STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 21, 2013

Suarez awazima Chelsea na kuiokoa Liverpool isiadhiriwe nyumbani


http://l.yimg.com/iu/api/res/1.2/xe0Me6hmQ6lkB64ccOBXnQ--/YXBwaWQ9eXZpZGVvO2NoPTMwMDA7Y3I9MTtjdz0xOTUwO2R4PTE4MDtkeT0xO2ZpPXVsY3JvcDtoPTEwMDA7cT03MDt3PTY1MA--/http://media.zenfs.com/en_us/News/gettyimages.com/liverpool-v-chelsea-premier-league-20130421-094053-652.jpg
Suarez akiwa sambamba na beki Branislav Ivanovic katika mechi yao ya leo

Chelsea walipokuwa wakishangilia nao lao la pili

BAO la dakika za jioni kabisa lilililofungwa na kinara wa mabao wa Ligi ya England, Luis Suarez imeiwezesha Liverpool kuepuka kipigo cha nyumbani mbele ya Chelsea kwa kulazimisha sare ya 2-2.
Suarez alifunga bao hilo dakika ya sita ya nyongeza za pambano hilo huku Liverpool wakiwa nyuma kwa muda mrefu kw mabao 2-1 na kuzima shamrashamra za vijana wa kocha wao wa zamani  Rafael Benitez.
Chelsea walianza kuwashtukiza wenyeji wao kwa bao la dakika ya 26 kupitia Oscar aliyefunga kwa kichwa akiunganisha krosi nzuri ya Juan Mata, bao lililodumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa wenyeji Liverpool kuandika bao la kusawazisha kupitia nyota wa zamani wa Chelsea, Daniel Strurridge aliyemalizia kazi murua ya Suarez, lakini dakika chache baadaye
Edin Hazard aliifungia Chelsea bao la pili kwa mkwaju wa penati bada ya Suarez kuunawa mpira wakati wa harakati za kulilinda lango lao na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Hata hivyo shujaa huyo wa Uruguay na kinara wa orodha wa wafungaji katika ligi hiyo alipowatibulia Chelsea ushindi ambao ungewang'oa Arsenal kwenye nafasi ya tatu kwa kufunga bao la kusawazisha dakika hizo za nyonyeza kwa kumalizia pasi ya Sturridge.
Kwa matokeo hayo ya Chelsea imeendelea kusalia nafasi ya nne ikiwa na pointi 62 wakati Liverpool wameongeza pointi zaidi na kufikisha  51 ikisalia nafasi ya 7 nyuma ya Everton.

Serikali yafafanua madai ya walimu
                          THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UFAFANUZI WA SERIKALI KUHUSU MADAI YA BWANA GRATIAN MUKOBA JUU YA MAZUNGUMZO YA SERIKALI NA CWT
____________________________________________________
            Jumanne, tarehe 09 Aprili, 2013, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bwana Gratian Mukoba, alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari, likiwamo Gazeti la Mwananchi ambalo katika Uk. 3 liliandika habari hiyo chini ya kichwa cha habari, CWT: Serikali inakaribisha mgomo mwingine.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Bwana Mukoba alitoa madai yafuatayo:-
·        Kwamba Serikali imekataa kukaa meza moja na CWT ili kuzungumzia nyongeza ya mishahara na posho za walimu pamoja na kwamba CWT yenyewe iko tayari kwa mazungumzo;
·        Kwamba Serikali imepuuza amri ya Mahakama inayotaka pande hizo mbili kukaa meza moja kujadili madai ya walimu;
·        Kwamba kikao hasa kilichokataa kuzungumzia mishahara na posho ni kile kilichofanyika tarehe 02 Aprili, 2013 chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue;
·        Na kwamba kwa sababu ya yote hayo, Bwana Mukoba amelitaka Bunge na wazazi kuingilia kati uamuzi wa Serikali kukataa kukaa meza moja na CWT.
            Serikali inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa madai haya yote hayana chembe ya ukweli na hayana nia njema, maana yanaweza kujenga chuki na mazingira ya kuzua mgogoro mwingine na Serikali usio na sababu wala maslahi kwa walimu wenyewe na Taifa.
·        Serikali haijakataa majadiliano na CWT, na wala haijapuuza amri ya Mahakama inayotaka pande zote mbili kurudi kwenye meza ya majadiliano. Tangu amri ya Mahakama itolewe tayari vimefanyika vikao vinne vya Baraza la Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa Walimu. Vikao viwili vilifanyika mwaka jana tarehe 12 Septemba, 2012 na 05 Desemba, 2012. Vikao viwili tayari vimefanyika mwaka huu tarehe 09-10 Januari na 22 Machi, 2013.
·        Kilichochelewesha suala la mishahara na posho kujadiliwa katika vikao hivyo si kwamba Serikali haikutaka mjadala huo. Sababu hasa ni kuwa CWT kilikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu, katika kesi Na. 96/2012, na Serikali iliwasihi sana viongozi wa CWT kuwa wafute rufaa hiyo ili kuruhusu majadiliano ya mishahara na posho, lakini walikataa. Kitendo hicho hakionyeshi nia njema upande wao. Nia njema (good faith) ni sharti muhimu kwenye majadiliano haya. Kwa upande wake, ili kuonyesha utayari na nia njema, Serikali sasa imekubali majadiliano hayo yaendelee licha ya CWT kukataa kufuta rufaa yao.
·        Sababu ya pili iliyochelewesha majadiliano ya maslahi ya walimu ni madai ambayo awali viongozi wa CWT walikuja nayo kuwa iteuliwe timu maalum ya kuzungumzia maslahi badala ya Baraza la Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa Walimu ambalo ndilo lipo kisheria kwa majadiliano haya. Ni kwenye kikao cha tarehe 09 – 10 Januari, 2013 ndipo walipokubali kurejesha majadiliano kwenye Baraza hilo.
·        Si kweli vilevile kuwa kikao kilichofanyika Ikulu, tarehe 2 Aprili, 2012 chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, ndicho kilikataa majadiliano kuhusu maslahi ya walimu. Kauli hiyo ni upotoshaji  wa makusudi usio na nia njema. Viongozi wa CWT wanajua vema kuwa Katibu Mkuu Kiongozi si sehemu ya mfumo wa majadiliano kuhusu maslahi ya walimu. Hivyo, kikao kinachoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi hakiwezi kuwa mahali pa majadiliano ya mishahara, posho na maslahi ya walimu.
·        Pili, mkutano huo wa tarehe 02 Aprili, 2013 uliitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwa maombi rasmi ya uongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) ambao walitaka kujulishwa jinsi utaratibu wa majadiliano ya mishahara ya wafanyakazi wote utakavyokuwa kufuatia kuanzishwa kwa mzunguko mpya wa bajeti ya Serikali. Kikao hicho kisingeweza kugeuka na kuwa kikao cha kujadili mishahara na posho za walimu.
·        Tunapenda wananchi na walimu wajue pia kuwa Bwana Gratian Mukoba hakuwepo kwenye hicho kikao cha tarehe 02 Aprili, 2013. Aidha, kikao hicho kilikuwa cha TUCTA, hakikuwa cha CWT.
Serikali inapata taabu kuelewa nia na dhamira ya viongozi wa CWT kupotosha kwa makusudi wananchi na walimu kwa mambo yaliyo wazi. Serikali imeonyesha nia na dhamira ya wazi ya kujadiliana na CWT, pamoja na vyama vyote vya wafanyakazi, kuhusu maslahi ya wafanyakazi. Vikao vingi vilivyofanyika na vinavyoendelea kufanyika kwenye Mabaraza ya kisekta na Baraza Kuu ni ishara ya wazi ya nia njema ya Serikali. Aidha, Serikali imekwisha kusema kutakuwepo na nyongeza nzuri kwenye mishahara, hasa mishahara ya watumishi wa ngazi za chini katika mwaka ujao wa fedha. Tunajiuliza, katika hali hiyo, juhudi hizi za viongozi wa CWT kuandaa mazingira ya mgogoro wa Serikali lengo lake ni nini hasa?
             
