STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 28, 2015

Mwili wa Kapteni Komba wahifadhiliwa Lugalo Hosp

http://api.ning.com/files/WeTmt906*BKaGszeajuNVr5dNk0HSypjN26QmHzMaFxTohOy6Y0MGC21Im0--55H01NauXCyaXGuZ4IFusMmfHQa9XH9hHlJ/CAPT.JOHNDAMIANOKOMBAMBUNGEMBINGAMANG.CCM.TEL.07442845.jpg
Kapteni Komba enzi za uhai wake
MWILI wa marehemu Kapteni John Komba umepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya kijeshi la Lugalo tayari kwa taratibu za mazishi ambayo hata hivyo hayajafahamika yafanyika lini na wapi.
Marehemu Komba alikumbwa na mauti jioni ya leo katika hospitali ya TMJ alipokimbiwa na wanafamilia yake kutokana na kuugua ghafla.\
Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na Presha na taarufa nyingine zikieleza ni ugonjwa kisukari.
MICHARAZO inaendelea kufuatilia taarifa zaidi na itawafahamisha, ila tunaendelea kutoa pole kwa wote walioguswa kwa namna moja au nyingine na kifo cha Kapteni Komba hususani wanasiasa na wadau wa muziki kwani marehemu alikuwa moja ya wapiganaji katika maendeleo ya sanaa hiyo husuani ubunifu wake wa mtindo wa ACHIMENENGULE aliotaka uwe utambulisho wa muziki wa Tanzania.

VITA YA LIGI KUU BARA BADO MBICHI KABISA!!

Simba angalau sasa inapumua
Polisi Moro
JKT Ruvu waliokuwa mapumzikoni wikiendi hii kabla ya kuvaana na Yanga Jumatano
Mtibwa Sugar wanaozidi kuporomoka
UGUMU wa Ligi Kuu Tanzania unazidi kuongezeka wakati ligi hiyo inaingia raundi ya 16 baada ya matokeo ya michezo ya leo.
Simba ambao wamepanda hadi nafasi ya tatu kwa muda wakisubiri kujua hatma ya pambano la Stand Utd na Kagera Sugar angalau sasa inapumua baada ya ushindi wa mabao 5-0 iliyopta kwa Prisons wakati wanachama na viongozi wao wakielekea kwenye Mkutano Mkuu utakaofanyika kesho Bwalo na Maafisa wa Polisi Oysterbay.
Hata hivyo hali ni mbaya kwa timu za Prisons ya Mbeya na Mgambo JKTambazo nafasi mbili za chini
Prisons Mbeya wana kila dalili za kurudi walipotoka kwa kuzibeba timu zote ikiwa na pointi 12 tu wakati wenzao kwa kipigo ilichopata kwa Coastal wanapointi zao 14 tu.
Ebu tazama msimamo na mbio za kuwania KIatu cha Dhahabu zilivyo mpaka sasa Mnigeria Absolom Chiidebele akiwafukizia waliopo juu yake.
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                            P   W    D    L    F    A   GD   Pts
01.  Yanga            15  09  04  02  21  08  13  31
02.  Azam             15  07  06  02  22  12  10  27
03.  Simba            16  05  08  03  20  12  08  23
04. Coastal Union  16  05  07  04  12  10  02  22
05. Kagera Sugar  15  05  06   04  12  11  01  21
06. Ruvu Shooting16  05  06   05  11  12   -1  21
07. Mtibwa Sugar  14  04  07   03  15  14  01  19
08. Polisi Moro      15  04  07   04  12  13   -1  19
09. JKT Ruvu        15  05  04   06  14  15   -1  19
10. Stand Utd       16  04  06   06  14  18   -4  18
11. Mbeya City      16  04  06  06   11  15   -4  18
12. Ndanda Fc       15  04  04  07   13  18   -5  16
13. Mgambo JKT    14  04  02  08   07  20  -13 14
14. Prisons            16  01  09   06   10  20  -10 12
Wafungaji:
8- Didier Kavumbagu(Azam)
7- Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
 

6- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ame Ali (Mtibwa), Simon Msuva (Yanga)
 

5-Danny Mrwanda (Yanga), Kipre Tchetche (Azam)Emmanuel Okwi (Simba), Absalom Chiibidele (Stand Utd)

4- Rama Salim (Coastal),  Ibrahim Ajibu (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Heri Mohammed,(Stand Utd)


3-
Ally Shomari (Mtibwa),  Jacob Massawe (Ndanda), Frank Domayo (Azam), Malimi Busungu (Mgambo), Atupele Green (Kagera), Amissi Tambwe, Mrisho Ngassa (Yanga), Yahya Tumbo (Ruvu Shooting)
 

2- Shaaban Kisiga, Dan Sserunkuma, Elias Maguli (Simba), Salum Kanoni, (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam),  Najim Magulu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Jerry Tegete, Coutinho (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Heri Mohammed, Mussa Said (Stand Utd), Ally Nassor (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi), Peter Mapunda (Mbeya City) Lutimba Yayo (Coastal Union)

Rooney aibeba Man Utd, Saint's wafa ugenini

3pm banner 10.jpg
Muunganiko wa picha kama zilizochapishwa na Daily Mail zikionyesha Man Utd walipoizamisha Sunderland
MABAO mawili kutoka kwa Mshambuliaji wa kimataifa wa England, Wayne Rooney wameiwezesha Manchester United kupata ushindi nyumbani dhidi ya Sunderland na kufufua matumaini yao ya kuwania nafasi ya ushiriki wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani.
Rooney ambaye kwa muda mrefu amekuwa akichezeshwa kama kiungo na kocha Louis Van Gaal, leo alichezeshwa kama mshambuliaji wa kati na kmufunga mabao hayo katika kipindi cha pili na kuipa Mashetani Wekundu ushindi huoi muhimu.
Nahodha huyo alifunga bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati dakika ya 66 kabla ya kuongeza la  pili dakika ya 84 na kupoza machungu na hasira walizokuwa nazo mashabiki wa timu hiyo baada ya wiki iliyopita kulala kwa Swansea City.
Katika mechi ya mapema West Ham United ikiwa nyumbani ilicharazwa mabao 3-1 na Crystal Palace, huku Swansea ikiendeleza ubabe katika ligi hiyo kwa kuilaza Burnley nyumbani kwao kwa bao 1-0 huku Newcastle United ikishinda nyumbani bao 1-0 dhidi ya Aston Villa.
Nayo timu ya Stoke City iliitambia nyumbani Hull City kwa kuilaza bao 1-0 sawa na ilivyokuwa kwa West Bromwich iliyoitambia Southampton waliowafuta kwao.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili za kuakta na mundu, kwa Liverpool kuikaribisha mabingwa watetezi Manchester City na Arsenal kuialika Everton, wakati Chelsea na Tottenh ham Hotspur wenyewe wataumana kwenye mchezo wa fainali za Kombe la Ligi (Capital One)

MASKINI AZAM! YAANGA AFRIKA KAMA KMKM

Azam waliokumbwa na bahati mbaya Khartoum kwa kung'olewa na El Merreikh
KLABU ya Azam imeungana na wenzao wa KMKM ya Zanzibar kuaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya usiku huu kunyukwa mabao 3-0 na El Merreikh ya Sudan na hivyo kutolewa kwa jumla a mabao 3-2.
Azam walienda Sudan wakiwa na hazina ya mabao 2-0 iliyopata katika mechi ya mkondo wa kwanza wiki mbili zilizopita, lakini wenyeji walitumia nafasi ya kucheza nyumbani kunadili matokea kama kocha wao alivyoatamba mapema na Azam kuaga mashindano. El Merreikh walikosa pia penati baada ya kupaisha.
Hii ni mara ya pili kwa Azam kuaga michuano katika raundi ya mapema baada ya mwaka jana pia kutolewa na timu ya Ferroviaro de Beira ya Msumbiji.
Azam imetoka ikiwa ni saa chache baada ya KMKM nayo licha ya kuopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya El Hilal ya Sudan, ilijikuta ikitoka mashindano kwa ujumla ya mabao 2-1 baada ya mechi ya kwanza nchini Sudan kulala mabao 2-0.
Timu ya Polisi Zanzibar waliokandikwa mabao 5-0 na Mounana ya Gabon kesho itajaribu kuweka rekodi mpya Afrika kama itaweza kuifunga wapinzani wao mabaop 6-0 na kuweza kuungana na Yanga walipenya kwa mbinde jana baada ya kulala 2-1 ugenini lakini ushindi wao wa nyumbani ukawabeba na kusonga mbele.
Yanga inayotarajiwa kutua kesho usiku ikitokea Gaborone, itaumana na Platnum ya Zimbabwe kati ya Machi 13-15 katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo baada ya Wazimbabwe kuing'oa Sofapaka ya Kenya kwa mabao 4-2 kutokana na kushinda leo 2-1 kama ilivyokuwa katika mechi ya mkondo wa kwanza nchini Kenya.

Ngoma ya Stand, Kagera yalala, Coastal yashinda

http://api.ning.com/files/cPakA0chAEyfyqjZRP3k2djpZ9GyxNW23W69D7FY4fYhsuNz2vmH6gr7yEITcci18IdnTvIgOej4xydmYu8LtJiXW0uQDhCL/16.jpg
Kagera Sugar watakaomaliza dakika 16 na Stand kesho asubuhi
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/HMB_8262.jpg
Stand wanaoongoza bao 1-0 mpaka sasa kabla ya kumalizia dakika 16 kesho
PAMBANO la timu za Stand United na Kagera Sugar linatarajiwa kumaliziwa kesho asubuhi huku wenyeji Stand wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Dakika 16 zilizosalia baada ya pambano hilo kuvunjika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kwenye dimba la Kambarage zitamalizwa saa 3 asubuhi ya kesho, ikiwa ni mara ya pili kwa pambano la ligi hiyo kuchezwa kwa siku mbili mfululizo.
Pambano la kwanza lilikuwa kati ya Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting lililoisha kwa sare ya 1-1, kila timu ikipata bao katika vipindi viwili, Mtibwa wakitunguliwa dakika 45 za kwanza na waliporudiana walirudisha bao kabla ya kurudiwa tena kwa pambano la Mtibwa na Kagera na matokeo kuisha kwa sare.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo leo, Mbeya City ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting, huku Coastal ikiwa  na kocha mpya, Jamhuri Kihwelu 'Julio' waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo JKT na kuendeleza ubabe kwa wapinzani wao hao.
Bao la Coastal liliwekwa kimiani na Lutimba Yayo na kuleta furaha kwa mashabiki wa Wagosi wa Kaya ambao kitambo walikuwa hawajaonja ushindi wowote.
Katika mchezo wa Mbeya City na Ruvu Shooting wenyeji wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha aibu cha mabao 3-1 toka kwa Yanga walirejesha bao dakika ya 75 kupitia Themi Felix baada ya wageni kutangulia kwa bao la mapema la Yahya Tumbo.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumatano kwa pambano kati ya Yanga dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa Taifa.

Simba yairarua Prisons, 'dogo' apiga hat trick

HAT Trick ya kwanza msimu huu iliyowekwa Ibrahim Hajibu na mengine ya Emanuel Okwi na Ramadhani Singano 'Messi' yameiwezesha Simba kuirarua Prisons Mbeya katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hajibu alifunga mabao katika dakika za 15, 21 na 42, kabla ya Okwi kuongeza dakika ya 73 na Messi kumaliza kazi dakika ya 83.
Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha pointi 23 na kuendelea kusalia nafasi ya tatu nyuma ya Kagera Sugar.

Breaking Newzz: Kapt John Komba hatunaye Duniani

http://api.ning.com/files/8KNI8B2SjT1ePQsfa9AOokVE6RIW8oxFgc*7KyWSQJstmtSfJD-qgiJyCgz83-xe8mTLl34zGqpA5MWQWGNYVtMK4y*tvtqP/1.png?width=650
Kapteni John Komba
 HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba amefariki dunia jioni hii jijini Dar es Salaam.
Taarifa hizo zinasema kuwa Mbunge huyo aliyekuwa pia Mkurugenzi wa kundi la TOT amefariki akiwa hospitalini ya TMJ akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa hizo zinasema kuwa, Mbunge huyo alizidiwa akiwa nyumbani kwake Mbezi na kukimbizwa hospitalini hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.

MICHARAZO inaendelea kufuatilia taarifa hizo kwa zaidi ili kuwajuza kwa undani zaidi na kujua juu ya taratibu za mazishi ya mwanasiasa huyo aliyekuwa mahiri kwa kuimba Kwaya aliyeanzia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kadhalika MICHARAZO inatoa pole kwa familia, ndugu jamaa na rafiki wa marehemu Kapteni Komba kwa msiba huo mzito ikiwakumbusha kuwa Kila Nafsi itaonja mauti na Kwa hakika sisi ni wa Allah (SW) na Kwake TUTAREJEA. Mungu aiwe roho ya marehemu mahali pema Ameen.

Simba kuvuna nini kwa Prisons, Ruvu wapo Mbeya

Simba watakaojiuliza kwa Prisons
Prisona watanusurika katika makucha ya Simba leo Taifa?

Ruvu Shooting watatoka salama uwanja wa Sokoine Mbeya?
Coastal Union kuendeleza ubabe kwa Mgambo JKT leo
KIVUMBI cha Ligi Kuu ya Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa michezo mitano, 'Mnyama' Simba atakuwa dimba la Taifa, Dar es Salaam kujiuliza kwa Prisons Mbeya, wakati maafande wa Ruvu Shooting watakuwa uwanja wa Sokoine Mbeya kupepetana na Mbeya City.
Simba imetoka kukung;utwa baoa 1-0 na Stand United na ina pointi tatu tu toka kwenye mstari wa janga la kushuka daraja, kitu ambacho kimeanza kuwapa hofu mashabiki wao juu ya mwenendo wa timu yao.
Hata hivyo viongozi wamewatuliza mashabiki wao na kuwaambia Prisons hawatoki salama Taifa kwa kupata ushindi, huku maafande hao wakiwajibu kwa kuwaambia 'Thubutu!'
Prisons inaburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo na kocha wake David Mwamaja ameapa iwe isiwe leo ni lazima waue mnyama ili kukusanya pointi zitakazowatoa mkiani.
Maafande hao wana pointi 12 tu na wiki iliyopita iliikomalia Azam na kwenda nao sare ya bila kufungana ikiwa ni siku chache toka ikung'utwe mabao 3-0 na Yanga.
Mechi nyingine zinazochezwa leo ni pambano lililoanza kuzua gumzo kati ya Ruvu Shooting na Mbeya City litakalochezwa jijini Mbeya.
Tayarui Ruvu wameanza kuonyesha mchecheto kwa kudai wametishwa na 'vitendo' vya hujuma toka kwa wenyeji waom, japo wameapa kupambana ili kuvuna pointi kama walivyofanya Yanga wiki iliyopita.
Jijini Tanga kuna 'Tanga Derby' kati ya Mgambo JKT dhidi ya Coastal Union ambayo itashuka dimbani ikiwa chini hya kocha Jamhuri Kihwelu 'Julio' kwa mara ya kwanza.
Mchezo huo unachezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani na Mgambo wanadeni la kipigo cha bao 1-0 walichopewa na wapinzani wao kwenye mchezo wa duru la kwanza.
Julio ametamba kuwa ameenda Coastal kurekebisha makosa na hasa kuwapa stamina wachezaji dosari aliyodai imeikwaza timu hiyo kutiosha, huku Bakar Shime wa Mgambo akisema awe Julio au James Nandwi wao wanataka kulipa kisasi na kujiweka pazuri baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo.
Mjini Shinyanga nako kuna pambano la kutaka na shoka kati ya wenyeji Stand United dhidi ya 'wakuja' Kagera Sugar wanaoutumia uwanja wa Kambarage kama uwanja wao wa nyumbani baada ya kuukimbia CCM Kirummba Mwanza.
Tangu watue Shinyanga Kagera Suagr imekuwa ikipata ushindi wa  bao 1-0 na kuweza kukamata nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo nyuma ya vinara Yanga na Azam ambao wapo kwenye majukumu yao ya kimataifa katika michuano ya KOmbe la Shirikisho na Ligi ya mabingwa Afrika.
nazo timu za Polisi Moro na Mtibwa Sugar ambazo zimekuwa na matokeo ya siyoridhisha katika mechi zao zilizopita zitapepetana kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro katika pambano jingine la 'Derby'.
Mtibwa waliokuwa wakiongoza msimamo wa ligi kabla ya kurudi kichovu toka kwenye Kombe la Mapinduzi itakuwa na kazi kubwa kumalizana na Polisi Moro ambao mechi zao mbili zilizopita walipoteza baada ya kuwa na mwendo nzuri wa kugawa dozi kwa wapinzani wao.
Je ni timu ipi itakayocheza au kununa leo baada ya dakika 90 bila shaka ni jambo la kusbiri kuona.

Vumbi la Ligi Kuu England kutimka hivi

http://i1.chroniclelive.co.uk/incoming/article6534322.ece/alternates/s615/MUFC-v-SAFC.jpgWAKATI macho na masikio ya mashabiki wa soka wanaofuatilia Ligi Kuu ya England yataelekezwa kwenye michezo miwili pekee ya kesho, lakini hata leo kuna mechi kali zinazovuta hisia za wengi.
Pambano la Manchester United iliyotoka kulala ugenini, itakuwa ikivaana na Sunderland, kabla ya kesho wapinzani wao wa jiji la Manchester, Manchester City kuwavuata Liverpool nyumbani kwao Anfield na Arsenal kuwakaribisha Everton.
Chelsea na Tottenham Hotspur wenyewe watakuwa na jukumu moja la kuwania taji la Kombe la Ligi (Capital One) kwwenye uwanja wa Wembley, jijini London.
Ratiba kamili ya ligi hiyo wikiendi hii ipo hivi;
Jumamosi Februari 28
15:45 West Ham v Crystal Palace
18:00 Burnley v Swansea
18:00 Man United v Sunderland
18:00 Newcastle v Aston Villa
18:00 Stoke v Hull
18:00 West Brom v Southampton

Jumapili: Machi 1
15:00 Liverpool v Man City
17:05 Arsenal v Everton
Jumanne: Machi 3
22:45 Aston Villa v West Brom
22:45 Hull v Sunderland 
22:45 Southampton v Crystal Palace

Bao la Ngassa laivusha Yanga Afrika, Azam KMKM kazini

Yanga waliomaliza kibarua chao salama nchini Botswana

Azam watakaoshuka dimbani leo nchini Sudan kujaribu kufuata nyayo za Yanga
Na Rahma Junior
BAO la kufutia machozi lililofungwa na 'Uncle' Mrisho Ngassa, limeiwezesha Yanga kufuzu raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, licha ya kipigo cha mabao 2-1 ilichopewa ugenini na BDF XI.
Goli la Ngassa aliyeiwezesha Yanga kuvuka hatua raundi ya awali na kwenda raundi kwa kwanza kwa jumla ya mabao 3-2, baada ya kushinda 2-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam.
Ngassa alifunga bao hilo dakika ya 30 kuisawazishia Yanga waliompoteza Danny Mrwanda aliyepewa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa ya njano ya pili.
Wenyeji wlaitangulia kufunga bao kabla ya mchezaji wao mmoja kutolewa nje kwa kandi nyekundu kwa kumchezea rafu mbaya Simon Msuva.
Yanga sasa wanajiandaa kuvaana ama na Sofapaka ya Kenya au Plantinum ya Zimbabwe ambao wanarudiana leo mjini Harare baada ya wiki mbili zilizopita Wakenya kulala nyumbani mabao 2-1.
Wawakilishi wengine wa Tanzania, Azam leo watakuwa kibaruani kuumana na Ekl Merreikh ya Sudan katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Azam imeifuata El Merreikh wakiwa na hazina ya ushindi wa mabao 2-0 iliyopata katika mechi wao wa kwanza uliochezwa uwanja wa Chamazi.
Azam inahitaji sare ya aina yoyote au hata kufungwa bao 1-0 kusonga mbele, na viongozi wa klabu hiyo wamenukuliwa wakitamba kuwa wapo kamili kwa vita.
Nazo timu za visiwani Zanzibar, KMKM leo itakuwa na kibarua kigumu cha kurudiana na Al Hilal ya Sudan waliowatandika mabao 2-0 wiki mbili zilizopita.
Wawakilishi wengine wa visiwani hiyo, Polisi wenyewe watashuka dimbani kesho kujaribu kurejesha mabao 5-0 iliyopewa na CF Mounama ya Gabon, jambo ambalo linaonekana kama ni ndoto.

Classic Mawe, Cheka kumaliza ubishi leo uwanja wa Taifa

Mabondia Mwinyi Mzengela (kushoto) na Shomari Milundi wakitunishiana misuri baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano utakaofanyika leo Uwanja wa ndani wa Taifa
Mabondia Mwinyi Mzengela (kushoto) na Shomari Milundi wakitunishiana misuri baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano utakaofanyika leo Uwanja wa ndani wa Taifa

Bondia Fadhili Majiha akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Francis Miyeyusho utakaofanyika leo Uwanja wa ndani wa Taifa

Bondia Epson John wa Morogoro (kushoto) akitunishiana misuli na Vicent Mbilinyi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa katikati ni mratibu Antony Rutta

Bondia Cosmas Cheka (kushoto) akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya pambano lao la ubingwa wa U.B.O Afrika utakaofanyika leo Uwanja wa ndani wa Taifa
Bondia Ibrahim Class akipima uzito kwa ajili ya pambano la UBO Afrika litakalofanyika leo
Bondia Francis Miyeyusho akipima uzito
Bondia Cosmas Cheka (kushoto) akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya pambano lao wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika leo kwenye Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam
BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amejigamba kumpiga bondia Cosmas Cheka kwenye pambano lao la raundi kumi kugombania ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika leo katika Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ibrahim aliyasema hayo wakati wakipima uzito na afya kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo ambalo limevuta hisia za mashabiki wa ndondi kutokana na ubora wa mabondia wote.
“Namfahamu vizuri Cheka ila nitahakikisha nampiga mapema ili kuhakikishia mashabiki kuwa mimi ni bora kuliko yeye”, alijigamba Ibrahim

Pambano huo utatanguliwa na ngumi kali kutoka kwa bondia Fransic Miyeyusho atakayepigana na Fadhili Majiha pambano la raundi nane.

Pia kutakuwepo na pambano lingine la ubingwa kati ya Alibaba Ramadhani na Jacobo Maganga ambalo litasindikizwa na mapambano makali ya bondia chipukizi, Vicent Mbilinyi ambaye ataoneshana umwamba na Epson John wa Morogoro.

 Naye Shomari Milundi atapambana na Mwinyi Mzengela huku Husein Mbonde atakabiliana na Shedrack Ignas na bondia Said Mundi wa Tanga atapambana na Ramadhani Shauri  pia kutakuwepo mapambano mengine mbalimbali kuhakikisha pambano huo unakuwa wa kihistoria na kuacha gumzo.

Pambano hili linasimamiwa na P.S.T chini ya rais wake Emanuel Mlundwa na mashabiki wamehakikishiwa usalama wa mali zao kwani kutakuwa na ulinzi wa kutosha.

Mabondia Mwinyi Mzengela (kushoto) na Shomari Milundi wakitunishiana misuri baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano utakaofanyika leo Uwanja wa ndani wa Taifa

Bondia Fadhili Majiha akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Francis Miyeyusho utakaofanyika leo Uwanja wa ndani wa Taifa

Bondia Epson John wa Morogoro (kushoto) akitunishiana misuli na Vicent Mbilinyi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa katikati ni mratibu Antony Rutta

Bondia Cosmas Cheka (kushoto) akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya pambano lao la ubingwa wa U.B.O Afrika utakaofanyika leo Uwanja wa ndani wa Taifa
Bondia Ibrahim Class akipima uzito kwa ajili ya pambano la UBO Afrika litakalofanyika leo
Bondia Francis Miyeyusho akipima uzito
Bondia Cosmas Cheka (kushoto) akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya pambano lao wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika leo kwenye Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam