STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 24, 2014

Hussein Bunu achekelea 'kuitungua' Simba Taifa


MSHAMBULIAJI wa JKT Ruvu, Hussein Bunu amesema amejisikia fahari mno kufanikiwa kuwatungua Simba na kupelekea kuipa kipigo timu hiyo kongwe akidai kuwa JKT walikuwa bora kuliko wapinzani wao.
JKT Ruvu iliizamisha Simba kwa mabao 3-2 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na Bunu alifunga bao la kuongoza dakika ya 13 tu ya mchezo kabla ya Emmanuel Switta kufunga mengine.
Akizungumza na MICHARAZO leo, Bunu alisema ingawa amekuwa akifunga mabao, katika mechi mbalimbali tangu aanze kucheza soka, lakini goli la juzi dhidi ya Simba limempata furaha kubwa kwa sababu limeibeba timu yao kuzoa pointi 3.
"Kwa kweli nimejisikia furaha sana kuwatungua Simba, bao langu nalitoa kwa familia yangu na hasa wanangu, naamini tulistahili ushindi kwani tulikuwa bora kuliko wapinzani wetu," alisema Bunu.
Bunu anayecheza pamoja na nduguye Abdallah Bunu katika timu hiyo alisema wachezaji wote wa JKT Ruvu walikuwa na lazima ya kushinda mechi hiyo baada ya kufanya vibaya mechi zao tatu zilizopita wakifungwa jumla ya mabao nane.
Walianza kwa kufungwa mabao 2-0 na Ruvu Shooting kisha kutoka suluhu na Oljoro kabla ya kuangamizwa 6-0 na Prisons.
Katika mechi hiyo ya jana mbali na Bunu mabao mengine yalioisaidia timu hiyo inayonolewa na kocha Fred Minziro yalifungwa na Emmanuel Switta aliyefunga mawili kabla ya Amissi Tambwe kuiopatia Simba mabao ya kufutia machozi.

HAYA NI MAMBO 9 USIYOYAJUA YA RAIS ROBERT MUGABERAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefikisha miaka 90 na wikendi hii alikuwa na bonge la sherehe siyo mchezo nchini humo katika kusherehekea maisha marefu ya kiongozi huyo.
Mugabe, alizaliwa katika kijiji cha Kutama, kusini-magharibi mwa jiji kuu Harare, alisomeshwa na wayesuti, na baadaye akawa mwalimu kabla kujiingiza katika harakati za kupigania uhuru wa Zimbabwe.
Uwanaharakati wake ulimfanya afungwe gerezani kwa miaka 11, na baadaye mwaka 1980 akawa rais wa kwanza wa Zimbabwe. Yafuatayo ni mambo tisa ambayo huenda huyajui kumhusu kiongozi huyu na ambaye yamemwezesha kuwa rais kwa muda mrefu mno.

1) Zoezi na vyakula vya kienyeji

Mugabe akionekana kuwa na furaha mno
Mugabe anapenda kufanya mazoezi. “Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya mazoezi ya viuongo vya mwili,” Bw. Mugabe alisema miaka mitatu iliyopita. Huwa anaamuka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri, na kutokana na jamaa zake wa karibu, husikiliza BBC idhaa ya dunia.
Siri nyingine ya kuishi kwake kwa muda mrefu ni kuwa ywapenda sana-chakula cha kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe. Kisha pia, havuti sigara, ila hunywa pombe kidogo anapokula.

2) 'Kufufuka'

Ingawa kumekuwa na uvumi mara nyingi kuwa Mugabe hana afya nzuri, afya yake na kazi yake ya kisiasa yaendelea vyema kabisa. Kuhusu afya yake Mugabe alipohojiwa wakati mmoja alisema,“ Nimekufa mara nyingi-hapo ndipo humwelekea Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na akafufuka mara moja,” alisema alipotimia miaka 88.
Ingawa alilelewa katika familia ya kikatoliki-mamake alikuwa mcha Mungu-alisema alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC, miaka michache iliyopita, kuwa yeye si Mkristo anayetumikia dini kwa sana.

3) Shabiki mkubwa sana wa kriketi

Kwa muda mrefu amedhihirisha hadharani mapenzi ya mchezo wa kriketi. Ni patroni wa jumuiya ya mchezo wa kriketi wa Zimbabwe, ambapo nyumba yake ipo karibu na uga wa michezo wa Harare, ambapo anaweza kutazama kwa makini wakati wa michezo wa kitaifa.
“Kriketi yafanya watu wawe wangwana, na pia inawafanya watu kuwa wema,” Bw. Mugabe alisema miaka kadhaa baada ya Zimbabwe kujinyakulia uhuru. “Nataka kila mtu acheze kriketi Zimbabwe; nataka nchi ya Zimbabwe iwe nchi ya wangwana.”

