STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 20, 2013

AZAM YAAPA KUTOFANYA MAKOSA LEO KWA WAMOROCCO

Kocha Msaidizi wa Azam, Kally Ongalla
KIkosi cha Azam

KOCHA Msaidizi wa Azam, Kally Ongala, amesema timu hiyo haitofanya makosa kama ya mechi dhidi ya Simba ya ligi kuu ya Bara Jumapili iliyopita, kwa kujaribu mfumo mpya uliopelekea kutoka sare ya 2-2, dhidi ya FAR ya Morocco katika mchezo wa kwanza wa kuwania kuingia hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika leo.
Azam ilitumia kwa mara ya kwanza mfumo wa 3-4-1-2 ambapo iliweka mabeki watatu, viungo wanne huku kukiwa na mchezaji mmoja aliyekuwa akiwasaidia washambuliaji wawili wa mbele.
Mtindo huo ni tofauti na inaotumia siku zote wa 4-2-3-1 na kuiwezesha si tu kushika nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya Bara lakini pia kuwa timu pekee ya Tanzania nzima iliyobaki imesiamama kwenye michuano hiyo ya kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ongala alisema kwenye mchezo dhidi ya FAR ambayo ni moja ya timu kubwa barani, watahitaji ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.
"Mfumo tulioutumia kwenye mchezo dhidi ya Simba tuliufanyia mazoezi kwa muda mfupi, lakini tumeona hatuuwezi kwa sasa," alisema.
"Mchezo wa kesho (leo) ni muhimu sana kwetu na lazima tupate ushindi hivyo tutatumia mfumo wetu wa siku zote.
"Tunaiheshimu timu hii kwa sababu ni timu nzuri na tumefanikiwa kupata mikanda yao ya video mitatu ambayo imetusaidia kuisoma na kujipanga jinsi ya kupamabana nao."
Alisema kuwa wachezaji wake wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na wanaamini mbele ya watanzania watafanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo.
Azam inakutana na FAR ikiwa ni siku chache tangu Taifa Stars iifunge Morocco 3-1 katika mechi ya michuano ya awali ya Kombe la Dunia kanda ya Afrika, kwenye Uwanja wa Taifa pia.
Kwa upande wake, Kocha wa AS FAR, Lahcen Ouabani, alisema kuwa hawaijui vizuri Azam lakini wanapata picha ya uwezo wa klabu hiyo kutokana na mafanikio ya soka la Tanzania kupitia timu ya Taifa 'Taifa Stars'.
"Hatuna ufahamu na Azam, lakini tunafahamu soka la Tanzania limekuwa kwa kiasi kikubwa ukiangalia timu ya Taifa ambayo tunaona jinsi inavyokuja juu," alisema kocha huyo ambaye klabu yake inarekodi ya kutwaa ubingwa wa Morocco mara 12 huku ikiwa imetwaa ubingwa wa Afrika mara moja mwaka 1985 na kombe la CAF mwaka 2005.
Timu hiyo imefika hatua ya kucheza na Azam baada ya kuitoa Al Nasri ya Libya kwa jumla ya magoli 2-1.

Uchaguzi wa CHANETA ni vita ya Kibira na ShyRose Dodoma