STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 27, 2014

Coutinho, Tegete wampa jeuri Maximo akiikabili Prisons Taifa kesho

Kocha Maximo wa Yanga akiwa na Jerson Tegete aliyerejea kikosini baada ya kufanikiwa kuponya majeraha yake
KOCHA Marcio Maximo ametamba kuibuka na ushindi kesho wakati kikosi chake kitakaposhuka dimbani kuwakabili Prisons-Mbeya hii ni baada ya nyota wake waliokuwa majeruhi kupona.
Nyota hao ni pamoja na Mshambuliaji matata, Jerry Tegete na Mbrazil mwenzake Andrey Coutihno ambao huenda wakawepo kikosi katika mechi hiyo ya Jumapili itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Akiongea na tovuti rasmi ya klabu ya Yanga mara baada ya mazoezi, kocha Maximo amesema vijana wake wako fit kuelekea mchezo huo huku wakiwa wamejipanga kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.
Maximo amesema baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar, kikosi chake kimekua kikiendelea na mazoezi kila siku katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola huku wakiyafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo wa awali.
Kuhusu timu ya Tanzania Prisons mbrazil Maximo amesema anatambua walishinda mchezo wa awali dhidi ya Ruvu Shooting hivyo wana morali bado ya kuendeleza ushindi siku ya jumapili, lakini pia kikosi changu kipo fit kwa mchezo huo kwa kusaka pointi tatu muhimu.
Aidha Maximo amesema habari njema kwa wana Yanga ni kurejea dimbani kwa kiungo Andrey Coutinho pamoja na mshambuliaji Jerson Tegete ambao wanatarajiwa kuonekana kwenye mchezo huo na kuhakikisha wanaisaidia timu yao kupata ushindi.
Wachezaji watakaoukosa mchezo wa siku ya jumapili ni Oscar Joshua na Hussein Javu ambao wote ni majeruhi, wakisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, na jumatatu wanatarajiwa kuanza mazoezi mepesi baada ya kuwa kwenye matibabu chini ya usimamizi wa daktari wa timu Dr Suphian Juma.
Mwisho kocha Marcio Maximo amewaomba wapenzi, washabiki, wanachama na wadau wa soka kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili katika mechi dhidi ya Prisons kuja kuwapa sapoti vijana na kuwashangilia muda wote wa mchezo.

No comments:

Post a Comment