4) Hapendi kushindwa

Alipokuwa kijana, Mugabe alikuwa mmakinifu na mzuri kabisa katika mchezo wa tennis,” alisema aliyekuwa mwalimu katika shule ya Wakatoliki alikosomea Mugabe. Ila, aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa raketi yake chini kwa hasira.
Mugabe amekiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila kwa sasa, anapenda kuutazama mchezo huo.
Yeye ni shabiki wa vilabu vya Chelsea na Barcelona vilivyoko Uingereza na Uhispania mtawalia. “ Ninapotazama kandanda, sitaki usumbufu kutoka kwa mtu yeyote,” alisema mwaka wa 2012. “Hata mke wangu anajua mahala pa kukaa wakati wanapofunga bao uwanjani, hata mimi pia hufunga bao kwangu kwa kupiga mateke vitu vyovyote vilivyoko mbele yangu.”

5) Alipata mtoto akiwa miaka 73

Familia ya Mugabe
Ana watoto watau na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani wake. Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997, mwaka mmoja baada ya wao kufunga ndoa.
Mwanawe wa kwanza, Nhamodzenyika, alikufa kutokana na Malaria akiwa miaka mitatu bado wakiwa Ghana. Bw. Mugabe alinyimwa ruhusa ya kuenda Accra kuungana na mkewe kwa mazishi ya mwanawe, kwani alikuwa mfungwa wa kisiasa wa serikali ya enzi hiyo ya Rhodesia.

6) Anampenda Cliff Richard kumliko Bob Marley

Mwanasiasa wa Zimbabwe ambaye kwa sasa ni hayati, Edgar Tekere, alimwambia mwandishi wa BBC, Brian Hungwe, kuwa alipokuwa akitayarisha kadhia ya kusherehekea uhuru wa Zimbabwe 1980, Bw. Mugabe hakumtaka muimbaji Bob Marley aalikwe kutumbuiza watu, ila alimtaka muimbaji maarufu wa Uingereza, Cliff Richard. Pia anampenda Muimbaji, Jim Reeves.
Mugabe anawachukia sana wanamitindo wa rasta, na waimbaji wa mitindo ya reggae. Aliwaonya vijana wa Zimbabwe: “ Nchini Jamaica, wana uhuru wa kutumia bhangi, na wanaume huwa wakati wote wamelewa. Hawataki kuenda shule; wanataka tu kuimba, na kufuga rasta. Kama Zimbabwe, tusielekee hapo.”

7) Mvaaji wa nguo maridadi

Anapenda sana suti zinazoutosha mwili wake visawasawa na tai zinazofanana na kitambaa. Hwavutia sana wanamitindo nchini Zimbabwe kwa mavazi yake. Ila, mwanamitindo ambaye humshonea nguo zake ,Khalil Parbhoo anasema: “Bado huavlia kama mabwana wa Uingereza –hivyo ndivyo anavyopenda."

8) Anamtazama Kwame Nkrumah kama kielelezo kwake

Taarifa kuhusu hali ya kiafya ya Mugabe zimekuwa zikigonga vichwa vya habari karibuni
Bw. Mugabe alipata azma ya siasa akiwa Ghana alipokuwa mwalimu; mahali alipokutana na mke wake wa kwanza, Sally Hayfron.
Aliporudi Zimbabwe, aliwaambia wananchi jinsi Ghana ilivyojinyakulia uhuru na jinsi uhuru ni kitu kizuri. Katika mahojiano mwaka 2003, Mugabe alisema: “Niliwaambia pia kuhusu Kwame Nkrumah jinsi alivyojitolea na kuiongoza Ghana kupata uhuru;Kwame aliwaambia wananchi wa Ghana kuwa Ghana haingekuwa nchi huru bila ya jitihada na kujitolea kwa kila mtu.”

9) Ni mtu mwenye shahada nyingi

Kwa jumla, Mugabe ana shahada saba. Digrii yake ya kwanza ni kutoka katika chuo kikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii zake zingine kwa njia Internet-mbili akiwa gerezani-shahada hizo ni za: elimu, sayansi, sheria na usimamizi.
Amejitapa kuwa na “shahada katika ujuhula” alipokuwa akivionya vyama vya kutetea haki za wafanyakazi nchini Zimbabwe 1998 kila vilipotishia kugoma.
BBC

'Yanga funga hao Al Ahly tupumue mitaani'

http://2.bp.blogspot.com/-2AgowyAqcZA/UMWSUxAbTGI/AAAAAAAABK8/fmQ5f4m08P4/s1600/mko+2.jpg
Mkono wa Mkonole
MCHEKESHAJI Fadhil Omar 'Mkono wa Mkonole' ameiangukia timu anayoishabiki ya Yanga, kuhakikisha inafanya kweli mbele ya Waarabu ili kuweza kuzima kebehi wanazopewa na watani zao mitaani.
Mkono aliyepo mjini Morogoro kwa sasa akirekodi filamu mpya alisema yeye ni mnazi mkubwa wa Yanga na amekuwa akiifuatilia katika mechi zake za ndani na za kimataifa, lakini hana furaha kwa kebehi toka kwa watu wa Simba.
"Watani wetu wanatucheka eti, sisi kwa Waarabu ni kama 'Mbwa kwa Chatu', nilikuwa nawaomba wachezaji wa Yanga wasituangushe mbele ya Al Ahly, waifunge kukata mzizi wa fitina na kuwaziba midomo watani wetu," alisema.
Mkono alisema anaamini Yanga wakijipanga vyema kwa mechi ya awali ya ugenini kabla ya kuja kumalizana nao jijini Dar es Salaam wanaweza kurejea rekodi ya Simba ya mwaka 2003 waliivua ubingwa Zamalek.
"Yanga ikikaza msuli na kujipanga vyema wanaweza kurejea yaliyofanywa na Simba mwaka 2003, tunajisikia wanyonge kwa kejeli za watu wa Simba wakidai eti safari yetu kimataifa imefikia tamati kwa Al Ahly," alisema.
Yanga iliyokuwa Comoro inatarajiwa kuvaana na Al Ahly mwishoni mwa wiki hii baada ya kutinga raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuing'oa Komorozine kwa jumla ya mabao 12-2.
Msanii huyo alisema haoni sababu ya Yanga kushindwa kuifanyizia Al Ahly ambao pia ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo kwa madai Jangwani wana kikosi imara na kocha mzoefu, Johannes van Der Pluijm.
Pambano hilo linatarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa, na Yanga inahitajika kushinda idadi kubwa ya mabao ili kurahisisha pambano lao la marudiano wiki ijayo mjini Cairo.
Al Ahly ndiyo mabingwa watetezi na pia wanashikilia taji la Super Cup iliyotwaa Alhamis iliyopita baada ya kuilaza CS Sfaxien ya Tunisia kwa mabao 3-2 huku wakishuhudiwa na kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa 'Master' aliyetumwa kwenda kufanya ushushushu.

Beki Atletico Madrid presha tupu dhidi ya Real Madrid jumapili

https://pbs.twimg.com/profile_images/378800000708295411/f912c666061f41dffd5b2d51ee982b30.jpeg
Filipe Luis wa Atletico Madrid
BEKI wa Atletico Madrid, Filipe Luis amesema akili zao kwa sasa zipo kwenye mechi yao ijayo dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Madrid, Real Madrid.
Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumapili kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Hispania huku zikiwa kwenye mbio za kuwania ubingwa unaoshikiliwa na Barcelona.
Vijana wa kocha Diego Simeone wataivaa Real wakiwa wanauguza kipigo cha mabao 3-0 walichopewa jana ugenini na Osasuna, ambapo Filipe alisema wasingependa kurudia makosa katika mechi hiyo ya mahasimu wao.
Makosa yaliyofanywa na safu yake ya Atletico yaliifanya wenyeji kupata mabao hayo matatu yaliyoibakisha timu hiyo kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Barcelona wakiachwa pointi tatu nyuma na Real Madrid wanaoongoza msimamo wa ligi.
Beki huyo wa Kibrazil, anafahamu ugumu unaowakabili dhidi ya timu hiyo kwenye kiwango bora kwa sasa Real Madrid.
Hata hivyo alinukuliwa akisema kuwa watahakikisha wanafanya kila njia kuhakikisha wanapata ushindi ili kuendeleza mbio zao za kuwania ubingwa.
"Tuna muda mrefu wa wiki nzima ya kufanya mazoezi na kujiandaa vyema kabla ya kuvaana na wapinzani wetu," Filipe alinukuliwa na tovuti ya klabu hiyo ya Atletico Madrid.
Beki huyo alisema kukabiliana na Real ni nafasi nzuri kwao ya kuthibitisha kuwa ni timu kubwa na matoeko ya jana hayawezi kuwavunja nguvu kwa sababu yanapaswa kusahauliwa na kuangali yaliyopo mbele yao.

