STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 23, 2013

Kimenuka Yanga! Brandts atimuliwa kisa 3-1 za Simba


KWA wanaokumbuka jana blog hii iliwadokeza kuwa kulikuwa na fununu kwamba Yanga kupitia Mwenyekiti wake, Yusuf Manji angemfuta kazi kocha wa Yanga, Ernie Brandts.
Ingawa Manji alichomoa kiaina kusema moja kwa moja kwamba Brandts ndiyo basi tena Jangwani, na kuonekana kama anamtetea, imebainika kuwa Mholanzi huyo hana chake tena Yanga.
Mchana huu klabu hiyo ya Yanga ilitangaza kusitisha mkataba na kocha wake Ernest Brandts baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, mkataba wa Brandts ambaye ni raia wa Uholanzi umesitishwa rasmi leo hii asubuhi na ameshakabidhiwa barua ya kumtaarifu juu ya hali hiyo.
“Tumesitisha mkataba na kocha wetu na ameshakabidhiwa barua yake, huo ni uamuzi wa uongozi mzima wa Yanga, kila kitu kimeenda sawa katika kuachana naye,” alisema Kizuguto.
Tetesi za Brandts kutimuliwa zilizagaa jijini Dar es Salaam tangu jana muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji kwamba hata kama klabu itaamua kuachana na kocha huyo itafuata taratibu zote.
Uamuzi huo wa Yanga unaonekana pia kuchagizwa zaidi na kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mchezo maalum wa kirafiki maarufu kama Nani Mtani Jembe uliochezwa wikiendi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment