STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 2, 2014

Hatem Ben Arfa atimkia Hull City kwea mkopo

Kiungo Ben Hatem wakati akiitumikia Newcastle United

MCHEZAJI Hatem Ben Arfa wa Newcastle United amejiunga na klabu ya Hull City kwa mkopo kwa kipindi kilicho baki cha msimu akimaliza safari yake ndani ya klabu yake ya Newcastle.
Ben Arfa amekuwa katika wakati mgumu katika kikosi cha Newcastle, licha ya mchango wake mkubwa tangu alipojiunga nao.

Blind atua Mashetani Wekundu mtazame katika uzi mpya

Daley Blind aliyekamilisha uhamisho United
KLABU ya Ajax imethibitisha kuwa Daley Blind amejiunga na  Manchester United.
Vilabu hivyo vimefikia makubaliano kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani wiki iliyopita ambapo United na Ajax walikubaliana ada ya uhamisho wake kufikia pauni milion £14.2 hii ikiwa ni baada ya mawindo ya muda mrefu ya mashitani wekundu.
Sasa imethibtishwa kua Blind atakuwa akiichezea United msimu huu baada ya kufanikiwa vipimo vya afya na kukubali maslahi ndani ya mshahara wake na kigogo hicho cha Premier League.
Blind ni mtoto wa nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi Danny, ambaye alikuwa ni msaidizi wa bosi wa United Louis van Gaal katika kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi katika michuano ya kombe la dunia na alianza kucheza soka kama mlinzi wa kushoto kabla ya kugeukia katika nafasi ya ulinzi wa kati katika klabu ya Ajax.

Miyeyusho kuyeyushana na Emilio Mkwakwani Nov 5

Miyeyusho na Emilio katika pozi
Wakitunishiana misuli
BONDIA machachari wa ngumi za kulipwa anayeshikilia mataji ya WBF na UBO, Francis Miyeyusho anatarajiwa kupanda ulingoni jijini Tanga kuzipiga na Mtanzania anayepigana nchini Kenyam Emilio Norfat.
Mabondia hao watapambana katika pigano la uzito wa Feather (kilo 57) siku ya Novemba 5 kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mratibu wa pambano hilo Anthony Rutta alisema maandalizi yameanza kwa kumalizana na mabondia hao wenye sifa zinazolingana kwa sasa katika medani ya ngumi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
"Mabondia Francis Miyeyusho na Emilio Norfat wanatarajiwa kupanda ulingoni kupigana kwa mara ya kwanza Novemba 5 na watasindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi siku hiyo," alisema Rutta.
Rutta alisema itakuwa mara ya kwanza kwa Miyeyusho kupanda ulingoni mkoani Tanga sawa na ilivyo kwa Emilio anayeshikilia nafasi ya pili nchini katika uzito huo wa Feather kati ya mabodia 60.
Emilio anashikilia kwa sasa taji la Afrika Mashariki na Kati la WPBC na rekodi zinaonyesha amecheza michezo 27 akishinda 23 na kupoteza minne, wakati Miyeyusho amecheza 51 ameshinda 38 na kupoteza 11 na kudroo miwili..
Pambano la mabondia hao litasimamiwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) ambalo Rutta ndiye Katibu Mkuu wake.

Falcao katika uzi mpya baada ya kutambulishwa Old Trafford

Falcao akiwa katika uzi mpya wa Mashetani Wekundu
Akiteta na Kocha msaidizi, Ryan Giggs

KLABU ya Manchester United imemtambulisha mshambuliaji wake mpya kutoka Monaco, Ramadel Falcao, huku baadhi ya mashabiki wakipigwa na butwaa na kitendo cha kuongezwa mshambuliaji kikosini badala ya mabeki safu inayoonekana kupwaya baada ya kuondoka kwa visiki Rio Ferdinand, Nemanja Vidic na patrci Evra.

Ndege yaanguka Serengeti na kuua abiria wote


Ndege iliyopotea mapema jana ikitokea Mwanza kuelekea Magadi nchini Kenya, imepatikana huko eneo la Serengeti Mara, na abiria wote watatu waliokuwa kwenye ndege hiyo imetaarifiwa wamekufa.

WWF yatoa mafunzo kwa watumishi wa Manispaa ya Kinondoni

http://www.tic.co.tz/media/kinondoni.jpgSHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la WWF, limeendesha mafunzo kwa watumishi wa idara mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni , kuhusiana na ueneaji wa hewa ukaa na matumizi sahihi ya nishati jadidifu nchini.
Mafunzo hayo yametolewa na Mratibu kutoka WWF.  Teresia Olemako aliyesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha  watumishi wa umma wanakuwa na ufahamu juu ya kukabiliana na madhara ya hewa ukaa na umuhimu wa kutumia nishati jadilifu.
Alisema mafunzo hayo yanahusu watumishi kutoka mikoa mitatu ambayo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha ambao majiji na miji yao imeingia katika shindano la kimataifa la kukabiliana na utunzaji wa mazingira ambalo litafanyika mwakani kwa kushirikisha nchi 18 duniani, Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza.
Olemako alisema juhudi za WWF kwa kushirkiana na ICLEI ni kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya nishati jadilifu kwa lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira ambao unachangia kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi kote duniani.
“WWF tumejipanga kushirikiana na watumishi wa mikoa hiyo niliyoitaja hapo juu kuhakikisha suala la kupunguza hewa ukaa na kuhimiza matumizi ya nishati jadilifu ni moja ya majukumu yao ambao watatumia mafunzo hayo kuwapatia wananchi elimu zaidi”, alisema.
Mratibu huyo wa Programu ya Nishati Jadilifu alisema mradi huo utakuwa ukitambaulika kwa kauli mbiu ya (Chakula, Nishati, Taka Ngumu na Maji) kutumika kama njia mbadala ya kukabiliana na uharibifu mazingira katika maeneo husika.
Alisema nishati jadilifu ikitumika ipasavyo itakuza uchumi wanchi pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na ukweli haina madhara na ipo kwa wakati wote hivyo ni vema kila mmoja kuwa balozi mzuri katika kuelimisha jamii.
Akizungumzia juu ya shindano hilo alisema ni vema kwa mikoa husika kufanya kila liwezekano ili kuweza kuleta ushindani wa kweli jambo ambalo linaweza kupelekea Tanzania kuibuka na ushindi ambao utakuwa kichochoe cha utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati jadilifu kuongezeka zaidi.
Aidha alisema kutokana na tathmin iliyofanywa na WWF inakadiriwa hadi mwaka 2025 jiji la Dar es salaam litakuwa na wakazi zaidi ya mil. 6.2 huku mahitaji ya kibinadamu yakiongezeka mara mbili zaidi ya sasa jambo ambalo linahitaji kufanyika maandalizi mapema kabla hali haijawa mbaya.
Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Injinia Mussa Natty, alisema kila idadi ya watu inapoongezeka, miundombinu na mahitaji ya kibinadamu pia huongezeka hivyo kuifanya jamii kuboresha mahitaji muhimu.
Natty alisema kutokana na hali hiyo WWF inapaswa kuongeza juhudi zaidi za kutoa elimu na kusaidia utekelezaji wa miradi ambayo inaweza kuwa na tija kwa Taifa na wananchi wake kwa vizazi vijavyo kwani kutokufanya hivyo kunaweza kuwa sababu ya kuleta mitafaruku mijini.
Mkurugenzi huyo alisema miradi kama hiyo ikiwa endelevu ni wazi kuwa kila mwanajamii atakuwa balozi mzuri wa kuhitaji mbadilo chanya ambao hayatamuathiri yeye na kizazi chache.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza WWF Tanzania kwa kushirikina na WWW Sweden kwa kuja na mradi huu na manispaa yangu ikawa moja wapo naamini tutaufanyia kazi vizuri kwani sisi Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla tumeathirika sana na mabadiliko ya Tania nchi”, alisema.
“Pia kila mmoja wetu ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es salaam, anahitaji kuwajibika katika sehemu yake ili kuhakikisha mahitaji muhimu ya kibinadamu yanapatikana jirani na jamii ili kuiondoa jamii katika hali ya umasikini unaosababisha ukataji na uharibifu wa misitu”, alisema.
Naye Mwanasheria wa Jiji, Philip Mwakyusa aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe alisema jiji limeupokea mradi kwa mikono yote na watatoa ushirikiano kwa WWF ili iweze kutekeleza mradi huo kwa mafanikio makubwa na ya yenye tija kwa jiji.

Arsenal yamnyakua Welbeck wa Man Utd

http://articles.squarefootball.net/.a/6a00e5521030508834019104738508970c-pi 
KOCHA Arsene Wenger amefanya jambo la maana katika kutatua tatizo la safu yake ya ushambuliaji baada ya kukubali kumsaini kwa Pauni Milioni 16 mshambuliaji wa England, Danny Welbeck.
Kocha huyo wa Arsenal, alikuwa Italia kuthibitisha ahadi ya kucheza mechi hisani, ameonyesha hisani inaanzia nyumbani baada ya kuwapiga bao Spurs kwa kumsaini mshambuliaji huyo wa Manchester United.
Welbeck, anayeondoka Old Trafford baada ya kushindwa kumvutia kocha Louis van Gaal tangu Mholanzi huyo awasili msimu huu, awali alitolewa kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kwa Pauni Milioni 3.
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akalazimishwa kuuzwa moja kwa moja aka pate mwanzo mzuri mpya na kuisaidia Arsenal kuilazimisha United kupunguza bei kutoka Pauni Milioni 18 walizotaka awali kabla ya mchezaji huyo kusaini Mkataba wa miaka mitano.

Ajali yaua baba, mtoto akiwa hoi kwa majeraha

MTU mmoja aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili  T. 495 ALM aina ya Nissan Pick Up amefariki dunia katika ajali mbaya, huku mtoto wake akijeruhiwa vibaya maeneo ya Nane Nane  jijini Mbeya usiku wa kuamkia jana majira ya saa saba za usiku.
Dereva huyo aliyefariki dunia amefahamika kwa jina la Boniface Mwasoba alifariki dunia baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka katika maeneo hayo ya Nane Nane achali iliyopelekea pia kujeruhiwa kwa mtoto wake anayefahamika kwa jina la Willy Boniface Mwasoba mwenye miaka 7 na mwanafunzi wa shule ya msingi Mkapa na amelazwa katika hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.
Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika japokuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini, lakini kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto kwa kuzingata sheria na alama za usalama wa barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.