STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, October 15, 2014

Suarez akiri ilikuwa vigumu kukiri kosa la kumng'ata Chiellini

http://vertienteglobal.com/wp-content/uploads/2014/06/luis-suarez-anota-gol.jpghttp://img2.timeinc.net/people/i/2014/news/140707/luis-suarez-600.jpgSTRIKA nyota wa Barcelona, Luis Suarez amesema ilikuwa ngumu kukubaliana na ukweli wa kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini katika michuano ya Kombe la dunia nchini Brazil. 
Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay aliyejiunga na Barcelona akitokea Liverpool kwa kitita cha Pauni Mil. 75 alifungiwa miezi minne kutokana na tukio hilo. 
Akihojiwa strika huyo amesema alikuwa akiona vigumu kukubali alichokifanya kwani yeye ni binadamu kama walivyo wengine. 
Suarez, 27, amesema alikuwa hataki kumsikiliza yeyote au kuongea na yeyote kwa sababu alikuwa hataki kukubaliana na ukweli. 
Suarez alimuomba radhi Chiellini Juni 30 zikiwa zimepita siku sita toka afanye tukio baada ya Uruguay kushinda bao 1-0 dhidi ya Italia, msamaha ambao ulipokelewa na beki huyo na kueleza matumaini yake kama Shirikisho la Soka Duniani-FIFA lingeweza kumpunguzia adhabu hiyo. 
Kabla kuomba radhi Suarez alikanusha kwa kudai kuwa aliteleza bahati mbaya na usoni mwa Chiellini na kumuangukia jambo ambalo lilikuwa kama vichekesho kwani tukio hilo lote lilionekana katika picha za video.

Ronaldo alibeba Ureno, Ujerumani bado gonjwa Ulaya

http://i.ytimg.com/vi/TevIMI1W8NI/0.jpg
Ronaldo akishangilia bao lake lililoiua Denmark nyumbani kwao
http://www.101greatgoals.com/wp-content/uploads/2014/10/Screen-Shot-2014-10-14-at-23.54.46.png
Wachezaji wa Ireland wakishangilia bao lao la kusawazisha dhidi ya Ujerumani
http://www.theglobeandmail.com/sports/soccer/article21090950.ece/BINARY/w620/510260433_534397343.JPG
Mabingwa wa Dunia, Ujerumani wakihenyeka uwanjani dhidi ya Jamhuri ya Ireland
WAKATI Mabingwa wa Kombe la Dunia Ujerumani wakiwa hawajatulia, Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo usiku wa jana aliifungia timu yao ya Ureno bao pekee lililowapa ushindi dhidi ya Denmark uwanja wa ugenini katika mbuio za kuwania Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya Euro 2016.
Ujerumani inayouguza kichapo cha mabao 2-0 ilichopewa na Poland wikiendi iliyopita ilishindwa kulinda bao lake na kujikuta wakilazimishwa sare ya baoa 1-1 nyumbani na Jamhuri ya Ireland waliochomoa bao 'jioni'.
Ton Kroos aliiandikia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 71, lakini wageni walikaza msuli na kulirejesha dakika za nyongeza kupitia John O'shea na kufanya timu hizo kugawana pointi huku Poland wakilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Scotland ikiwa nyumbani.
Matokeo ya mechi nyingine ni kwamba Ureno ikiwa ugenini iliizabua Denmark kwa bao 1-0 lililofungwa na nahodha wake Cristioano Ronaldo katika dakika ya lala salama mashabiki wakiamini kuwa timu hizo zimetoka suluhu na kuifanya Ureno kufikisha jumla ya pointi tatu na kushika nafasi ya tatu.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo, Gibraltar imeendelea kutoa takrima baada ya kugongwa nyumbani mabao 3-0 na Georgia, San Marino kulazwa mabao 4-0 nyumbani na Uswisi, wakati Visiwa vya Faroe walilala nyumbani pia kwa bao 1-0 kutoka kwa Hungary, Finland ikafa pia nyumbani kwa mabaop 2-0 kw akipigo cha Romania na Ugiriki ikaendeleza unyonge kwa timu zilizocheza nyumbani jana kwa kulazwa mabao 2-0 na Ireland ya Kaskazini.

