STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 23, 2014

Azam kuacha nane, Kocha kutimka zake kesho

Kakolaki atakayesomea ukocha
MABINGWA wapya wa Ligi Kuu Tanzania, Azam imetangaza kuwa mbioni kuwaacha wachezaji nane waliokuwa kwenye kikosi cha timu hiyo.
Kwa mujibu wa Meneja wa klabu hiyo, Jemedari Said akinukuliwa na kupitia kipindi cha michezo cha Magic FM, wachezaji hao wamependekezwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog katika ripoti yake aliyowasilisha kwa uongozi akijiandaa kutimkia kwao kwenye mapumziko mafupi.
Jemedari alisema miongoni mwa wachezaji hao nane waliopendekezwa kutemwa, wawili kati yao akiwemo mkongwe Luckson Kakolaki na majeruhi wa muda mrefu Sameer Haji Nuhu wao watapewa ofa za kusomeshwa ukocha na kupewa majukumu mengine katika brand za SSB.
"Kakolaki ambaye ni mmoja wa wachezaji wakongwe wa klabu hii atapelewa kusomea ukocha ili aje kuinoa timu ya vijana na Sameer anayesumbuliwa na majeraha ya muda mrefu, atapangiwa kazi nyingine katika makampuni baada ya wenyewe kuridhia na kuomba iwe hivyo," alisema Jemedari.
Meneja huyo alidokeza kuwa kocha wao amependekeza pia timu ianze kambi kwa msimu mpya wa ligi asubuhi ya Juni 16.

No comments:

Post a Comment