STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, October 24, 2014

Sikia hii! Ruvu Shooting 'yamchimba' mkwara RPC Morogoro

Ruvu Shooting
RPC wa Morogoro-Leonard Paul
Msemaji wa Ruvu Masau Bwire
http://2.bp.blogspot.com/-MEnr9q0y77Q/UvZqEQrK58I/AAAAAAAAAh0/SEJunSkyKUM/s1600/IMG_0104.JPG
Kikosi cha Polisi Morogoro
KLABU ya Ruvu Shooting imemchimba mkwara na kumtaka RPC wa Morogoro, Leonard Paul awe mvumilivu wakati kikosi cha timu yake Polisi-Moro kitakapokuwa kikiadhibiwa uwanja wa Mabatini-Mlandizi katika pambano la Ligi Kuu dhidi ya vijana wao Mkenya Tom Oloba.
Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire ametamba kuwa kipigo walichowapa Ndanda Fc wakiwa nyumbani kwao Mtwara ndicho ambacho wataipa Polisi katika mchezo wao wa kesho akidai kuwa wapo kamili kuendeleza wimbi la ushindi wakiwa nyumbani baada ya kufanya vibaya katika mechi zao tatu za awali.
Bwire alisema wameona ni vema amtahadharishe mapema RPC Leonard kwa kumtaka awe mvumilivu wakati vijana wake watakapokuwa wakiadhibiwa na Ruvu kwani vijana wa Oloba wamesharekebisha makosa yaliyowafanya washindwe kupata ushindi katika mechi tatu za awali kabla ya kuzinduka kwa kuicharaza Ndanda mabao 3-1.
"Kwa kifupi pambano la kesho tumeshalimaliza na akili zetu zipo kwa mechi ijayo dhidi ya Coastal Union, ila tungependa kumtahadharisha RPC wa Morogoro, Kamanda Leonard Paul awe mpole na mvumilivu wakati vijana wake wakiadhibiwa na Ruvu, asije akaudhika kama walivyoudhika watu wa Mtwara wakati tukiwanyuka Ndanda mabao 3-1," alisema Bwire.
Msemaji huyo alisema kikosi chao chote kipo kamili bila ya kuwa na majeruhi hata mmoja, kitu ambacho kocha wao ameahidi ni nafasi nzuri ya kuendeleza maangamizi kwa wapinzani kabla ya kuwafuata Coastal  Union nyumbani kwao Mkwakwani Tanga.
Ruvu waliomaliza nafasi ya sita msimu uliopita wakilingana pointi na timu za Simba na Kagera Sugar waliokuwa juu yao, ina pointi nne mpaka sasa baada ya mechi nne ikishinda mchezo mmoja, kutoka sare moja na kufungwa mbili na inabanana na timu za JKT Ruvu, Simba na Prisons zote zikiwa na pointi nne na zikifuata kwenye msimamo wa Ligi inayoongozwa na Azam na Mtibwa zenye pointi 10. kila mmoja.

Mtibwa Sugar waenda Mbeya kulipa kisasi kwa Mbeya City

Kocha Mecky Mexime
Mtibwa Sugar
BENCHI la ufundi la Mtibwa Sugar limesema limeenda jijini Mbeya kwa lengo moja tu, la kuhakikisha timu yao inazoa pointi zote tatu mbele ya wenyeji wa Mbeya City katyika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara litakalochezwa Jumapili uwanja wa Sokoine jijini humo.
Mecky Mexime, kocha mkuu wa Mtibwa alisema kuwa, wanajua pambano hilo litakuwa gumu ila wamejiandaa kuhakikisha wanashinda ikiwa ni pamoja na kulipiza kisasi cha mabao 2-1 walichopewa katika mechi ya msimu uliopita kwenye uwanja huo.
Mexime alisema vijana wake wapo 'fiti' kwa mtanange huo ambao unasubiriwa kwa hamu kutokana na timu zote mbili kushindwa kufanya vema katika mechi zao zilizopita, Mtibwa ikisitishiwa wimbi lake la ushindi mfululizo kwa kulazimisha suluhu na timu iliyorejea ligi hiyo Polisi Moro wakati wapinzani wao Mbeya City wakilala 1-0 kwa mabingwa watetezi na kutibua rekodi yao ya kuwa timu isiyoruhusu bao.
"Tupo njiani kwa sasa, lakini tunaenda Mbeya kwa lengo moja ya kushinda, suluhu dhidi ya Polisi hatukuifurahia kwani imetunyima fursa ya kuendelea kubaki kileleni," alisema Mexime.
Aliongeza kuwa, anatarajia kupata upinzani mkali toka kwa wenyeji wao, lakini kwa namna walivyojiandaa anatarajia kuibuka na ushindi ili kuzoa pointi tatu na kulipa kisasi cha 2-1 walichopewa katika mechi ya marudiano ya msimu uliopita iliyochezwa jijini humo baada ya mchezo wao wa awali uliochezwa Manungu-Turiani kumalizika kwa kutoka suluhu.
Mabingwa hao wa zamani mpaka sasa wanalingana pointi 10 na watetezi Azam kila moja akiwa amecheza mechi nne na kushinda tatu na kutoka sare moja na ni kati ya timu tatu pekee ambazo hazijaonja vipigo msimu huu mpaka sasa, nyingine ikiwa ni Simba ambao wenyewe watacheza kesho na Prisons huku wakiwa hawajaonja ushindi wowote katika mechi zao nne walizoambulia sare.
Hata hivyo Azam wapo kileleni kwa faida ya herufi A, huku timu ya tatu inayowafukuzia ni Coastal Union ikifuatiwa na Yanga ambayo watakuwa na kibarua mjini Shinyanga dhidi ya wageni wa ligi hiyo Stand United. Coastal na Yanga kila moja ana pointi saba.

Maximo kutumia 4-4-2 na 4-2-3-1 kuiangamiza Stand Utd Shy Town

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/07/118.jpg
Maximo akiwa na msaidizi wake
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
KOCHA wa timu yaYanga, Mbrazil Marcio Maximo amepania kutumia mfumo wa 4-4-2 na 4-2-3-1 ili kupata ushindi dhidi ya wapinzani wao Stand United watakaoumana nao kesho kwenye uwanja wa Kambarage mjini hapa.
Aidha kocha huyo amesema wachezaji wake hawatakuwa na cha kujitetea endapo watashindwa kupata ushindi kwenye mchezo huo ambao umevuta hisia za mashabiki wengi wa soka wa Kanda ya Ziwa.
Maximo alisema, mashabiki wana matumaini makubwa na timu yaio hivyo wana kila sabbau ya kushinda ili kuwaopa moyo mashao hao hasa baada ya  kutoka suluhu dhidi ya mahasimu wao Simba.
"Kiufundi timu ipo vizuri na hakutakuwa na mabadiliko makubwa na kikosi kilichocheza na Simba, kikubwa hatupaswi kuwadharau wapinzani wetu. Nimewambia wachezaji wangu kuwa hatutaeleweka nikipoteza mchezo dhidi ya Stand United," alisema Maximo.
Alidokeza kuwa katika mchezo huo atatumia mfumo wa 4-4-2 na 4-2-3-1 kutokana na uwezo wa wapinzani wao.
"Kasi na uwezo wa wapinzani wetu ndiyo utanifanya niwe nabadilisha mfumokama ilivyokuwa  katika mchezo dhidi ya Simba, najua wapinzani wetu watakuwa kwenye uwanja wao na mbele ya mashabiki wao, ila Yanga ni timu kubwa na tutapambana kupata ushindi," alisema.
"tunataka kumiliki mpira na kutengeneza nafasi ambazo ni lazimawachezaji wazitumie. Nimefanyia kazi mapungufu niliyoyaona kwnye mchezo uliopita ambapo tulikosa umakini katika umaliziaji," aliongeza Mbrazili huyo aliyewahi kuwa kocha wa Taifa Stars.
Kikosi cha Yanga kiliwasili mjini hapa leo Ijumaa kikitokea mjini Dodoma walipokuwa wameweka kambi fupi na kucheza mechi ya kirafiki na CDA mechi iliyoisha kwa timu hizo kushindwa kufungana.
Yanga wanavaana na timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu ikiwa imekusanya jumla ya pointi saba kutokana na mechi nne ikipoteza moja dhidi ya Mtibwa Sugar, kushinda mbili dhidi ya Prisons-Mbeya na JKT Ruvu na kuambulia suluhu kwa watani zao Simba.

Morocco awarejesha Cannavaro, Mwadini, Morris, Znz Heroes

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/12/031.jpg
Cannavaro
http://static.goal.com/157000/157068_heroa.jpg
Morris
http://2.bp.blogspot.com/-uaSjh3bfIAw/ULe2MFz6wXI/AAAAAAAAYd8/8kuqYQ0yIQE/s1600/IMG_2147.JPG
Dua baada ya kufunga bao
http://4.bp.blogspot.com/-cMdZ2yQc2DM/UR5WnC7EoXI/AAAAAAAAAws/hzVMJfubpDo/s640/SAM_1110.JPG
Kocha Hemed Morocco
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman 'Morocco' amewarejesha kikosi nyota wa Yanga na Azam, Nadir Haroub 'Cannavaro', Aggrey Morris na mlinda mlango Mwadini Ali.
Akitangaza wachezaji watakafanya mazoezi kwa ajili ya kupata kikosi kitakachoshiriki Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka huu yatakayofanyika nchini Ethiopia, Morocco, alisema amewaita wachezaji hao  na wengine waliokuwa wametemwa katika michuano ya mwaka jana kwa nia ya kurejesha mshikamano kwa timu yao.
Morocco ameita jumla ya wachezaji 36 ambao watakauwa wanachunjwa mpaka kupata kikosi cha vijana 20 watakaoshiriki michuano hiyo itakayofanyika mwezi ujao.
Kikosi kizima kilichotangazwa na nyota huyo za zamani wa Tanzania na aliyekuwa kocha wa JKt Oljoro na Coastal Union ni pamoja na makipa; Mwadini Ali (Azam), Khalid Mahadhi (Mafunzo), Mudathir Yahya (KMKM) na Mwalimu Ali (Prisons).
Mabeki; Mohammed Othman (Polisi), Said Mussa (Mafunzo), Shafii Hassan (Zimamoto), Ismail Khamis (JKU), Adeyoum Saleh (Chuoni), Edward Peter (Hard Rock), Nadir Haroub 'Cannavaro' (Yanga SC), Nahoda Bakari( Polisi Moro), Aggrey Morris na Abdallah Sebo (Azam), Nassor Masoud ‘Chollo’ na Abdulaziz Makame (Simba SC), Mohammed Faki ( JKT Ruvu) na Khamis Ali (KMKM).
Viungo ni Mohammed Issa (Chuoni), Mohammed Abdulrahim, Ali Juma (Mafunzo), Amour Suleiman (Malindi), Makame Hamad (Zimamoto), Awadh Juma (Simba), Khamis Mcha 'Vialli', Mudathir Yahya (Azam), Abdulhalim Humoud (Sofapaka-Kenya) na Suleiman Kassim 'Selembe' (Polisi Moro).
Washambuliaji; Omar Juma (Hard Rock), Mohammed Seif (Dogomoro), Fasihi Hija (Malindi), Simai Masoud (Fufuni), Nyange Othman, Ibrahim Hilika (Zimamoto), Said Juma ‘Kizota’ (Yanga) na Ame Ali (Mtibwa Sugar).

Spurs yaua Europa League, Everton yabanwa, Fiorentina yashinda

Harry Keane akifunga moja ya mabao yake ya 'Hat Trick'
Entiene Couples akimiliki mpira
Wachezaji wa Fiorentina wakishangilia bao lao la dakika ya 38 lililowapa ushindi ugenini
Samuel Eto'o akijaribia kuipigania Everton mbele ya Lille bila mafanikio timu hizo zilitoka 0-0
VIJIGOO wa London, Tottenham Hotspur usiku wa kuamkia leo ilifanya 'mauaji' ya kutisha baada ya kuikung'uta Asteras Tripolis ya Ugiriki kwa mabao 5-1 katika mechi ya makundi ya Ligi Ndogo ya Ulaya, huku Everton ikibanwa ugenini.
Spurs ambayo imekuwa ikichechemea kwenye Ligi Kuu ya England, ilipata ushindi huo ikiwa nyumbani kwa mabao yaliyofungwa na Harry Kane aliyefunga 'hat trick' katika dakika ya 13, 75 na 81, wakati Erik Lamela 'Rabona' aliyesajiliwa kwa Pauni Mil. 30 alifunga mengine mawili katika dakika ya 29 na 66.
Wageni walipata bao lao dakika ya 89 kupitia kwa mtokea benchi, Jeronimo Barrales aliyefunga kwa mpira wa adhabu na kufanya Spurs kumaliza mechi hiyo ya kundi C wakiwa wababe kwa mabao 5-1.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo Besiktas iliisasambua Partizan nyumbani kwao kwa mabao 4-0, huku kwenye mechi za makundi mengine Everton ikiwa ugenini ililazimishwa shuluhu na Lille ya Ufaransa.
Matokeo mengine ni kama yafuatavyo;
Metalist 0-1 Legia Warszawa, 
Krasnodar 2-4 Wolfsburg  
Rijeka   3-1  Feyenoord
Standard Liège  0-0   Sevilla
Lille     0-0    Everton 
Slovan Bratislava     0-3   Sparta Praha 
Young Boys     2-0     Napoli   
AaB     3-0     Dynamo Kyiv   
Steaua Bucureşti     2-1  Rio Ave  
Dinamo Minsk     0-0     Guingamp      
PAOK     0-1     Fiorentina     
Trabzonspor     2-0     Lokeren     
Villarreal     4-1     Zürich     
Borussia M'gla…     5-0     Apollon    
Torino     2-0     HJK    
Club Brugge     1-1     København     
Celtic     2-1     Astra     
Salzburg     4-2     Dinamo Zagreb     
Estoril     1-2     Dinamo Moskva     
PSV     1-1     Panathinaikos    
Internazionale     0-0     Saint-Étienne      
Dnipro Dniprop…     0-1     Qarabağ

Ronaldo azuga akijiandaa kuwavaa Barcelona katika El Classico

NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema hawazii suala la kushindwa kwake kuvunja rekodi ya mabao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inayoshikiliwa na Raul aliyokuwa na uwezo wa kufanya hivyo wakati walipoiangushia kipigo Liverpool  kwa madai kuwa anaweza kuivunja katika mechi nyingine.
Ronaldo alibakisha goli moja kuifikia rekodi ya Raul baada ya kufunga bao lake la 70 katika ushindi wa 3-0 kwenye Uwanja wa Anfield, idadi ambayo inamtangulia Messi kwa bao moja.
Mreno huyo alikuwa na nafasi nyingi za kuweza kuifikia na hata kuipita rekodi hiyo lakini alibaniwa na kipa wa wenyeji, Simon Mignolet.
Lakini hakuwa mnyonge kutokana na jambo hilo hata hivyo, na akaiambia Sky Sports: "Sihofii kuhusu rekodi. Najua nitaipiku tu, kama haijawa leo, basi itakuwa katika mechi nyingine. Messi ameikaribia pia."
Ronaldo ambaye alikuwa hajawahi kufunga goli Anfield tangu alipokuwa akiichezea Manchester United, alisema: "Ilikuwa ni 'spesho', goli langu la kwanza hapa Anfield na najivunia kwa hilo. Tumepata pointi tatu, ilikuwa ni babkubwa."  
Mshambuliaji huyo aliye katika kiwango cha juu ambaye sasa amefunga magoli 20 katika mechi 13 za michuano yote msimu huu, alisema inawezekana wao wakawa timu ya kwanza kutetea taji la Klabu Bingwa Ulaya licha ya kwamba haitakuwa rahisi.
Mshambuliaji huyo kesho anatarajiwa kuiongoza timu yake katika pambano la kwanza la El Classico kwa msimu huu dhidi ya Barcelona, ambayo nyopta wake Lionel Messi anatarajiwa kuvunja rekodi ya mabao ya La Liga kama atafanikiwa kufunga katika mchezo huo zaidi ya bao moja.