STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 6, 2013

Samatta akwama tuzo za CAF, Yaya Toure, Tresor Mputu wapeta

Mbwana Samatta akikimbiza mtu uwanjani akiitumikia timu ya taifa
SHIRIKISHO la Soka Afrika limetoa orodha ya wachezaji 10 wa mwisho wa kuwania tuzo kuu ya Mwanasoka Bora Afrika na nyingine ya wachezaji watano wa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika kwa wanaocheza Afrika pekee, huku jina la Mfungaji Bora wa Kombe la Shirikisho, Mbwana Samatta likiwa halipo.
Mbwana anayeichezea TP Mazembe ya DR Congo na ambaye kwa sasa yupo Kenya na kikosi cha timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars alikuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika. 
Hata jivyo CAF imemchuja katika orodha ya mwisho iliyotangazwa ambapo orodha kamili ni kama ifuatavyo kwa wachezaji wanaowania tuzo kuu ni; Yaya Toure Ivory Coast na Manchester City.
Mshindi huyo wa tuzo ya BBC-2013, anashindana na Ahmed Musa CSKA Moscow na Nigeria, Asamoah Gyan na Ghana na Al Ain, Didier Drogba wa Ivory Coast na Galatasaray, Emmanuel Emenike wa Nigeria Fenerbahce, John Obi Mikel wa Nigeria na Chelsea, Jonathan Pitroipa wa Burkina Faso na Stade Rennes, Mohamed Aboutreika wa Misri na Ahly, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund, Vincent Enyeama wa Nigeria na Lille.
Kwa tuzo ya wachezaji wanaocheza Afrika, watano wanaochuana katika hatua ya mwisho ni Ahmed Fathy, Mohamed Aboutreika wote wa Misri na Al Ahly, Rainford Kalaba wa Zambia na Tresor Mputu wa DRC wanaoichezea TP Mazembe ya DRC na Sunday Mba wa Nigeria na Warri Wolves.
Mshindi atatangazwa katika hafla ya utoaji tuzo hizo Alhamisi ya Januari 9, mwakani mjini Lagos, Nigeria.

Kili Stars kuivaa Uganda Chalenji kesho

*Kenya vs Rwanda, Zambia na Burundi, Zanzibar yaaga

 Na Somoe Ng'itu, Nairobi
TIMU ya Taifa ya Uganda imemaliza mechi za hatua ya makundi kwenye michuano ya Kombe la Chalenji 2013 bila kupoteza mchezo wowote baada ya jana kuichapa Sudan kwa bao 1-0, hivyo sasa kesho itakutana na Kilimanjaro Stars katika mechi ya robo fainali itakayopigwa Uwanja wa Manispaa ya Mombasa.
Mechi nyingine ya robo fainali itakayopigwa kesho itamkutanisha mwenyeji, Kenya dhidi ya Rwanda ambayo jana iliichapa Eritrea kwa bao 1-0, hivyo kufuzu kama mshindwa bora (best looser) na kuifanya Zanzibar Heroes kuyaaga rasmi mashindano hayo.
Bao pekee la Rwanda katika mechi hiyo liliwekwa kimyani na Micheli Ndahinduka.
Mechi hizo za robo fainali zitaendelea Jumapili kwa Zambia inayoshiriki michuano hiyo kama timu alikwa ikivaana na Burundi wakati Ethiopia ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya Sudan.
Wakati huo huo Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen, amesema haihofii timu yoyote watakayokutana nayo katika michuano hiyo inayoelekea hatua ya robo fainali nchini hapa.
Poulsen aliliambia NIPASHE jana asubuhi baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Wavulana ya Starehe kuwa, wachezaji wake wako tayari kuivaa timu yoyote.
Alisema kila timu itahofia mpinzani wake na kwamba amekipanga kikosi chake kucheza mfumo wa pasi nyingi fupi fupi badala ya ndefu.
Alisema ushindi wa mechi ya juzi dhidi ya Burundi, umekiimarisha kikosi chake na umewaongezea wachezaji wake hali ya kujiamini na kuona kwamba hakuna kinachoshindikana.
"Tuko tayari kuivaa timu yoyote, tumejiandaa vyema na tunataka kufanya vizuri zaidi mwaka huu, hatuna hofu na yoyote tutakayekutana naye," aliongeza kocha huyo.
Alisema pia timu yake inatarajia kusafiri leo mchana kuelekea mjini Mombasa tayari kwa mechi hiyo ya mtoano.
Daktari wa timu hiyo, Mwankemwa Mwanandi, alisema wachezaji wote wako vizuri na wamefanya mazoezi kama ilivyopangwa.
Jana katika mazoezi ya asubuhi Kim aliwagawa wachezaji hao katika makundi matatu, la kwanza likiwa ni la makipa, Ivo Mapunda, Deogratius Munishi na Aishi Manula.
Kundi la pili lililoongozwa na kocha msaidizi, Sylivester Marsh lilikuwa na Mbwana Samatta, Mrisho Ngasa, Amri Kiemba, Himid Mao, Said Morad, Frank Domayo, Erasto Nyoni, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Thomas Ulimwengu na nahodha, Kelvin Yondani.
Wachezaji wengine waliobakia walikuwa ni Athuman Iddi 'Chuji', Haroun Chanongo, Ramadhan Singano 'Messi', Hassan Dilunga, Elias Manguli, Gambo Ismail na Michael Pius, wao walikuwa wanaongozwa na Poulsen.

NIPASHE

Wanamichezo, wasanii wa muziki wamlilia Nelson Mandela


http://umuhanzi.com/IMG/jpg/3_nelson_mandela_boxing_2.jpg
Nelson Mandela enzi za ujana akiwa bondia
WANASOKA na wasanii nyota wa muziki duniani wameonyeshwa kusthushwa na kifo cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyefariki usiku wa kuamkia leo kwa kuandika jumbe mbalimbali kuonyesha hisia zao juu ya kifo cha Shujaa huyo wa Afrika.
Nyota kama akina Cristiano Ronaldo, Gerard Pique, Sergio Ramos na wengine wameandika katika akaunti zao za mitandao ya kijamii kuonyesha walivyoguswa na kifo cha Mandele.
Hali hiyo ipo pia kwa wasanii mbalimbali nyota wa muziki duniani kama Rihanna, Akon, Ludacriss, P Diddy na wengine nao walitumia jumbe zao za rambirambi kuhusiana na kifo cha Mzee Mandela aliyekuwa akitibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Ebu soma baadhi ya jumbe za wasanii hao kupitia akaunti zao za Tweet uone namna gani Mzee Mandela alivyokuwa maarufu siyo kwenye siasa tu, bali hata kwa watu wa kada nyingine ikikumbukwa kuwa enzi zake aliwahi kuwa mahiri katika mchezo wa ngumi.

 
Golden Bush Veterani kupeleka maujuzi yao Zenji, kuivaa KMKM J'2

Kikosi cha Golden Bush
TIMU ya Golden Bush Veterans itakuwa na ziara ya siku moja huko Zanzibar kwa mwaliko wa timu ya KMKM Veterans. Tukiwa Zanzibar Golden bush tutacheza mecho moja siku ya jumapili jioni na ndugu zetu wa KMKM katika uwanja wao wa nyumbani. Tukiwa Zanzibar Golden bush tutafikia katika Hotel ya Baraste iliyoko maeneo ya Michenzani karibu kabisa na hotel  iliyokuwa maarufu sana enzi hizo, Bwawani Hotel.

Mipango yote imekamilika na timu yetu iko sawasawa kwa ajili ya mpambano huo ambao utakuwa unafungua ukurasa mpya kabisa wa kutengeneza ushirikiano na ndugu zetu wa Visiwani.

Msafara wa wachezaji wa Golden bush utaanza saa moja kamili asubuhi pale bandarini Dar es salaam huku ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi na mambo ya kale bwana Jeremiah Mulungu, Kocha Mkuu Madaraka Selemani “Mzee Wa Kiminyio” Kocha msaidizi bwana Herry Morris, Nahodha wa timu bwana Yahaya Issa na wachezaji wegine wandamizi .

Tukitoka Zanzibar, tutakamilisha taraibu za kuomba  game na timu ya Waheshimiwa Wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuko kwenye hatua za mwisho kabisa za mazungumzo na kocha Mkuu wa timu ya Bunge Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Tunasikitika wapenzi wetu wa Dar es Salaam mtatukosa weekend hii lakini weekend inayofuata tutakuwa jijini kutoa burudani ya soka kwa wapenzi wetu.

Karibuni sana.

