STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 28, 2014

Chelsea chupuchupu, yalazimisha sare ugenini

Sadio Mane  akishangilia bao la Southampton
Eden Hazard akishangilia bao la kusawazisha la Chelsea
VINARA wa Ligi Kuu ya England, Chelsea imeponea chupuchupu leo ugenini baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton katika pambano lililomalizika muda mfupi uliopita.
Southampton waliwakaribisha Chelsea katika uwanja wa St Mary kwa bao la mapema la dakika ya 17 kupitia kwa Sadio Mane kabla ya Chelsea kuchomoa dakika chache kabla ya mapumziko kupitia kwa Eden Hazard akimalizia kazi nzuri ya Cesc Fabregas.
Southampton ilijikuta ikicheza pungufu baada ya Morgan Schneiderlin kuonyesha kadi nyekundu dakika chache kabla ya kumalizika kwa pambano hilo

Kwa sare hiyo Chelsea wameendelea kung'ang'ania kileleni wakiwa na pointi 46, baada ya mechi 19 na kwa sasa mechi nyingine zinaendelea ambapo Manchester City wanaoongoza mabao 2-1 dhidi ya Burnley huku Arsenal ikiwa ugenini inaoongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United.

Kavumbagu afufuka Taifa, Ndanda majanga

Ndanda Fc waliporomoka hadi mkiani katika msimamo wa Ligi ikiuaga 2014 na kukaribisha 2015
Didier Kavumbagu akishangilia moja ya mabao yake na wachezaji wenzake Himid Mao na Aggrey Morris
BAO la kuongoza la Azam limemzindua Didier Kavumbagu ambaye alikuwa hajafunga muda mrefu kuwakimbia washambuliaji wenzake na kuongoza msimamo wa orodha ya wafungaji bora katika Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Amissi Tambwe akifungua akaunti ya mabao Jangwani.
Didier alifunga bao la kuongoza la Azam leo na kumfanya kufikisha mabao matano na kuongoza orodha ya wakali wa mabao wakati ligi kuu ikimaliza mwaka 2014 na kusubiri kuendelea tena mwakani.
Simon Msuva aliyefunga bao la pili la Yanga naye ameingia kwenye orodha ya wakali wa mabao akiwa na mabao manne akilingana na wachezaji wengine, Danny Mrwanda wa Yanga, Rama Salim (Coastal Union), na Ame Ally (Mtibwa)
Ligi ikiaga mwaka 2014, Mtibwa ipo kileleni, huku Ndanda ikiachiwa nafasi ya mkiani na Mbeya City waliowanyuka bao 1-0 leo jijini Mbeya.
Ndanda inazibeba timu zote ikiwa na pointi sita, wakati Mbeya City kwa ushindi wa leo imechupa hadiu nafasi ya 12.
Msimamo kamili wa ligi hiyo baada ya kumalizika kwa mechi za raundi nane ni kama ifuatavyo;
                                          P   W    D    L    F    A   GD   Pts
 01. Mtibwa Sugar              08  04   04   00  11  04   07   16
02. Yanga                          08  04   02   02   11  07  04   14
03.  Azam                          08  04   02   02   10  06  04   14
04.  Kagera Sugar             08   03   04   01   07  04  03   13
05.  Coastal Union             08   03   03   02   09  07  02  12
06.  Polisi Moro                 08   03   03   02   08  07  01  12
06. JKT Ruvu                    08   03   01   04   07   08  -1  10
07. Ruvu Shooting             08   03   01   04   05   07  -2   10
08.Stand Utd                     08  02   04    02   06   10  -4  10
09.Simba                           08  01   06    01   07   07  00  09
09. Mgambo JKT              08  03   00    05   04   09  -5  09
12. Mbeya City                 08   02  02     04  03   06   -3  08
13. Prisons                        08   01  04     03  06   07   -1  07
14. Ndanda Fc                  08   02  00     06  08   13   -5  06
Wafungaji Bora:
5-
Didier Kavumbagu (Azam)
4-
Rama Salim (Coastal), Danny Mrwanda, Simon Msuva (Yanga) Ame Ally (Mtibwa)
3-
Ally Shomari, Emmanuel Okwi (Simba), Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
2- Shaaban Kisiga, (Simba), Nassor Kapama (Ndanda) Salum Kanoni (Kagera), Aggrey Morris (Azam),  Najim Magulu, Samuel Kamuntu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Amissi Tambwe, Jerry Tegete (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Heri Mohammed (Stand Utd), Ally Nassor (Mgambo),  Malimi Busungu (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi)
Mechi zijazo;
Jan 03, 2014
Coastal Union vs  JKT Ruvu
Ruvu Shooting vs Kagera Sugar
Azam vs Mtibwa Sugar
Stand United vs Polisi Moro
Mbeya City  vs  Yanga

Jan 4, 2015
Mgambo JKT vs  Simba 
Prisons vs  Ndanda

Salha wa Hammer bado aota albamu na mumewe

Salha Abdallah
Salha Abdallah na mumewe, Hammer Q
MUIMBAJI mahiri wa taarab nchini  Salha Abdallah 'Salha wa Hammer' amesema licha ya kurejea kwenye muziki wa makundi, bado ataendelea kushirikiana na mumewe kutengeneza kazi zao binafsi.
Salha aliyejiunga na kundi la Five Star akitokea kwenye likizo ya uzazi alisema kuwa, bado mipango ya kutengeneza albamu ya pamoja na mumewe ipo pale pale japo anaendelea kupiga mzigo kazini kwake.
Muimbaji huyo wa zamani wa Dar Modern na aliyekuwa akilifanyia kazi King' s Modern kabla ya kwenda likizo ya uzazi, alisema kurejea kwake kwenye makundi hakuna maana kumemzuia mipango yake.
"Sidhani kama kurejea kwangu kuiimbia makundi kutanizuia kuendelea na mipango yangu na mwenza wangu kutengeneza albamu, nitaendelea nayo," alisema.
Wanandoa wao walishaachia nyimbo za 'Tunapendana' na 'Safiri Salama' na walikuwa katika mipangop ya kukamilisha nyimbo nyingine kuhitimisha albamu yao kabla ya Salha kupata likizo ya uzazi.

Yanga, Azam zashindwa kuing'oa Mtibwa kileleni

* Polisi Moroyainyoa Mgambo 2-0

* Mbeya City yainyuka Ndanda yatoka mkiani

http://1.bp.blogspot.com/-s5DKJ66I-uI/VKASWSksnnI/AAAAAAAG6Ik/eJj5rbWvwok/s1600/MMGM0086.jpg
Tambwe akifunga bao la kusawazisha la Yanga
http://1.bp.blogspot.com/-zjoebZty438/VKARRDjm0iI/AAAAAAAG6IM/E6B43jVIZA8/s1600/MMGM0090.jpg
Tambwe akishangilia bao lake sambamba na Simon Msuva ambaye pia aliifungia Yanga bao la pili
Azam wakishangilia bao lao la kwanza dhidi ya Yanga leo kwenye uwanja wa Taifa
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/08/Mbeya-City.jpgPAMBANO la kukata na shoka baina ya Yanga na Azam limemalizika matokeo yakiwa ni yale yale ya mabao 2-2 na kuendelea kuwa nyuma ya Mtibwa Sugar wanaoongoza msimamo.
Yanga walikuwa 'nyumbani' walitanguliwa kufungwa bao dakika ya tano na Didier Kavumbagu baada ya mabeki wa Yanga kuchanganyana na kipa wao Deo Munishi 'Dida' na kumpa nafasi nyota huyo wa zamani wa Jangwani kukwamisha bao kirahisi.
Yanga walicharuka dakika mbili baadaye Amissi Tambwe aliisawazishia Yanga bao baada ya kuunganisha mpira wa krosi iliyopigwa na kiungo Salum Telela na kufanya matokeo yadumu hivyo hadi mapumziko.
Yanga iliingia kipindi cha pili wakiwa wamecharuka na kuandika bao la pili dakika ya 52 kupitia Simon Msuva aliyeunganisha kwa kichwa bao lililotokana na pasi murua ya Haruna Niyonzima aliyeshirikiana vema awali na Kpah Sean Sherman aliyeonekana tishio langoni  mwa Azam muda wote wa mchezo huo.
Hata hivyo nahodha John Bocco aliyekuwa akitokea benchi mpira wake wa kwanza kuugusa uwanjani ulizaa bao la kusawazisha la Azam baada ya mabeki wa Yanga kujichanganya tena na mchezaji huyo aliyekuwa majeruhi kufunga kirahisi kwa kichwa mpira wa krosi ya Himid Mao dakika ya 65.
Kwa matokeo hayo Yanga imeendelea kung'ang'ania nafasi ya pili nyuma ya Mtibwa ikiwa na pointi 14 sawa na zile za Azam isipokuwa wanatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Matokeo ya mechi nyingine Polisi Moro imeifyatua Mgambo JKT ya Tanga kwa mabao 2-0, mabao katika pambano hilo yalifungwa na Nicolaus Kibopile katika dakika ya 21 na Imani Mapunfda aliyekwamisha bao la ushindi dakika ya 85, huku Mbeya City ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda Fc ya Mtwara na hivyo kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo.

Diamond tena, atwaa tuzo Nigeria, Vee Money naye ang'ara

Vee Monye akiwa na tuzo yake
Peter Msechu akiwa na tuzo ya Diamond
NYOTA ya Supastaa wa Bongo, Diamond Platnumz imeendelea kung'ara baada ya usiku wa jana kunyakua tuzo nyingine ya AFRIMA 2014 nchini Nigeria, sambamba na mwanadada Vanessa Mdee 'Vee Money'.
Wasanii hao wametwaa tuzo hizo kupitia vipengele vya Wasanii Bora wa Afrika Mashariki, Diamond akinyakua kwa upande wa kiume na Vee Money kwa upande wa wasanii wa kike.
Tuzo hizo za AFRIMA zilizofanyika huko jijini Lagos nchini Nigeria, ambapo msanii mwingine wa Tanzania aliyekuwa akiwania tuzo hizo sambamba na Diamond ni Peter Msechu ambaye alimpokelea Diamond Tuzo yake.
Hiyo ilikuwa ni tuzo ya 13 kwa mwaka 2014 kwa Diamond baada ya awali kunyakua tuzo saba kwa mpigo katika Kili Music, kisha AFRIMMA, akafuatia na tatu za CHAOMVA na kumalizia ya The Future aliyotwa nchini Nigeria mara baada ya kutoka Afrika Kusini kunyakua tuzo tatu.
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Vanessa Mdee akiwa na tuzo yake ya Best Female Artist in East Africa. Peter Msechu akiwa amebeba tuzo kwa niaba ya Diamond Platnumz. Peter Msechu, Vanessa Mdee na Victoria Kimani katika pozi huko Lagos, Nigeria. MWANAMUZIKI Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa kuamkia leo ametwaa tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika Mashariki (Best Male Artist in East Africa) kutoka Tuzo za 2014 AFRIMA zilizofanyika huko jijini Lagos nchini Nigeria. Mwanadada Vanessa Mdee yeye ameshinda tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki (Best Female Artist in East Africa). Tuzo ya Diamond imepokelewa na mwanamuziki Peter Msechu aliyekuwepo katika zoezi hilo la utoaji tuzo maana na yeye alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hizo

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Mtibwa Sugar yaendeleza rekodi Ligi ya Bara

* Ruvu Shooting yaizamisha JKT Ruvu

* Yanga, Azam zashikana mashati Taifa

* Mpaka sasa mabao 2-2

Mtibwa Sugar
http://3.bp.blogspot.com/-c8YFHqfoGQ0/UXZpy7CgJtI/AAAAAAAAHIk/Nf9mAwQFKoM/s640/DSC_0125.JPG
JKT Ruvu waliochezea kichapo usiku wa jana kwa Ruvu Shooting
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mtibwa Sugar imeendeleza rekodi yake ya kuwa imu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote msimu huu, baada ya asubuhi ya leo kulazimisha sare ya bao 1-1 na Stand United baada ya mchezo huo kushindwa kuendelea kuchezwa jana sababu ya mvua kubwa.
Pambano hilo lilichezwa jana kwa dakika sita na kurudiwa leo asubuhi dakika zilizosalia kwa timu hizo kushindwa kutambiana kwenye uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro.
Wageni Stand ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Shaaban Kondo aliyefunga katika dakika ya 22, kabla ya Mtibwa kusawazisha katika dakika ya lala salama kupitia beki wake Saidi Mkopi na kuifanya timu hiyo iendelee kukaa kileleni ikiwa na pointi 16 baada ya mechi nane, ingawa inaweza lkujikuta iking'oka kileleni kama Yanga inayoumana na Azam itapata ushindi katika mchezo wao.
Azam pia ina nafasi ya kukwea kileleni kama itaishinda Yanga kwa uwiano mzuri wa mabao, ingawa hadi sasa timu hizo zimefungana mabao 2-0.
Azam walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Didier Kavumbagu kabla ya Amissi Tambwe kusawazisha kwa kichwa dakika chjache baadaye na katika kipindi cha pili, Simon Msuva aliiongezea Yanga bao la pili dakika ya 53 kabla ya John Bocco kufunga bao la kusawazisha hivi punde.
Katika mechi nyingine ya jana ya ligi hiyo Ruvu Shooting iliendelea ubabe wake kwa JKT Ruvu baada ya kuichapa bao 1-0 katika mechi iliyochezwa usiku kwenye uwanja wa Chamazi.
Bao pekee la Ruvu liliwekwa kimiani kwa mkwaju wa penati na Hamis Kasanga na kuifanya timu hiyo kufiksiha pointi 10 na kulingana na 'ndugu zap hao wa JKT ila wanatofautiana kwa mabao ya kufunga nba kufungwa.

