STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 27, 2014

Pascal Ndomba ampania Francis Cheka Morogoro

http://www.thisday.co.tz/media/picture/large/Boxing.jpg
Pascal Ndomba
http://4.bp.blogspot.com/-x37B8w0JJmE/VA7WqjFR1HI/AAAAAAAANEw/Kjt1LsssxTo/s1600/Bondia-Francis-Cheka.jpg
Francis Cheka
 BONDIA Pascal Ndomba anayetarajiwa kupanda ulingoni Novemba Mosi kupigana na aliyekuwa Bingwa wa Dunia wa WBF, Francis Cheka wiki ijayo anatarajiwa kuingia kambini kujiwinda na pambano lisilo la ubingwa.
Aidha bondia huyo ametamba kumsambaratisha Cheka ili kuvunja mwiko wa kutopigwa na bondia yeyote katika ardhi ya Tanzania tangu mwaka 2008.
Mabondia hao watapambana kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Morogoro katika uzito wa Light Heavy raundi 8.
Akizungumza na MICHARAZO, Ndomba alisema ataingia kambini wiki ijayo kujiandaa na pambano hilo akiwa na nia moja tu ya kumtandika Cheka na kuziba ubabe kwa mabondia wa Tanzania.

Nahodha Coastal Union awaponda akina Jaja

NAHODHA wa timu ya Coastal Union, Mbwana Kibacha amewaponda washambuliaji wa kulipwa wa klabu za Simba na Yanga akiwamo Genilson Santana 'Jaja' akidai hawa lolote zaidi ya kubebwa na vyombo vya habari.
Kibacha alisema viwango vya Jaja na wengine wanaoichezea Yanga na wale wa Simba ni wa kawaida mno tofauti na waliopo Azam aliowafagilia akidai ni moto wa kuotea mbali.
Akizungumza katika mahojiano maalum na MICHARAZO, Kibacha aliyepewa mikoba ya unahodha baada ya kuwa msaidizi wa Juma Nyosso msimu uliopita ambaye kwa hayupo kikosini humo..
"Mapro wa Simba na Yanga ni wa kawaida sana, hawana viwango vya kutisha ila wanafagiliwa na kupambwa sana na magazeti kiasi cha kuwafanya waonekane kama akina Cristiano Ronaldo au Angel di Maria.
Beki huyo alikiri kuwa, wachezaji wanaostahili kuendelea kuwepo nchini kwa viwango vyoa vya soka ni wale waliopo Azam na pengine wenzake anaocheza nao Coastal Union.
"Mapro wa Azam ni wa ukweli, lakini waliopo Simba na Yanga wanapambwa tu kwenye magazeti, hawana lolote, wanazidiwa hata na wakali wetu wa Coastal Union," alisema Kibacha.

Washindi TMT warekodi filamu ya aina yake 'TMT Movie'

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AKh2imIAABCBVCU0VAAAAE%2FiWx0&midoffset=2_0_0_1_3332247&partid=7&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Baadhji ya washiriki wa filamu hiyo ya TMT Movie
WASHINDI wa shindano la kusaka vipaji vya filamu nchini, TMT, wakishirikiana na wakali wengine wa fani hiyo wanatarajiwa kuibuka na filamu ya aina yake iitwayo 'TMT Movie' ambayo imewashirikisha wasanii zaidi ya 200.
Kwa mujibu wa mratibu wa filamu hiyo, Staford Kihore, filamu hiyo imeanza kurekodiwa ikiwa ni moja ya malengo ya Proin Promotion iliyoendesha shindano la TMT, kuwajenga wasanii wa filamu na kuwapa uwezo wa kuigiza na kufanya kazi kimataifa.
Kihore alisema kuwa wanataka kuthibitishia umma kwamba TMT haikuwa kazi bure bali kuwafanya wenye vipaji vya fani hiyo 'kutusua' ili wafike mbali ndani na nje ya nchi.
“Tasnia ipo na inafanya vizuri lakini inahitaji uthubutu kwa kati ya wanaotengeneza sinema wawe tayari kufanya kitu kizuri kinachoweza kuvuka mipaka ndio tunachokifanya sasa baada ya kuwatengeneza kitaaluma wanafanya kazi,”anasema Staford.
Wasanii wa TMT wamefundishwa na kuiva katika fani ya uigizaji na moja ya alama yao wanayojivunia ni pale ambapo wamepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao kupitia filamu ya TMT Movie na kuonyesha kile wanachoongea kwa watazamaji na wapenzi wa filamu Swahilihood.
Filamu kubwa ya TMT Movie inatarajiwa kuonyeshwa katika majumba ya Sinema Afrika Mashariki na Ulaya pia sinema inaongozwa na Muongozaji mahiri wa filamu Karabani na imeandikwa na Novatus Mgulusi ‘Ras Nova’ zaidi ya wasanii 200 kushiriki katika filamu hiyo.
Mhusika mkuu wa filamu hiyo ni Milionea kutoka Mtwara kwa maana mshindi wa shindano la TMT, Mwanaafa Mwizango na nyota wote wa TMT, huku wasanii nyota kibao kutoka tasnia ya filamu Bongo wakipatia nafasi za ushiriki wa filamu hiyo inayojenga ajira kwa jamii nzima.

