STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 12, 2017

Dude linaamshwa Champion League, nani kucheka?




Picha tofauti zikionyesha Juventus wakipasha kwenye Uwanja wa Nou Camp kabla ya leo usiku uliamsha dude dhidi ya Barcelona
BARCELONA, Spain
KAZI imeanza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati mechi za makundi kwa msimu huu wa 2017-2018 ukianza rasmi usiku wa leo kwa kushuhudiwa mechi nane, lakini macho na masikio yakielekezwa Nou Camp, wakati Kibibi Kizee cha Turin, Juventus itakapoifuata Barcelona katika mechi iliyovuta mashabiki wengi wa michuano hiyo.
Juventus imeenda Hispania ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa fainali zilizopita dhidi ya mahasimu wa Barcelona, Real Madrid, lakini wakijivunia rekodi ya kuanza Ligi Kuu ya Italia Serie A ikishinda mechi zao tatu zote na kufunga mabao 10 na kukaa kileleni ikizizidi ujanja Napoli na Inter Milan kwa tofauti na uwiano wa mabao.
Kikosi hicho cha Juve kilifanya mazoezi jana kwenye Uwanja wa Nou Camp kikiwa na nyota wake wote wakiwamo wakali kinara wa mabao Paul Dyabala, Gonzalo Higuain na Mario Mandzukic.
Wenyeji wataendelea kumtegemea zaidi nyota wao Lionel Messi na Luis Suarez kuweza kulinda heshima yao katika michuano hiyo baada ya msimu uliopita kukwamia njiani kwa aibu.
Mbali na mechi hiyo, pia leo kuna gemu kali yenye mvuto Manchester United waliorejea kwenye michuano hiyo kwa mlango wa uwani itakuwa nyumbani kukabiliana na Basel, huku Chelsea wakicheza na Qarabag, PSG ikiwa na wachezaji ngali zaidi kwa sasa duniani Neymar na Kylian Mbappe watakuwa ugenini nchini Scotland kuvaana na Celtic.

RATIBA KAMILI  LIGI YA MABINGWA ULAYA
Leo, Jumanne
Celtic v PSG         (Saa 3:45 usiku)
Benfica v CSKA Moskva (Saa 3:45 usiku)
Man United v Basel         (Saa 3:45 usiku)
Olympiakos v Sporting CP         (Saa 3:45 usiku)
Bayern Munichv Anderlecht (Saa 3:45 usiku)
Roma v At.Madrid         (Saa 3:45 usiku)
Chelsea v Qarabag (Saa 3:45 usiku)
Barcelona v Juventus (Saa 3:45 usiku)

Kesho Jumatano
Maribor v Spartak Moskva (Saa 3:45 usiku)
Tottenham v B.Dortmund         (Saa 3:45 usiku)
RB Leipzig v Monaco (Saa 3:45 usiku)
Feyenoord v Man City         (Saa 3:45 usiku)
Shakhtar v Napoli         (Saa 3:45 usiku)
Liverpool v Sevilla         (Saa 3:45 usiku)
Porto v Besiktas (Saa 3:45 usiku)
Real Madrid v APOEL (Saa 3:45 usiku)


EUROPA LEAGUE
Alhamis, Septemba 14,  2017
Young Boys v Partizan (Saa 2:00 usiku)
Atalanta v Everton (Saa 2:00 usiku)
Slavia Praha v Maccabi Tel Aviv(Saa 2:00 usiku)
Dynamo Kyiv v Skënderbeu Korçë(Saa 2:00 usiku)0
Hoffenheim v Sporting Braga (Saa 2:00 usiku)
Apollon v Lyon         (Saa 2:00 usiku)
Zlín         v Sheriff   (Saa 2:00 usiku)
Rijeka v AEK Athens (Saa 2:00 usiku)
Istanbul Basaksehir v Ludogorets (Saa 2:00 usiku)
København v L'tiv Moskva (Saa 2:00 usiku)
Austria Wien v Milan          (Saa 2:00 usiku)
Villarreal v Astana         (Saa 2:00 usiku)
Hapoel B.Sheva v Lugano (Saa 4:05 usiku)
Zorya v Östersunds FK (Saa 4:05 usiku)
Real Sociedad v Rosenborg         (Saa 4:05 usiku)
Vitesse v Lazio         (Saa 4:05 usiku)
Zulte-Waregemv Nice      (Saa 4:05 usiku)
Arsenal v Koöln         (Saa 4:05 usiku)
Marseille v Konyaspor         (Saa 4:05 usiku)
Vitoria Guimarães v Salzburg (Saa 4:05 usiku)
Crvena Zvezda v BATE (Saa 4:05 usiku)
Hertha BSC v At.Bilbao      (Saa 4:05 usiku)
Vardar v Zenit         (Saa 4:05 usiku)
FCSB v Viktoria Plzen (Saa 4:05 usiku)

Andre Ayew aitibulia Huddersfield akiibeba West Ham

Andre Ayew akiifungia West Ham bao la pili
 

Andre Ayew akishangilia bao lake

Obiang akishangilia bao lake 
LONDON, England
WEST Ham United usiku wa kuamkia leo walipata ushindi muhimu nyumbani baada ya kuichapa Huddersfield na kuitibulia rekodi yao ya kupototeza mchezo wowote tangu msimu huu wa Ligi Kuu England kuanza.
Straika Andre Ayew aliyetokea benchi alihusika na mabao yote mawili ya Wagonga Nyundo hao baada ya awali kumtengenezea bao Pedro Obiang katika ya 72 kabla ya mwenyewe kutumbukiza wavuni bao la pili dakika tano baadaye kwenye mchezo mkali uliopigwa Uwanja wa London.
Nyota huyo wa Ghana na mtoto wa Mwanasoka Bora wa zamani Afrika, Abedi Ayew Pele aliingia uwanjani dakika ya 64 kuchukua nafasi ya nyota wa zamani wa Manchester United, Javier Hernandez 'Chicharito' kabla ya kuibeba West iliyotoka kupoteza mechi yao dhidi ya NewCastle United waliowafumua mabao 3-0 ugenini.

Okwi awazidi ujanja Ngoma na Ajibu, Mtibwa yatikisa

Emmanuel Okwi akiwa na mpira wake baada ya kupiga hat trick dhidi ya Ruvu Shooting
Ibrahim Ajibu katika mazoezi ya Yanga

Donald Ngoma
Mtibwa Sugar
NA TARIQ JUNIOR
STRAIKA wa Simba, Emmanuel Okwi anayeichezea Simba amewazidi ujanja mastraika wa Yanga, Donald Ngoma na Ibrahim Ajibu, baada ya kusalia kileleni mwa orodha ya wafungaji akiwa na mabao manne, licha ya  nyota hao wa Jangwani kushuka dimbani kwa  dakika nyingi zaidi ya Mganda huyo.
Okwi ametumia dakika 90 tu kufunga mabao yake akicheza mchezo mmoja tu na kuukosa mchezao mmoja, lakini  Ngoma na Ajibu kila mmoja amecheza mechi mbili na kufunga bao moja kila mmojam, jambo lililowapa kiburi mashabiki wa Msimbazi kuwatambia wenzao wa Jangwani.
Mganda huyo aliyewahi kuichezea Yanga misimu mitatu iliyopita, aliukosa mchezo wa timu yake dhidi ya Azam Jumamosi iliyopita ulioisha kwa suluhu, lakini hilo halikumfanya ashindwe kukalia kiti cha uongozi wa wafungaji.
Okwi ambaye jana asubuhi alishindwa kuhudhuria mazoezi ya timu yake yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam ili kujiandaa na mchezo wao ujao dhidi ya Mwadui Jumapili hii, alishindwa kuwahi mechi ya Azam kutokana na kuwa na timu yake ya taifa ya Uganda The Cranes iliyoenda kuvaana na Misri katika mechi ya makundi ya kuwania Fainali za Kombe la Dunia 2018.
Ngoma aliyeifungia Yanga bao la kusawazisha katika mchezo wa kwanza dhidi ya Lipuli na kutolewa katika kipindi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji, bado hajarudi kwenye ubora wake tangu atoke kwenye majeraha ya muda mrefu yaliyomfanya ashindwe kuitumikia timu hiyo kwenye mechi za nusu wa msimu uliopita aliomaliza na mabao nane.
Ajibu aliyecheza dakika 180 za mechi mbili za Yanga za msimu huu, naye alifunga bao moja lililokuwa la pekee katika mchezo wao na Njombe Mji na kuzidi kuwapa kiburi Simba kuamini kuwa, licha ya Yanga kuwa na safu kali ya washambuliaji lakini jeshi la mtu mmoja, yaani Okwi ni funika bovu.
Okwi alifunga mabao manne katika mechi ya ufunguzi wa ligi dhidi yas Ruvu Shooting ambapo Simba walishinda mabao 7-0 na timu yake kushindwa kupata matokeo kwenye Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Azam.
Mpaka sasa wachezaji 27 wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao 32, huku Mohammed Rashid wa Prisons na Marcel Bonventure wa Majimaji wenye mabao mawili kila mmoja wakionekana kumkimbiza Okwi.
Mpaka sasa Ligi ikiwa imeshacheza mechi 16, Ruvu Shooting ndio klabu yenye ukuta mlaini baada ya kuruhusu mabao tisa na yenyewe kufunga bao moja tu, huku Chama la Wana Stand United ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haijafanikiwa kufunga bao hata moja, licha ya yenyewe kuruhusu mabao mawili nyavuni mwao.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo nane, Ijumaa Azam itaikaribisha Kagera Sugar kabla ya Simba na Yanga kucheza katika miji ya Dar es Salaam na Ruvuma dhidi ya Mwadui na Majimaji, wakati vinara wa ligi hiyo, Mtibwa Sugar wenyewe wataendelea kuwa nyumbani kuwakaribisha Mbao FC iliyotoka kujeruhiwa mjini Dodoma na Singida United Jumapili iliyopita.

Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara 2017-2018 ulivyo kwa sasa
         P W D L F A PTS
1.Mtibwa  2 2 0 0 2 0 6
2.Simba    2 1 1 0 7 0 4
3.Prisons  2 1 1 0 4 3 4
4.Lipuli  2 1 1 0 2 1 4
5.Yanga  2 1 1 0 2 1 4
6.Azam  2 1 1 0 1 0 4
7.Singida  2 1 0 1 3 3 3
8.Mwadui 2 1 0 1 2 2 3
9.Mbao  2 1 0 1 2 2 3
10.Mbeya 2 1 0 1 1 1 3
11.Ndanda2 1 0 1 1 1 3
12.Majimaji2 0 1 1 2 3 1
13.Kagera2 0 1 1 1 2 1
14.Ruvu 2 0 1 1 1 8 1
15.Njombe2 0 0 2 1 3 0
16.Stand 2 0 0 2 0 2 0

WAFUNGAJI:
4 Emmanuel Okwi (Simba)
2 Marcel Boniventure (Majimaji)
Mohammed Rashid (Prisons)
1 Ibrahim Ajibu (Yanga)
Erasto Nyoni (Simba)
Juma Liuzio (Simba)
Shiza Kichuya (Simba)    
Donald Ngoma (Yanga)
Paul Nonga (Mwadui)
Yahaya Mohammed (Azam)
Salim Khamis (Mwadui)
Kenny Ally (Singida United)
Boniface Maganga (Mbao FC)
Hussein Javu (Mtibwa Sugar)
Eliud Ambukile (Mbeya City)
        Kassim Khamis (Prisons)
Nurdin Chona (Prisons)
Hassan Kapalata (Njombe Mji)
Seif Karihe (Lipuli)
Jerome Lambele (Lipuli)
Mudathir Yahya (Singida)
Michelle Katsvairo (Singida)
Seleman Kihimbwa (Mtibwa)
Habib Kayombo (Mbao)
Majid Bakar (Ndanda)
Raphael Kyara (Ruvu Shooting)

RATIBA WIKIENDI HII:
Ijumaa Sept 15, 2017
Azam v Kagera Sugar

Jumamosi Sept 16, 2017
Mtibwa Sugar v Mbao FC
Majimaji v Yanga
Prisons v Ndanda
Stand United v Singida United
Lipuli v Ruvu Shooting

Jumapili Sept 17, 2017
Simba v Mwadui
Mbeya City v Njombe Mji

MCL MAGAZETINI SEPTEMBA 12, 2017: LOWASSA AMFUATA LISSU NAIROBI