MBAO FC YAKAMATA USUKANI SDL

TIMU ya soka ya Mbao ya Mwanza imekamata uongozi wa Kundi B la michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya jana (Desemba 27 mwaka huu) kuizamisha JKT Rwamkoma ya Mara mabao 2-1.
Kwa matokeo hayo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mbao FC imeitoa kileleni JKT Rwamkoma baada ya kufikisha pointi tisa kwa kushinda mechi zote tatu dhidi ya Arusha FC, Pamba na JKT Rwamkoma.
Mbao FC inafuatiwa na JKT Rwamkoma yenye pointi sita, Arusha FC pointi sita wakati Bulyanhulu na Pamba zikiwa za mwisho kwa pointi moja kila moja. Kundi hilo litakamilisha mzunguko wa kwanza Januari 3 mwakani kwa mechi kati ya JKT Rwamkoma na Arusha FC, na Bulyanhulu na Mbao FC.
Katika kundi A, Mji Mkuu (CDA) na Singida United ndizo zinazochuana kileleni kwa kufikisha pointi saba kila moja.
Timu hizo zinafuatiwa na Milambo yenye pointi nne, Mvuvumwa FC yenye pointi moja wakati Ujenzi Rukwa ni ya mwisho ikiwa haina pointi.
Hata hivyo, Mvuvumwa FC na Milambo ziko nyuma kwa mechi moja. Mechi hiyo ya kukamilisha raundi ya tatu kati ya timu hizo itachezwa kesho (Desemba 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Kiluvya United imeendelea kuchachafya kundi C baada ya kushinda mechi zote ne ilizocheza, hivyo kufikisha pointi 12. Inafuatiwa na Mshikamano yenye pointi saba huku Abajalo ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 6.
Nafasi ya nne inashikwa na Transit Camp yenye pointi nne, Cosmopolitan yenye pointi mbili ni ya tano wakati Kariakoo ambayo haina pointi ni ya mwisho. Hata hivyo, Cosmopolitan na Kariakoo zina mchezo mmoja mkononi.
Mechi zinazofuata za kundi hilo ni Januari 3 mwakani kati ya Kariakoo na Mshikamano na Mshikamano (Ilulu), Transit Camp na Abajalo (Mabatini), na Cosmopolitan na Kiluvya (Karume).
Kundi D, vinara bado ni Njombe Mji yenye pointi 12 ikifuatiwa na Wenda yenye pointi sita wakati Volcano FC iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi tano. Mkamba Rangers ina pointi nne, Town Small Boys ina pointi moja wakati Magereza FC haina pointi.
Katika kundi hilo leo (Desemba 28 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Town Small Boys na Magereza itakayochezwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea.  Januari 3 mwakani kutakuwa na mechi kati ya Town Small Boys na Njombe Mji, Volcano FC na Magereza, na Wenda na Mkamba Rangers.

