingwa msimu huu, lilifungwa na Sergio Kun Aguero zikiwa zimesaliwa dakika 11 kabla ya pambano hilo kumalizika huku matokeo yakiwa bao 1-1.
City walitangulia kupata bao mara baada ya timu kutoka mapumziko kupitia kwa James Milner katika dakika ya 51 kabla ya Vincent Kompany kuizawadia Man Utd bao dakika nane baadaye.