STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 23, 2014

PSG yabakisha pointi tatu kutetea taji Ufaransa

MABINGWA watetezi wa Ligi ya Ufaransa (Ligue 1) PSG usiku huu imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Evian TG na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji hilo ikibakisha pointi tatu
Bao pekee lililowekwa kimiani na Blaise Mataudi dakika moja kabla ya pambano hilo kwisha lilitosha kuwa ushindi muhimu kaioka pambano hilo lililoshuhudia wageni wa PSG wakicheza pungufu.
Beki Kassim Abdallah wa Evian alilimwa kadi ya njano ya pili dakika ya 61 na kusindikizwa na nyekundu na kuacha pengo kwa timu yake iliyoelekea kuikomalia wenyeji wao kabnla ya Mataudi kufunga bao hilo na kuifanya PSG kufikisha jumla ya pointi 82, 10 zaidi ya Monaco yenye 72.
Timu zote zimecheza michezo 34 na kukasaliwa na mechi nne kila moja kufungia msimu ambapo ushindi wa mechi moja kati ya hizo tatu utaipa nafasi PSG kutete taji hilo kwa mara ya pili mfululizo.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa pia leo, Toulouse ikiwa nyumbani ililazimishwa suluhu ya 0-0 dhidi ya wageni wao Olympique Lyon

Azam kuacha nane, Kocha kutimka zake kesho

Kakolaki atakayesomea ukocha
MABINGWA wapya wa Ligi Kuu Tanzania, Azam imetangaza kuwa mbioni kuwaacha wachezaji nane waliokuwa kwenye kikosi cha timu hiyo.
Kwa mujibu wa Meneja wa klabu hiyo, Jemedari Said akinukuliwa na kupitia kipindi cha michezo cha Magic FM, wachezaji hao wamependekezwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog katika ripoti yake aliyowasilisha kwa uongozi akijiandaa kutimkia kwao kwenye mapumziko mafupi.
Jemedari alisema miongoni mwa wachezaji hao nane waliopendekezwa kutemwa, wawili kati yao akiwemo mkongwe Luckson Kakolaki na majeruhi wa muda mrefu Sameer Haji Nuhu wao watapewa ofa za kusomeshwa ukocha na kupewa majukumu mengine katika brand za SSB.
"Kakolaki ambaye ni mmoja wa wachezaji wakongwe wa klabu hii atapelewa kusomea ukocha ili aje kuinoa timu ya vijana na Sameer anayesumbuliwa na majeraha ya muda mrefu, atapangiwa kazi nyingine katika makampuni baada ya wenyewe kuridhia na kuomba iwe hivyo," alisema Jemedari.
Meneja huyo alidokeza kuwa kocha wao amependekeza pia timu ianze kambi kwa msimu mpya wa ligi asubuhi ya Juni 16.

Burundi kutua nchini kesho kuifuata Stars

Burundi
TIMU ya Taifa ya Burundi 'Intamba Murugamba' inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Intamba Mu Rugamba itakuwa na msafara wa watu 28 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, na itafikia hoteli ya Accomondia. Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10 jioni.
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000. Mechi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Chelsea, Atletico ngoma droo, leo ni Real, Bayern

KLABU ya Chelsea imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya usiku wa jana kulazimishwa sare isiyo na magoli ugenini dhidi na vinara wa La Liga, Atletico Madrid katika pambano la nusu fainali mkondo wa kwanza wa ligi hiyo.
Chelsea ambayo ilimpoteza kipa wake nyota Petr Cech dakika ya 17 baada ya kuumia na baadaye nahodha wake, John Terry pia kwa majeraha, kwa kutoka suluhu hiyo kwenye uwanja wa Vincente Calderon, itahitaji ushindi wowote nyumbani dhidi ya Atletico.
Katika mfululizo wa ligi hiyo usiku huu timu za Real Madrid na mabaingwa watetezi Bayern Munich zitapepetana leo katika mchezo mwingine wa nusu fainali pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, mjini Madrid nchini Hispania.
Pambano hilo linarejesha kumbukumbu ya mechi ya nusu fainali ya Ligi ya mabingwa ya mwaka 2012 ambapo Bayern iliiondosha Madrid kwa mikwaju ya penati na kwenda kufa mikononi  mwa Chelsea kwenye mchezo wa fainali.