Hakuna kama Lionel Messi-Pedro

http://images.latinpost.com/data/images/full/11964/lionel-messi.jpgMSHAMBULIAJI wa klabu ya Barcelona, Pedro amedai kuwa mchezaji mwenzake Lionel Messi ndiyo mchezaji bora kuliko yeyote duniani na anastahili kushinda tuzo ya Ballon d’Or mbele ya Cristiano Ronaldo. Messi amewahi kushinda tuzo hiyo kwa mara nne mfululizo kabla ya Ronaldo kuingilia kati na kunyakua tuzo hiyo mwaka jana ikiwa ni mara ya pili kwa upande wake.
Baada ya kuisaidia Real Madrid kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Mfalme mwaka huu, Ronaldo ndiye anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kunyakuwa tuzo hiyo katika sherehe zitakazofanyika Januari 12 mwakani.
Mafanikio makubwa aliyopata Messi kwa mwaka huu ni kuiongoza timu yake ya taifa ya Argentina kucheza fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil wakati golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer yeye ni mchezaji mwingine wa tatu aliyeyopo katika orodha hiyo.
Pamoja na kutopewa nafasi mwaka huu, Pedro anaamini kuwa hakuna mchezaji yeyote katika sayari hii anayeweza kumfikia Messi katika ubora wake uwanjani.

Tottenham Hotspur yaisimamisha Manchester United

Harry Kane tries to get away from Manchester United defender Paddy McNair as both sides looked to protect their recent unbeaten records
Harry Kane kimtoka beki wa Manchester United
Hugo Lloris makes himself big to deny Robin van Persie as United spurned several great chances in a goalless first half
Van Persie akikosa bao la wazi
Juan Mata sees his free kick deflected off the Tottenham wall and onto Hugo Lloris' post, resulting in a goalmouth scramble
Juan Mata akikosa bao la wazi langoni mwa Spurs
KLABU ya Tottenham Hotspur ikiwa uwanja wa nyumbani wa White Hartlane imeibana Manchester United na kwenda nao suluhu katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya England mchezo uliomalizika hivi punde.
Pamoja na kosa kosa nyingi katika kipindi cha kwanza, Manchester imeshindwa kuendeleza wimbi lake la ushindi na kuambulia pointi moja ugenini na kuifanya timu hiyo iendelee kukalia nafasi ya tatu.
Mashetani Wekundu walikosa mabao mengi ya wazi na kukosa makali kwenye kipindi cha pili na kufanya mechi hiyo iishe kwa timu hizo kutofungana na na kuifanya Spurs kufikisha pointi 31 na kuitambuka Arsenal wakati Mashetani Wekundu wamefikisha pointi 36.
Pambano linaloendelea kwa sasa ni lile la 'vinara' Chelsea iliyopo ugenini dhidi ya Southampton.

Kama Ustaadh, mcheki Cristiano Ronaldo katika vazi takatifu


Cristiano Ronaldo akiwa kwenye mavazi ya kiislam akipiga picha na mashabiki huko Dubai.

NYOTA wa klabu ya Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo alionekana na kupigwa picha na mapaparazi kwenye matembezi yake binafsi Dubai akiwa amevalia mavazi ya Kiislam na yaliompendeza sana.

Cristiano Ronaldo ambaye yeye si Muislam, alionekana kupendeza kupita kiasi katika vazi hilona alidai alipendezwa na uvaaji huo baada ya kuina watu wengi waishio Dubai katika vazi hilo kuu na kujihoji vipi naye asiwe miongoni mwa waliovaa vazi hilo. 
Pia hakuwahi kuvaa vazi la dini hiyo alionelea avae kwa ishara ya kuiheshimu dini hiyo na kuona sio kitu kibaya kuwa miongoni kwao kimavazi.

Cristiano Ronaldo akiwa kwenye vazi jingine la kiislamu huko Dubai

Mchezaji huyo alikuwa Dubai wiki iliyopita kwenye mapumziko yake binafsi mbali na shughuli za kimpira. Alienda kutembea huko kabla ya wiki ya sikukuu za Krismasi sambamba na mwanae aliyemvisha pia vazi hilo la kanzu.
Alionekana ni mwenye kufurahishwa na mandhali ya mji huo pia utamaduni wao wa chakula pia kimavazi ndio mana nae alipendezwa kuvaa kama wao.

Vazi lingine alilovaa mchezaji Cristiano Ronaldo akiwa kwenye matembezi yake binafsi Dubai.

Mchezaji huyo alikaa Dubai kwa siku nne wiki iliyopita na baadae aliondoka kurejea Hispania ambapo alijiunga na wachezaji wenzake kwenye kambi ya maandalizi ya mechi zilizoendelea katika ligi ya nchi hiyo anakochezea.