TCAA yatumia Mil. 200 kuboresha ya Mawasiliano Mnyusi Tanga

http://3.bp.blogspot.com/-NEDfQ7HuvmA/VCVr-WlwKhI/AAAAAAACrt0/_u7vRusREJQ/s1600/1.jpgNa Kipimo Abdallah
ZAIDI ya shilingi milioni 200 zimetumika katika maboresho ya kituo cha mawasiliano cha Mnyusi mkoani Tanga kinachotumika kupokea na kutuma mawasiliano ya radio zinazo tumika katika usafiri wa anga.
Hayo yamebainishwa na Afisa habari wa TCAA  Bestina Magutu wakati akizungumza na mwandishi wahabari hii leo jijini Dar es Salaam.
Alisema maboresho hayo yametokana na ukweli kuwa kituo hicho kilikuwa hakifanyi kazi kwa muda mrefu hali ambayo ilikuwa inaasababisha kukosekana kwa mawasiliano katika ukanda wa mashariki kutoka usawa wa bahari.
Kabla ya kukamilika kwa maboresho haya baadhi ya maeneo mchini yalikuwa hayapati mawasiliano ya kitekonologia kutoka nchini na badala yake walikuwa wanapata huduma hiyo kutoka nchi jirani,"alisema.
"Mradi huo umekamilika na kukabithiwa kwenye mamlaka ya usafiri wa anga mwezi agost mwaka huu na kukabithiwa kwenye kituo cha Mnyusi jijini Tanga,umegharimu shilingi za kitanzania milioni 292,887,921," alisma.
Magutu aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kumeongeza ufanisi wa usafirishaji wa anga kwa kurahisisha huduma ya kuongoza ndege,utaongeza mapato kwa mamlaka hiyo.
"Nimategemeo yangu kwamba kupitia maboresho haya mamlaka itajiongezea mapato kupitia tozo ya huduma ya uongozaji ndege,
Kwa upande wake Mkaguzi Mwandamizi,Redemptus Rugombe alisema mamlaka inandelea kupanua miondombinu ya kuongeza ndege sanjari na mabadiliko ya teknolojia ili kumudu ukuaji wa sekta ya usafirirshaji wa anga.
"Takwimu za mwaka 2031 zinaonyesha ongezeko la miruko ya ndege (flight movement) imeongezeka hadi kufikia miruko 230,458 sawa na ongezeko la asilimia3.6 kotoka miruko 222,430 mwaka 2012,
Kadharika katika kipindi hicho idadi ya abilia imeongezeka kutoka 4,056,925 hadi kufikia 4,626,016 sawa na ongezekola asilimia 14,kwa sasa idadi ya abilia inatarajiwa kuongezeka zaidi kufikia mwishoni mwa mwaka huu," alifafanua.
Mkaguzi Mwandamizi huyo aliongeza kuwa katika kuhakikisha watanzania wanapata uelewa wa elimu ya mamlaka ya anga mamlaka inaendelea kuwapatia wanafunzi mafunzo kwa njia ya udhamini na hadi sasa kuna wamnafunzi watano wanaendelea ma mafunzo ya urubani.
"Kwa tarifa za wanafunzi wetu ambao wako Afrika ya kusini kwa masomo ya urubani chini ya udhamini wa mamlaka wanaendelea vizuri,huu mpango kwa mamlaka ni endelevu ili kusaidia kuwawezesha watanzania kpambana katika soko la ajira, "alisema.

'Ukosefu wa Uwazi ni Chanzo cha Rushwa Tanzania'

http://3.bp.blogspot.com/-eFGl7xIlKmg/Ub1Td_CVpwI/AAAAAAAAP30/Fs3mARbvMxw/s640/dkhosea.jpg
Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk  Hosea

Na Kipimo Abdallah
KUTOKUWEPO kwa uwazi, uadilifu na uwajibikaji katika mikataba mbalimbali ambayo serikali inaingia na wawakezaji kutoka nje ni moja ya sababu ya kuongezeka kwa rushwa kwa baadhi ya watumishi wa umma na wawekezaji.
Hayo yamebainishwa na Mwahadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi Profesa Humphrey Moshi wakati akizungumza na mwandishi habari hii kwenye kongamano ambalo linaratibiwa na taasisi ya Jukwaa la Sera (Policy Forum).
Alisema kukosekana kwa  uwazi katika  mikataba mbalimbali ni moja ya sababu ambayo imekuwa ichangia rushwa kwenye michakato na makubaliano mengi ambayo yanahusisha serikali na wawakezaji.
Profesa Mushi alisema Serikali imekuwa inapata kigugumizi katika kuweka wazi baadhi ya mikataba kwa kile kinachodaiwa kuwa ni siri baina ya mwekezaji na serikali jambo ambalo halina ukweli tofauti na rushwa.
“Mimi nimekuwa nikifanya tafiti mbalimbali hasa za mausuala ya kukua kwa uchumi ni wazi kuwa zipo fedha nyingi ambazo zinapotea ambapo mwanzo wake unaanzia kwenye uingia ji wa mikataba hadi katika utekelezaji  ambazo zinaelekezwa katika rushwa”, alisema Mushi.
Mwahadhiri huyo wa UDSM alisema kuonyesha kuwa serikali haina dhamira ya kuondoa hiyo changamoto imekuwa ikiwaruhusu wawekezaji hao kutoweka hata akaunti zao wazi kama ilivyo kwa nchi zingine duniani.
Profesa Mushi ambaye pia aliwahi kuwa mshauri wa masauala ya uchimi wa Rais wa Zanzibar Abeid Aman Karume pamoja na Ofisi ya Hazina ya Tanzania alisema iwapo Tanzania itajikita katika uwazi, uwajibikaji na uadilifu maendeleo yatapatikana kwa haraka.
Mchumi huyo mwandamizi alisema ni dhahiri kuwa kumekuwepo kwa ukiukwaji mkubwa katika maamuzi hivyo ni vema kujiangalia upya kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya kwa maslahi ya Taifa.
Alisema Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa fursa mbalimbali ila kukosekana kwa uadilifu na uwazi kwa baadhi ya watendaji rasilmali hizo zipo hatarini kupotea.

'Leteni filamu zenu DFF 2014 mjitangaze zaidi'

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AKh2imIAABCBVCU0VAAAAE%2FiWx0&midoffset=2_0_0_1_3332247&partid=2&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000KAMPUNI ya Haak Neel Production na Filamucentral waandaaji wa Tamasha la Dar Filamu Festival wanawakaribisha watengenezaji wote wa filamu  zinazotumia Lugha ya Kiswahili kutuma au kuwakilisha filamu zao katika ofisi za Haak Neel Production zilizopo Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere.

TAMASHA kubwa kabisa la filamu Swahilihood hilo linapokea kazi zilizotoka mwaka 2013/2014 kwa ajili ya kuonyeshwa katika tamasha kubwa linalounganisha wadau na watengeneza filamu kutoka sehemu mbalimbali za Ulimwengu na kutoa fursa kwa wadau wengi kutengeneza soko lingine.

Akiongea na FC mkurugenzi wa Haak Neel Production Godfrey Katula amesema kuwa tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani litafika kila kona ya Wilaya za Dar es Salaam na kutoa burudani ya kazi nzuri zinazotengenezwa na watanzania.

“Kama ilivyo kauli mbiu yetu inasema “FILAMU ZETU, MAISHA YETU” ni kauli mbiu ya kutia matumaini kwa watengenezaji na watazamaji kwani filamu tuaamini kuwa ni kazi inayoweza kutengeneza ajira kubwa kwa kila mtu,”anasema Katula.

Tamasha hili ambalo limelenga kukuza Lugha ya Kiswahili na kufanya kuwa ni biashara na alama kubwa kwa filamu zetu zinateka soko Afrika ya Mashariki kwa kuongea Kiswahili kitamu na kinzuri kinachovutia kwa wanaAfrika mashariki na Ulaya.

Mtengenezaji wa filamu au mtayarishaji  unatakiwa kuwakilisha filamu nakala mbili za filamu ambayo imetoka mwaka na kuonyeshwa kwa mwaka 2014, ikiwa samba na utambuzi wa mtayarishaji, imekaguliwa na Bodi ya Filamu pamoja na taratibu husika katika taasisi za filamu.

Kwa mawasiliano na jinsi ya kuwakilisha filamu zenu wasiliana na +2552773113, +255754 578 730, +255754 260 688 Ongea na Dada Unce anakupatia maelekezo ya kufika katika ofisi za Haak Nell Production.

NCCR-Mageuzi yalia na Wabunge wa BMK

Faustin Sungura (kulia) katika moja ya mikutano yake na wanahabari
Na Kipimo Abdallah
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesikitishwa na kitendo cha Bunge Maalum la Katiba kuhitaji wajumbe ambao hawapo nchini au ndani ya Bunge kuruhusiwa kupiga kura wakati ukweli ni kwamba ushiriki wao katika utengenezaji wa rasimu hiyo ulikuwa mdogo.
Kaimu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Faustin Sungura, aliyasema hayo juzi alipozungumza na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu.
Alisema utaratibu huo wa kuruhusu wajumbe walioko nje kupiga kura haujawahi kutokea katika Bunge lolote duniani jambo ambalo linatia aibu kwa Taifa.
Kaimu Katibu huyo alisema iwapo wajumbe hao ambao hawakushiriki katika mchakato kwa kiwango cha kuridhisha wataruhusiwa kupiga kura hali hiyo ingekuwa hata kwa wale wa UKAWA kwani uwepo wao nje una sababu kama hao wengine.
“Jamani Watanzania tuamke hii sasa aibu tunapopelekwa pabaya haiwezekani watu wapo nje ya Bunge alafu wapewe nafasi ya  kupiga kura jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa kwani linatia aibu nchi”, alisema.
Alisema katika Bunge hilo linaloendelea mkoani Dodoma mambo mengi yamekiukwa ila hapo walipofikia ni vema jamii ya Kitanzania ikafungua macho na kuamua kufanya maamuzi mazito kwani kinachoonekana ni watu kuhitaji kwa maslahi yao.
Sungura alisema ni vema Wabunge waliopo Dodoma wakatambua kuwa mambo megine hayalazimishwi kwani yanahusu jamii kubwa na sio kama wanavyofikiria kuwa wao ndio wanahusika pekee.
Alisema NCCR-Mageuzi imejipanga kuhakikisha kuwa katiba hiyo inakataliwa kutokana na ukweli kuwa kilichopo ndani sio yaliyokuwa mapendekezo ya wananchi ambayo yaliwakilishwa na iliyokuwa Tume ya Katiba.
Sungura alisema ukweli dhidi ya UKAWA kutoka Bungeni umedhihirika hivyo juhudi zao ni kuhakikisha kuwa rasimu hiyo haipitishwi na wananchi kutokana na kudharauliwa kwa maoni yao ambayo walipendekeza katika rasimu ya Jaji Joseph Warioba.
Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema nguvu yao pia inaongezwa na maamuzi ya Mahakama Kuu hivi karibuni ambapo imeweka bayana kuwa kitendo kilichofanywa na Mwenyekiti wa Bunge hilo kupokea maoni mapya ni ukiukwaji wa sheria.
Sungura alisema mabadiliko na maingizo mapya yaliyofanywa na Bunge hilo ambalo alilitaja kuwa ni la upande mmoja yamekiuka sheria kwa kiwango kikubwa na cha kusikitisha.
Alisema kwa sasa NCCR- Mageuzi ipo katika mikakati ya kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi juu ya mchezo mchafu unaofanywa na Bunge hilo jambo ambalo litawajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika upigaji kura.

Mwisho

Vyombo vya Habari vyaaswa kujenga Maadili ndani ya Jamii

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/07/Wapigapicha.jpg
Wanahabari wakiwa kazini
Na Suleiman Msuya
RAI imetolewa kwa vyombo vya habari, taasis mbalimbali, vikundi vya kijamii, wananchi na serikali kushirikiana kwa pamoja katika kujenga jamii yenye maadili kuanzia ngazi ya familia ili kuleta maendeleo katika nchi.
Hayo yamebainishwa na Afisa kutoka IQ Management Solutions Joel Nanamka wa wakati akizungumza na MICHARAZO jijini Dar es Salaam.
Alisema iwapo kutakuwepo kwa ushirikiano baina ya sekta hizo ni wazi kuwa jamii itazingatia maadili katika suala lolote ambalo linafanyika kwa maslahi ya Taifa.
Nanamka alisema vyombo vya habari kama moja ya muhimili usio rasmi bado havijafanya kazi ya dhati ili kuweza kuibadilisha jamii ambayo inaonyesha dhahiri kupotea katika misingi ya utu.
Afisa huyo alisema ukosefu wa maadili hasa katika sekta mbalimbali za serikali kumekuwa kukichangia ukosefu wa huduma bora na zenye viwango kwa jamii.
“Kimsingi suala la kuwepo kwamaadili ni mtambuka ila kwa mtazamo wetu katika tafiti mbalimbali tunaona kuwa nafasi ya vyombo vya habari katika kufanikisha hilo ni kubwa hivyo vinapaswa kubadilika kutokana na ukweli kuwa watu wengi wanafikiwa”, alisema.
Alisema IQ Management Solutions imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha kuwa maadili yanakuwepo kwa kanuni, sheria, zawadi na matisha pamoja na adhabu ambazo zitakuwa katika mtazamo hasi.
Kwa upande wake Afisa Programu kutoka taasisi ya Afrika Leadership Initiative Foundation Limited Alice Mwiru alisema katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo kwa jamii yenye maadili taasisi yao imejikita kufanya kazi na vijana ambao wanaonyesha nia za kuongoza.
Mwiru alisema wao wanaamini kuwa kuwepo kwa viongozi wenye maadili ni chachu ya kuwepo kwa jamii ambayo itakuwa katika misingi hiyo.
“Sisi ALI EAF tunaamini kuwa jamii ikikuwa kwa misingi ya maadili hasa kuanzia utotoni  ni wazi kuwa kila Mtanzania atakuwa kwenye misingi hiyo kwa faida yake na nchi kwa ujumla”, alisema

