STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, May 30, 2013

M to the P hatimaye azindua na kumuulizia Ngwair

 
 
BAADA ya kuwa katika hali mbaya, hatimaye M To The P amezinduka na kuanza kuuliza kuhusiana na rafiki yake Mangwea
M To The P alipelekwa kwenye wodi ya wagonjwa wa kawaida leo mchana.

“Kweli anaendelea vizuri sana, sasa amepelekwa kwenye wodi ya wagonjwa wa kawaida,” alisema Ruta Bushoke, msanii wa muziki wa kizazi kipya anayeishi nchini humo.

Lakini baadaye Mtanzania mwingine anayeishi nchini humo alisema M To The P amezinduka.

“Jamaa anauliza Ngwea yuko wapi, sasa tunashindwa hata kumjibu. Lakini kuna wengine wamemuambia kwamba atakuja hivi karibuni. Ametoka kidogo,” alisema.

Mangwea na M To The P walikutwa na mkasa ambao ulipelekea Ngwea kuaga dunia nay eye kubaki akiwa katika hali mbaya.

Ashanti United haina mpango na 'Mafaza'

Kikosi cha Ashanti kilichopanda Ligi Kuu

Kocha Mbaraka Hassani

Wakati wa Ashanti wakipewa maelekezo na kocha waoKLABU ya soka ya Ashanti United iliyorejea tena kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, imeweka bayana kuwa itafanya usajili wake kwa wachezaji vijana wenye uwezo kisoka badala ya kuwakimbilia 'mafaza' wakiwa na lengo la kutaka kuendelea kuzionyesha mfano klabu nyingine umuhimu wa kuzalisha 'jeshi' lao wenyewe.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbaraka Hassani aliiambia MICHARAZO kwenye mazoezi ya timu hiyo uwanja wa Msimbazi, kwamba hawatawapapatikia mafaza kwa kuhofia kuja kujichanganya mbele ya safari ilihali wamejiwekea mikakati ya kutotaka kurudi walipotoka ambapo walisota kabla ya kurudia Ligi Kuu.
Mbaraka ambaye ndiye aliyeipandisha mwaka 2004 kabla ya kuzama msimu wa 2007-2008, alisema kutoa nafasi kwa vijana kutasaidia kuwatangaza wachezaji hao kama walivyofanya miaka ya nyuma na kuwaibua mastaa kadhaa  wanaotamba hivi sasa katika soka la Tanzania.
Baadhi ya nyotga hao ni pamoja na kipa wa kutumainiwa wa Yanga, Ally Mustafa Barthez, Jabir Aziz, Juma Jabu, Mohammed Kijuso, Juma Nyosso, Deo Ngassa na wengineo.
"Hatujaanza rasmi kufanya usajili, lakini tukianza tutajikita kwa vijana zaidi kwa lengo la kuwapa nao nafasi ya kuonwa, si unajua Ashanti ni kama chuo kazi yetu kuzalisha wengine wachukue ndivyo tutakavyofanya hata safari hii kwa vile tumepania kuonyesha mfano kwa klabu nyingine," alisema Mbaraka.
Mbaraka, alisema anaamini kuwapa nafasi vijana kunasaidia kukuza soka la Tanzania kuliko kuendelea sera ya kung'ang'ania wachezajki wenye majina ambao mara nyinbgi usumbua hasa kwenye suala la masilahi ikizingatiwa klabu yao haina wafadhili zaidi ya wanachama na wadau wake kuchangishana fedha kuiendesha.
Ashanti imerejea ligi kuu msimu ujao pamoja na klabu za Rhino Rangers ya Tabora na Mbeya City na wanaendelea kupima wachezaji kwa ajili ya kupata itakaowasajili.

Ombaomba feki akiona cha moto Iringa

WAKAZI wa mjini Iringa hivi karibuni wameshuhudia kituko cha mwaka baada ya kumnasa mzee mmoja akijifanya ombaomba kwa kuigiza ulemavu asiokuwa nao.

