STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 9, 2013

Tanzanites yasonga mbele, yailaza Msumbiji mabao 5-1

Tanzanite walipong'ara katika mechi ya kwanza hapa Tanzania.

TIMU ya soka ya Vijana ya wanawake, Tanzanite imefanikiwa kuendeleza  manyanyaso yake kwa madada wenzao wa Msumbiji baada ya kushinda ugenini mjini Maputo kwa mabao 5-1.
Ushindi huo umeifanya Tanzanite imesonga mbele kwa jumla ya mabao 15-1 baada ya kupata ushindi wa mabao 10-0 katika pambano lililochezwa wiki mbili zilizopita nchini Tanzania.
Mabao ya ushindi ya Tanzanite katika mchezo wa leo yametumbukizwa kimiani na Selda Boniface aliyefunga matatu, Vumilia Maarifa, na Dionisia Athanas waliofunga bao moja kila mmoja.
Tanzanits sasa inasubiri kucheza ama na Botswana au Afrika Kusini kwa ajili ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani.
MICHARAZO inawapa pongezi vijana hao pamoja na kocha wake Kaijage kwa kuitoa kimasomaso Tanzania licha ya ugeni wao katika michuano mikubwa kama hiyo.

No comments:

Post a Comment