STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 21, 2014

Ghana, Libya zasonga mbele, Ethiopia yaweka rekodi CHAN 2014

http://mtn.ensight-cdn.com/content/rsz_chan2014~21.jpg
Ghana
http://drum.co.za/wp-content/uploads/2014/01/Libya-CHAN1.jpg
Libya

BAO pekee lililofungwa na Kwabena Adusei katika dakika ya 77 limeisaidia kuivusha Ghana hadi hatua ya robo fainali ya michuano ya CHAN baada ya kuinyuka Ethiopia, huku Kongo ikiduwazwa na Libya baada ya kuchomoa kipigo dakika za jioni na kupata sare ya 2-2.
Abdelrahman Fetori aliifungia Libya bao wakati Kongo wakiamini wamepata ushindi wao wa pili katika michuano hiyo kutoka kundi C na kujihakikishia tiketi ya kucheza robo fainali.
Fetori alifunga bao hilo dakika ya pili ya nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika na kufanya matokeo kuwa 2-2- na hivyo Libya kuungana na Ghana iliyoongoza kundi hilo kufuzu mtoano.
Kongo ilitangulia kupata mabao mawili na kuonekana kuikamata vilivyo libya katika pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Peter Mokaba, Polokwane (Pietersburg), wakati Ghana iliichapa Ethiopia uwanja wa Free State, mjini Bloemfontein.
Mabao ya Kongo katika mchezo huyo yalifungwa na Nkounkou dakika ya 36 na Binguila dakika ya 54, kabla ya  Abdulsalam Omar kufunga bao la kwanza katika dakika ya 75.
Kwa matokeo hayo Ghana imemaliza mechi zake tatu kwa kukusanya pointi saba na kuongoza na kufuatiwa na Libya yenye pointi tano na Kongo imesaliwa na pointi tatu, huku Ethiopia ikitoka patupu na kuweka rekodi ya kutofunga bao hata moja wala kupata pointi katika michuano hiyo tofauti na wengi walivyoitegemea.
Timu hizo mbili zimeungana na zimeungana na Nigeria, Mali kutoka kundi A na Morocco na Zimbabwe za kundi B kucheza hatua ya mtoano na timu za mwisho zitapatikana kesho katika mechi za mwisho za makundi wakati kundi D litakalofunga dimba usiku.
Burundi inayoongoza kundi hilo itapepetana na majirani zao DR Congo na Mauritania itaumana na Gabon.

MAAFA! Watatu wafa kwa kusombwa maji Dodoma

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjcGpz8x4b-vfTrH7zLQOyLxrb-q1lVxcGeTeHRt1HeIzc31S9Yrcz4xAjdyUMcpstGqm2W3K08uuQEDstq3onBqtzjvsn6T9wKCv1pgb6Rbl-5qZzMQdDA5NzvbwIh0kYk-3nEwhSLmK8/s1600/DSC_0000556.jpg
WATU watatu wamekufa baada ya kusombwa na maji wakati gari walilokuwa wakiendesha wakitokea   katika kijiji cha Chilonwa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma kupoteza muelekeo.
Habari zilizotufikia kutoka mjini humo kupitia Msemaji wa wilaya ya chamwino Richard Masimba aliwataja waliofariki ni Jane Ntimba , mkazi wa Area C, Sharifa Saidi  na Sapiencia Augustino waliokuwa kwenye gari aina ya Toyota lenye namba za usajili T694 BMA na mmoja aitwaye David Lukoka kufarikiwa kujiokoa kwa kuruka wakati gari hilo likisombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Babi waanza msimu kwa kipigo Malaysia

Babi (kushoto mbele) akiwa na kikosi cha timu yake ya UiTM iliyolala nyumbani mabao 3-2

KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim Babi ameanza vibaya mechi ya kwanza ya mashindano akiwa n klabu yake mpya ya UiTM ya Malaysia baada ya leo kudunguliwa mabao 3-2 katika pambano la Kombe la FA.

Akizungumza muda mfupi uliopita na MICHARAZO, Babi alisema timu yake imelowa nyumbani dhidi ya PBDKT T-Team katika mchezo uliochezwa uwanja wa nyumbani wao wa Mini UiTM, mjini Shah Alam.

Babi alisema pambano hilo lilikuwa kali na lenye ushindani na mwishowe PBDKT T-Team, walibuka na ushindi huku yeye mwenyewe akishindwa kutupia bao lolote.

Ijumaa Babi anatarajiwa kuingoza timu yake kushuka dimba ikiwa ugenini dhidi ya Kuala Lumpur SPA katika mechi ya Ligi Kuu ya Malaysia itakayochezwa kwenye uwanja wa Hang Jebat mjini Melaka.

Baada ya mechi hiyo UiTM itarejea nyumbani tena siku ya Jumatatu kuikaribisha Johor katika pambano jingine  la ligi hiyo.

Katika msimu uliopita timu hiyo anayoichezea Babi ilikamata nafasi ya tisa kati ya timu 12.

Balotelli amkaribisha Seedorf kwa ushindi Milan

Super Mario Bal;otelli

KOCHA mpya wa AC Milan Clarence Seedorf ameanza vyema kazi ytake ya kuiinoa timu hiyo aliyowahi kutamba nayo kwa ushindi wa bao 1-0,  shukrani zikimwendea Mario Balotelli aliyefunga kwa mkwaju wa penalti  kwenye mechi ya Serie A dhidi ya Verona juzi.
Mshambuliaji huyo alizamisha penalti hiyo kimiani katika dakika ya 82 baada ya Alejandro Gonzalez kumchezea madhambi Kaka ndani ya eneo la hatari.
Licha ya ushindi huo, mabingwa hao mara 18 wa Serie A, bado wanashika nafasi ya 11 katika ligi hiyo ambayo walikuwa wakiishika wiki iliyopita wakati Seedorf aliporithi mikoba ya Massimiliano Allegri aliyetimuliwa kutokana na matokeo mabaya.

Abdi Kassim kuanza rasmi kibarua kilichompeleka Malaysia leo

Abdi Kassim
KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' anatarajiwa kuanza rasmi kibarua chake nchini Malaysia leo( Jumanne) atakashukla dimbani na timu yake ya UiTM kuumana na PBDKT T-Team katika mechi ya Kombe la FA.
Pambano hilo linaloashiria kuanza upya kwa msimu wa Ligi nchini Malaysia  litachezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa UiTM wa  Mini UITM, uliopo mji wa Shah Alam.
Kwa mujibu wa Babi mechi hiyo ndiyo ya kwanza ya mashindano kwake kabla ya Ijumaa kuanza kipute cha Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa kuumana ugenini na klabu ya Kuala Lumpur SPA.
"Kesho (leo) tunatarajia kushuka dimbani kwenye mechi ya FA dhidi ya T-Team inayocheza Super League, kabla ya Ijumaa kuanza kipute cha Ligi kwa kuvaana na Kuala Lumpur SPA  ugenini na baadaye kurejea nyumbani kucheza na Johor," alisema.
Babi alisema yupo fiti kwa ajili ya msimu huo anaoucheza kwa mara ya kwanza nchini humo akiwa mmoja wa wachezaji tegemeo hasa baada ya kufanya mambo kwenye mechi kadhaa za kirafiki za kujipima nguvu.
Mchezaji huyo alitua katika timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea KMKM iliyomsajili na kuichezea klwa muda mfupi akitokea Azam aliomaliza nao mkataba na kuichezea kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita
.