Ombaomba huyo feki alijifanya hana mkono wa kushoto na mguu wa kulia na kuweka pozi la kuomba kama vile ni mlemavu katika eneo la Hazina Ndogo, mjini hapa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mlemavu huyo feki ameumbuliwa na mtu mmoja ambaye alimuona asubuhi ya siku ya tukio akiwa hana ulemavu wowote kabla ya kumkuta mchana akiomba kwa kujifanya ni mlemavu wa mkono na mguu.
Mtu huyo aliwaambia baadhi ya wananchi siri ya ombaomba huyo na kuwafanya kupandwa na hasira na kuanza kumshushia kipigo wakitaka kuhakikisha kama kweli ni mzima kiasi cha kumuumiza usoni.
Kwa hofu ya kuuawa, mlemavu huyo feki alijinusuru kwa kuonesha mkono wake wa kushoto aliokuwa ameuficha ndani ya koti alilolivaa na mguu aliokuwa ameukunja na kuukalia.
Wakati wananchi wenye hasira wakiendelea kumpiga, mzee huyo alijitahidi kupata upenyo na kutimua mbio ndefu kukimbilia eneo la Miyomboni na kuwaacha watu wengine wakiwa hawana mbavu kwa vicheko.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walipoongea na mwandishi wetu walisema wakati mwingine ombaomba huyo hujifanya bubu na kuwaomba watu fedha za matibabu.
Inadaiwa kuwa hii si mara ya kwanza kwa ombaomba huyo kushtukiwa akifanya mchezo huo, awali alishawahi kufukuzwa katika Kitongoji cha Santoni mjini hapa.


“Bahati yake amekimbia kama tukimkuta tena akijidai ni mlemavu tutamvunja mkono na mguu ili awe mlemavu kweli,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Tuhuma nyingine zinasema kuwa ombaomba huyo hutumia mbinu hizo za kitapeli kwa kuwa amekimbiwa na mpenzi kutokana na kutokuwa na kipato.
Wananchi hao wenye hasira wameutaka uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana ombaomba wote wanatumia udanganyifu kujipatia fedha na kutaka kuwepo kwa utaratibu maalum wa kuwasaidia wanaohitaji misaada ya kweli.

Matokeo Mapya ya Kidato cha Nne haya hapaWaziri wa Elimu na Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa aliyetangaza matokeo hayo leo

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
   

TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)  ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012
1.0          UTANGULIZI


MtihaniwaKidatochaNne, 2012ulifanyikanchinikotekuanziatarehe8/10-25/10/2012. Baraza la Mitihani la Tanzaniakatikakikaochakecha 94 kilichofanyikatarehe 30 Mei, 2013 liliidhinishamatokeo haya

2.0          USAJILI NA MAHUDHURIO


Jumlayavituo5,058vilitumikakatikakufanyamtihanihuoikilinganishwa na vituo4,795vilivyotumikamwaka 2011.

2.1          TaarifazaWatahiniwa

Jumlayawatahiniwa480,029  walisajiliwakufanyaMtihaniwaKidatochaNne 2012 wakiwemowasichana217,587sawa na asilimia45.33 na wavulana262,442sawa na asilimia54.67.WatahiniwawaliofanyamtihaniwaKidatochaNne 2012  ni 458,139sawa na asilimia95.44.Watahiniwa21,890 sawa na asilimia4.56yawatahiniwawotewaliosajiliwa, hawakufanyamtihani.2.2          WatahiniwawaShule


Watahiniwawashulewaliosajiliwa ni  411,225 wakiwemowasichana182,982sawa na asilimia44.50 na wavulana228,243sawa na asilimia55.50.Watahiniwawashulewaliofanyamtihaniwalikuwa397,138sawa na asilimia96.57. Aidha, watahiniwa14,087sawa na asilimia3.43 hawakufanyamtihanikutokana na sababumbalimbalizikiwemoutoro, ugonjwa na vifo.

