STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, August 17, 2013

Tabata washinda tena taji la Redd's Miss Ilala


Miss Tabata 2013, Dorice Mollel akitabasamu baada ya kuvikwa taji la shindano la Redd's Miss Ilala 2013
Miss Tabata 2013, Dorice Mollel (kati) akiwa na warembo wenzake waliongia Tatu Bora baada ya kushinda taji la Redd's Miss Ilala 2013 usiku wa jana.


Mshindi wa Redd's Miss Ilala akiwa na tabasamu pana baada ya kutwaa taji hilo
MISS Tabata 2013, Dorice Mollel  (22) usiku wa kuamkia leo aliwashinda warembo wengine 13 na kunyakua taji la Redds Miss Ilala 2013 katika shindano iliyofanyika kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar es Salaam.
Dorice alimrithi Noela Michael ambaye alishinda taji hilo mwaka jana pia akitokea kitongoji hicho cha Tabata.
Dorice alizawadiwa 1.5milioni/-, na mshindi wa pili Alice Isaac (Dar City Centre) alipata 1milioni /-.
Mshindi wa tatu katika shindamo hilo ni Clara Bayo (Dar City Centre) ambaye  alizawadiwa 700,000/-. Mshindi wanne Pendo Lema (Tabata) alizawadiwa 400,000/- na watano  Shamim Mohamed alipata 300,000/-.
Mrembo Juanita Kabunga kutoka Tabata alizawadiwa 500,000/- baada ya kushinda Miss Talent na Kabula Kibogoti pia kutoka Tabata alishinda taji la Miss Rio and Spa na kuzawadiwa 200,000/- na ajira ya kudumu kwenye kampuni hiyo.
Warembo waliosalia kila moja alipata kifuta jasho cha 200,000/-.
Warembo hao ni Clara Paul, Anna Johnson, Irene Mwelolo, Rehema Mpanda,  Martha Gewe, Diana Joachim, Natasha Mohamed,  Kazumbe Mussa, Kabula Kibogoti na Juanita Kabunga. 

KONYAGI YAWAPIGA MSASA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (kushoto), akieleza mafanikio ya TDL ikiwa ni pamoja jinsi inavyolipa kodi serikalini ambapo kwa mwezi hulipa sh. bil. 7.  Mgwassa alikuwa akizelezea mafanikio hayo wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari ya kuwajengea uwezo wa kuthamini bidhaa za ndani leo kwenye Hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.Kulia ni mgeni rasmi katika semina hiyo, Mbunge wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania, Mussa Zungu.
 Mgeni rasmi katika semina hiyo, Mbunge wa Jimbo la Ilala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, akitoa pongezi kwa Mkurugenzi wa TDL, David Mgwassa kwa kukipatia mafanikio makubwa kiwanda hicho. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

 Mkurugenzi wa Masoko wa TDL, Joseph Chibehe 9kulia) akielezea mbele ya wahariri, historia ya kinywaji cha Konyagi.
 Baadhi ya wahari walioalikwa kwenye semina hiyo, wakisikiliza kwa makini wakati Chibehe aielezea historia ya TDL.
 Seheumu ya wahariri wa vyombo vya habari waliohudhuria semina hiyo
 Baadhi ya wahari walioalikwa kwenye semina hiyo, wakisikiliza kwa makini wakati Chibehe aielezea historia ya TDL.
 Picha juu na chini ni baadhi ya wahariri na wanahabari wakiwa katika semina hiyo iliyoandaliwa na TDL.

 Mgeni rasmi, Mussa Zungu 9katikati waliokaa) akiwa na MD wa TDL , Mgwassa, Mkurugenzi wa Masoko, Chibehe katika picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari nchini.
 MD wa TDL, Mgwassa (katikati) akimuaga Mussa Zungu. Kulia ni Chibehe.
Baadhi ya wahariri walioalikwa kwenye semina hiyo, wakisikiliza kwa makini wakati Chibehe aielezea historia ya TDL.

