STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 18, 2015

Christian Bentekeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

Benteke, signed in a £32.5million deal this summer, jumps for joy and is congratulated by Dejan Lovren after scoring on his Anfield debut
Chistian Benteke akishangilia bao lake aliyoisaidia Liverpool kushinda usiku wa jana
Benteke lets out a roar and clenches his fist as he looks towards the fans after scoring in front of the Kop midway through the first halfBenteke embraces captain Henderson after the England international assisted the former Aston Villa man with his first Liverpool goalBAO pekee la straika mpya wa Liverpool, Christian Benteke usiku wa kuamkia leo limeiwezesha Majogoo hao wa Anfield kubuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu iliyopanda daraja ya Bournemouth.
Pambano hilo pekee la Ligi Kuu ya England lililochezwa usiku wa jana lilipigwa kwenye Uwanja wa Anfield na iliwachukua wenyeji dakika 27 kuandika bao hilo tamu baada ya Benteke kuunganisha pasi ya nahodha wake, Jordan Henderson.
Ushindi huo umeifanya Liverpool kukwea hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 6 sawa na vinara, Manchester City na Manchester United,huku wageni hao wa EPL wakikamata nafasi ya 19 wakiwa hawana pointi hata moja kama ilivyo kwa Sunderland wanaoburuza mkia.
Kipute hicho cha Ligi ya England kitandelea wikiendi hii na Jumatatu ijayo.

Maxime kutumia kasi ile ile iliyopita kufunika VPL

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/03/Mecky-Mexime1.jpg
KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa ile kasi waliyoanza nayo msimu uliopita ndiyo watakayoitumia msimu ujao kuweza kurejesha heshima ya mabingwa hao wa zamani.
Mtibwa iliianza ligi ya msimu uliopita kwa mkwara ikishinda mfululizo na kuongoza msimamo hadi ligi iliposimama Novemba 9, kisha kwenda kwenye Kombe la Mapinduzi na kufika fainali dhidi ya Simba.
Baada ya kichapo cha Simba cha mikwaju ya penalti, Mtibwa ilirudi katika ligi kuu kichovu na kupoteza mechi mfululizo, kiasi cha kuwa hatarini kushuka daraja kabla ya kuzinduka mwishoni.
Hata hivyo Maxime, alisema kwa namna anavyowaandaa vijana wake ana hakika mambo yatakuwa bambam katika msimu ujao ili kurejesha heshima ya klabu yao.
Maxime anasema ingawa hana maproo waka kufanya usajili mkubwa, lakini kurejesha baadhi ya majembe yake kama Issa Rashid 'Baba Ubaya', Said Bahanuzi na kipa Hussein Sharif 'Casillas' ni vitu vinavyompa jeuri kuamini msimu ujao wapinzani wao lazima wakae.
Mtibwa iliwahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 1999 na 2000 na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutwaa mataji mengi nje ya Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikipokezana miaka nenda rudi.
Pili ilikuwa ni klabu ya kwanza nje ya Dar kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo.

Machuppa azitonya klabu Ligu Kuu ya Bara

http://4.bp.blogspot.com/-Yb0UND2s9Dw/Tur0o7WeCwI/AAAAAAAABV4/Y0frlAm0-4A/s1600/MACHUPA%5B1%5D.jpg
STRAIKA wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Athuman Machuppa 'Smilling Killer' amezitaka klabu za Tanzania kuachana na ulimbukeni wa kuwapapatikia wachezaji wa kigeni na badala yake kutumia vipaji vilivyojazana nchini kuzijenga timu zao.
Machuppa alisema ni kweli wachezaji wa kigeni ni muhimu katika klabu, lakini sio wanaokuja nchini ambao wengi wao huwa ni wazee na walio na viwango vizivyotisha au kupitwa hata na wazawa.
"Nadhani klabu ziwekeze kwenye vipaji vya nyumbani, kuna wachezaji wengi wazuri Tanzania kama watatengenezwa na kuaminiwa, wageni waje lakini wenye viwango kama vya akina Emmanuel Okwi, Kipre Tchetche au wengine siyo kuletwa ilimradi tu na kulipwa fedha nyingi bila sababu," alisema Machuppa.
Mshambuliaji huyo aliyeweka maskani yake nchini Sweden kwa sasa akijiandaa kuwa raia wa nchi hiyo panapo majaliwa Mei mwakani, alisema hata idadi ya mapro katika vikosi vya klabu za Ligi kuu kutoka watano mpaka saba hakukuwa na sababu yoyote ya maana.
"Watano wangetosha tu, watatu wacheze na wawili wakae benchi, saba ni wengi na ninavyojua viongozi wa soka wa Tanzania walivyo na mzuka na wageni watalazimisha wote wacheze kama ruksa ilivyo, je wazawa wataonekana wapi, tutapata timu nzuri ya taifa vipi?"
"Watu wawekeze kwa vijana, Simba ilipata mafanikio ikiwa na wazawa waliojituma na kutumia vyema vipaji vyao, ila tusiwakatae wageni wanongeza chachu kama wakiwa ni wakali," alisema.

Yanga warudi Dar, wakitamba kuiva tarari kuiua Azam

MABINGWA wa Soka Tanzania Yanga inatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam leo Jumanne ikitokea Mbeya ilipoenda kupiga kambi ya siku kama 10 na kucheza mechi tatu za kirafiki na timu za jijini humo.
Yanga ilianza kuumana na Kimondo Fc na kuishinda kwa mabao 4-1 kabla ya kuicharaza Prisons-Mbeya kwa mabao 2-0 na kumaliza kazi kwa Mbeya City ikiichapa mabao 3-2.
Kikosi hicho kilinatarajiwa kutua leo na kuingia kambini moja kwa moja kusubiri pambano lao dhidi ya Azam ambao walijichimbia Zanzibar na leo nao watarudi jijini Dar es Salaam kusubiri pambano hilo la Ngao ya Jamii liatakalopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.
Kocha wa Yanga Hans Pluijm amenukuliwa kwamba kikosi chake kimeiva na kazi waliyoenda kuifanya Mbeya imemalizika na sasa ni kuonyesha makali yao hasa kuimarika kwa safu yao ya ushambuliaji.
Pluijm anasema washambuliaji wake wameonekana kukamilika kwa michezo hiyo mitatu na ana tumaini kubwa la kuilaza Azam ambayo ina rekodi ya kucheza mechi 11  mfululizo bila kuruhusu nyavu zake kuguswa, kati ya michezo 12 iliyocheza chini ya kocha Stewart Hall.
Mechi pekee iliyoruhusu wavu wao kuguswa kabla ya kukaza buti ni ile ya kirafiki dhidi ya Friends Rangers ambapo walishinda kwa mabao 4-2.
Baada ya hapo imekuwa ikiendelea kugawa dozi, lakini bila kuruhusu bao langoni mwake kuanzia kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyotwaa msimu huu kwa mara ya kwanza na hata mechi nyingine za kirafiki.
Azam licha ya kushiriki mechi za Ngao ya Hisani mara tatu haijawahi kushinda hata mara moja, mwaka 2012 ilipoteza mchezo kwa Simba kwa kupigwa mabao 3-2, kabla ya kulazwa bao 1-0 na Yanga mwaka uliofuata na mwaka jana ilipigwa mabao 3-0.
Redodi za Azam chini ya Hall baada ya kurudishwa kwa mara ya tatu;

Azam 4-2 Friends Rangers (kirafiki-Dar)
Azam 1-0 JKT Ruvu (kirafiki-Dar)
African Sports 0-1 Azam (kirafiki-Tanga)
Coastal Union 0-1 Azam (kirafiki-Tanga)
Azam 1-0 KCCA Uganda (Kagame-Dar)
Azam 2-0 Al Malakia Sudan Kusini (Kagame-Dar)
Azam 0-0 (pen 5-3) Yanga (Kagame-Dar)
Azam 1-0 KCCA-Uganda (Kagame-Dar)
Azam 2-0 Gor Mahia Kenya (Kagame-Dar)
KMKM 0-1 Azam (Kirafiki-Zanzibar)
Mafunzo 0-3 Azam (Kirafiki-Zanzibar)