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
 19 Aprili, 2013

BREAKING NEWSSS MWENYEKITI WA UMOJA WA SACCOS TAIFA NA PIA NI MFANYAKAZI WA TAZARA MBEYA AMBROSE LUCAS SHAYO APIGWA ATESWA NA KUCHOMWA MOTO KAWETELE MBEYA

HAPA NDIPO ALIPOTESWA NA KUUWAWA AMBROSE SHAYO
HAPA NDIPO ALIPOCHOMWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA

HILI NDILO ENEO GARI YAKE ILIPINDUKA NA WAUWAJI WALIPOPATA NAFASI YA KUMUUA AMBROSE
HAPA NDIPO GARI YA AMBROSE ILIPOGONGA NA KUPINDUKA WAKATI ANAKIMBIZWA NA WAUWAJI HAO

HABARI KAMILI YA TUKIO HILI TUTAZIDI KUWAJULISHA KWANI  POLISI WANAENDELEA NA KAZI YAO

PICHA NA MBEYA YETU

Yanga yakihakikishia ubingwa wa 23 Tanzania Bara

Kikosi cha Yanga
NI Miujiza tu itakayoizuia Yanga kuwa Mabingwa Wapya msimu huu baada ya jioni ya leo kuifumua maafande wa JKT Ruvu kwa mabao 3-0 katika pambano pekee la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ushindi huo umnewafanya vinara hao kufikisha pointi 56 ambazo zinawaweka katika nafasi nzuri ya kutwaa taji lake la 23 la Ligi Kuu kutokana na ukweli ni Azam pekee inayoweza kuzifikia pointi hizo ikishinda mechi zake zote, wakati Yanga ikiwa bao na mechi mbili mkononi.
Hata hivyo Yanga inawabidi wasubiri kuanza kusherekea ubingwa huo ambao ni dhahiri ni wao msimu huu mpaka jumamosi kusikilizia mechi ya Azam na Coastal Union itakayochezwa mjini Tanga.
Iwapo Azam italazimishwa sare yoyote basi itatoa fursa ya wana Jangwani kusherehekea ubingwa wa 23 wa Ligi hiyo bila kushuka dimbani.
Mabao yaliyoihakikishia Yanga ushindi huo na kuifanya ilishike kombe la ubingwa kwa mkono mmoja, yalitupiwa kambani na Simon Msuva dakika moja kabla ya mapumziko.
Hamis Kiiza Diego aliiandikia Yanga bao la pili kwa kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na David Luhende katika dakika ya 58.
Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliiongezea Yanga bao la tatu kwenye dakika ya 62 na kuwafanya maafande wa JKT Ruvu kupoteza dimbani.
Kipigo hicho cha leo kimezidi kuiweka pabaya JKT Ruvu ambayo inanolewa na kocha Kennedy Mwaisabula aliyechukua nafasi ya Charles Kilinda katika eneo la hatari la kushuka daraja.
Timu hiyo iliyopo nafasi ya 11 ikiwana pointi 23 inahitajika kushinda mechi zake tatu zilizosalia iwapo inataka kuepuka kushuka daraja.

Maafande hao wamesaliwa na mechi dhidi ya African Lyon mechi itakayochezwa Jumatano kabla ya kuvaana na Prisons Mbeya kisha kumalizia na Mtibwa Sugar.