Momba, Mwamakula kumaliza ubishi kesho katika ndondi


Bondia Sadiki Momba kushoto akitunishiana misuli na Amos Mwamakula baada ya kupima uzito jana  kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa Taifa PST utakaofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa friends corner ManzeseDar es salaam

Bondia Sadiki Momba kushoto akitunishiana misuli na Amos Mwamakula baada ya kupima uzito jana  kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa Taifa PST utakaofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa friends corner ManzeseDar es salaam 
Bondia Habibu Pengo kushoto akitunishiana misuli na Iddy Mkwera baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofaNyika Manzese Dar es salaam siku ya jumapili.

Pendekeza blogu yetu iingie katika kinyang'anyiro cha Tuzo za Blogs Tanzania 2013



WASOMAJI  wa blogu hii ya MICHARAZOMITUPU unaombwa uipendekeza kuingia kwenye shindano la kila mwaka la Tuzo za Blogu Tanzania 'Tanzania Blogs Award'.
Tuna ujumbe kwako kupitia email kwenda: nomination@bloggersassociationoftanzania.com au tanzanianblogawards@gmail.com. Ukishapendekeza jina la blogu hii ya micharazomitupu.blogspot.com
Katika sehemu ya Subject unaandika jina la blogu unayopendekeza iingie kwenye shindano hilo nayo ni micharazomitupu.blogspot.com kisha katika sehemu ya ujumbe andika vipengele vya;
Best Entertainments
Best Sports Blog
Best General Blog

Kwa maelezo zaidi kwa shindano hilo ambalo limeanza Agosti 17, 2013 mpaka Agosti 30 tembelea http://tanzanianblogawards.blogspot.com. 
Tunawategemea  na iwapo tutapitishwa msisite kutupigia kura kuanzia Sept8-14, 20013.

Tanzania yazidi kuchafuka duniani kisha biashara ya dawa za kulevya, mwingine anaswa Hongkong

Vitu vinadodaiwa kuwa 'unga' ukiwa umefichwa kwenye mashine
KWA mara nyingine Tanzania imeendelea kucahfuka mbele ya uso wa dunia kutokana na raia wake kujihusisha na dawa za kulevya, baada ya Mbongo mwingine kunaswa na  maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege  akiingiza 'unga' aliouficha kwenye chuma cha mashine alichokuwa akisafiri nacho kutokea Tanzania.
 
Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.

Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.

Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini. 





Kifungo cha miaka 40 chamsubiri Mbongo aliyeingiza 'Unga' Marekani

Mtu aliyetambuliwa kuwa Mtanzania yumo hatarini ya kufungwa miaka 40 jela nchini Marekani baada ya kukamatwa na dawa za kulevya dawa aina ya heroin zikiwa ndani ya kompyuta pakato (laptop).

Shirika la habari la The Associated Press tarehe 15 Agosti 2013 limechapisha habari hiyo na kusema kuwa Mtanzania huyo ametambulika kwa jina la Joseph Mackubi (miaka 33), alikamatwa katika kiwanja cha ndege cha LAX mjini Los Angeles akitokea Nairobi.

Mackubi alipandishwa atika kizimba cha mahakama (Federal court) jijini LA na kusomewa mashitaka siku ya
Jumatano, Agosti 14, 2013 ambapo alikiri kukutwa na dawa hizo zilizokuwa zimefichwa kwenye laptop isiyofanya kazi.

Inaripotiwa kuwa maafisa waligundua uzito usio wa kawaida wa laptop aliyokuwa nayo Mackubi mwezi Oktoba mwaka jana walipompekua.  Walipompeleka kumpekua kwa mara ya pili kwa kina zaidi, walijaribu kuwasha komyputa hiyo bila mafanikio, na kugundua kuwa ilikuwa ina alama za kufunguliwa awali (tampered with), na ndipo walipoifungua kabisa ndani ambapo walikuta gramu 800 za heroin zimefichwa.

Mackubi alisema alikuwa akutane na mwanamke anayeishi jimboni Alabama, ambaye walifahamiana kwenye mtandao wa internet. Maafisa wamesema kuwa Watanzania ni miongoni mwa watu wanaokamatwa LAX wakisafirisha dawa za kulevya kwa njia hiyo.

Hukumu impasayo Mackubi imepangwa kutolewa tarehe 11 Septemba.

Uongozi wa Shule awatolea uvivu wazazi, kisa...!


Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Makumbusho
UONGOZI wa Shule ya Msingi Makumbusho umewajia juu wazazi kwa tabia yao waliyonayo ya kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha hasa kwa watoto wao wasiojua kusoma na kuandika na kutishia kuanzia mwakani hawatapokea mtoto yeyote ambaye hajapitia shule ya awali.
Pia uongozi huo umesema kuanzia sasa shule yao itaanza kuwatimua wanafunzi wote watakaokuwa na maendeleo duni darasani ili kuiepushia aibu shule yao.
Mwalimu Mkiuu wa Shule hiyoi,  Mama Lyimo akizungumza na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo katika kikao cha pamoja kilichofanyika jan Ijumaa, alisema uongozi wao wamekuwa na wakati mgumu kwa wazazi wasiopenda kuotoa ushirikiano kwa walimu.
Mwalimu Lyimo alisema walimu wamekuwa wakitaka kuwasaidia baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika, lakini wamekuwa wakikosa ushirikiano kwa wazazi wa watoto hao pale wanapoitwa shuleni kujadiliana nao kitu kinachowakatisha tamaa.
"Wazazi mnatukatisha tamaa katika kuwasaidia watoto wenu kwa kushindwa kutupa ushirikiano pale mtunawapowaita tuje kujadiliana namna ya kuwainua watoto wenu ambao baadhi huwa hawajui kusoma wala kuandika," alisema.
Aliongeza walimu pekee yao hawawezi kuwasaidia watoto wenye matatizo hayo bila kupata ushirikiano kwa wazazi, hivyo akawahimiza baadhi ya wazazi kuwe wepesi kuitikia wito wa walimu wanapoitwa kwa sababu wakati mwingine ni faida kwao na watoto zao.
Alisema kwa idadi kubwa ya wanafunzi ndani ya darasa moja huwa vigumu kwa walimu kufanya kazi yake kwa ufasaha, hivyo kuwaita wazazi kunaweza kurahisisha kuwatatulia matatizo wanafunzi, lakini wazazi wamekuwa wazito kitu kinachowasononesha.
Mwl Lyimo alisema katika kuhakikisha shule yao inaepukana na kuwa na watoto wasiojua kusoma wala kuandika kuanzia mwakani hawatawapokea wanafunzi wa darasa la kwanza wasiopitia elimu ya awali kwa uthibitisho wa vyetu vya kuhitimu shule hizo.
"Hili ndilo tunalohisi ni suluhu ya kwanza ya kuepuka shule yetu kuwa na mambumbumbu, hatutapokea mwanafunzi wa kuanza darasa la kwanza bila kuwa amepitia masomo ya awali ambayo huwarahisisha kujua kusoma na kuandika," alisema.
Nao baadhi ya wazazi walitoa lawama zao kwa walimu ambao wanashindwa kuwafundisha watoto wao vyema darasani na kulazimisha wasome masomo ya ziada (twisheni) na kudai jambo hilo limekuwa likiwaumiza wanafunzi wenye uwezo mdogo wa kifedha.
"Kuwalazimisha watoto wabaki kwa ajili ya twisheni kunapelekea watoto wasio na uwezo wa kulipa masomo hayo kukosa masomo kikamilifu kutokana na ukweli walimu wamekuwa wakifundisha vyema huko kuliko darasani, hii siyo sawa, walimu badilikeni," alisema mmoja wa wazazi waliohudhuria kikao hicho.
Shule hiyo ya Makumbusho imekuwa na desturi ya kuitisha kikao pamoja na wazazi mara kwa mara kwa nia ya kujadili na kutathmini maendeleo ya wanafunzi na shule kwa ujumla.