King Kapita Binadamu Sghida Tupu!

 https://thumbp4-ne1.thumb.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AH5bimIAAC0VUqBzDAAAABE58m4&midoffset=2_0_0_1_1087541&partid=2&f=1214&fid=Inbox&w=3000&h=3000
BAADA YA KUFANYA VIZURI KWENYE NGOMA ZAKE ALIZOACHIA TOKA ALIPOANZA KUTOKA SOLO BAADA YA KUACHANA NA KUNDI LAKE LA WAKACHA KINGKAPITA AMESHA ACHIA NYIMBO KAMA:-
1.SHIKAMOO PESA  FT. TASH
2.MTOTO WA FISADI
3.KASEMA POA FT. NIGERIAN STARS
4.KUNATATIZO KWANI FT. GODZILLA
  NA ZOTE KUWA MISEMO KATIKA JAMII YETU SASA ANARUDI TENA NA NYIMBO INAYOHUSU BINADAMU NA UGUMU WA KUISHI NA BINADAMU
 BAADA YA KUFANYA UCHUNGUZI NA UCHAMBUZI WAKE KUHUSU BINADAMU KINGKAPITA AMEWEZA KUFANYA NYIMBO MPYA
CHINI YA STUDIO ZA KIRI RECORD KINONDONI
NYIMBO ALIOMSHIRIKISHA CHORUS KILLER AMINI KUTOKA THT
 NYIMBO INAITWA BINADAMU NI SHIDA
UNAWEZA DOWN LOAD APO CHINI KAMA IFUATAVYO
HULKSHARE LINK http://hu.lk/gp599f9b95a8

Ibrahim Class kuzidunda na Kashinde mkesha wa Mwaka Mpya


BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ameingia kambini kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika desemba 31 siku ya kufunga mwaka katika ukumbi wa msasani klabu ambapo atatupiana makonde na Mohamed Kashinde katika mpambano wa raundi sita siku hiyo

akizungumza na waandishi wa habari kocha wa kimatafa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  amesema kuwa king class kesha ingia kambini kwa ajili ya mpambano uho wa kufunga mwaka kwani ndio itakuwa mpambano wa mwisho kabisa kwa mwaka uhu

bondia king class mawe yupo fiti na ana juhudi binafsi ya kujituma mazoezini ndio siri ya mafanikio aliyo nayo mpaka sasa na kuweza kuwachachafya mabondia mbalimbali nchini ikumbukwe kuwa class ni bondia chipkizi lakina amesha wachakaza mabondia wakongwe kama Amosi Mwamakula,Simba Watunduru na Said Mundi wa Tanga na Patrick Kavako wa Morogoro ambao wote hawo kawachakaza kwa vipindi tofauti hivyo Kashinde ajiandaee sana

kwa ajili ya kupambana na King Class Mawe

Katika mchezo huo kutakuwa na michezo mingine ambapo bondia Iddy Mnyeke ataoneshana ubabe na Cosmasi Cheka,Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha katika mchezo mwingine ni kati ya Fransic Miyeyusho wa Tanzania akizichapa na David Chalanga kutoka Kenya

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo vitakaokuwa vikitolewa na Super D kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha ngumi

Rais Kikwete atuma salamu za rambirambi kifo cha Mzee Mandela

http://25thcenturyyy.com/wp-content/uploads/2013/11/Nelson-Mandela-by-Eli-Weinberg-1961-II.jpg
Mzee Nelson Mandela enzi za ujana wake


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini  na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea  tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa  machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu".
Ameongeza Rais Kikwete.

Rais amemuelezea  Mzee Mandela kuwa ni  kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha  kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa  taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

"Mandela  ni mfano bora kwa wanadamu wa  jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake" .Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela  mahali pema peponi".
Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.

Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza  kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee  nusu mlingoti.

Mwisho.

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR AS SALAAM.

Jack Kibirigi afunga mwaka akiwashukuru wadau wa Filamu

 Inline image 2Inline image 3
MUONGOZAJI bora wa filamu Swahiliwood Jackson Kabirigi ‘Jack’ anawashukru wadau wote wa tasnia ya filamu kwa ujumla wake kutokana na mchango wake ambao wamempa kupitia kazi zake ambazo ameshiriki katika kuigiza na kuongoza sambamba na filamu ya Mdundiko iliyomletea sifa baada kuchaguliwa nchini Marekani.

Akiongea na wanahabari msanii huyo ambaye ana sifa za kimataifa amesema kuwa baada ya filamu yake ya Mdundiko kushinda tuzo nje ya nchi na si ndani ya nchi ambapo hata tuzo za ZIFF ilinyimwa, lakini Jack anasema kuwa amejifunza mengi na anatoa shukrani kwa wadau wa filamu ambao wamekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha anasonga mbele kisanaa.

“Nawashukru wote wanahabari jamaa zangu hata wale ambao wamekuwa wakinishauri kupitia njia mbalimbali, kila mtu kwangu ana mchango mkubwa sana naheshimu hilo kwa kila mtu kwa nafasi aliyo nayo na kuhakikisha wanafanya jambo kubwa kwa ajili yangu mimi Jack nasema Asanteni sana na Mungu awabariki,”anasema Jack.

Aidha msanii huyo ameamua kuanzisha utaratibu wa kutoa taarifa za maendeleo ya kazi yoyote ambayo atakuwa akiifanya na taarifa kuwafikia wapenzi wa filamu nchini nzima na kuwa ndio njia ya wasanii kujenga mahusiano mema na watazamaji wao ambao kuna wanataka kujua maisha ya wasanii ya kawaida nje ya uigizaji lakini si rahisi.

Jack pia anawashukru sana wapenzi wa filamu Swahiliwood baada ya kuipokea kazi yake vema ya Kisate filamu iliyoingia sokoni hivi karibuni na kufanya vizuri kwa kuteka soko la filamu Bongo, sinema hiyo kaongoza na kuigiza mwenyewe akishirikiana na wasanii wengine wakali kama Tino, Dino, Dennis, Mzee Magari, Hamis Korongo na wasanii wengine wanofanya vizuri.

Msanii huyo ana filamu nyingi sana lakini yeye amechagua filamu kadhaa kuwatambulisha wanahabari na wadau wote kwa ujumla, sinema hizo ni  My Nephew, Money Transfer, filamu hizo kaigizia Afrika ya kusini, Born to Suffer, filamu ya Nunda, The Close, Home village,Ania.

Filamu zingine  ambazo kaingiza na kuzingoza ni Filamu ya Hatia Nguvu ya Imani, CID, Single O, Kigodoro, Kisate na filamu bora ya Mdundiko hizi ni baadhi ya filamu ambazo zote zipo katika ubora wa juu na ameahaidi kufanya mambo makubwa mwaka ujao.

Kazi nzuri ya Jack kutoka Bongo filamu yake aliyoongoza ya Mdundiko kuibuka kama filamu bora iliyofanikiwa katika kipengere cha mafanikio ya hadithi katika filamu (Achievement Narrative in Feature Film) ni ushindi mkubwa kwa mapinduzi ya filamu Bongo Movie. Huyu ndio Jackson Kabirigi muongozaji wa filamu wa Kimataifa 

“NAWAPENDA SANA NAOMBA USHIRIKIANO HUU UENDELEE MIMI NI KIJANA WENU SITOWAANGUSHA KATIKA KULETA MAPINDUZI YA KWELI YA FILAMU TANZANIA MUNGU AWABARIKI NYOTE,” 
Jackson Kabirigi. 05.December. 2013
Inline image 4

Huyu ndiye Nelson Mandela 'Madiba' aliyetutoka Afrika

http://lifeofkyle.co.za/wp-content/uploads/2013/06/mandela.jpg
Nelson Mandela enzi za uhai wake
KWA wale waliofuatilia maisha yake kwa karibu, Nelson Mandela alikua kama mtu aliyezaliwa kuwa kiongozi.
Kama rafiki yake waliyefungwa naye pamoja,Ahmed Kathrada, alivyosema hivi karibuni, Mandela alizaliwa katika familia ya kifalme na ilikuwa kaiwada kwake kua alizaliwa kua kiongozi.
Mandela alijibeba vyema sana alipokuwa kiongozi wa wa chama cha ANC na kwamba hakuna hata nusu ya Imani yake iliwahi kumuondoka miaka yote 27 aliyokuwa gerezani.
Ingawa Mandela alijitaja mwenyewe kuwa kama sehemu tu ya uongozi wa ANC, hapakuwa na shaka kuwa alikuwa kiongozi mkuu wa chama hicho kwa kizazi chake wakati huo nchini Afrika Kusini.