 Msimamo Kamili wa Ligi Kuu baada ya mechi ya leo:
                                   P      W     D     L     Gf     Ga     Gd    PTS
1.  Young Africans     24     17     5     2     44     13     +31     56
2. Azam                      23     14     5     4     41     19     +22     47    
3. Kagera Sugar          23     11     7     5     26     18      +8      40     
4.  Simba                     22      9      9     4     32     21     +11     36
5.  Mtibwa Sugar         24      9      9     6     27     24      +3      36   
6. Coastal Union          23      8      9     6     23     20     +3      33    
7.  Ruvu Shooting        23      8      6     9     21     22      -1      30     
8.  JKT Oljoro FC        24      7      7     10   22     28      -6      28     
9. Tanzania Prisons      24      6      8     10   14     21      -7      26    
10.JKT Mgambo          23      7      4     12   15     23      -8      25       11.Ruvu Stars              23      6      5     12    19     37     -18     23
12. Toto Africans         25     4     10     11    22     33     -11     22
13.  African Lyon        23     5       4     14     16     35     -19     19
14. Polisi Morogoro     23     3     10     10     11     21     -10     19

Tottenham yauweka rehani ubingwa wa Man City yainyuka 3-1

http://l.yimg.com/iu/api/res/1.2/HKjEQEGwnP7rEbYTCElotQ--/YXBwaWQ9eXZpZGVvO2NoPTIxNDE7Y3I9MTtjdz0xMzkxO2R4PTgwNTtkeT0xO2ZpPXVsY3JvcDtoPTEwMDA7cT03MDt3PTY1MA--/http://media.zenfs.com/en_us/News/gettyimages.com/tottenham-hotspur-v-manchester-city-20130421-054449-536.jpg
Carlos Tevez akiwania mpira na mchezaji wa Tottenham Hotspur jioni hii
TIMU ya soka ya Tottenham Hotspur jioni hii ikiwa nyumbani kwao imeweza pabaya mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya England Manchester City baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 katika mfululizo wa ligi hiyo na kutoa nafasi kwa vinara Manchester United kujiandaa kusherehekea taji lake la 20 la ligi hiyo.
Mabingwa hao watetezi wamediwa na wapinzani wao wa jiji la Manchester kwa pointi 13 katika msimamo zote zikiwa zimecheza mechi 33 na kuifanya Man United kuhitaji kushinda mechi yake ya kesho dhidi ya Aston Villa kutangaza ubingwa huo ikiwa ni mara yao ya 20 katika historia.
Wageni walianza makeke kwa kuwashtukiza wenyeji wao kwa bao la mapema la dakika 5 lililotupiwa kimiani na Samir Nasir na kulifanya lidumu hadi wakati wa mapumziko licha ya Hotspur kucharuka kutaka kusawazisha.
Hata hivyo Tottenham iliingisa kipindi cha pili wakiwa kama mbogo wa kuwakimbiza wageni wao kwa muda mrefu kabla ya kuandika bao la kusawazisha dakika ya 75 lililofungwa na Clint Dempsey kabla ya dakika nne baadaye Jarmain Defoe kuongeza la pili.
City wakijiuliza jinsi ya kusawazisha bao hilo ili angalau kupata sare ya mabao 2-2, winga nyota na mmoja wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi hiyo, alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu dakika ya 82.
Ushindi huo umeifanya Hotspurs kufikisha pointi 61 ikilingana na Chelsea ambayo jioni hii inatarajiwa kuvaana na Liverpool katika pambano jingine linalosubiriwa kwa hamu katika ligi hiyo ya England.

Miss Tabata 2013 kufanyika Mei 31


 
Miss Tabata 2012 Noela Michael


SHINDANO la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2013, litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa shindano hilo litakuwa ni ya aina yake kulinganisha na mashindano ya miaka ya nyuma kwani mwaka huu wamemejitokeza warembo wazuri zaidi.
 
“Warembo wazuri wamejitokeza zaidi kuliko mashindano ya tuliyowahi kuyafanya nyuma. Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts.
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park.
Warembo hao ni Pendo Judica Moshi (20), Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Queen Eliakim Masha (19), Upendo Dickson Lema (22), Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),  Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
Wengine ni Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rafhel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Brath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass (22). 
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa kuendelea kujitokeza ili waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda ya Ilala.
"Bado milango iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza.
Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Waliyojitokeza kudhamini shindano hilo ni Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.