Barua ya wazi kwa Wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar

http://1.bp.blogspot.com/-Tefvw458x_8/Uw88mMQrDFI/AAAAAAAFP_U/cFqjPeAuPC0/s1600/WABUNGE+WAKIPITIA+RASIMU+YA+MAPENDEKEZO+YATAKAYO+TUMIWA+NA+KIKAO+CHA+BUNGE+LA++KUJADILI++RASIMU+YA+KATIBA.JPG
Assalam alaykum
Natumai hamjambo ndugu, kaka na dada zangu. Inshallah Mwenyenzi Mungu akupeni afya na uzima kuelekea kipindi hiki muhimu cha kupiga kura kuamua Katiba Inayopendezwa na pia Mola akupeni busara na maamuzi mema.
Nakuandikieni barua hii kama Mzanzibari mwenzenu sina zaidi ya hilo. Ni kutokana na Uzanzibari wangu nimeona kuwa nijaribu kukuaidhini, kunasihini, kukushawishini, kukusemeshini, kukuombeni kuwa msiikubali Katiba Inayopendekezwa na muipigie kura ya HAPANA.
Tafadhalini wekeni mbali ushindani, itikadi na mitazamo ambayo inatutenganisha Wazanzibari na muamue kwa maslahi makubwa, mapana na ya muda mrefu ya Zanzibar. Msitizame tulipojikwaa bali tizameni tulipoanguka. Msitizame nyuma mkahesabu visa na mikasa ila nyinyi hapo mlipo ndio wenye fursa ya kuikoa, kuinusuru na kuihuisha Zanzibar.

Naam, ni kura ya HAPANA ndio ambayo itaibakisha, itaiokoa, itaisimamisha Zanzibar. Mjue mkipigia kura ya NDIYO maana yake ni kuwa Zanzibar tuipendayo inazidi kupungua, kuchukuliwa na kumezwa kama ambavyo imekuwa khofu yetu kwa miaka kadhaa ya Muungano huu.
Nataka muamini ndani ya dhati yangu mimi ni muumini wa Muungano. Nataka Muungano wa haki na hadhi sawa baina ya Washirika wa Muungano – Tanganyika na Zanzibar- ili kila nchi ipate fursa sawa za kuhudumia watu wake.
Wengi wenu kwa kauli zenu mara kadhaa mmekuwa mkisema Muungano hauakisi hali ya usawa, haki na hadhi sawa lakini mkawa mnatumia neno KERO kuwasilisha fikra zenu hizo, na wengi tukawa na matumaini kwamba fursa hiiya kuunda upya Katiba yetu itapunguza kama si kuondosha kabisa KERO hizo.
Ila baada ya kuiona Katiba inayopendekezwa nimeona kuwa andiko hilo halina msaada, halina muelekeo na halina wema na Zanzibar. Kulikubali andiko hilo ni kujitia kitanzi wenyewe na sasa imekuwa ni kusokotwa, kubanwa na kudhibitiwa Zanzibar lakini mara hii itakuwa kwa kujitakia wenyewe.

Huko nyuma tumekuwa tukisema kuwa kumekuwa na hadaa, sijui ujanja, sijui ghalat,sijui unyemela wa kuongeza Mambo ya Muungano ambayo yamekuwa yakipunguza madaraka ya Zanzibar, lakini mara hii tunajichinja wenyewe kwa mikono yetu.
Hii ilikuwa ni fursa kubwa kwetu kusimama kama Zanzibar. Zanzibar ilipaswa kusimama kama kundi zima ndani ya Bunge na kukaa na kundi zima la upande wa pili yaani Tanganyika, na watu wa pande mbili hizi kuamua umbo, hadhi na sifa gani tunataka Tanzania iwe.
Hili la pande mbili lilikuwa lisionewe aibu kwa sababu ndio ukweli na uhalisia kwamba tuko pande mbili. Haiwezekani kuwa na Muungano, ambapo upande mmoja una kila sifa za kuwa nchi, halafu upande mwengine uwe na sifa za kuwa dola na nchi ifichwe ndani yake.

Ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Zanzibar kudai haki zake, stahiki zake, fursa zake ili iweze kukidhi mahitaji ya watu wake, maana hata kama tumo ndani ya Muungano basi bado tuna chumi mbili zinazoshindana na kwa kweli zinazopigania na kunyang’anyiana rasilmali karibu zile zile.
Ilikuwa ni wakati wa kufanya kila njia ili Zanzibar ijitengenezee fursa ya kuwa na mafanikio kama ya Visiwa vya Seychelles au Mauritius ambavyo wastani wa kipato cha mwananchi wa nchi hizo mbili ni zaidi ya dola 14,000 na dola 15,000 mtawalia.
Najua hoja itakuja basi haya yangefanywa kwa umoja, na mbona umoja huo haukuwepo, nakiri kuwa hilo kweli limetokea, lakini ni kama katika mchezo iwapo mchezaji mmoja ametolewa ama kwa kuonewa na mwamuzi au kwa kitendo chake cha makusudi, haina maana kuwa waliobakia uwanjani wakubali kupoteza mchezo, badala yake hujibidiisha kushinda ili iwe njia moja ya kumsuta mwenzao aliyetolewa na sifa kwa kweli inakuja kwa waliobakia uwanjani.
Kwa kuendelea kujigandisha katika ubavu, kuendelea kuamini kuwa hatuwezi kujitegemea na kwa hivyo mambo kadhaa kuyabakisha katika Muungano ni kujiviza akili, ni kujidhalilisha kimkakati na kujidogosha kihadhi.
Si kweli na si kweli kabisa kuwa Katiba Inayopendekezwa ina maslahi na Zanzibar. Haina, haina katu, haina Abadan, kamwe haina. Ni katiba ambayo inatuweka pabaya na pagumu zaidi na imeendelea kuyachukua mamlaka ya Zanzibar na kuyatia katika Muungano.

Vipi Katiba hii itakuwa na maslahi na sisi? Hebu tutizame mambo machache:
1. Kundosha au kuukataa mfumo wa Shirikisho ina maana
a) Zanzibar haiwezi kuwa na hadhi na haki sawa na Serikali ya Muungano.
b) Tumejibakisha pale pale Zanzibar haina mshirikia mwenziwe kwenye Muungano
c) Tumerudi pale pale mshirika wa Zanzibar ni Tanzania na kwa hivyo hakuna usawa
d) Tumeganda pale pale kuwa Tanganyika inasimamiwa na Serikali ya Muungano
e) Tumesalia papo kuwa Bunge la Muungano linatunga sheria za Tanganyika na tunajua kuwa sheria kama hizo hazina nguvu Zanzibar
f) Tumejizuga vile vile kumwita Waziri wa Muungano hata asiesimamia jambo la Muungano kama kilimo bila ya kuwa na hadhi kama hiyo.
g) Tumekwama pale pale Mahakama Kuu ya Tanganyika inaitwa ya Muungano
h) Tumejidanganya vile vile wafanyakazi wote wa Tanganyika wanabaki ni wa Muungano na wale wa Zanzibar mwisho wao Chumbe.

Fikiria hii ndio Zanzibar tuitakayo?
2. Tunajipa moyo kuwa kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa ni Makamo wa Rais wa Muungano kuna manufaa kwa Zanzibar ilhali hakutakuwa na msaada wowote.
Tumewapa watu matumaini kuwa hilo litawezesha Rais wa Zanzibar akitoka nje atakuwa na hadhi ya kimuungano wakati tunajua hilo litaleta utata mkubwa zaidi huko mbele. Kwanza kwa suala la gharama pili kutakuwa na mgongano wa maslahi na majukumu yake kama Rais wa Zanzibar vs Umakamo wa Muungano

3. Haiwezekani Rasimu Inayopendekezwa iwe imenyofoa mamlaka zaidi yaliokuwa yameanza kuikaribia Zanzibar kutokana na Rasimu ya Warioba, halafu isemwe kuwa kuna maslahi kwa Zanzibar.
a) Kuondoa uwezo wa Zanzibar kuunda Benki yake
b) Kurudisha nguvu za kuigawa Zanzibar kwa Rais wa Muungano
c) Kukubali ardhi kurembwa
d) Tumerudisha suala la Tume ya Pamoja ya Fedha ambayo imeshindikana kwa miaka kadhaa toka nia hiyo ilipotiwa kwenye Katiba ya 1977.
4. Uamuzi wa kuyatia madaraka ya Serikali ya Zanzibar ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ilhali hakuna sehemu yoyote ya Katiba Inayopendekezwa ambapo madaraka ya Serikali ya Tanzania Bara kama inavyoitwa yameainishwa ni kuendelea kujidanganya.

Pili, kwa kufanya hivyo tunarudi tena pale pale ambapo Zanzibar inaonekana inakiuka Katiba ya Jamhuri pale inapotaka kufanya mabadiliko yenye maslahi yake, ilhali jambo kama hilo halionekani na wala halipo kwa upande wa mshirika mwenziwe, maana mshirika ni huyo huyo Serikali ya Jamhuri na Serikali ya Tanzania Bara.
Ndugu, kaka na dada zangu ujue wazi kuwa maamuzi unayotaka kuyafanya ni makubwa na yana athari ya muda mrefu kwa vizazi vingi vya Zanzibar, ambayo pamoja na tofauti zetu, lakini naamini tunakubaliana kuwa Zanzibar tuipendayo iwepo. Na kuwepo kwake lazima iwe na nguvu na matao yake.
Na kwa dalili zote Rasimu Inayopendekezwa inapopotoa nguvu na matao ya Zanzibar. Inaondosha uzuri na haiba yake kwa kuifanya kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano badala ya kuwa ni nchi moja kamili ndani ya Muungano huu.

Fikirini, pimeni na muvuke nje ya itikadi na mitizamo. Fanya uamuzi ili nafsi yake iwe na amani kwa sababu umefanya uamuzi wako bila ya shindikizo, maelekezo au utashi wa kisiasa, maana wewe kwanza ni Mzanzibari kisha mengine ndio yanafuata.
Nawaomba radhi kwa uamuzi huu wa kuandika barua ya wazi maana isingewezekana kumfika kila mmoja wenu, lakini nataka muamini kuwa barua hii nimeiandika kwa sababu nimeona kuna wajibu kwangu kufanya hivyo.
Unapotaka kupiga kura fikiria, wazia na pimia juu ya uzito wa mchoro wako mmoja tu wa kalamu utavyokuwa na athari kwa nchi yako, watu wako na watoto na wajukuu wako. Fumba macho, rudisha nyuma fikra zako,
kumbubuka wema na ihsani za waliokuzunguka, uliokuwa nao pamoja katika maisha yako na uwafikirie khatma njema ya muda mrefu.

Kumbubuka jukumu lako kwa Mwenyenzi Mungu na fikiria kama hicho ni kitendo cha mwisho cha maisha yako ili ukitie katika mizania nzuri ya maamuzi yako.
Piga HAPANA kwa faida ya Zanzibar na usinitizame mimi kama Ally Saleh, la. 

Mimi ni mtu mmoja tu tena tunaweza kuwa tuna mzigo wa tofauti zetu, lakini pamoja na yote mimi na wewe ndio Zanzibar.
Kwa maslahi ya Zanzibar piga HAPANA.

Ally Saleh
Zanzibar

Kocha Liverpool akiri Balotelli bado sana, japo amemsifu Anfield

http://4.bp.blogspot.com/-qxoy2_IXmQs/VAKymzUbQoI/AAAAAAAAAfo/BW28VyCZYd0/s1600/baloooooooooo.jpgMENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amekiri kuwa Mario Balotelli bado hajafikia hadhi ya kiwango cha dunia lakini amemuunga mkono kuwa anaweza kuvaa viatu vya Luis Suarez na kufanya vitu vikubwa Anfield. 
Suarez aliuzwa Barcelona kwa kitita cha euro milioni 88 katika usajili wa kiangazi huku nafasi yake ikizibwa na Balotelli aliyesajiliwa akitokea AC Milan kwa kitita cha euro milioni 20. 
Rodgers anaamini kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Italia anapswa kufuata nyayo za Suarez akiwa hapo na kuonyesha thamani yake akiwa kama mshambuliaji. 
Rodegrs amesema pamoja na kwamba Balotelli hajafikia hadhi ya kiwango cha dunia lakini hana shaka na kipaji chake kwani ana uwezo wa kufikia huko kama akitilia maanani kazi yake hiyo.

Nasibu Ramadhani, Moh' Matumla kumaliza ubishi leo Manzese

  MABONDIA Nasibu Ramadhani na Mohammed Matumla wakitunishiana misuli jana wakati wakipimwa uzito. Mabondia hao wanatarajiwa kuonyeshana kazi leo kwenye ukumbi wa Friends Corner -Manzese Dar.
Mratibu wa mpambano wa ngumi Ibrahimu Kamwe katikati akiwangalia mabondia wa kike Lulu Kayage kushoto na Fatuma Yazidu wanavyo tunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao
Lulu Kayage na Fatuma Yazidu wakitambiana baada ya kupima uzito
Bondia Nassibu Ramadhani akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Mohamedi Matumla

Mohamed Matumla akipima uzito
Bondia Nassibu Ramadhani na Mohamed Matumla wakinuliwa mikono juu na Mratibu wa mpambano huo Ibrahimu Kamwe katikati  mpambano utakaofanyika leo Jumamosi hii katika ukumbi wa Friends Corner Manzese
Bondia Juma Fundi na Issa Omari wakinuliwa mikono juu na Mratibu wa mpambano huo Ibrahimu Kamwe katikati  mpambano utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Friends Corner Manzese
Bondia Lulu Kayage akipimwa na Daktari baada ya kupima uzito kushoto ni mpinzani wake Fatuma

Kocha Mkwasa apata ulaji TFF baada ya kurejea umangani

ALIYEKUWA kocha wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa 'Master' ameteuliwa kuwa Ofisa Mtaalamu wa Elimu ya Mafunzo wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF.
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa ameithibitisha juu ya Mkwasa kupewa nafasi hiyo baada ya kurejea kutoka Uarabuni, alipokwenda kufundisha klabu.  
Kwa upande wake, Mkwasa, amesema kuwa amekwishaanza kazi yake hiyo mpya TFF na anatarajia kuifanya kwa ufanisi kwa sababu ana utaalamu nayo.
Juu  ya mkataba wake na Yanga, Mkwasa alisema kwamba wakati anakwenda Uarabuni alipewa likizo ya mwaka mmoja, kwa sababu amerudi kabla ya muda huo ameona bora kukubali kazi hiyo ya TFF kuliko kukaa bure.  
“Kama Yanga SC watanihitaji kurudi kazini kabla ya muda huo, ni suala la kuzungumzika tu, kwa sababu TFF ipo kwa ajili ya maendeleo ya soka hapa nchini na Yanga ni klabu ya Tanzania,” amesema Mkwasa.
Mkwasa alijiunga na Yanga Desemba mwaka jana akitokea Ruvu Shooting ya Pwani, lakini baada ya msimu Mei mwaka huu akaondoka pamoja na aliyekuwa kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mholanzi Hans va der Pluijm kwenda Uarabuni.  
Hata hivyo, baada ya muda mfupi wa kufanya kazi huko, Pluijm aliyemchukua Mkwasa kwenda naye huko- akatofautiana na uongozi wa timu na kusitishiwa mikataba.

Jackson Chove apigwa 'stop' VPL, kisa....!

http://2.bp.blogspot.com/-HEQ-Dp1OT9s/UUbYTc9SA_I/AAAAAAAAFVw/GrGFWKuZJVM/s640/Chove.jpg
Chove (Kulia) wakati akiichezea Coastal Union. TFF imemzuia kucheza mpaka ithibitishwe usalama wa afya yake
SHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF, limetangaza kumpiga 'stop' kipa wa JKT Ruvu, Jackson Chove 'Mandanda' kushuka dimbani kwa usalama wake.
Mandanda aliumia na kuzimia kwa zaidi ya dakika 10 katika mechi ya kwanza kati ya JKT Ruvu ilipokuwa ikiivaa Mbeya City mjini Mbeya.
Katika mechi hiyo ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara, timu hizo zilimaliza kwa sare ya bila kufunga.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema hadi Chove atakapowasilisha vipimo vyake kwa shirikisho hilo nalo kuviwasilisha kwa wataalamu ili kujiridhisha kama yuko sawa.
“Kitendo cha mtu kuzimia kwa dakika 15 si kidogo, tungependa kuhijirisha.
“Lakini tunawashauri wenzetu wa klabu kuhakikisha wanalizingatia suala la kuwapima wachezaji wao kwa kuwa mchezo wa soka si kitu lahisi,” alisema Malinzi.
Timu nyingi za Ligi Kuu Bara na hata ligi nyingine, zimekuwa hazifanyi vipimo vya uhakika kwa wachezaji wake kabla ya kuanza kwa ligi hiyo.

Kivumbi VPL, Simba 'gonjwa' kujiuliza kwa Polisi leo, Yanga kesho


Simba itavuna nini kwa Polisi Moro leo ikiwa na mapengo ya nyota wake
Mbeya City kubanana na Coastal

Mtibwa Sugar itavuna nini kwa Ndanda leo Jamhuri!

Ndanda kuendeleza undava hata kwa Mtibwa Sugar?
http://2.bp.blogspot.com/-AmdeM53ePZ4/U-DhYQITAHI/AAAAAAAAA-U/1zmEdcZBM7w/s1600/AZAM+FC.JPG
Mabingwa watetezi Azam watakaovaana na Ruvu Shooting
http://2.bp.blogspot.com/-IjcTroMvHi4/VAQIjtTyzMI/AAAAAAAANR4/-eytuZU705U/s1600/cb4a0-1375766_581274061909694_1850204431_n-Copy.jpg
Prisons-Mbeya kuendeleza ubabe wa Yanga

Simba itawamudu maafande wa Polisi Moro?
JKT Ruvu nao kibarua chao kipo kesho kwa Kagera Sugar

