STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 28, 2015

MASKINI AZAM! YAANGA AFRIKA KAMA KMKM

Azam waliokumbwa na bahati mbaya Khartoum kwa kung'olewa na El Merreikh
KLABU ya Azam imeungana na wenzao wa KMKM ya Zanzibar kuaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya usiku huu kunyukwa mabao 3-0 na El Merreikh ya Sudan na hivyo kutolewa kwa jumla a mabao 3-2.
Azam walienda Sudan wakiwa na hazina ya mabao 2-0 iliyopata katika mechi ya mkondo wa kwanza wiki mbili zilizopita, lakini wenyeji walitumia nafasi ya kucheza nyumbani kunadili matokea kama kocha wao alivyoatamba mapema na Azam kuaga mashindano. El Merreikh walikosa pia penati baada ya kupaisha.
Hii ni mara ya pili kwa Azam kuaga michuano katika raundi ya mapema baada ya mwaka jana pia kutolewa na timu ya Ferroviaro de Beira ya Msumbiji.
Azam imetoka ikiwa ni saa chache baada ya KMKM nayo licha ya kuopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya El Hilal ya Sudan, ilijikuta ikitoka mashindano kwa ujumla ya mabao 2-1 baada ya mechi ya kwanza nchini Sudan kulala mabao 2-0.
Timu ya Polisi Zanzibar waliokandikwa mabao 5-0 na Mounana ya Gabon kesho itajaribu kuweka rekodi mpya Afrika kama itaweza kuifunga wapinzani wao mabaop 6-0 na kuweza kuungana na Yanga walipenya kwa mbinde jana baada ya kulala 2-1 ugenini lakini ushindi wao wa nyumbani ukawabeba na kusonga mbele.
Yanga inayotarajiwa kutua kesho usiku ikitokea Gaborone, itaumana na Platnum ya Zimbabwe kati ya Machi 13-15 katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo baada ya Wazimbabwe kuing'oa Sofapaka ya Kenya kwa mabao 4-2 kutokana na kushinda leo 2-1 kama ilivyokuwa katika mechi ya mkondo wa kwanza nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment