STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 23, 2013

Hii ndiyo taarifa rasmi ya Yanga juu ya kocha Brandts

http://4.bp.blogspot.com/-YB6d8UvPgYA/UP-5jvNxjFI/AAAAAAAAjb8/alnHLb8rjrE/s1600/BIN+KLEB.jpg
UONGOZI wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
 
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
 
Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
 
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
 
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
 
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.
 
Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix “Minziro”.
 
Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha.
 
Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
 
Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.

Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.
DAR ES SALAAM
23 Disemba, 2013
 

Yanga, Simba waingia Mil. 422

PAMBANO la Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba lililochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 limeingiza sh. 422,611,000.

Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.

Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.

Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.

Mwesigwa ndiye Katibu Mkuu TFF?

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/mweigwachequetbl.jpg
Celestine Mwesigwa
HABARI zilitufikia hivi karibuni zinasema kuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga, Celestine Mwesigwa ndiye Katibu Mkuu  mpya wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) na Katibu Mkuu wa Simba Evodias Mtawala ameukwaa ukurugenzi ndani ya shirikisho hilo.
Hata hivyo taarifa rasmi juu ya jambo hilo litawekwa bayana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi kesho atakapotangaza safu mpya ya waajiriwa wa shirikisho hilo ikiwa ni mwezi mmoja na ushei tangu ashinde Urais katika Uchaguzi Mkuu wa TFF uliofanyika Oktoba 27.
Ila MICHARAZO inazo habari kwamba Mwesigwa aliyetimuliwa kihuni Yanga, ametwaa nafasi hiyo akiwashinda waombaji wengine. Ila vuteni subira hadi hiyo kesho mpate uhakika wa jambo hili toka mdomoni mwa Malinzi mwenyewe.

Kimenuka Yanga! Brandts atimuliwa kisa 3-1 za Simba


KWA wanaokumbuka jana blog hii iliwadokeza kuwa kulikuwa na fununu kwamba Yanga kupitia Mwenyekiti wake, Yusuf Manji angemfuta kazi kocha wa Yanga, Ernie Brandts.
Ingawa Manji alichomoa kiaina kusema moja kwa moja kwamba Brandts ndiyo basi tena Jangwani, na kuonekana kama anamtetea, imebainika kuwa Mholanzi huyo hana chake tena Yanga.
Mchana huu klabu hiyo ya Yanga ilitangaza kusitisha mkataba na kocha wake Ernest Brandts baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, mkataba wa Brandts ambaye ni raia wa Uholanzi umesitishwa rasmi leo hii asubuhi na ameshakabidhiwa barua ya kumtaarifu juu ya hali hiyo.
“Tumesitisha mkataba na kocha wetu na ameshakabidhiwa barua yake, huo ni uamuzi wa uongozi mzima wa Yanga, kila kitu kimeenda sawa katika kuachana naye,” alisema Kizuguto.
Tetesi za Brandts kutimuliwa zilizagaa jijini Dar es Salaam tangu jana muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji kwamba hata kama klabu itaamua kuachana na kocha huyo itafuata taratibu zote.
Uamuzi huo wa Yanga unaonekana pia kuchagizwa zaidi na kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mchezo maalum wa kirafiki maarufu kama Nani Mtani Jembe uliochezwa wikiendi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Breaking News! Lunyamila mahututi tumuombeeni
akiishuhudia Yanga ikichehzea kichapo cha mabao 3-0 mjini Morogoro toka kwa Mtibwa Sugar msimu uliopita

WINGA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Edibily Lunyamila leo hii asubuhi amekimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kusumbuliwa na kifua na sasa anapumua kwa msaada wa mashine.

Mtandao huu ulifanikiwa kufika hospitalini hapo muda mfupi baada ya winga huyo kukimbizwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa tangu jana usiku akiwa nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam.

Shaffihdauda.com imemshuhudia Lunyamila akiwa amelala kitandani katika wodi ya wanaume namba namba 5 kitanda namba 16 katika hospitali hiyo ya rufaa ya Kinondoni.Daktari Madirisha Pascal anayemuhudumia winga huyo wa zamani, Lunyamila anasumbuliwa na tatizo la kifua ambalo linamfanya ashindwe kupumua vizuri.

“Kama mnavyomuona anapumua kwa msaada wa mashine na bado tunaendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini nini kinachomsumbua zaidi,” alisema Pascal.

Mmoja wa ndugu wa Lunyamila, Lameck John alisema kwamba, mchezaji huyo wa zamani alianza kujisikia vibaya jana Jumapili na leo asubuhi hali yake ilibadilika ndipo walipomkimbiza hospitali.
 Lunyamila alivyokuwa enzi anaichezea Yanga..
“Alianza kulalamika hawezi kupumua na kifua kinamsumbua pia mbavu zilikuwa zikimuuma, baada ya majibu ya vipimo tutajua kinachomsumbua zaidi,” alisema Lameck.
Kutokana na hali iliyoonekana hospitalini hapo, Lunyamila anahitaji huduma ya haraka ili kuweza kuokoa uhai wake kwani anapumulia mashine akiwa katika sehemu yenye joto kali hivyo anapambana na vitu vingi kwa wakati mmoja... Taarifa za kiuchunguzi zilizofanywa na mwandishi wetu zimebaini Lunyamila anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo. ''Nilikuja jana hospitali ya mwananyaala ikagundulika moyo wangu umekuwa mkubwa,hivi sasa naenda muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi nikifika na kukutana na daktari nitakujulisha '' ilipofika mchana wa leo mwandishi alipokea simu kutoka kwa Lunyamila akimwambia ameambiwa arejee tena hospitali ya Mwananyamala.
SHAFII Dauda

Inter Milan waikausha AC MIlan Seria A, Muntari akilimwa RC jioni

AC Milan's forward Mario Balotelli kicks the ball during the Italian Serie A football match Inter Milan vs AC Milan at San Siro Stadium in Milan on December 22, 2013
Mario Balotelli akikosa bao la wazi langoni mwa Inter Milan
AC Milan's French defender Kevin Constant fights for the ball with Inter Milan's Argentinian forward Rodrigo Palacio during the Italian Serie A football match on December 22, 2013
Inter Milan's Argentinian forward Rodrigo Palacio celebrates after scoring during the Italian Serie A football match Inter Milan vs AC Milan at San Siro Stadium in Milan on December 22, 2013
'Muuaji; akishangilia bao lake
BAO lililofungwa na Rodrigo Palacio dakika nne kabla ya kumalizika kwa pambano la watani wa jadi wa mji wa Milan, liliisaidia Inter Milan kupata ushindi muhimu dhidi ya mahasimu wao Ac Milan katika mechi ya Ligi Kuu ya Italia, Seria A lililochezwa usiku wa kumakia leo.
Licha ya kipigo hicho pia, Milan ilipata pigo dakika za lala salama wakati kiungo wake, Sulley Muntari alipolimwa kadi nyekundu wakati mchezo ukielekea kumalizika.
Palacio raia wa  Argentina aliifungia Inter bao hilo akimalizia kazi nzuri ya Fredy  Guarin na kuzidi kuicha Milan izidi kuchechemea kwenye ligi hiyo ikishika nafasi ya 13, huku wapinzani wao kwa ushindi huo wamekwea hadi nafasi ya tano ikifikisha pointi 31.
Kipigo hicho kimekuja baada ya Milan kupata sare mfululizo katika mechi zake za hivi karibuni katika ligi na kuliacha benchi la ufundi la mabingwa hao wa zamani wa Ulaya wakiweweseka kujiweka sawa kabla ya kuwakuta yaliyowakuta makocha wa klabu nyingine waliotimuliwa.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Livorno ililala nyumbani kwa mabao 2-1 dhidi ya Udinese, Cagliari ililazlimishwa sare ya 1-1 na Napoli kwa mechi zilizochezwa Jumamosi.
Mechi zilizochezwa jana Bologna ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Genoa, Atlanta ikalala kwa mabao 4-1 nyumbani kwake mbele ya mabingwa watetezi Juventus, huku Hellas Verona ikiishindilia Lazio kwa mabao 4-1.
Nayo Roma iliendeleza mauaji kwa kuilaza Catania kwa mabao 4-0,  Sampodoria na Parma zikitoka sare ya 1-1 na Fiorentina ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Sassuolo na Chievo Verona ikilala ugeninikjwa mabao 4-1 toka kwa Torino.

Everton yaua ugenini, Chelsea ikiifuata Arsenal Emirates leo