STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 7, 2014

Nimenja Vidic aanza kuaga rasmi Old Trafford

115865491_football_356415c
Nahodha wa klabu ya Manchester United Nemanja Vidic amethibitisha rasmi kwamba ataondoka Manchester United baada ya msimu wa huu kuisha.
Katika taarifa yake aliyotoa kwa mtandao rasmi wa ManUtd.com, beki huyo kutoka Serbia alisemathe: “Ni mwaka wa mwisho wa mkataba wangu na nimekuwa na miaka nane mizuri nikiwa hapa. Muda wangu katika klabu hii kubwa siku zote utabaki kuwa kumbukumbu yangu zaidi katika maisha yangu ya soka.
“Sikuwahi kufikiria kama ningeshinda makombe 15 na kwa hakika sitousahau usiku ule mkubwa jijini Moscow, kumbukumbu zile nitaishi nazo milele. Hata hivyo, nimefikia uamuzi kwamba nitaondoka klabuni mwishoni mwa msimu huu. Nataka kujipa changamoto mpya kwa mara nyingine na kujaribu kufanya vizuri zaidi katika miaka ijayo.
“Sifikirii kuendelea kubakia England kwa sababu klabu pekee ambayo nilitaka kuichezea nchi hii ni Manchester United na nilipata bahati kubwa ya kuwa sehemu ya klabu hii kwa miaka mingi. Nina machaguo kadhaa na nitachagua chaguo la timu nzuri kwangu na familia yangu.
“Kwa sasa nitaweka umakini na jitihada zangu zote katika kuichezea Manchester United na kujituma kwa kila hali mpaka mwisho wa msimu.Natumaini taarifa hii inatosha kuachwa kusambaza tetesi zozote kuhusu hatma yangu.”

Babi ang'ara Malaysia, licha timu yake kulala 1-0

Abdi Kassim (wa kwanza kulia mbele) akiwa na kikosi cha timu yake ya UiTM
 KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Malaysia, Abdi Kassim 'Babi' leo amechaguliwa kuwa Nyota wa Mchezo (Man of the Match) baada ya kung'ara katika pambano la Ligi Kuu ya nchi hiyo, licha ya timu yake ya UiTM kulazwa bao 1-0 ugenini.
UiTM iliifuata Palau Pinang kwenye uwanja wao wa Bandaraya, mjini Penang na kukumbana na kichapo hicho kinachoifanya timu hiyo kusaliwa na pointi zao nne ikijikusanyia pointi nne kutokana na mechi tatu ilizocheza mpaka sasa katika ligi.
Hata hivyo kiwango alichokionyesha mchezaji, kilimfanya kuchaguliwa nyota pambano hilo, kitu ambacho mwenyewe amekielezea kama faraja kubwa kwake tangu atue nchini humo kucheza soka la kulipwa akitokea KMKM aliyoichezea kwa kipindi kifupi.
Akizungumza na MICHARAZO, Babi alisema pambano lao la leo lilikuwa kali na lenye ushindani kutokana na wenyeji kuwakamia, lakini alionyesha uwezo mkubwa na mwishoni pamoja na timu yao kulala alitangazwa Mchezaji Bora.
"Licha ya timu yetu kupoteza pambano letu la leo ugenini, lakini nashukuru nimeweza kung'ara na kuchaguliwa mchezaji bora kwa kiwango cha soka nilichoonyesha, nimefarijika na ninapigana zaidi ili kufanya vizuri na kuisaidia timu yangu,' alisema Babi.
Babi alisema timu yake itashuka tena dimbani siku ya Jumatatu kuikaribisha timu ya PDRM katika pambano jingine la ligi hiyo inayozidi kushika kasi tangi ilipoanza Januari 24.

Hii ndiyo taarifa rasmi ya uteuzi wa Wabunge wa Bunge la Katiba


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
UTANGULIZI
1.    Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.

2.    Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i)    Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii)    Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii)    Wajumbe 201 kwa mujibu wa  Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.

3.    Makundi hayo ni  kama ifuatavyo:-

(i)    Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii)    Taasisi za Kidini (20)
(iii)    Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv)    Taasisi za Elimu (20);
(v)    Watu wenye Ulemavu (20);
(vi)    Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii)    Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii)    Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix)    Vyama vya Wakulima (20); na
(x)    Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).

4.    Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
5.    Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

6.    Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.

7.    Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:
1.   

Na.    Kundi/Taasisi    Taasisi zilizoleta mapendekezo    Idadi ya Watu Waliopendekezwa    Idadi ya Wajumbe Wanaotakiwa    Idadi ya Walioteuliwa      
        Tanzania Bara    Zanzibar    Tanzania Bara    Zanzibar        Tanzania Bara    Zanzibar      
1.        Taasisi zisizokuwa za Kiserikali    246    98    1,203    444    20    13    7      
2.        Taasisi za Kidini    55    17    344    85    20    13    7      
3.        Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu    21    14    129    69    42    28    14      
4.        Taasisi za Elimu    9    9    84    46    20    13    7      
5.        Makundi ya Walemavu    24    6    97    43    20    13    7      
6.        Vyama vya Wafanyakazi    20    1    89    13    19    13    6      
7.        Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji    8    1    43    4    10    7    3      
8.        Vyama vinavyowakilisha Wavuvi    7    3    45    12    10    7    3      
9.        Vyama vya Wakulima    22    8    115    44    20    13    7      
10.        Makundi yenye Malengo Yanayofanana    142    21    613    114    20    14    6      
    Mapendekezo Binafsi    -    -    118    -                  
    Jumla    672    178    2,880    874    201    134    67      
    Jumla Kuu    850    3,754               

8.    Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
9.    Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
10.    Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a)    Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana, watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b)    Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
(c)    Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.
Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:



TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20)      
TANZANIA BARA (13)      
1.    Magdalena Rwebangira     2.    Kingunge Ngombale Mwiru      
3.    Asha D. Mtwangi    4.    Maria Sarungi Tsehai      
5.    Paul Kimiti    6.    Valerie N. Msoka      
7.    Fortunate Moses Kabeja    8.    Sixtus Raphael Mapunda      
9.    Elizabeth Maro Minde    10.    Happiness Samson Sengi      
11.    Evod Herman Mmanda    12.    Godfrey Simbeye      
13.    Mary Paul Daffa          
TANZANIA ZANZIBAR (7)      
1.    Idrissa Kitwana Mustafa    2.    Siti Abbas Ali      
3.    Abdalla Abass Omar    4.    Salama Aboud Talib      
5.    Juma Bakari Alawi    6.    Salma Hamoud Said      
7.    Adila Hilali Vuai          
          
TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)      
TANZANIA BARA (13)      
1.    Tamrina Manzi    2.    Olive Damian Luwena      
3.    Shamim Khan    4.    Mchg. Ernest Kadiva      
5.    Sheikh Hamid Masoud Jongo    6.    Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela      
7.    Magdalena Songora    8.    Hamisi Ally Togwa      
9.    Askofu Amos J. Muhagachi    10.    Easter Msambazi      
11.    Mussa Yusuf Kundecha    12.    Respa Adam Miguma      
13.    Prof. Costa Ricky Mahalu          
TANZANIA ZANZIBAR (7)      
1.    Sheikh Thabit Nouman Jongo    2.    Suzana Peter Kunambi      
3.    Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu    4.    Fatma Mohammed Hassan      
5.    Louis Majaliwa    6.    Yasmin Yusufali E. H alloo      
7.    Thuwein Issa Thuwein          

          
VYAMA VYOTE VYA SIASA
VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42)      
TANZANIA BARA (28)      
1.    Hashim Rungwe Spunda    2.    Thomas Magnus Mgoli      
3.    Rashid Hashim Mtuta    4.    Shamsa Mwangunga      
5.    Yusuf  S. Manyanga    6.    Christopher Mtikila      
7.    Bertha Ng’angompata    8.    Suzan Marwa      
9.    Dominick Abraham Lyamchai    10.    Mbwana Salum Kibanda      
11.    Peter Kuga Mziray    12.    Isaac Manjoba Cheyo      
13.    Dr. Emmanuel John Makaidi    14.    Prof. Ibrahim Haruna Lipumba      
15.    Modesta Kizito Ponera    16.    Prof. Abdallah Safari      
17.    Salumu Seleman Ally    18.    James Kabalo Mapalala      
19.    Mary Oswald Mpangala    20.    Mwaka Lameck Mgimwa      
21.    Nancy  S. Mrikaria    22.    Nakazael Lukio Tenga      
23.    Fahmi Nasoro Dovutwa    24.    Costantine  Benjamini Akitanda       
25.    Mary Moses Daudi    26.    Magdalena Likwina      
27.    John Dustan Lifa Chipaka    28.    Rashid Mohamed Ligania Rai      
TANZANIA ZANZIBAR (14)      
1.    Ally Omar Juma    2.    Vuai Ali Vuai      
3.    Mwanaidi Othman Twahir    4.    Jamila Abeid Saleh      
5.    Mwanamrisho Juma Ahmed    6.    Juma Hamis Faki      
7.    Tatu Mabrouk Haji    8.    Fat –Hiya Zahran Salum      
9.    Hussein Juma    10.    Zeudi Mvano Abdullahi      
11.    Juma Ally Khatibu    12.    Haji Ambar Khamis      
13.    Khadija Abdallah Ahmed    14.    Rashid Yussuf Mchenga   



TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)      
TANZANIA BARA      
1.    Dr. Suzan Kolimba    2.    Prof. Esther Daniel Mwaikambo      
3.    Dr. Natujwa Mvungi    4.    Prof. Romuald Haule      
5.    Dr. Domitila A.R. Bashemera    6.    Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa      
7.    Prof. Bernadeta Kilian    8.    Teddy Ladislaus Patrick      
9.    Dr. Francis Michael    10.    Prof. Remmy J. Assey      
11.    Dr. Tulia Ackson    12.    Dr. Ave Maria Emilius Semakafu      
13.    Hamza Mustafa Njozi          
TANZANIA ZANZIBAR (7)      
1.    Makame Omar Makame    2.    Fatma Hamid Saleh      
3.    Dr. Aley Soud Nassor    4.    Layla Ali Salum      
5.    Dkt. Mwinyi Talib Haji    6.    Zeyana Mohamed Haji      
7.    Ali Ahmed Uki          
          
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)      
TANZANIA BARA (13)      
1.    Zuhura Musa Lusonge    2.    Frederick Msigala      
3.    Amon Anastaz Mpanju    4.    Bure Zahran      
5.    Edith Aron Dosha    6.    Vincent Venance Mzena      
7.    Shida Salum Mohamed    8.    Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.      
9.    Elias Msiba Masamaki    10.    Faustina Jonathan Urassa      
11.    Doroth Stephano Malelela    12.    John Josephat Ndumbaro      
13.    Ernest Njama Kimaya          
TANZANIA ZANZIBAR (7)      
1.    Haidar Hashim Madeweyya    2.    Alli Omar Makame      
3.    Adil Mohammed Ali    4.    Mwandawa Khamis Mohammed      
5.    Salim Abdalla Salim    6.    Salma Haji Saadat      
7.    Mwantatu Mbarak Khamis   

      
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)      
TANZANIA BARA (13)      
1.    Honorata Chitanda    2.    Dr. Angelika Semike      
3.    Ezekiah Tom Oluoch    4.    Adelgunda Michael Mgaya      
5.    Dotto M. Biteko    6.    Mary Gaspar Makondo      
7.    Halfani Shabani Muhogo    8.    Yusufu Omari Singo      
9.    Joyce Mwasha    10.    Amina Mweta      
11.    Mbaraka Hussein Igangula    12.    Aina Shadrack Massawe      
13.    Lucas Charles Malunde          
TANZANIA ZANZIBAR (6)      
1.    Khamis Mwinyi Mohamed    2.    Jina Hassan Silima      
3.    Makame Launi Makame    4.    Asmahany Juma Ali      
5.    Mwatoum Khamis Othman    6.    Rihi Haji Ali      
          
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10)      
TANZANIA BARA (7)      
1.    William Tate Olenasha    2.    Makeresia Pawa      
3.    Mabagda Gesura Mwataghu    4.    Doreen Maro      
5.    Magret Nyaga    6.    Hamis Mnondwa      
7.    Ester Milimba Juma          
TANZANIA ZANZIBAR (3)      
1.    Said Abdalla Bakari    2.    Mashavu Yahya      
3.    Zubeir Sufiani Mkanga          
          
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI –(WAJUMBE 10)      
TANZANIA BARA (7)      
1.    Hawa A. Mchafu    2.    Rebecca Masato      
3.    Thomas Juma Minyaro    4.    Timtoza Bagambise      
5.    Tedy Malulu    6.    Rebecca Bugingo      
7.    Omary S. Husseni          
TANZANIA ZANZIBAR (3)      
1.    Waziri Rajab    2.    Issa Ameir Suleiman      
3.    Mohamed Abdallah Ahmed       


VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)      
TANZANIA BARA (13)      
1.    Agatha  Harun Senyagwa    2.    Veronica Sophu      
3.    Shaban Suleman Muyombo    4.    Catherine Gabriel Sisuti      
5.    Hamisi Hassani Dambaya    6.    Suzy Samson Laizer      
7.    Dr. Maselle Zingura Maziku    8.    Abdallah Mashausi      
9.    Hadijah Milawo Kondo    10.    Rehema Madusa      
11.    Reuben R. Matango    12.    Happy Suma      
13.    Zainab Bakari Dihenga          
TANZANIA ZANZIBAR (7)      
1.    Saleh Moh’d Saleh    2.    Biubwa Yahya Othman      
3.    Khamis Mohammed Salum    4.    Khadija Nassor Abdi      
5.    Fatma Haji Khamis    6.    Asha Makungu Othman      
7.    Asya Filfil Thani          
          
WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)      
TANZANIA BARA (14)      
1.    Dr. Christina Mnzava    2.    Paulo Christian Makonda      
3.    Jesca Msambatavangu    4.    Julius Mtatiro      
5.    Katherin Saruni    6.    Abdallah Majura Bulembo      
7.    Hemedi Abdallah Panzi    8.    Dr. Zainab Amir Gama      
9.    Hassan Mohamed Wakasuvi    10.    Paulynus Raymond Mtendah      
11.    Almasi Athuman Maige    12.    Pamela Simon Massay      
13.    Kajubi Diocres Mukajangwa    14.    Kadari Singo      
TANZANIA ZANZIBAR (6)      
1.    Yussuf Omar Chunda    2.    Fatma Mussa Juma      
3.    Prof. Abdul Sheriff    4.    Amina Abdulkadir Ali      
5.    Shaka Hamdu Shaka    6.    Rehema Said Shamte   

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Februari, 2014

Hawa ni baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Dk Florence Turuka ametangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum la katiba jioni hii katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mawasiliano Ikulu jijini Dar es salaam. 