Yanga wenyewe kazi yao ni kesho kwa Prisons
KLABU ya Simba ikiwa  bila ya nyota wake wanne, Paul Kiongera, Haruna Chanongo, Issa Rashid 'Baba Ubaya' na kipa Ivo Mapunda inatarajiwa kushuka dimba la Taifa jioni ya leo kupepetana na Polisi Morogoro, huku kocha wake Patrick Phiri akichekelea pambano lao na Yanga kusogezwa mbele wiki moja.
Simba iliyoanza na sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union wiki iliyopita wakati wakiwa mbele kwa mabao 2-0 watawakosa wachezaji hao muhimu katika kikosi cha kwanza kutokana na kuwa majeruhi, hata hivyo kocha Phiri ametamba wachezaji waliosalia kikosini wapo tayari kuisambaratisha Polisi waliorejea ligi kuu tena.
Polisi inayonolewa na nyota wa zamani wa Yanga, Pan Afrika na Taifa Stars, Mohammed Rishard Adolph, ilikaribishwa ligi hiyo kwa kipigo cha mabao 3-1 na Azam wiki iliyopita na leo itakuwa ikitaka kurekebisha makosa, licha ya ukweli pambano hilo ni gumu kwao.
Phiri alinukuliwa wasingependa kurejea makosa ya wiki iliyopita kwa kuhakikisha wanapata ushindi leo ili kujiweka pazuri kabla ya mechi yao ya mwisho kuisubiri Yanga ambapo aliongelea kusogezwa mbele kwa pambano hilo la watani kutoka Oktoiba 12 hadi Oktoba 18 ni faraja na nafuu kubwa kwao.
Pambano la watani limesogezwa mbele kwa wiki moja toka ratioba ya awali ili kupisha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya taifa, Taifa Stars dhidi ya Benin.
Ukionoa pambano la Simba na Polisi ratiba ya ligi hiyo inaonyesha kuwa, Coastal Union baada ya kuidindia Simba itasafiri hadi mjini Mbeya kupepetana na wenyeji wao Mbeya City, huku Azam itaialika Ruvu Shooting uwanja wa Chamazi, wakati Ndanda Fc itakuwa wageni wa Mtibwa Sugar mjini Morogoro.
Mechi nyingine ni Mgambo JKT baada ya kuizabua Kagera Sugar itakuwa tena nyumbani kuwakaribisha Stand United iliyoanza ligi hiyo kwa kichapo cha amabo 4-0.
Kipute cha pili hiyo kitaendelea tena kesho kwa mechi mbili zitakazochezwa jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa Taifa, Yanga iliyoanza kwa 'mkosi' wa kubamizwa mabao 2-0 na Mtibwa mjini Morogoro itaialika Prisons-Mbeya na JKT Ruvu ya Fred Felix Minziro itaikaribisha Kagera Sugar uwanja wa Chamazi.

Msechu, Vanessa, Diamond katika tuzo za AFRIMA-2014

Peter Msechu, Vanessa Mdee na Diamond watakaowanmia tuzo za AFRIMA
DIAMOND Platnumz, Vanessa Mdee na Peter Msechu wametajwa kuwania tuzo za AFRIMA za nchini Nigeria.
Wimbo wa Come Over imemuwezesha Vanessa kutajwa kuwania tuzo katika vipengele viwili vya Best African RnB Soul na Best Female Artist in Eastern Africa.
Peter Msechu kupitia wimbo wake Nyota na Diamond kupitia Number One wametajwa kuwania tuzo ya Best Male Artiste In Eastern Africa.
Diamond naye amepata nafasi mbili katika kinyang’anyiro kupitia wimbo wake wa Number One unawania pia tuzo ya Best African Collaboration.


Bofya hapa kuangalia orodha kamili

Hapatoshi England, Liver vs Eveton, Arsenal v Spurs

http://tvnewsroom.org/wp-content/uploads/2013/09/Sky-Sports-1-NAR-Live-Ford-Super-Sunday-09-01-15-41-28-600x339.jpg
http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2008/01_03/arsenalspursccG_468x306.jpg
Nani atakayecheka kati ya Arsenal na Spurs
http://www.theevertonforum.co.uk/wp-content/uploads/2013/05/lolza.jpg
http://static.guim.co.uk/sys-images/Football/Clubs/Club_Home/2010/2/7/1265568899742/Tempers-flare-between-Liv-001.jpg
Presha ya pambano la mji wa Merseyside huwa hivi. Leo itaakuwaje? Tusubiri tuone
 KIVUMBI cha Ligi Kuu ya England kinatarajiwa kuendelea kutimka leo kwa kushuhudiwa mechi za watani wa jadi wa miji ya London Kaskazini na Merseyside wakati Arsenal itakapoumana na Tottenham Hotspur na Liverpool kuwakaribisha Everton uwanja wa Anfield.
Klabu hizo zote nne yenye upinzani wa jadi katika miji yao, zitashuka dimbani zikiwa hazina mwenendo mzuri kulinganisha na msimu uliopita na kuwafanya mashabiki wao kuwa roho juu kujua wataibuka vipi.
Mbali na mechi hiyo, pia kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo timu nyingine 12 wakiwamo Manchester United na Chelsea watakuwa dimbani kusaka pointi tatu muhimu.
Mashetani WEkundu wanaouguza kipigo cha mabao 5-3 toka kwa Leicester City itakuwa uwanja wa nyumbani wa Old Trafford kuwakaribisha West Ham United na Chelsea watakuwa darajani kuivaa Aston Villa.
Ratiba kamili ya ligi hiyo kwa leo ni kama ifuatavyo;
Liverpool    v Everton   
Chelsea        v Aston Villa       
Crystal Palace       v Leicester
Hull City    v Manchester City
Manchester United    v West Ham 
Southampton    v QPR
Sunderland    v Swansea City
Arsenal        v Tottenham

