STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 9, 2013

Borussia Dotmund yafa tena, Bavarian waifumua Augusburg

Frank Ribery mmoja wa wauaji wa leo wa Bavarian

SIKU chache tangu itokee kupata kipigo nyumbani cha bao 1-0 toka kwa Arsenal, Borussia Dotmund jioni hii imeendelea kuumizwa baada ya kunyukwa mabao 2-1 na Wolfsburg katika mechi za Ligi ya Ujerumani, huku wapinzani wao wa karibu katika kuwania ubingwa wakipata ushindo mnono.
Dotmund ilikumbana na kipigo hicho ugenini kupitia mabao ya Ricardo Rodriguez na Ivica Olic waliochomoa bao la kipindi cha kwanza la wageni hao lililofungwa na Marco Reus.
Mabingwa watetezi Bayern Munich ameendelea kupata ushindi kwa asilimia 100 baada ya kuinyuka Augsburg kwa mabao 3-0, huku Shalke 04 kuzinduka kwa kuinyuma Werder Bremen kwa mabao 3-1 na Bayer Leverkusen iliikung'uta Humburger SV kwa magoli 5-3, Hertha BSC ilipata ushindi nyumbani kwa mabao 3-2 dhidi ya Hoffenheim.
No comments:

Post a Comment