Bunge la Katiba litakalokuwa na wajumbe 640, litakutana kwa siku 70 (na kuongezewa siku 20 kama hawatoafikiana)  kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Desemba 30, mwaka jana. 
Chini ni baadhi ya wabunge hao waliotangazwa

Dr Christina tina Mzava, Paul Makonda, Jesca Mtavasavangu, Julius Mtatiro, Abdallah Bulembo, Panzi, Dk Zainab Gama, Paulinus Mtenda, Almas Maige, Pamela Masae, Kajubi Mukajanga, Kadari Singo, Yusuph Omar Chunda, Fatma Musa, Profesa Abdul Sherif, Rehema Said Shamte.
Asha Mtwangi, Paul kimiti, Elizabeth Minde, Evod Mmanda, Mary Dafa, Kingunge Ngombale Mwiru, Maria Sarungi na Valerie Msoka, Sixtus Mapunda, Happiness Msengi, Godfrey Simbeye, Shamsa Mwangunga.

Wengine ni;
 
Wajumbe Vyama vya siasa

Hashim Rungwe, Rashid Mtuta, Yusuph Mwanyanga, Mchungaji Mtikila, Bertha Mpata, Dominic Nyachae, Mbwana Kibanda, Peter Mziray, Isack Cheyo, Emmanuel Makaidi, Prof Ibrahim Lipumba, Modesta Ponera, Profesa Abdallah Safari, Salum Selemani, James Mapalala, Mary Mpangala, Nancy Mrikarya, Nazael Tenga, Fahmi Dovutwa, Costantine Akitanda, John Chipaka, Rashid Lae, Hashim Rungwe,

Rashid Mtuta, 

Taasisi za Elimu;


Dk Suzan Kolimba, Prof Esta Mwaikambo, Dk Natujwa Mvungi, Dk Domitila Bashemela, Prof Bernadeta Killian, Tedy Patrick, Prof Tulia Akson, Hamza Mustafa Njozi, Makame Omar Makame, Dk Alei Nasor, Leila Ally, Zeyana Hajji

Vyama vya wafugaji

William Ole Nashi, Mabada Matagu, Dorin Maro, Hamis Mlondwa, Esta Chuma, Said Abdala Bakari, Zuberi Khan

Wavuvi
Hawa Mchafu, Rebeca Masato, Tomas Minyaro, Teddy Malulu, Omary Hussein.

Mengine yatawajia baadaye

Azam Fc yapania rekodi Afrika 2014

WAWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam watawakosa nyota wao wanne katika mechi ya awali dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbuji, itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

Nyota wa Azam watakaokosekana katika mechi hiyo ni pamoja na mshambuliaji hatari, John Bocco na beki Hajji Nuhu, ambao ni majeruhi. Wengine ni chipukizi Ismail Lugambo na Farid Musa.

Ofisa Habari wa Azam, Jaffari Iddi alisema mjini Dar es Salaam kuwa, Bocco bado majeruhi wakati Nuhu aliumia goti juzi baada ya kuanguka ghafla wakati wa mazoezi yaliyofanyika Chamazi.

Jaffari alisema Lugambo alivunjika mguu mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Azam na Ashanti wakati Farid amekuwa akisumbuliwa na majeraha mara kwa mara na itabidi afanyiwe vipimo vikubwa.

"Farid itabidi afanyiwe vipimo vya MRY kwenye mgongo ili tujue sababu ya kuumia mara kwa mara na Bocco bado goti lake halijawa sawa. Alipewa mapumziko ya wiki mbili na tayari ameshamaliza wiki moja, hivyo hatacheza mchezo huo," alisema Jaffari.

Pamoja na kuwakosa nyota hao, Jaffari alisema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Ferroviario na kusisitiza kuwa, wamepania kuweka rekodi ya kufika mbali zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka jana.

Aliongeza kuwa, wamefurahi kupata ruhusa kutoka kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ya kucheza mechi hiyo kwenye uwanja wa Chamazi kwa vile wachezaji wao wameuzoea na watautumia vizuri kupata ushindi.

Msimu uliopita, Azam iliiwakikisha Tanzania katika mashindano hayo baada ya kumaliza ligi kuu ikiwa mshindi wa pili, lakini ilitolewa raundi ya tatu. Iwapo Azam itaitoa Ferroviario,  itamenyana na mshindi kati ya St. Michel ya Shelisheli na ASSM Elgeco Plus ya Madagacar

Mashujaa, wengine kibao kuwasindikiza Extra Bongo Dar Live

Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Kamarade Ally Choki
 
Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kimya cha muda mrefu sasa albamu ya 'Mtenda Akitendewa' ya Extra Bongo Next Level Wazee wa 'Kimbembe' ipo tayari kwa ajili ya mashabiki wa muziki wa dansi kupata burudani ya kusikiliza mitupio ya sauti kama ya kundi la Wenge Musica ambapo inatarajiwa Februari 22 mwaka huu kwenye Ukumbi wa maraha Dar Live Mbagala jijiji Dar es Salaam.
Safu ya unenguaji ya Extra Bongo inayotarajiwa kuonyesha manjonjo siku ya uzinduzi wa albamu yao mpya
Mtenda Akitendewa ni albamu ya nne kwa bendi hiyo iliyoasisiwa kwa mara kwanza mwaka 2003 ikiwa na waimbaji Ally Choki, Bashiri Uhadi, Bob Kissa, Richard Maarifa, Khalidi Chokoraa, Flora Moses, rapa Greyson Semsekwa, (solo) Bonzo Kwembe, Efraim Joshua,George Gama (besi) Rythm na kinanda Thabit Abdul drum (ngoma) zikipigwa na Imma Chokolate.
Albamu ya kwanza iliitwa '3x3' ambao ni wimbo uliokuwa kwenye albamu nyimbo nyingine ni 'Regina Zanzibar', 'Tuchunge Wazazi au Fikiri
Madinda', 'Nunu Milenium' 'Walimwengu Remix' na 'Odise'.
Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alisema albamu hiyo imekamilika kwa asilimia zote na mashabiki wataanza kuipata siku hiyo ukumbini
ambako kutakuwa na burudani ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' wakiongozwa na Amin na Lina Sanga.
Khadija Omar Kopa sambamba na kundi la Makirikiri wa Bongo.
Licha ya wasanii hao pia bendi ya Mashujaa Watoto wa mama 'Sakina' itapamba uzinduzi huo huku 'Malikia wa Mipasho'.
Aidha Choki alisema, Prince Muumin Mwinjuma 'Kocha Dunia' naye ni miongoni mwanamuziki watakaoupamba usiku wa Mtenda Akitendewa.
Extra Bongo ilitikisa anga ya muziki wa dansi wakati huo na kuwa tishio kwa bendi kama African Stars 'Twanga Pepeta', FM Academia, Tanzania One Theatre (TOT) na nyinginezo hasa pale ilipoibuka na albamu ya pili iliyoitwa 'Bullet Proof' ikiwa na nyimbo kama 'Double Double' na 'Regina Zanzibar' kabla ya kusambaratika mwaka 2004.

Manchester United wawakumbuka wenzao waliokufa kwa ndege 1958

Forever there: United have a poignant memorial wall for supporters to always go and visitKLABU ya Manchester United leo inatarajia kuwakumbuka watu 23 ambao walipoteza maisha katika ajali ya ndege jijini Munich Februari 6 mwaka 1958. Wachezaji nane wa United na viongozi watatu ni miongoni mwa waliokufa wakati ndege iliyowabeba wachezaji wa timu hiyo kutoka katika mchezo wa Kombe la Ulaya jijini Belgrade kushindwa kupaa. Ndege hiyo ilitua jijini Munich kwa ajili ya kuongeza mafuta na baada ya kushindwa kuruka mara mbili ndege hiyo ilipata ajali wakati ikijaribu tena kuruka kwa mara ya tatu. Watu 21 walifariki katika eneo la tukio huku rubani wake Kenneth Rayment alifariki wiki tatu baadae na Duncan Edwards ambaye anahesabika kuwa mmoja wa wachezaji nyota kabisa wa Uingereza yeye alifia hospitali siku 15 baadae. Turnout: As always, a large group of fans were there on the anniversaryGolikipa wa United Harry Gregg yeye alifanikiwa kutoka salama lakini alirejea katika eneo la tukio kujaribu kuwaokoa majeruhi katika sehemu salama. Wachezaji wawili Johnny Berry na Jackie Blanchflower wote walishindwa kucheza soka tena kutokana na majeraha ya ajali hiyo.Mashabiki wa United
Remembered: Sir Bobby Charlton and Gary Neville were among those who made their way to Old Trafford
Sir Bobby Charlton na Gary Neville walifika Old Trafford

Uchaguzi Mkuu TASWA wapigwa dochi hadi Machi 2

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhf0BHUHvIcL5-2NP5BJ1cLGd-dO7nkX4M6QQQQ1juGpgd4p19qMpmQJ-7rGHrMW7-u3bn6Oy2uDW3HDTt5h0-0pXsaq3YjJigDZwWW1xCe4mwGMvqtctAng9pJasFadQ85OFyN9NuOFJ4/s640/amii+mhando.jpg
UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 16 umesogezwa mbele kwa wiki mbili na sasa utafanyika Machi 2, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
 
Uamuzi wa kusogeza mbele tarehe ya kufanyika uchaguzi huo imechukuliwa na Sekretarieti ya TASWA kutokana na sababu mbalimbali, lakini kubwa ni kutoa nafasi kwa wanachama wengi zaidi kulipia ada zao kwa ajili ya kushiriki mkutano huo wa uchaguzi.
 
Hadi kufikia leo mchana idadi ya wanachama waliokuwa wamelipia ada ni 57 kati ya wanachama karibu 150 waliopo katika leja na kati ya waliolipa ni wanne tu ndiyo wamelipia ada ya miaka mitatu kama walivyotakiwa wakati waliobaki wamelipia mwaka mmoja.
 