2.3          WatahiniwawaKujitegemea


Watahiniwawakujitegemeawaliosajiliwawalikuwa ni 68,804wakiwemowasichana34,605 sawa na asilimia50.30 na wavulana34,199sawa na asilimia49.70.Watahiniwa61,001 wakiwemowasichana 30,918 nawavulana 30,083  wamefanyamtihaniwakatiwatahiniwa7,803 sawa na asilimia 11.34 hawakufanyamtihani.
3.0          MATOKEO YA MTIHANI

3.1          Maandaliziyamatokeo


MatokeoyaMtihaniwaKidatochaNnemwaka 2012 yalitangazwatarehe 18 Februari 2013 na kufutwaMachi 2013 kutokana na sababuzakitaalamukatikamatumiziyataratibuzakuchakatamatokeo. MatokeoyaliyofutwayalikuwayamechakatwakwakutumiautaratibuwaFixed Grade Ranges. MatokeoyanayotangazwasasayamechakatwakwautaratibuhuohuolakiniyamefanyiwaStandalization.


Kimataifakunaainakuumbilizakuchakatamatokeoyamtihani : Flexible ‘Grade Ranges na Fixed Grade Ranges’.


‘Flexible Grade Ranges’ hutumiaviwangotofautikuchakatamatokeoyawatahiniwakwakuzingatiakiwangochaufauluchasomohusikakwakilamwaka. Hivyoviwangovyakuchakatamatokeohubadilikakilamwakakulingana na ufauluwawatahiniwakwakilasomohusika.


Katikamfumowa ‘Fixed Grade Ranges’ viwangovyaainamojahutumikakuchakatamatokeokwamasomoyote bila kujalikiwangochakufaulukwasomohusika. Viwangovyakuchakatamatokeohutumikahivyohivyokilamwaka bila mabadiliko.


KwamiakamingiBaraza la Mitihani la Tanzanialimekuwalikitumiamfumowa ‘Flexible Grade Ranges’. Mwaka 2012, mfumowa ‘Fixed Grade Ranges’ ulitumikakuchakatamatokeokwamaraya kwanza


Mabadilikohayoyalitokana na maoniyawadauyaliyotokana na utafitiuliofanywa na Wizaramwaka 2010 kufuatiakushukakwaufauluwamtihaniwaKidatochaNnemwakahuo. Pia kwakuzingatiamaelekezoyaTumemaalumiliyochunguzadosarizilizojitokezakwenyematokeoyamtihaniwaKidatocha Sita mwaka 2012 katikasomo la IslamicKnowledge.

3.2 MatokeoyaWatahiniwawaShule


Jumlayawatahiniwawashule159,609katiyawatahiniwa397,138


waliofanyaMtihaniwaKidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichanawalikuwani60,751nawavulanawalikuwani98,858.
3.3 MatokeoyaWatahiniwawaKujitegemea

Idadiyawatahiniwawakujitegemeawaliofaulumtihanini26,191 katiyawatahiniwa61,001 waliofanyamtihani. Wasichanawaliofauluni11,581nawavulanani14,910.

4.0          UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI

Uborawaufaulukwakuangaliamadarajawaliyopatawatahiniwawashuleunaoneshakuwajumlayawatahiniwa35,349wamefaulukatikamadaraja I – III ambapokatiyaowasichanani10,924 nawavulanani24,425.

 MchanganuowaufaulukwakiladarajakwajinsikwaWatahiniwawaShulemwaka 2012 nikamaifuatavyo:Wavulana
Wasichana
Jumla
Idadi
Asilimia
Idadi
Asilimia
Idadi
Asilimia
I
2,179
1.07
1,063
0.64
3,242
0.88
II
7,267
3.58
3,088
1.85
10,355
2.8
III
14,979
7.37
6,773
4.05
21,752
5.87
I-III
24,425
12.02
10,924
6.54
35,349
9.55
IV
74,433
36.65
49,827
29.78
124,260
33.54
I-IV
98,968
48.66
60,779
36.30
159,747
43.08
0
104,259
51.33
106,587
53.7
210,846
56.92
5.0      SHULE KUMI BORA NA SHULE KUMI ZA MWISHO

Uborawashuleumepangwakwakutumiakigezo cha “Grade Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 na F = 5.  Shulezimegawanywakatikamakundimawilikulingananaidadiyawatahiniwakamaifuatavyo:


(i)            Shulezenyewatahiniwa40 na zaidi  (Jumlani 3,396)


(ii)           Shulezenyewatahiniwapungufuya 40 (Jumlani  753).

5.1     Shule Kumi bora katikakundi la shulezenyewatahiniwa 40 na zaidi

Shulezifuatazozimepangwakwakuanzanaya kwanza hadiyakumikatikakundi la shulezenyewatahiniwa40nazaidi.
NAFASI
JINA LA SHULE
IDADI
MKOA
RANK
CENTRE NAME
REGISTERED
REGION
1
ST. FRANCIS GIRLS  S  S
90
MBEYA
2
MARIAN BOYS'  S S
75
PWANI
3
FEZA BOYS' S S
69
DAR ES SALAAM
4
MARIAN GIRLS S  S
88
PWANI
5
CANOSSA S S
66
DAR ES SALAAM
6
FEZA GIRLS' S S
50
DAR ES SALAAM
7
ROSMINI S S
78
TANGA
8
ANWARITE GIRLS  S S
49
KILIMANJARO
9
ST. MARY'S MAZINDE JUU S S
83
TANGA
10
JUDE MOSHONO SS
51
ARUSHA
5.2     ShuleKumizamwishozenyewatahiniwa 40 nazaidi

Shulezifuatazozimepangwakwakuanzanaya kwanza hadiyakumikutokamwisho.


NAFASI
JINA LA SHULE
IDADI
MKOA
1
MIBUYUNI  S  S
40
LINDI
2
MAMNDIMKONGO S  S
63
PWANI
3
CHITEKETE  S  S
57
MTWARA
4
KIKALE   S  S
60
PWANI
5
ZIRAI   S S
41
TANGA
6
MATANDA SECONDARY SCHOOL
53
LINDI
7
KWAMNDOLWA   S  S
89
TANGA
8
CHUNO   S.  S
143
MTWARA
9
MBEMBALEO S  S
56
MTWARA
10
MAENDELEO S  S
103
DAR ES SALAAM

5.3          ShuleKumi bora katikakundi la shulezenyewatahiniwachiniya 40

Shulezifuatazozimepangwakwakuanzanaya kwanza hadiyakumikatikakundi la shulezenyewatahiniwa 40 nazaidi.

NAFASI
JINA LA SHULE
IDADI
MKOA
1
THOMAS MORE MACHRINA SS  S
20
DAR ES SALAAM
2
QUEEN OF APOSTLES-USHIROMBO SEMINARY
24
SHINYANGA
3
BETHELSABS GIRLS   S  S
33
IRINGA
4
PRECIOUS BLOOD   S  S
34
ARUSHA
5
MAUA SEMINARY
31
KILIMANJARO
6
ST. MARY'S JUNIOR SEMINARY
28
PWANI
7
CARMEL  S    S
36
MOROGORO
8
SANU SEMINARY
37
MANYARA
9
BROOKEBOND  S  S
27
IRINGA
10
ST.CAROLUS SECONDARY   S  S
37
SINGIDA
5.4     Shulekumi (10) zamwishozenyewatahiniwachiniya 40

Shulezifuatazozimepangwakwakuanzanaya kwanza hadiyakumikutokamwisho.


NAFASI
JINA LA SHULE
IDADI
MKOA
1
DODEANI TECH.    S  S
10
PEMBA
2
KALAMBA    S  S
11
DODOMA
3
HURUI    S   S
12
DODOMA
4
USUNGA    S   S
13
TABORA
5
MANDWANGA    S  S
13
LINDI
6
BETTY MITCHEL  S   S
17
MOROGORO
7
CHONGOLEANI   S  S
17
TANGA
8
MMULUNGA   S   S
17
MTWARA
9
NYUAT    S   S
20
ARUSHA
10
MWAKIJEMBE    S   S
13
TANGA
6.0.      HITIMISHO


KuanziasasamatokeoyamithaniyakidatochaNne na Sita yatachakatwakwakutumiaFixed Grade Range na Standardisation. Natoawitokwawadauwotewaelimukutoaushirikianotuwezekuboreshaelimunchini.
7.0.        KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012

MatokeoyaMtihaniwaKidatochaNne (CSEE), 2012 yanapatikanakatikatuvutizifuatazo :


·         www.matokeo.necta.go.tz


·         www.necta.go.tz


·         www.udsm.edu.ac.tz, au


·         www.moe.go.tz


  


Mhe. Dkt. ShukuruKawambwa (Mb)


WaziriwaElimu na MafunzoyaUfundi30/5/2013
******************************************
MATOKEO YA AWALI YALIYOFUTWA YALIKUWA HIVI

TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)

ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012


1.0                 UTANGULIZI

Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012.  Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :


2.0                 MTIHANI WA MAARIFA (QT)

2.1           Usajili na Mahudhurio

Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176

Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani. 


2.2          Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT)

Watahiniwa 5,984 kati ya 17,137 waliofanya mtihani wamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).


3.0                 MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012

Jumla ya vituo 5,058 vilitumika katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa wa kujitegemea.


3.1                 Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa

(a)           Watahiniwa Wote

Jumla ya watahiniwa 480,036 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67.  Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012  ni 456,137 sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa 21,820 sawa na asilimia 4.55 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya mtihani.


(b)            Watahiniwa wa Shule

Watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 411,230 wakiwemo wasichana 182,978 sawa na asilimia 44.50 na wavulana 228,252 sawa na asilimia 55.50.  Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57. Aidha, watahiniwa 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro,  ugonjwa na vifo.

(c)             Watahiniwa wa Kujitegemea

Watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 68,806 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia 50.29 na wavulana 34,201 sawa na asilimia 49.71. Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,917 na wavulana 30,084  wamefanya mtihani wakati watahiniwa 7,730 sawa na asilimia 11.23  hawakufanya mtihani.


4.0                 MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE


(a)                 Watahiniwa wa Shule

Jumla ya watahiniwa wa shule 126,847 kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 46,161 na wavulana ni 80,686.


(b)                Watahiniwa wa Kujitegemea

Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 16,112 kati ya watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani.  Wasichana waliofaulu ni 6,751 na wavulana ni 9,361. 5.0                 UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI

Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,520 wamefaulu katika madaraja I – III ambapo kati yao wasichana ni 7,178 na wavulana ni 16,342.


Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:Idadi ya Wavulana
Idadi ya Wasichana
Jumla
I
1,073
568
1,641
II
4,456
1,997
6,453
III
10,813
4,613
15,426
I-III
16,342
7,178
23,520
IV
64,344
38,983
103,327
0
120,664
120,239
240,903


6.0        SHULE ISHIRINI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI

Ubora wa ufaulu wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 hadi F = 5.  Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule ya kwanza hadi ya ishirini zimeainishwa kwenye Jedwali lifuatalo :

NAFASI
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
ST. FRANCIS GIRLS
90
MBEYA
2
MARIAN BOYS S.S
75
PWANI
3
FEZA BOYS S.S
69
DAR ES SALAAM
4
MARIAN GIRLS S.S
88
PWANI
5
ROSMINI  S S
78
TANGA
6
CANOSSA S.S
66
DAR ES SALAAM
7
JUDE MOSHONO S S
51
ARUSHA
8
ST. MARY’S  MAZINDE JUU
83
TANGA
9
ANWARITE GIRLS S S
49
KILIMANJARO
10
KIFUNGILO  GIRLS S S
86
TANGA
11
FEZA GIRLS
49
DAR ES SALAAM
12
KANDOTO SAYANSI GIRLS SS
124
KILIMANJARO
13
DON BOSCO SEMINARY SS
43
IRINGA
14
ST.JOSEPH MILLENIUM
133
DAR ES SALAAM
15
ST.JOSEPH’S ITERAMBOGO SS
64
KIGOMA
16
ST.JAMES SEMINARY SS
44
KILIMANJARO
17
MZUMBE SS
104
MOROGORO
18
KIBAHA SS
108
PWANI
19
NYEGEZI SEMINARY SS
68
MWANZA
20
TENGERU BOYS SS
76
ARUSHA


7.0        SHULE KUMI AMBAZO HAZIKUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI

NAFASI
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
MIBUYUNI S.S
40
 LINDI
2
NDAME  S.S
41
UNGUJA
3
MAMNDIMKONGO S.S
63
PWANI
4
CHITEKETE S.S
57
MTWARA
5
MAENDELEO S.S
103
DAR ES SALAAM
6
KWAMNDOLWA S.S
89
TANGA
7
UNGULU S.S
62
MOROGORO
8
KIKALE S.S
60
PWANI
9
NKUMBA S.S
152
TANGA
10
TONGONI S.S
56
TANGA


8.0           TATHMINI YA UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

8.1           Tathmini ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule mbalimbali inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.  Aidha, shule zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:

(i)         Baadhi ya shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na pia zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;

(ii)        Kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba kwa ajili ya kujisomea; na

(iii)       Upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.

8.2           Mkakati wa Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya mambo yafuatayo:

(i)             Kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012 Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imeajiri walimu 12,973 ambao wamepangwa katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na wastani wa walimu 2-3 kwa shule.  Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.

(ii)            Kuboresha miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara na nyumba za walimu.

(iii)           Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50 ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kitaaluma.

(iv)           Wizara kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule.

(v)            Wizara itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na kuwawezesha Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa ndani katika Shule za Sekondari zilizo katika maeneo yao.


9.0           MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA


Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:

(a)           Watahiniwa 28,582 wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada wanayodaiwa pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.

(b)           Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71 waliofanya Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012 bila ya kulipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada hiyo katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.


10.0        MATOKEO YA MITIHANI  YALIYOFUTWA


10.1              Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Udanganyifu


Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo yao yote ya mtihani kwa mujibu wa kifungu Na.52(b) cha Kanuni za Mitihani baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika mitihani ya Oktoba 2012. Kati yao, watahiniwa wa shule ni 624 na watahiniwa wa kujitegema ni 148 na watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa (QT) ni 17.


Aina ya udanganyifu uliobainika na idadi ya watahiniwa husika ni kama ifuatavyo:S/N
AINA YA UDANGANYIFU
IDADI YA WATAHINIWA
(i)        
Watahiniwa kubainika kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika skripti ya somo moja au zaidi ya moja.
04
(ii)       
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa na ‘notes.’
170
(iii)      
Watahiniwa kubainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu.
590
(iv)      
Watu kukamatwa wakiwafanyia watahiniwa wengine mtihani ‘impersonation”.
04
(v)       
Watahiniwa kukamatwa na simu ndani ya chumba cha mtihani.
06
(vi)      
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi wakibadilisha karatasi za maswali au skripti kwa lengo la kufanya udanganyifu.
15

JUMLA
789


10.2              Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Watahiniwa Kuandika Matusi Katika Skripti Zao

(i)          Jumla ya watahiniwa 24 waliandika matusi kwenye skripti zao za masomo mbalimbali. Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5(13) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:

Written responses to any examination question which carry words, drawings or pictures connected to sex or abusive language in such a way that it becomes offensive shall consitute an examination offence and a candidate who commits such an offence shall be punished by the Council.”


Kutokana na kosa hilo Baraza la Mitihani limefuta matokeo  yao yote kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2)(a) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka: 

“A candidate found to have committed an examination offence shall - (a) have his examination results nullified”

(ii)         Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu (skripti) kinaonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Serikali haitaweza kuwavumilia hata kidogo watahiniwa wa aina hiyo. Hivyo, Serikali itaangalia hatua zaidi za kisheria za kuchukua dhidi ya watahiniwa wote walioandika matusi.

Kwa mujibu wa kifungu Na. 6(2)(b) cha Kanuni za Mitihani, watahiniwa wote waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani au kuandika matusi katika skripti zao hawataruhusiwa kufanya mitihani inayoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania  kwa kipindi cha mwaka mmoja (01) kuanzia tarehe ya kutangazwa kwa matokeo.


11.0        KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA CSEE na QT, 2012


(a)           Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), 2012  yanapatikana katika tovuti zifuatazo: 

·               www.matokeo.necta.go.tz,

·               www.necta.go.tz,     

·               www.udsm.edu.ac.tz, au

·               www.moe.go.tz


(b)           Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya  ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe andika:


MATOKEOXNAMBA YA KITUOXNAMBA YA MTAHINIWA

(Mfano : matokeoxS0101x0503)
Dkt.  Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)


WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

18 Februari 2013