Tomas Rosicky haondoki Arsenal-Wenger

http://img.thesun.co.uk/aidemitlum/archive/00861/Tomas_Rosicky_861146a.jpg
Tomas Rosicky
MENEJA wa Arsene Wenger, amethibitisha kuwa, Kiungo kutoka Czech Tomas Rosicky atasalia katika kikosi hicho hata baada ya msimu huu.
Rosicky aliyejiunga na Arsenal mwaka 2008 akitokea Borussia Dotmund ya Ujerumani na ameichezea klabu hiyo jumla ya mechi 208 mpaka sasa.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha kwanza kwa siku za karibuni, jambo lililozua maneno kwamba huenda angeondoka mapema klabu hapo.
Lakini kocha Wenger alinukuliwa jaa akisisitiza kuwa mchezaji huyo ataendelea kusalia klabu kwao kwa msimu mwingine ujao.

Mugabe asherehekea miaka 90 akipinga ushoga

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake
 
RAIS mzee kuliko wote barani Afrika na aliyedumu madarakani kwa muda mrefu nchini Zimbabwe, Robert Mugabe jan Jumapili alisherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake mjini Harare. Katika hotuba iliyotolewa kwa zaidi ya saa nzima, Kiongozi  huyu mkongwe kabisa barani Afrika  alisema hataruhusu wapenzi wa jinsia moja nchini Zimbabwe. Alisema  hilo ndilo linalochangia kusambaa kwa virusi vya HIV na Ukimwi. Mugabe alinukuliwa na vyombo vya habari akielezea kuwa; “tumeumbwa kama wanaume na wanawake ili tuweze kuzaa watoto. Na hivyo ndivyo ilivyo.”
 Bw. Mugabe ambaye ametawala Zimbabwe tangu ilipopata uhuru wake mwaka wa 1980, alisema pia kuwa atapambana na ufisadi.
Matamshi yake yalifuatia kukamatwa kwa baadhi ya maafisa wa ngazi ya juu kutoka kwa shirika la ndege la kitaifa kutokana na  tuhuma za ufisadi uliohusisha dola milioni 10. Baada ya hotuba yake bwana Mugabe alikata keki kadhaa, mojawapo ikiwa na uzani wa kilo 90. Kisha wafuasi wake wakaanza kugawa zawadi ikiwemo mifugo 90 huku mfanyabiashara mmoja akimpa dola elfu 20 taslimu.
Sherehe hizo zaaminika kugharimu takriban dola milioni moja.Wanachama wa upinzani hawakuhudhuria sherehe hizo wakisema wanapinga kushindwa kwa bwana Mugabe kuokoa uchumi wa nchi unaozidi kuzorota. 
VOA

Carlos Tevez aibeba Juventus nchini Italia

Juventus striker Carlos Tevez
NYOTA wa zamani wa Manchester United na Manchester City, Carlos Teves ameendelea kuonyesha makali yake nchini Italia baada ya jana usiku kuisaidia timu yake ya Juventus kupata ushindi kiduchu wa bao 1-0 na kuzidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Seria A nchini Italia.
Tevez aliifungia Juve bao pekee katika katika pambano lao dhidi ya Torino lililochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani mjini Torino na kuwazima wapinzani wao wa mji huo na kuzoa pointi tatu.
Muargentina huyo alifunga bao hilo lililokuwa la 14 msimu huu katika dakika ya 30 akimalizia kazi ya Kwadwo Asamoah na kuifanya Juve kufikisha jumla ya pointi 66 ikiiwaacha wanaowafukia Roma walioshinda ugenini juzi kwa pointi 9.
Katika mechi nyingine iliyochezwa jana, Lazio ilipata ushindi wa mabao 3-2 nyumbani dhidi ya Sassuolo na leo ligi hiyo itaendelea kwa mechi mbili zitakazowakutanisha OParma dhidi ya Fiorentina na Napoli kuvaana na Genoa.


Atletico Madrid yafumuliwa ugenini

 Osasuna celebrate
KLABU ya Atletico Madrid usiku wa kuamkia leo imeangukia pua baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 ugenini dhidi ya Osasuna na kushindwa kuiengua Barcelona ambao walipoteza mechi yao juzi katika Ligi Kuu ya Hispania.
Kipigo cha timu hizo mbili zimeifanya Real Madrid kupumua kileleni, ikiwa na piinti 63, huku Barcelona na Atletico zikisaliwa na pointi zao 60 kila mmoja baada ya kucheza mechi 25 kila mmoja.
Mabao yaliyoinyong'onyesha Atletico ugenini yalifungwa naCejudo katika dakika ya 6 kabla ua Armenteros kufunga la pili dakika ya 21 na kisha Robert Torres kumalizia kazi dakika tatu kabla ya mapumziko.
Katika mechi nyingine, Rayo Vallecano iliifumuliwa nyumbani na Sevilla kwa bao 1-0, Real Betsi kulala pia nyumbani Athletic Club  na Valencia kutakata kwao kwa kuilaza Granada kwa mabao 2-1.

Ngumi zavumuka tena kanisa la Moravian

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/c/c1/AgnusDeiWindow.jpg
WIKI ya tatu mfululizo vurugu zimeendeleakatika kanisa la Moravian baada ya jana tena kuibuka kitimtim katika kanisa la Mwananyamala Msisiri A Kinondoni Dar Es Salaam. 
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alilidokeza MICHARAZO kuwa chanzo ilikuwa ni Maaskofu kutoka makao makuu ya kikanda ambao walifika na kutaka kuingia ndani ya Kanisa hilo na kuzuiwa na mmoja wa waumini.
Muumini huyo alidai kwamba Maaskofu hao wasiingie kwani mgogoro uliopo ndani ya kanisa hilo kwani utamalizwa na waumini wenyewe na kwamba kuwepo kwao kungechochea vurugu zaidi.
Wakati Maaskofu wakipinga amri hiyo, waumini ambao walikua ndani ikiwa ndio wanaanza ibada ya kwanza walisikia na ndipo wachache wakatoka nje, wengine wakishinikiza Maaskofu hao waingie huku wengine wakitaka waondoke.
Mabishano makali yaliyofuatiwa na ngumi yalizukabaina ya pande hizo mbili hadi maaskari ambao inaonekana walitonywa mapema hivyo kuwa karibu na eneo la tukio walipoingialia kati na kutuliza mtafaruku huo. 
Hata hivyo bado waumini walishinikiza kutoendelea na ibada hadi Maaskofu wa Kikanda waondoke eneo hilo na waumini kuamua kubaki nje badala ya kuendelea na ibada, wengine wakitimka kwa kuhofia vurugu zaidi.
Baadhi ya waumini waliokuwa wakiondoka walissikika wakisema kuwa heri wahamie makanisa mengine kwani hamkani si shwari tena kanisani hapo.
Inasemekana Maaskofu hao wa Kikanda walifika kanisani hapo ili kuamuru Baraza la Kanisa hilo kuvunjwa ili kupisha uchaguzi mwingine wa viongozi baada ya Baraza hilo kutuhumiwa kufuja pesa za kanisa kwa kutowasilisha mahesabu kwa waumini.
Udondozi zaidi umebaini kwamba kanisa hilo limekuwa na vurugu za chini chini ambazo inasemekana zimeanzia makao makuu ya Kanisa hilo, huku ikielezwa kwamba kumeibuka kambi mbili za uhasama, moja ikishinikiza viongozi waliopo sasa waondoke madarakani huku nyengine ikiunga mkono viongozi hao wabaki hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika.
Chimbachimba zaidi toka kwa shuhuda huyo zimebaini kwamba tatizo la msingi ni uongozi uliopo madarakani kutowasilisha mahesabu yaliyokaguliwa (Audited Account) ya Kanisa hilo lenye vitega uchumi vingi ikiwemo Chuo Kikuu cha Theophile Kisanji.
Mgogoro ambao ulifikishwa hadi Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo viongozi waliamuriwa kufanya mahesabu hayo na leo kuyawasilisha kwa waumini wao jambo ambalo halikufanyika hadi vurugu zilipoibuka tena.

Mabondia waonyeshana kazi Mbagala

BONDIA Mussa Shuza kushoto akioneshana umwamba na Dackson Kawiani wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub mbagala rangi tatu Kawiani alishinda kwa point

Mabondia Ibrahimu Ahmed kushoto na Mohamed Kashinde wakioneshana ubabe wakati wa mpambano wao uliofanyika mbagala Dar es salaam Kashinde alishinda kwa point 

Bondia Hassani Kidebe kushoto akioneshana ufundi wa kutupa makonde na Shabani Mtengela wakati wa mpambano wao Mtengela alishinda kwa point mpambano.