Kumekuwa na changamoto mbalimbali zimejitokeza katika suala hili la kulipia ada, ikiwa ni pamoja na maombi ya baadhi ya wanachama walipie mwaka mmoja na kisha ada nyingine chama kiwawekee utaratibu wa kulipa siku za usoni kadri itakavyoonekana inafaa.
 
Kutokana na hali hiyo sekretarieti ya TASWA imepokea maombi hayo na kwa vile uamuzi huo ulifikiwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TASWA, itayawasilisha kwenye kikao kama hicho kitakachofanyika Jumatatu Februari 17 kujadili masuala mbalimbali yahusiyo mkutano huo, ikiwa ni pamoja na kupitia orodha ya wanachama wanaostahili kushiriki mkutano wa uchaguzi.
 
Hatua ya awali ambayo imefanyika ni kusogeza mbele tarehe ya mwisho ya kulipia ada, ambayo awali ilikuwa Februari 4 na sasa itakuwa Februari 15 mwaka huu saa kumi alasiri na hakutakuwa na muda wa ziada.
 
 Imetolewa na;
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
07/02/2014.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA ‘FOUNDATION FOR BENEFACTOR OPPORTUNITY EDUCATION’

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na Joe Ricketts Kiongozi wa ‘Foundation for Benefactor Opportunity Education’, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Februari  7, 2014 kwa mazungumzo. Kulia ni Martin Russell Kiongozi wa Taasisi hiyo nchini Tanzania.   Ujumbe huo una lengo la kusaidia Tanzania kuboresha mfumo wa utoaji elimu kwa matumizi ya ‘Tablet’. Picha na OMR



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib BIlal, akizungumza na ujumbe wa ‘Foundation for Benefactor Opportunity Education’, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo  kwa mazungumzo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib BIlal, akizungumza na ujumbe wa ‘Foundation for Benefactor Opportunity Education’, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.  Makame Mbarawa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, pamoja na ujumbe wa ‘Foundation for Benefactor Opportunity Education’, baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.Picha na OMR

UNAJUA MADHARA YA KUSIKILIZA SIMU KWA MUDA MREFU?


TANGU teknolojia ya Simu za Mkononi kuingia nchini, Watanzania wamekuwa kama waliowehuka na kifaa hicha cha mawasiliano ya kisasa.
Iwe kwenye daladala, vijiweni na hata majumbani na ofisini tymekuwa tukishuhudia ndugu, jamaa na rafiki zetu na penginee wewe mwenyewe msomaji unatumia muda mrefu kusikiliza au kuongea na simu dhidi ya unawapigia au wanaokupigia.
Je umeshawahi kujiuliza madhara yanayotokana na kusikiliza au kuongea kwa muda mrefu na simu? 
Ebu shuka na taarifa hii ujue namna gani tunavyohatarisha maisha yetu bila kujua au kule kusumbuliwa na ulimbukeni wa teknolojia hii mpya ambayo imekuwa ikiwazuzua watu wengi bila kujali rika, jinsia au nafasi yao ndani ya jamii.

Leo tutaangalia jambo la ajabu kidogo na kama unabisha utajaribu mwenyewe kisha utajionea. Matumizi ya Simu za kiganjani yameongezeka sana ndani na nje ya nchi. 


Simu hizi licha ya kuwa na msaada mkubwa katika maendeleo ya jamii pia zina mambo yake ambayo yanashangaza na kutisha kidogo/sana!!!! 

Leo nitawaelekeza namna ya kupika yai kwa kutumia simu mbili za mkononi. 
Baada ya somo hili jaribu kufanya jaribio na ujionee mwenyewe. Mahitaji: Simu mbili za kiganjani, Glasi/Bilauri ya maji na Yai ambalo halijapikwa wala kuvunjika. 
Yai likiwa limeelekezewa simu mbili zilizounganishwa kwa mawasiliano

Hatua: Chukua simu ya kwanza na upige kwenda namba ya simu yapili, pokea simu ya pili na kuiacha hewani kisha chukua glasi yenye yai na uiweke kati ya simu hizo mbili kwa dakika 65, ni vema ukajiunga na vifurushi ili usiingie gharama kubwa. 
Angalia mfano katika picha hii hapa chini. 

Baada ya dakika 65 yai litakuwa limeiva kabisa kama limechemshwa vile, Sikushauri ule yai hilo kwakuwa sijafanya utafiti wa kutosha endapo kuna madhara yoyote mtu akila au la. 
Sasa chakujiuliza hapo ndugu zangu ni je, endapo mionzi hii ya simu inaweza kuivisha protein iliyopo katika yai vipi kuhusu ubongo wako, hasa kwa wale watumiaji wakubwa wa simu!! 

Source:Kijiwe cha Wasomi

Original from: http://googlehabari.blogspot.com/2014/02/yajue-madhara-ya-kuongea-na-simu-kwa.html
Copyright EXEIdeas - All Rights Reserved

UNASUMBULIWA NA VIDONDA VYA TUMBO? SOMA HAPA!