Kivumbi Afrika, Nigeria vs Sudan, Uganda v Togo hapatoshi!!

https://media.premiumtimesng.com/wp-content/files/2014/06/Eagles-Getty-images.jpg
Watetezi Nigeria
http://static.pulse.ng/img/incoming/origs3188111/4750486101-w980-h640/The-Sudanese-national-team.jpg
Sudan
http://www.goal-news.com/wp-content/uploads/2014/10/Guinea-vs-Ghana.jpg
Ghana
http://www.redpepper.co.ug/wp-content/uploads/2014/08/1.-EBOLA-OR-NOT-The-Cranes-are-ready-to-fly-to-Morocco-Picture-by-John-Batanudde-445x350.jpg
Uganda watacheka kama hivi leo kwa Togo
VUMBI la michuano ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON-2015 linatarajiwa kuendelea kutimka leo wakati mechi kadhaa zitapigwa kwenye mataifa mbalimbali barani Afrika.
Cameroon iliyong'ang'aniwa katika mechi iliyopita na Sierra Leone itakuwa nyumbani kurudiana na majirani zao hao, wakati Togo iliyoiduwaza Uganda The Cranes mjini Kampala itaialikia wapinzani wao hao katika pambano la kusisimua.
Mabingwa watetezi waliofumuliwa mjini Khartoum na wenyeji wao Sudan itajiuliza nyumbani huku Angola na Lesotho zitaonyeshana kazi mjini Luanda.
Mechi nyingine za makundi hayo zitakuwa kama ifuatavyo;
Ghana vs    Guinea
Zambia vs    Niger
Côte d'Ivoire vs    Congo DR   
Egypt vs Botswana   
Cape Verde Islands vs Msumbiji
Mali vs Ethiopia
Burkina Faso vs    Gabon
South Africa vs    Congo
Tunisia vs    Senegal   
Algeria vs    Malawi

Msiba! Muimbaji wa zamani Extra Bongo afariki dunia

http://1.bp.blogspot.com/-Ljz9e_U8Cps/TxiB-zJjIfI/AAAAAAAAPP4/ddcta9nBFz4/s400/P1191212.JPG
Suzuki enzi za uhai wake
http://2.bp.blogspot.com/-kIX-KBZtV84/TyWuKERucVI/AAAAAAAAPSo/YM6VjTOyW4k/s400/P1211580.jpg
Seleman Ramadhan Suzuki Sauti ya Malaika enzi za uhai wake
MWANAMUZIKI nyota wa zamani wa bendi za Mikumi Sound, Levent Musica na Extra Bongo 'Wana Next Level', Suleiman Ramadhani 'Suzuki Sauti ya Malaika' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua muda mrefu.
Kwa mujibu wa mwanamuziki mwenzake ambaye alikuwa akifuatilia afya yake kipindi akiugua, Ramadhani Mhoza 'Pentagone' ameiambia MICHARAZO, Suzuki amefariki akiwa nyumbani eneo la Magomeni Kagera, jijini Dar es Salaam na huenda akazikwa leo au kesho.
Pentagone aliyefanya kazi na mwanamuziki huyo aliyekuwa na uwezo wa kutunga, kuimba na kurapu  katika bendi za Levent Musica 'Wazee wa Kumuvuzisha' na Extra Bongo, alisema Suzuki alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari na alikuwa akitibiwa nyumbani kwa dawa za kienyeji.
"NIlitaka kukutaarifu kubwa swahiba yetu Suzuki hatunaye kwani amefariki usiku wa leo na kwa sasa tunaangalia mipango ya mazishi kwa kuwasiliana na ndugu zake wa karibu," alisema Pentagone ambaye kwa sasa anaiimbia African Stars 'Twnaga Pepeta'.
Enzi za uhai wake, Suzuki anayetokea Kigoma alitamba na bendi za Tabiora Jazz kabla ya kutua Morogoro katika bendi ya Mikumio Sound iliyowahi kutamba na albamu ya Mlinzi wa Godown kabla ya kuitua Levent Musica na baadaye yeye na wanamuziki wenzake watatu, Bob Kissa, Pentagone na Athanas Montanabe walihamia kwa mpigo Extra Bongo na kupakua albamua ya Mjini Mipango.
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi na MICHARAZO inatoa pole kwa wote walioguswa kwa namna moja au nyingine na msiba huio na kuwaomba kuwa na moyo wa Subira kwa kukumbuka kuwa 'Kila Nafsi Itaonja Mauti' na Sisi ni wa Mola na Kwake Hakika Tutarejea'.