Suarez aitwa 'Stars' ya Uruguay, akitwa Bonge Hispania

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/08/18/1408396240290_wps_5_Barcelona_s_Luis_Suarez_f.jpgWAKATI akitajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uruguay, Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Luis Suarez amejikuta akibatizwa jina la Bonge, jina ambalo hakuwahi kuitwa hata alipokuwa Liverpool.
Televisheni ya jijini Madrid imemtaja mshambuliaji kuwa ni mwenye uzito kupindukia na kulalamikiwa kuwa anaonekana ni kama mchezaji mstaafu katika taarifa iliyorushwa mchana wa alhamisi siku ambayo Suarez alifunga magoli mawili katika mchezo wa kirafiki akiichezea Barcelona B dhidi ya kikosi cha Indonesian U19.
Ikiwa imesalia mwezi mmoja kabla ya mchezo wa watani wa jadi Clasico katika msimu huu mchezo ambao utakuwa unaashiria kumalizika kwa adhabu ya mshambuliaji huyo kufuatia kumng'ata mlinzi wa timu ya taifa ya Italia mambo yanaonekana kumuendelea kombo nchini Hispania.
Bosi wa Barcelona Luis Enrique amejibu lawama hizo katika mkutano wake na waandishi wa habari akionekana kushangazwa na tuhuma hizo kwa Suarez.
Katika hatua nyingine mshambuliaji huyo amejumuishwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa ya hapa Uruguay kwa ajili ya mechi za kirafiki za mwezi ujao dhidi ya Saudi Arabia na Oman, shiriksiho la soka (AUF) limesema juzi.
Mshambuliaji mwenye matata wa Barcelona huyo amefungiwa kucheza kwa miezi minne, pamoja na mechi tisa za mashindano za timu ya taifa, baada ya kituko chake cha kumng'ata beki wa Italia Giorgio Chiellini kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Anaweza kucheza kwenye mechi za kirafiki, hata hivyo, baada ya Mahakama ya Michezo (CAS) kuondoa kipengele ambacho kilimfungia kujihusisha na "jambo lolote la kisoka" katika kifungo chake cha miezi minne.
Baada ya kuachwa kwenye kikosi cha mechi za kirafiki za mwezi huu dhidi ya Japani na Korea Kusini, Suarez ameitwa na kocha Oscar Tabarez katika kikosi cha wachezaji 29 kwa ajili ya mechi hizo za ugenini Saudi Arabia Oktoba 10 na Oman siku tatu baadaye.

Simba, Yanga sasa kutifuana Oktoba 18

PAMBANO la watani wa jadi wa soka nchini, Simba na Yanga ambalo lilikuwa lichezwe Oktoba 12, sasa litafanyika Oktoba 18 baada ya mabadiliko ya ratiba.
Mabadiliko hayo yamekuja kutokana na kuwepo kwa pambano la kirafiki la kimataifa linalotambulishwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA kati ya Taifa Stars dhidi ya Benin litakalochezwa Oktoba 12 jijini Dar.
Kwa mujibu wa marekebisho madogo yaliyofanywa na Shirikisho la Soka nchini, TFF, ni kwamba mechi zote zilizokuwa zichezwe Oktoba 12 na 13 sasa zitachezwa Oktoba 18 na 19 sambamba na pambano la watani wa Jadi.

Coutinho, Tegete wampa jeuri Maximo akiikabili Prisons Taifa kesho

Kocha Maximo wa Yanga akiwa na Jerson Tegete aliyerejea kikosini baada ya kufanikiwa kuponya majeraha yake
KOCHA Marcio Maximo ametamba kuibuka na ushindi kesho wakati kikosi chake kitakaposhuka dimbani kuwakabili Prisons-Mbeya hii ni baada ya nyota wake waliokuwa majeruhi kupona.
Nyota hao ni pamoja na Mshambuliaji matata, Jerry Tegete na Mbrazil mwenzake Andrey Coutihno ambao huenda wakawepo kikosi katika mechi hiyo ya Jumapili itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Akiongea na tovuti rasmi ya klabu ya Yanga mara baada ya mazoezi, kocha Maximo amesema vijana wake wako fit kuelekea mchezo huo huku wakiwa wamejipanga kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.
Maximo amesema baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar, kikosi chake kimekua kikiendelea na mazoezi kila siku katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola huku wakiyafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo wa awali.
Kuhusu timu ya Tanzania Prisons mbrazil Maximo amesema anatambua walishinda mchezo wa awali dhidi ya Ruvu Shooting hivyo wana morali bado ya kuendeleza ushindi siku ya jumapili, lakini pia kikosi changu kipo fit kwa mchezo huo kwa kusaka pointi tatu muhimu.
Aidha Maximo amesema habari njema kwa wana Yanga ni kurejea dimbani kwa kiungo Andrey Coutinho pamoja na mshambuliaji Jerson Tegete ambao wanatarajiwa kuonekana kwenye mchezo huo na kuhakikisha wanaisaidia timu yao kupata ushindi.
Wachezaji watakaoukosa mchezo wa siku ya jumapili ni Oscar Joshua na Hussein Javu ambao wote ni majeruhi, wakisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, na jumatatu wanatarajiwa kuanza mazoezi mepesi baada ya kuwa kwenye matibabu chini ya usimamizi wa daktari wa timu Dr Suphian Juma.
Mwisho kocha Marcio Maximo amewaomba wapenzi, washabiki, wanachama na wadau wa soka kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili katika mechi dhidi ya Prisons kuja kuwapa sapoti vijana na kuwashangilia muda wote wa mchezo.

Liverpool wapewa Swansea, Man City v Newcastle Capital One


Suso wa Liverpool akishangilia bao lililosaidia kuivusha timu yao katika michuano ya Kombe la Ligi (Capital One)


Frank Lampard akishangilia goli lake la tatu katika mechi mbili dhidi ya Sheffield jana

SHREWSBURY Town, timu pekee ya daraja la chini zaidi iliyosalia katika michuano ya kombe la ligi 'Capital One Cup' amepangwa kukutana na timu ngumu ya ligi kuu ya England, Chelsea kwenye mechi ya raundi ya nne.
Raundi iliyopita Shrews inayocheza daraja la pili iliwaondoa mabingwa wa Championship, Norwich na sasa itawakaribisha Chelsea walioshinda 2-1 dhidi ya Bolton jana usiku.
Mabingwa watetezi, Manchester City, walioitoa Sheffield jana kwa kuifunga mabao 7-0 katika dimba la Etihad watachuana na Newcastle inayocheza ligi kuu.
Liverpool waliosonga mbele kwa penati 14-13 dhidi ya Middlesbrough jumanne usiku, watachuana na Swansea City, zote zinacheza ligi kuu.
Stoke wataikaribisha Southampton , wakati Tottenham watakuwa nyumbani dhidi ya Brighton.
Mechi nyingine za raundi ya nne zitawakutanisha Sheffield United watakaosafiri kuifuata MK Dons na Fulham watakabiliana na Derby.


Ratiba kamili hii hapa:
Tottenham Hotspur vs Brighton
Stoke City vs Southampton
Bournemouth vs West Brom
Shrewsbury vs Chelsea
Liverpool vs Swansea City
MK Dons vs Sheffield United
Manchester City vs Newcastle United