MFUMO wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo katika mwili unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili. 
Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'. 
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'.
Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'
Chanzo cha Vidonda vya Tumbo
Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu. 
Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers' Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. 
Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo. 
Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo. 
Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo. 
Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. 
Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda. Chembe za urithi 'Genetics'. 
Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa cembe za urithi zinahusika pia. 
Uvutaji sigara/tumbaku. 
Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta. 
Matumizi ya pombe/vilevi.
Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/ pombe. Msongo wa mawazo 'Mental stress'
Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa. 

Dalili za ugonjwa
Hata hivyo ni mara chache sana mtu kuugua vidonda vya tumbo na kutoonyesha dalili. 
Zifuatazo ni dalili zinazotokea kwa wagojwa wengi:- 
-Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda. Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain' Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo.
-Kushindwa kumeza vizuri chakula. Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni. Kujisikia vibaya baada ya kula. 
- Kupungua uzito. 
- Kukosa hamu ya kula. 
 
Dalili Hatari
- Kutapika damu. 
- Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito.
- Kichefuchefu na kutapika. 

Jinsi ya Kugundua Vidonda
- Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteja wake ni vidonda vya tumbo. 
Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika : 
- Kupima damu 'Blood test'. 
- Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative' - Kupima pumzi 'Breath test'. Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi. 
- Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'. Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi. Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria. 
- X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'. Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray. 
- Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'. 
 
Matibabu Yake
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa. Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole, Esomeprazole & Lansoprazole. Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni. Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatalithiwa na dawa kama Paracetamol. 
Vilevile dawa aina ya H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine, hutumika kama mbadala kama dawa aina ya 'PPIs' hazitokuwepo. 
H2-Receptor Antagonists hufanya kazi ya kuzuiia utendaji wa protini iitwayo 'Histamine' ambayo inahusika na kuchochea utengenezaji wa asidi tumboni. 
Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya haraka. 
Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine. 
Makala ijayo itakusaidia jinsi ya kujizuia usipate vidonda vya tumbo na jinsi kuishi na vidonda vya tumbo.
Credit:manyandahealthy.blogspot.com

Original from: http://googlehabari.blogspot.com/2013/12/zijue-sababu-za-vidonda-vya-tumbo.html
Copyright EXEIdeas - All Rights Reserved
ZIJUE SABABU ZA VIDONDA VYA TUMBO PAMOJA NA TIBA YAKE Written By umar makoo on Saturday, December 7, 2013 | 9:53 PM Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo katika mwili unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili. Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'. Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'. Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer' VINAVYOSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu. Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers' Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo. Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo. Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo. Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda. Chembe za urithi 'Genetics'. Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia. Uvutaji sigara/tumbaku. Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta. Matumizi ya pombe/vilevi. Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/ pombe. Msongo wa mawazo 'Mental stress'. Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa. DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO Hata hivyo ni mara chache sana mtu kuugua vidonda vya tumbo na kutoonyesha dalili. Zifuatazo ni dalili zinazotokea kwa wagojwa wengi:- · Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda. Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain' Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo. · Kushindwa kumeza vizuri chakula. Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni. Kujisikia vibaya baada ya kula. Kupungua uzito. · Kukosa hamu ya kula. DALILI HATARI · Kutapika damu. Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito.· Kichefuchefu & kutapika. JINSI VIDONDA HUGUNDULIWA:- Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteka wake ni vidonda vya tumbo. Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika : · Kupima damu 'Blood test'. Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative' · Kupima pumzi 'Breath test'. Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi. · Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'. Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi. Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria. · X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'. Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray. Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'. MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa. Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole, Esomeprazole & Lansoprazole. Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni. Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatalithiwa na dawa kama Paracetamol. Vilevile dawa aina ya H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine, hutumika kama mbadala kama dawa aina ya 'PPIs' hazitokuwepo. H2-Receptor Antagonists hufanya kazi ya kuzuiia utendaji wa protini iitwayo 'Histamine' ambayo inahusika na kuchochea utengenezaji wa asidi tumboni. Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya haraka. Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine. Makala ijayo itakusaidia jinsi ya kujizuia usipate vidonda vya tumbo na jinsi kuishi na vidonda vya tumbo.http://manyandahealthy.blogspot.com

Original from: http://googlehabari.blogspot.com/2013/12/zijue-sababu-za-vidonda-vya-tumbo.html
Copyright EXEIdeas - All Rights Reserved
ZIJUE SABABU ZA VIDONDA VYA TUMBO PAMOJA NA TIBA YAKE Written By umar makoo on Saturday, December 7, 2013 | 9:53 PM Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo katika mwili unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili. Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'. Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'. Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer' VINAVYOSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu. Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers' Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo. Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo. Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo. Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda. Chembe za urithi 'Genetics'. Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia. Uvutaji sigara/tumbaku. Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta. Matumizi ya pombe/vilevi. Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/ pombe. Msongo wa mawazo 'Mental stress'. Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa. DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO Hata hivyo ni mara chache sana mtu kuugua vidonda vya tumbo na kutoonyesha dalili. Zifuatazo ni dalili zinazotokea kwa wagojwa wengi:- · Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda. Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain' Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo. · Kushindwa kumeza vizuri chakula. Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni. Kujisikia vibaya baada ya kula. Kupungua uzito. · Kukosa hamu ya kula. DALILI HATARI · Kutapika damu. Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito.· Kichefuchefu & kutapika. JINSI VIDONDA HUGUNDULIWA:- Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteka wake ni vidonda vya tumbo. Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika : · Kupima damu 'Blood test'. Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative' · Kupima pumzi 'Breath test'. Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi. · Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'. Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi. Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria. · X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'. Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray. Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'. MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa. Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole, Esomeprazole & Lansoprazole. Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni. Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatalithiwa na dawa kama Paracetamol. Vilevile dawa aina ya H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine, hutumika kama mbadala kama dawa aina ya 'PPIs' hazitokuwepo. H2-Receptor Antagonists hufanya kazi ya kuzuiia utendaji wa protini iitwayo 'Histamine' ambayo inahusika na kuchochea utengenezaji wa asidi tumboni. Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya haraka. Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine. Makala ijayo itakusaidia jinsi ya kujizuia usipate vidonda vya tumbo na jinsi kuishi na vidonda vya tumbo.http://manyandahealthy.blogspot.com

Original from: http://googlehabari.blogspot.com/2013/12/zijue-sababu-za-vidonda-vya-tumbo.html
Copyright EXEIdeas - All Rights Reserved

TFF yaziombea baraka Yanga, Azam kufanya kweli Afrika

Yanga
Azam Fc
 SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazitakia kila la kheri klabu za Yanga na Azam ambazo timu zake zinatuwakilisha kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).

Yanga inacheza na Komorozine ya Comoro katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya CL itakayochezwa kesho (Februari 8 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Nayo Azam inaikaribisha Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya CC utakaochezwa Jumapili (Februari 9 mwaka huu) saa 10 kamili kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Ni matumaini yetu kuwa timu hizo mbili zitatuwakilisha vizuri kwenye michuano hiyo, na kuwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi viwanjani kuziunga mkono hasa kwa vile zinacheza nyumbani.


Wapinzani wa timu hizo tayari wameshawasili tayari kwa mechi hizo ambazo wawakilishi hao wa Tanzania wanahitaji kupata ushindo mnono ili kuwa na kazi nyepesi mechi zao za marudiano. 

Twiga Stas yahamishia kambi Dar

TIMU ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) imehamishia kambi yake jijini Dar es Salaam kutoka Mlandizi mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya michuano ya Afrika (AWC) dhidi ya Zambia.

Kikosi hicho chini ya Kocha Rogasian Kaijage kimepiga kambi katika hosteli ya Msimbazi Center kikiwa na wachezaji 25 kutoka 30 ambao kilianza nao katika kambi ya Mlandizi mkoani Pwani.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza dhidi ya Zambia itachezwa Februari 14 kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka. Timu zitarudiana wiki mbili baadaye jijini Dar es Salaam.

Wachezaji waliopo katika kikosi hicho ni Amina Ally, Amisa Athuman, Anastasia Anthony, Asha Rashid, Esther Chabruma, Eto Mlenzi, Evelyn Sekikubo, Fatuma Bashiri, Fatuma Hassan, Fatuma Issa, Fatuma Mustafa na Fatuma Omari.

Wengine ni Flora Kayanda, Happiness Hezron, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Najiat Abbas, Pulkeria Charaji, Shelder Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa, Winfrida Daniel na Zena Khamis.

Rais TFF aeleza mikakati siku 100 ofisini


RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameelezea hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Ilani yake siku 100 tangu alipoingia madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (Februari 7 mwaka huu) katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, Rais Malinzi aliainisha maeneo kadhaa yaliyopewa kipaumbele na tayari yameanza kufanyiwa kazi pamoja na changamoto zilizopo.

Alisema muundo wa Idara ya Ufundi umebadilishwa kwa kuundwa vitengo vya ufundi, elimu na maendeleo ya mpira wa miguu huku maeneo ambayo tayari yameanza kufanyiwa kazi kuwa ni;

Ujenzi wa kituo cha mpira wa miguu (football centre of excellency), timu kupanda daraja, kuanzisha mashindano mapya na kufufua ya zamani, mpira wa miguu wa wanawake, maandalizi ya vijana (grassroot football), tiba, walimu na makocha, utawala, uhusiano na Zanzibar, klabu za mpira wa miguu, wachezaji, masoko na uwekezaji, kitengo cha habari, viwanja na timu ya Taifa (Taifa Stars).

Rais Malinzi amesema changamoto zilizopo kwa sasa ni matumizi ya tiketi za elektroniki, ufinyu wa bajeti, madeni, nidhamu, maadili na uchezeshaji wa waamuzi.

Ametoa mwito kwa wadau wote nchini wakiongozwa na Serikali, Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Afrika (CAF), Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), vyombo vya habari, mashirika ya umma na kampuni binafsi kushikamana na kuwa kitu kimoja kwa nia ya kuinua kiwango cha mpira wa miguu Tanzania.