STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 13, 2014

Steve Nyerere atema cheche Bongo Movie

Steve Nyerere (kushoto) akiwa na Mkwere kwenye msiba wa Mzee Small
MWENYEKITI wa Bongo Movie, Steve Nyerere amesema umefika wakati wasanii wa filamu nchini na waigizaji kwa ujumla kujenga utamaduni wa kupenda kusaidiana wakati wanapokuwa na shida badala ya kuonyesha umoja na mshikamano kwenye misiba tu.
Steve alisema wasanii wamekuwa wepesi kujitokeza na kuonyesha umoja na mshikamano kwenye mazishi ya wenzao, lakini wamekuwa wazito wakati wasanii wenzao wanapokuwa na matatizo ikiwamo kuugua au janga lolotge linalowapata kitu ambacho alidai siyo kizuri.
Akizungumza na MICHARAZO kwenye msiba wa Mzee Small, Steve Nyerere ambaye majina yake kamili ni Steven Mengele alisema ni aibu wasanii na wadau wa sanaa kuchangishana fedha wakati wa misiba ya wenzao wakati wanapokuwa wagonjwa wanashindwa kutoa fedha kuwasaidia kuokoa uhai wao.
Muigizaji huyo na muigaji wa sauti za watu mashuhuri duniani, alisema anajisikia aibu na kujifunza mambo mengi kupitia msiba wa Mzee Small ambaye amekufa huku akisononeka kutengwa na waigizaji wenzake wakati akihitaji msaada wa matibabu.
"Ifike wakati wasanii sasa tukajenga utamaduni wa kusaidiana wakati wa matatizo, Mzee Small alikuwa anaugua naamini fedha ambazo zinatumika leo kugharamia mazishi yake ingetosha kusogeza uhai wake hata kama kifio kimeumbwa kwa kila mtu na hakuna wa kuweza kuzuia kisimfikie yeyote," alisema.
Alisema tayari chini ya uongozi wake wameunda mfuko wa kusaidia wasanii wenye matatizo na wapo katika mchakato wa kufanya mazungumzo na taasisi za kijamii na fedha kama NSSF, PSPF na GPRF na Bima ya Afya ili kuwezesha wasanii kujiunga nayo na kujiwekea akiba inayoweza kuwasaisdia wanapokuwa wamekwama.
"Pia kama wazo alililotoa Mkuu wa Mkoa, Meck Sadick wakati wa kuagwa marehemui George 'Tyson' Otieno juu ya kuanzisha Saccos au benki tunalifanyia kazi na Inshallah mambo yakikaa vyema tutaanika kila kitu hadharani, kwa sababu hali inatosha na wasanii wamekuwa wakiumia wanapokumbwa na matatizo kama haya," alisema

Newz Alert! Bondia Iraq Hudu 'Kimbunga' afariki, kuzikwa kesho

MISIBA imeendelea kuiandama fani ya michezo na burudani baada ya alfajiri ya leo bondia nyota wa zamani wa ngumi za kulipwa, Iraq Hudu 'Kimbunga' kufariki akiwa amelazwa kwenye hiospitali ya  Hindu Mandal, Dar es Salam.
Kwa mujibu wa mpwa wa bondia huyo aliyetisha kwa ngumi nzito na kutwaa ubingwa katika ngumi za ridhaa kabla ya kuingia zile za kulimwa miaka ya 1990, Rajab Mhamila 'Super D', Kimbunga alikuwa akisumbuliwa na tatizo la Figo na kwamba anatarajiwa kuzikwa kesho majira ya saaa saba mchana.
Super D alisema msiba wa biondia huyo upo nyumbani kwake  Buguruni Kisiwani na mazishi yatafanyika kwenye makaburi ya Kisutu.
Msiba huo wa Kimbunga umekuja wakati wadau wa michezo na burudani wakiwa bado wanaendelea kuomboleza vifo vya wasanii na wanamichezo kadhaa waliokumbwa na mauti ndani ya kipindi cha mwezi mmoja sasa.
Baadhi ya waliokumbwa na mauti kwa siku za karibuni ni wanamuziki Muhidini Mwalimu Gurumo, Amina Ngaluma 'Janapese', Recho Haule, Adam Kuambiana, George Tyson, Mzee Small, Abdallah Sumbwa, Ally Mwanakatwe na nahodha wa zamani wa KMKM ya Zanzibar.

Balotelli kutua Arsenal kwa msaada wa Puma

KAMPUNI ya usambazaji wa vifaa vya michezo, Puma itaisaida Arsenal kufanikisha mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Italia, Mario Balotelli kutoka AC Milan.

Mpachika mabao huyo anadhaminiwa na Puma, ambao pia mapema Januari walitangaza kuidhamini Arsenal.

Mustakabali wa Balotelli ndani ya Milan uko shakani baada ya Rais Silvio Berlusconi kusema bado hajaamua lolote kuhusu mchezaji huyo na mchambuzi wa Sky Sport nchini Italia, Mario Giunta akaandika: "Arsenal inamtaka sana Balotelli na Arsene Wenger atafanya kitu chochote kumhamishia London. 
Kutua kwa mshambuiliaji kwa Wapiga Mitutu hao wa Londo kutakuwa msaada mkubwa katika safu ya ushambiuliaji inayomtegemea Oliver Giroud.

Fabregas atua rasmi Chelsea kama utani

CHELSEA wamekamilisha usajili wa kiungo wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas kutoka Barcelona kwa ada ya uhamisho inayoaminika ya paundi milioni 30 na amesaini mkataba wa miaka mitano.
Fabregas aliiambia tovuti rasmi ya klabu hiyo: "Kwanza napenda kumshukuru kila mmoja klabuni FC Barcelona ambako nimefurahia miaka mitatu mizuri. Ilikuwa ni klabu yangu ya utotoni na daima nitajivunia kwamba nilikuwa na fursa ya kuchezea timu kubwa kiasi hicho.
"Najiona bado nina kazi ambayo sijaimaliza katika Ligi Kuu ya England na sasa ni wakati mwafaka kurejea.
"Nilitafakari ofa nyingine zote kwa umakini na nikaona kwamba Chelsea ni chaguo bora. Wanalingana na malengo yangu ya soka kutokana na njaa yao ya kutwaa makombe. Wana kikosi cha wachezaji wazuri na kocha babkubwa. Nimeingia kikamilifu katika timu hii na nashindwa kuendelea kusubiri kuanza kazi."
Fabregas alifunga magoli nane katika La Liga akiwa na Barcelona na kutoa pasi za mwisho zilizozaa magoli 19 katika mechi 36 msimu uliopita.

Neymar aiongoza vyema Brazil, yaitungua Croatia 3-1

20140613-010343-3823241.jpg
WENYEJI wa michuano ya Fainali za Kombe la Dunia, Brazili imeanza vyema fainali hizo kwa kuicharaza Croati kwa mabao 3-1, huku nyota wa timu hiyo na blabu ya Barcelona, Neymer akifunga mabao mawili moja likiwa la penati iliyolalamikiwa na wageni.
Goli jingine la Brazili lilifungwa na Oscar dakika za lala salama, baada ya awali kutanguliwa na bao la kujifunga la Marcelo dakika ya 11 ya mcvhezo huo ulioptanguliwa na sherehe za ufungizi zilizofana.
Ushindi huio umeiweka Brazil katika nafasi nzuri ya kuwatuliza mashabiki wao ambao wamekuwa hawana amani na timu yao na hasa kutawaliwa na vurugu za watu wanaopinga michuano hiyo kufanyika nchini kwao kwa madai ni gharaa kubwa ambazo fedha zilizotumika kuandaa zingewasaidia katika huduma za kimaendeleo.
Michuano hiyo itaendelea tena leo saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kati ya Mexico dhidi ya wawakilishi wa Afrika Cameroon kabla ya timu za Uholanzi kuvaana na mabingwa watetezi Hispania baadaye.