STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 15, 2013

Ngumi kuipamba Ghana Mei 3


Nchi ya Ghana ambayo ni moja ya nchi zenye vipaji vingi vya wanamichezo mahiri na majina makubwa hususan mchezo wa ngumi, itawaka moto tarehe 3, Mei wakati mabondia mahiri sita watakapogombania mataji ya IBF katika ubingwa mbalimbali.

Bondia atakayeanza kupanda ulingoni kufukisha moto huo ni “Mtoto wa Kijiweni” Albert Mensah ambaye amejizolea sifa kemkem za kupambana na mabondia mahiri duniani. Mensah yuko kwenye viwango vya IBF vya dunia na amewekwa namba 7 kwa ubora duniani katika uzito wa Welter.
 
                 Helen Joseph
Mbabe huyu atakumbana na bondia mwenye maringo na “Mtoto wa Mjini” Ben Odamettey ambaye amekulia katika viunga vya Jamestown katika kata ya Bukom jijini Accra, ambayo ni maarufu kwa kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na Poison Kotey. Wawili hawa watapambana kugombania ubingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa Junior Middleweight.
               Marriana Gulyas (kushoto)
 
Mpambano wa pili na unaongojewa kwa hamu kubwa ni ule wa mwanadada na mrembo kutoka Nigeria ambaye anaishi nchini Ghaba, Helen Joseph atakapombana na binti Mfalme kutoka Himaya ya Austrohungrian (Hungary) bi. Marianna Gulyas. Warembo hawa wanagombania mkanda wa IBF wa Mabara wa wanawake katika uzito wa unyoya (Featherweight) na moto mkubwa unategemewa kuwaka kutokana na umahiri wa warembo hawa wa kurusha makonde ulingoni.

Helen atakuwa anarudisha heshina yake baada ya kupoteza pambano la ubingwa wa dunia kwa mwanadada Dahianna Santana wa Dominican Republic mwezi wa Desemba mwaka jana. Hii ni heshima pekee kwa kina mama kutoka bara la Afrika wa kuonyesha umahiri wao kwa binti huyo wa Kifalme kutoka Hungary.
 
                                                          Albert Mensah (kulia)
Ndipo litakapokuja pambano la kukata na shoka kati ya mbabe kijana anayeinukia katika ulimwengu wa masumbwi nchini Ghaha na Afrika kwa ujumla bondia Issa Samir kutoka Ghana atakapopambana na mbabe kutoka kwenye jangwa la barafu la Siberia, bondia Robison Omsarashvili kutoka katika nchi ya Georgia ambayo ni moja ya nchi zilizokuwa kwenye Muungano wa Kishoshalisti wa Sovieti ya Urusi (USSR).

Ni nderemo na vifijo kwa Waghana na watu wote wa Afrika wakati mabondia hawa watakapo pambana kugombea mataji haya makubwa kabisa ya IBF na kuliwakilisha bara la Afrika katika ramani ya dunia.

Mapambano haya yanaandaliwa na kampuni ya GoldenMike Boxing Syndicate ya Accra, Ghana chini ya Henry Many-Spain na Michael Tetteh na yatafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Accra (Accra International Conference Center) na yatasimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi.

Simba, Azam wafunika mapto ya Yanga Oljoro




Na Boniface Wambura
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Aprili 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000 kutokana na watazamaji 11,458.
 Kiwnago hicho ni kikubwa kuliko pambano lililochezwa Jumamosi kati ya Yanga na JKT Oljoro ambapo mchezo huo uliingiza kiasi cha Sh Milioni 63.
Kwa pambano la jana, viingilio katika mechi hiyo namba 155 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,849,326.14.
Katika pambano la Yanga na Oljoro jumla ya Watazamaji 11,021 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Oljoro JKT iliyochezwa juzi (Aprili 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 63,170,000.

Viingilio katika mechi hiyo namba 156 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,853,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,636,101.69.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,552,501.25, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,531,500.75, Kamati ya Ligi sh. 4,531,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,265,750.37 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,762,250.29.