STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 6, 2013

Amuua mpenzie akidai katumwa na mizimu

Mtuhumiwa wa mauaji Darrius Johnson
Msichana aliyeuwawa, Monica Gooden

MWANAUME mmoja wa mjini Florida, Marekani amefikishwa mahakamani akikabiliwa na shitaka la kumuua rafiki wake wa kike kwa kumchoma visu mara kadhaa sehemu mbalimbali mwilini.
Kijana huyo, Darrius Johnson, 22, anatuhumiwa kumuua rafiki huyo wa kike aliyetambulika kwa jina la Monica Gooden, 23, katika nyumba waliokuwa wakiishi pamoja kwenye mji mdogo wa Lauderhill, Florida.
Mtuhumiwa anadaiwa kufanya mauaji hayo baada ya kugundua kuwa rafiki wake huyo wa kike alikuwa amezaliwa katika tarehe za nyota ya Ng'ombe.
Baada ya polisi kupekua nyumbani kwake, waliukuta mwili wa Gooden ukiwa chumbani wanakolala ukiwa na majeraha kadhaa ya shambulio la kitu chenye makali kinachodhaniwa kuwa ni kisu.
Polisi walithibitisha pasipo shaka kwamba, marehemu alishambuliwa wakati akiwa amelala na hakuweza kujitetea kwa namna yoyote kuokoa maisha yake.
"Mwili wake ulikuwa na majeraha kadhaa ya kuchomwa na kisu. Tulimkuta akiwa kwenye wimbi kubwa la damu chumbani alikokuwa akilala na mpenzi wake," ilisema taarifa ya polisi.
Mtuhumiwa mwenyewe aliiambia polisi: "Niliamua kufanya hivyo ili kutoa sadaka kulingana na maelekezo ya nyota ya Ng'ombe."
Afisa wa Polisi wa kituo cha Lauderhill, Mike Butkus alithibitisha kumhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kutenda kosa hilo.
 Wakati akifanya tendo hilo halifu la mauaji, alisema: "Nilikuwa najisikia kama vile napigana na Dragon, na baadaye nilijiona nimekuwa mwanaume mpya ulimwenguni."
Alipokamilisha mauaji hayo, alisema alishindwa kujizuia hivyo akalazimika kwenda sehemu jirani na nyumbani kwake na kumvamia mwanamke mmoja mzee na akafanya hivyo hata kwa watu waliokuwa wakipita jirani, polisi walisema zaidi katika taarifa yao.
Hata hivyo, mmoja wa wanawake waliovamia alisalimia baada ya shuhuda mmoja kuona tukio hilo na hivyo kuingilia kati na kumpiga Johnson.
Kinachoshangaza zaidi ni kwamba, polisi baada ya kumuuliza mtuhumiwa wapi alipo Gooden, alijibu: "Yuko mbinguni."
Aliwaambia polisi kwamba baada ya kufanya tukio hilo la mauaji ya rafiki yake ya kike, sadaka nyingine aliyopanga kuitoa ni kumuua mama yake mzazi ambaye pia yuko kwenye nyota ya Ng'ombe.
Gooden alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Broward ambapo alikuwa akisoma mambo ya sanaa. Pia aliwahi kufanya kazi kwenye taasisi ya babysitter.
"Hata kama ningeishi kwa miaka milioni moja, sikuwahi kutegemea kama tukio hili lingemkuta mjukuu wangu wa kwanza. Bado naendelea kutafakari," alisema bibi wa mtuhumiwa Mamie William.
William alisema mara nyingi alikuwa akimsikia mjukuu wake Johnson akirumbana na mpenzi wake.
Kwa upande wake, Johnson anasema tukio alilofanya lilikuwa kwa lengo la kutekeleza kile alichosema kutumwa na mizimwi yake ambayo kila wakati ilikuwa ikimtaka kufanya hivyo.
Baada ya kubitiwa hospitali kufuatia majeraha aliyopata wakati akijaribu kumchoma kisu mwanamke mwingine, Johnson alisema kulikuwa na mabishano na mpenzi wake karibu usiku wote.
Johnson yuko kwenye jela ya Broward County akisubiri hukumu ya kesi ya mauaji ya kukusudia na kujeruhi.