Hakuwa na machungu na De Klerk

Kwa dunia nzima Mandela alikua ishara ya mambo mengi, sio kiongozi tu lakini mfano wa viongozi ambao dunia insatahili kua nao enzi hizo.
Wengi wanamfahamu Mandela kwa kua na moyo mwepesi wa kusamehe na wengi wanamkumbuka hivyo kwani baadhi walimshangaa sana miaka ya tisini, aliposema kuwa hana chuki na mtu na kuwa amewasamehe waliomtendea ubaya na hata kumfunga. Hakuwa na uchungu wowote na FW De Klerk.
Msimamo wake ulijulikana na kufafanuliwa vyema katika kesi iliyohujumiwa mwaka 1964. Alisema, ‘Nimepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi na pia nimepigana dhidi ya utawala wa waaafrika weusi usiofaa.’’
"Nimekuwa nikiota kuhusu jamii huru, ambapo kila mtu ataishi na jirani yake bila uhasama, wala chuki na kuwa na fursa nzuri. Lakini pia ikiwa itahitajika, ninaweza kutoa uhai wangu kwa ajili ya vita kama hivi."
Alizaliwa mwaka 1918,katika Rolihlahla Dalibhunga, na kulelewa katika kijiji cha Mvezo Mashariki mwa mkoa wa Cape. Alikuwa na ndugu zake 13 katika familia iliyokuwa na uhusiano wa karibu na familia ya kifalme ya Thembu.
Nelson Mandela alienziwa na wengi ka sababu ya vita alivyopigana dhidi ya utawala wa wazungu
Babake alifariki Mandela akiwa na umri wa miaka tisa. Alimtaja babake kama mtu mkali mwenye kutaka watu kufuata maadili mema.
Lakini alimsifu sana babake kwa kumsisitizia kuwa na maadili mema kwani yeye ndiye alimfanya kua mtu mwema maishani.
Miaka mingi baadaye Mandela alisema kuwa babake alikuwa mtu mtukutu ila alifanya hivyo kwa misingi ya usawa, kutaka kila mtu aishi bila kudhulumiwa, alisema babake alibadili maisha ya kijana mdogo mwenye ndoto kubwa.
Mandela aliishi kijijini ambako alifunzwa namna ya kua kiongozi.
Ilikua muhimu kwake kupata elimu. Na hivyo akasomea katika shule ya kimethodisti, na kisha mwaka 1939 akaenda katika chuo kikuu cha Fort Hare 
 http://resources3.news.com.au/images/2013/06/27/1226670/400847-nelson-mandela.jpg
1918 Alizaliwa katika mkoa wa Eastern Cape
1943 Akajiunga na chama cha ANC
1956 Alifunguliwa kesi ya uhaini lakini baada ya miaka mine kiasi ikatupiliwa mbali
1962 Alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la uchochezi na kufungwa jela miaka mitano
1964 Alishitakiwa kwa kosa la kuhujumu serikali na kufungwa maisha jela
1990 Aliachiliwa kutoka gerezani
1993 Ashinda tuzo ya Amani ya Nobel
1994 Alichaguliwa Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini
1999 Ang’atuka mamlakani
2001 Aligunduliwa kua na Saratani ya tezi kibofu
2004 Alistaafu
2005 Alitangaza kua mwanawe alifariki kutokana na maradhi ya
Mandela alikutana na Oliver Tambo,ambaye alianzisha naye kampuni ya sheria ya kwanza kumilikiwa na waafrika weusi nchini humo.
Wote wawili walifukuzwa kutoka chuoni kwa sababu za kisiasa
Mwanzo alikua wakili kisha mwanaharakati na kisha akaanza vita dhidi ya utawala wa wazungu.
Miaka ya hamsini na mapema miaka ya tisini, wakati maandamano yao yalipotibuliwa kwa nguvu, chama cha ANC kikaanza vita haslisi dhidi ya utawala wa wazungu.
Alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la uhaini mwaka 1956.
Baada ya kesi yake kudumu miaka mitano, aliachiliwa huru.
Lakini ANC kikawa kimepigwa marufuku naye Oliver Tambo akatoroka nchi hiyo.
Mandela naye pia alijificha na kuendeleza harakati zake kichinichini na kuanza safari zake nje ya nchi kutaka usaidizi kwa mataifa mengine. Pia alimtembelea Tambo mjini London.
Lakini aliporejea ndiposa akakamatwa na kufungwa maisha jela, kwa miaka 27 kwa madai ya kuhujumu serikali.
Alifanya kazi katika machimbo ya mawe akiwa gerezani katika kisiwa cha Roben. Daima alisema gerezani alikua na muda mwingi wa kutafakari maisha.
Baada ya kuondoka jela mwishoni mwa kifungo chake cha miaka 27, maisha ya Mandela yalikuwa yamekomaa, na ilikua dhahiri kua walimnyang’anya Mandela ujana wake.
Ndoa yake kwa Winnie Mandela ilimalizika baada ya wawili hao kuachana. Marafiki zake wakawa hawapo tena.
Lakini alipokewa vyema sana na umati mkubwa wa watu alipoondoka gerezani.
Katika hali hiyo, angekuwa kiongozi mwingine, angemlaumu adui wake lakini Mandela pia aliwalaumu waafrika wenzake hasa wa chama cha ANC aliosema wanawaua watu na kua waache tabia hiyo.
Alijua watu wasingependa ujumbe wake, lakini pia alijua hawatamsikiliza.
Chama cha ANC kilishinda kwani watu wengi walikuwa na imani nacho.

BBC