STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 8, 2014

Waliokufa ajali ya Airbus ni wanne tu


AJALI mbaya iliyotokea mjini Gairo ikihusisha basi la Airbus lililokuwa likitokea Dar kuelekea Tabora imedaiwa kusababisha vifo vya watu wanne tu na wengine kadhaa kujeruhiwa tofauti na taarifa za awali toka kwa waliokuwa kwenye tukio hilo kuwa zaidi ya watu 10 walikuwa wamekata roho.
Ajali hiyo ambayo imekuja siku chache baada ya roho za watu 39 kupotea kwenye ajali ilitokea mkoani Mara ikihusisha magari matatu, ilielezwa ilitokea majira ya asubuhi baada ya basi la Airbus kupinduka mara kadhaa na kuharibika huku baadhi ya abiria wakijeruhiwa vibaya na kutupwa nje na kuleta hofu kubwa.
Hata hivyo jeshi la Polisi la Morogoro limethibitisha waliokufa ni abiria wanne tu na siyo zaidi ya idadi hiyo na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali mjini Dodoma na Morogoro.

Babu Seya kaachiwa Huru nani kasema?!


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwRW3gfI8pIOBdf65LIaHBQzTJ_1ntCBcOUCbVgGXfnYmqtU3SHV7m-AwX-0lbIjBGHCaHue_ZEMjMXIbUG_yEMgBpwzHNRoPzdrO-7TdW4Ty2zIlsJ0rEa-XwtfKBbMj9-yR0jH_ECJA/s640/bauseya.jpg
Babu Seya na mwanae Papii Kocha
TANGU majira ya mchana kuna taarifa zilizagaa kwamba Babu Seya na mwanae Papi Kocha walikuwa wameachiwa huru na kuanza kusambazwa ujumbe mfupi wa simu za mkononi na kwenye mitandao ya kijamii.
Hata hivyo Jeshi la Magereza limefunguka na kuweka bayana juu ya ukweli wa taarifa hizo kama taarifa yao inavyosomeka hapo chini;
Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014

Fabregas afunguka ya moyoni kuhusu Chelsea

http://e1.365dm.com/14/07/800x600/Fabregas_3179732.jpg?20140728165853
Sikuwahi kuota kuja kuzaa uzi wa Chelsea kabisa aisee....dunia inabadilika sana
CESC Fabregas amekiri kwamba hakuwahi kufikiria hata mara moja kama angekuja kuitumikia klabu yake ya sasa ya Chelsea.
Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal na Barcelona, alisema wazo la kuitumikia klabu hiyo chini ya Jose Mourinho lilikuwa halifikiriki katika kipindi cha nyuma. 
Fabregas aliyerejea tena kwenye Ligi Kuu katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi baada ya kushindwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Barcelona, alisema kama mtu angemuambia miaka mitano nyuma kwamba atakwenda kucheza Chelsea chini Mourinho ni jambo ambalo asingeamini lakini maisha yanabadilika. 
Kiungo huyo alidai alianza kufikiria kuondoka Barcelona baada ya fainali ya Kombe la Mfalme ambayo walifungwa na Real Madrid ambapo baada ya kuzungumza na mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta aliona kama amewapunguzia bugudha kutokana na kauli yake. 
Baada ya hapo alimuomba wakala wake amtafutie timu nyingine na Chelsea wakatoa ofa ambapo baada ya kuzungumza na Mourinho na kumwambia mambo anayohitaji akaona hapo ndio patakapomfaa.

Mwamuzi afa ajalini, TFF yamlilia

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmRpmlPP9xJpBS_8mLZgKPLic2CoFHDnUT8GcHzIpatlFFo_XCz6NyaPIHEvMTTpcnILwpDDOKuRpWx7EePjClPxJ3LrbQ_Eais1BNmwIRmy2yv_eSiPMEEdCtgKP-2adLWq6lJncprglB/s640/Wajumbe.jpg
Luteni Lugenge (kushoto) enzi za uhai wake
 SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mwamuzi wa daraja la kwanza (class one), Luteni  David Lugenge kilichotokea jana (Septemba 7 mwaka huu) kwa ajali ya gari katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Luteni Lugenge ambaye mwishoni mwa wiki alishiriki mitihani ya utimamu wa mwili kwa waamuzi wa Ligi Kuu alikuwa na ndugu yake Christopher Alexander Lunyungu katika gari dogo wakienda mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Handeni, Peter Juma, Luteni Lugenge alikuwa akimsindikiza mwenzake aliyekuwa anakwenda kujitambulisha kwa wakwe zake watarajiwa.
Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Luteni Lugenge alikuwa ni mmoja wa waamuzi wanaoinukia nchini, hivyo mchango wake ulikuwa bado unahitajika. Hivyo tutamkumbuka daima.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Luteni Lugenge, Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu nchini (FRAT) na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Yanga waendelea kumkomalia Emmanuel Okwi, sasa wamshtaki FIFA

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe (kulia) akimtambulisha mshambuliaji Emmanuel Okwi kurejea katika klabu hiyo jijini Dar es Salaam jana. Picha: Halima Kambi 
SIKU moja baada ya Shirikisho la soka Tanzania, TFF kumtangaza mchezaji Emmanuel Okwi kuwa huru na hivyo anaweza kusajiliwa na klabu ya Simba, uongozi wa Yanga umesema haujakubali.
Uongozi wa Yanga umesema utatinga katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kupinga maamuzi ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumtangaza Emmanuel Okwi kuwa ni mchezaji huru na anaweza kuichezea Simba.
Baada ya kukutana jijini Dar es Salaam juzi kupitia masuala mbalimbali ukiwamo mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na Okwi, kamati hiyo ilisema imebaini kwamba mkataba kati ya pande hizo mbili ulikuwa umevunjika.
Hata hivyo, Yanga wamepinga maamuzi hayo na katika taarifa yao iliyotolewa na Kaimu Ofisa Habari, Baraka Kizuguto jana saa 7:08 mchana, klabu hiyo ya Jangwani imejipanga kuyakatia rufaa maamuzi hayo.
Kizuguto alisema Mwenyekiti wa Kamati  ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema hawajaridhishwa na maamuzi ya TFF huku akidai yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo.
Katika maelezo yake yaliyochapishwa kwenye mtandao wa klabu ya Yanga jana mchana, Mapande alidai kuwa Kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume cha malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.
Alisema wameshangaa kuona kamati hiyo ya TFF inaamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi yanayoshangaza.
“Kwanza, kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande katika taarifa hiyo.
Alisema mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwahi kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la Okwi limetoka wapi, kama lilikuwapo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama utaratibu ulivyo?” Alihoji Mapande.
Alisema kamati hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hanspoppe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba kuwamo katika kikao hicho ni kinyume cha taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa kimaslahi.
Lakini, katika maelezo ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, yaliyotolewa juzi usiku kupitia kwa Kaimu Karibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura, Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili katika mkataba huo wa pande mbili.
Wambura alieleza kuwa Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27, mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.
"Mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), kamati imebaini kuwa uhusiano huo haupo, hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi pamoja," inasomeka sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Wambura juzi.
Wambura ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, alisema kuwa pamoja na Yanga kuwasilisha pingamizi la kuwapo mmoja wa wajumbe katika kikao kwa sababu za kimaslahi (conflict of interests) (Hanspoppe), walifahamishwa kuwa kilichokuwapo mbele ya kamati ni mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na Okwi, na si usajili.
Pia lilijitokeza suala la Okwi kutakiwa na klabu ya Wadi Degla ya Misri. Kamati imeiagiza Sekretarieti ya TFF kulifanyia uchunguzi suala hilo na kulitolea taarifa katika kikao kijacho.
Wambura alidai kuiwa mjumbe huyo (Hanspoppe) hakushiriki katika kuchangia hoja na kutoa maamuzi na kwamba uamuzi wa kamati ulifanyika baada ya majadiliano, hivyo hakukuwa na suala la kupiga kura.
Okwi raia wa Uganda, ambaye juzi alikuwapo wakati mkataba huo ukipitiwa na kamati pamoja na wawakilishi wa Yanga, alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu kuitumikia timu hiyo ya Jangwani akitokea SC Villa ya Uganda.

Serena Williams atwaa taji la US Open

Williams akilala chini kwa furaha uwanja wa Arthur Ashe Arena baada ya kumshinda Caroline Wozniacki
MCHEZA tennis Serena Williams wa Marekani ametwaa ubingwa wa US Open.
Williams ameshinda katika mchezo uliofanyika usiku wa kuamkia leo baada ya kumtwanga Caroline Wozniacki wa Denmark kwa ushindi wa moja kwa moja.

Mpambano huo wa fainali ulipigwa mjini New York ambapo Serena ameshinda kwa seti 6-3, 6-3 na kujinyakulia ubingwa huo kwa mara ya 6.

Kwa sasa Serena ndiye mchezaji nambari 1 duniani kwa mchezo huo na pia bingwa mara 18 wa Grand Slam, amekuwa bingwa wa kombe hilo mara tatu mfululizo tangu mwaka 2012.

Wozniacki ambaye ni rafiki wa karibu wa Serena alimpongeza rafiki yake huyo baada ya mchezo na kusema alistahili ushindi huo kutokana na jinsi alivyocheza.
Over the moon: Serena Williams celebrates her US Open victory with a jump for joy with the trophy
Serena Williams akishangilia ushindi wa US Open dhidi ya Caroline.
Overwhelmed: Serena Williams drops to the court after beating Caroline Wozniacki for the US Open title
Serena Williams akianguka kwa furaha baada ya kumchapa Caroline Wozniacki katika US Open
Formidable: Williams dominated as she claimed an 18th career Grand Slam title
Passion: Williams screams in anguish despite being well in control of the match from the outset 
Out of reach: Wozniacki stretches for a forehand as she falls to Williams in 75 minutes
Kashindwa kufikia malengo: Wozniacki akijinyoosha msuli dhidi ya Williams dakika ya 75
Good spirits: Wozniacki and Williams share a laugh after the presentation in New York
Wozniacki na Williams wakionyesha tabasamu jijini New York

Sepp Blatter athibitisha kutetea kiti FIFA

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani,FIFA Sepp Blatter amethibitisha kuwa atakitetea kiti chake katika uchaguzi ujao wa shirikisho hilo. 
Akihojiwa jijini Manchester, Blatter 78 alithibitisha uamuzi wake japo alidai atatoa taarifa rasmi katika mkutano mkuu wa kamati ya utendaji ya FIFA utakaofanyika Septemba 25 na 26. 
Tayari rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Michel Platini ameshatangaza kutogombea nafasi hiyo ya Blatter. 
Blatter ambaye amekuwa katika kiti hicho cha FIFA tangu mwaka 1998 amesema amechukua uamuzi huo kwa vile kazi alioianza anaona bado haijamalizika. 

Huzuni! Watoto wa3 wateketezwa moto kinyama

http://zanzibardaima.files.wordpress.com/2013/01/moto.jpg?w=400&h=369&crop=1

WATOTO watatu wa familia moja wamekufa na wengine wanne kujeruhiwa baada ya nyumba yao kumwagiwa petroli kisha kuteketezwa kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kumkia jana.Tukio hilo lililotokea katika mtaa wa Elimu kata ya Kalangala wilayani Geita.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya, Dk. Adam Sijaona, amethibitisha kupokea miili ya watu hao, Mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Ukombozi Reginald Robert (9), Sophia Robert (6) (darasa la kwanza)na Remijius Robert (4).Dk. Sijaona aliwataja waliojeruhiwa sehemu za kifua, kichwani, mikono na miguu na makalio kuwa ni baba wa familia hiyo, Robert Remijius (45), mkewe, Angelina Gaspar (42) na mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Mwatulole, Scolastica Robert (15), aliyehamishiwa hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza kutokana na kuungua vibaya.

Alisema Salvance Reginald (47), ambaye ni dada wa Remijius amelazwa baada ya kupatwa na mshtuko kutokana na kushuhudia miili ya marehemu hao, akiwa miongoni mwa akinamama wengi waliokumbwa na mshtuko. Wakisimulia tukio hilo, baadhi ya wananchi wakiwamo viongozi wa serikali za mitaa na kata, walisema limetokea usiku wa manane baada ya walinzi wa jadi na mgambo wa doria kupiga filimbi za utambulisho, hivyo kwenda eneo la tukio na kusaidia uokoaji.

Ofisa Mtendaji wa kata ya Kalangalala, Hamad Hussein, alisema chanzo cha ‘wauaji’ kumwaga petroli milangoni na madirishani, huenda ni chuki za mgogoro wa ardhi.

Mwenyekiti wa mtaa wa Elimu na Ofisa Mtendaji wa mtaa huo, Simfukwe Ally, alisema kwa nyakati tofauti katika eneo la tukio kuwa taarifa za awali zinahusisha unyama huo na mgogoro wa ardhi uliokuwapo kwa muda mrefu bila kumtaja mtuhumiwa.

Akitoa pole eneo la tukio kwa niaba ya serikali ya wilaya Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Omary Mangochie, alieleza kusikitishwa na unyama huo na kuagiza ngazi ya mtaa hadi wilaya washirikiane kuhakikisha waliohusika wanakamatwa.

''Naagiza waliohusika wote wamekamatwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, kamwe serikali na jamii haiwezi kuona unyama wa aina hiyo wala kuuvumilia nafahamu jamii itakuwa inawatambua maana wanatoka na wanaishi ndani ya jamii yenyewe,” alisema Mangochie.

Awali shuhuda wa tukio hilo, Lunyili Tekamisa, aliyeongoza walinzi wenzake wa doria kufika eneo la tukio, alisema walikuta moto mkali ukiwaka katika milango na madirisha yote.

''Tulichofanya ni kuvunja milango na madirisha...kwa tahadhari na pembeni kulikuwa na kindoo kidogo chenye ujazo wa lita tano kikiwa na mabaki ya mafuta ya petroli ambacho baadaye tulikikabidhi kwa polisi,” alisema Tekamisa.

Tukio hilo limeutikisa mji wa Geita na viunga vyake na pia kuzua hofu kubwa huku likileta majonzi makubwa na vilio kila kona likifananishwa na wale wanaotumia tindikali kutekeleza uhalifu wao.
CHANZO: NIPASHE

Mabasi ya Dar Exp, Simba Mtoto yagongana



HABARI zilizotufikia punde zinasema mabasi mawili ya Simba Mtoto na Dar Express yamegongana Muheza mjini Tanga mchana huu, japo haijafahamika madhara ya ajali hiyo.

Tamasha la Handeni Kwetu lapania rekodi mpya



MRATIBU Mkuu wa Tamasha la Utamaduni Handeni, maarufu kama ‘Handeni Kwetu’, Kambi Mbwana, ameapa kuhakikisha kuwa tamasha lao msimu wa 2014 linakuwa la aina yake na kuvunja rekodi ya mwaka jana lilipofanyika kwa mara ya kwanza wilayani Handeni, mkoani Tanga.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mbwana alisema kuwa hiyo ni kutokana na kutamani kushirikisha wasanii wengi kutoka Tanga na Tanzania kwa ujumla.


Alisema kwamba mwaka jana wasanii zaidi ya 200 walionyesha uwezo wao kutoka kwa vikundi mbalimbali vya wilayani Handeni na jijini Dar es Salaam.


“Mwaka jana vikundi zaidi ya 10 vyenye wasanii wasiopungua 15 walipata nafasi ya kupanda jukwaani kuonyesha vipaji vyao, ukiacha wasanii wanaotoka kwenye Kambi ya jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa Mgambo waliozidi 80.


“Wakati tunajivunia mafanikio haya, tunaamini msimu huu utakuwa mzuri zaidi tukiamini kuwa tutavunja rekodi ya mwaka jana, ambapo tulishuhudia burudani mbalimbali, ikiwamo hadithi zilizohusu watu wa Handeni, bila kusahau vyakula vya asili pamoja na michezo waliyokuwa wakicheza wazee wetu enzi hizo,” alisema Mbwana.

Kwa mujibu wa Mbwana, mipango ya kuboresha tamasha hilo imepamba moto ambapo kwa sasa utafiti wa ubora wa vikundi nje ya wilaya ya Handeni inafanywa ili kuhakikisha kuwa wasanii watakaopanda jukwaani wanakuwa na uwezo wa juu na kufanikisha kwa dhati kukuza sekta ya utamaduni pamoja na uchumi wa Tanzania.

Breaking News: Ajali nyingine yaua zaidi ya watu 10 Gairo


ajali tabora 1
Baadhi ya waokozi wakiitoa miili ya abiria ndani ya gari hilo
AJALI za barabarani zimeendelea kupoteza uhai wa watanzania baada ya muda mfupi uliopita kudokezwa kuwa mapema leo asubuhi bao la Airbus lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tabora kupinduka ewneo la Kuegeya mjini Gairo na kusababisha vya watu kadhaa huku wengine wakiwa majeruhi.
MICHARAZO inafuatilia taarifa hizo na zitawafahamisha vyema na idaidi ya waliokufa katika ajali hiyo inayoelezwa kuwa ni mbaya kutokana na basi hilo kupinduka na kuwarusha baadhi ya abiria.
Hata hivyo taarifa za awali zinasema watu zaidi ya 10 wamekufa katika ajali hiyona Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Faustine Shilogile amethibitisha ajaliu hiyo akiwa eneo la tukio.
Kamanda Shilogile alisema angetoa taarifa baadaye kuhusu idadi kamili ya waliofariki na majeruhi, ila alikiri ni ajali mbaya.
Ajali imekuja ikiwa ni siku chache tangu watu zaidi ya 30 kufa katika ajali iliyohusisha magari matatu yakiwamo mabasi mawili ya J4 na Mwanza Coach kugongana mjini Musoma na kujeruhi wengine zaidi ya 70. 

Huyu ndiye Afisa Habari Mpya wa Yanga

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEid5_k8DKcGymZ7yAk-68_Z73tXvM_lM05ZvoBGr43yLtAx51OQfVZnTntd_ZM9zjcgq70Oxrtyr5xg7N6mBaQWuR0jqL8zsAF9b-6_5gaG31CxK7dLCQP2AbIdiqNkvJOfSFhyphenhyphenGb2DD21H/s1600/jerry-muro.jpg
Jerry Muro ndiye Msemaji Mkuu wa Yanga
 MTANGAZAJI mahiri nchini aliyewahi kufanya kazi na vituo vya ITV na TBC1, Jerry Muro amekula shavu baada ya kuteuliwa kuwa Msemaji wa Yanga.
Muro anatarajia kuanza kazi ndani ya siku chache zijazo kuchukua nafasi ya aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto ambaye sasa atakuwa akifanya kazi nyingine za klabu hiyo.
Muro alijipatia umaarufu mkubwa katika kuendesha vipindi vya uchunguzi akiwa ITV kabla ya kuja kuangushiwa jumba kwa kufunguliwa kesi ya Rushwa ambayo hata hivyo aliibuka kidedea dhidi ya waliomfungilia kesi hiyo.

Stars bado nyanya kwa Burundi yapigwa 2-0

http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/09/stars-1.jpgTIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars bado haijapata dawa ya kufuta uteja kwa Burundi baada ya kukandikwa mabao 2-0 katika mechi ya marudiano ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa jijini Bujumbura Burundi.
Stars iliyoenda Burundi ikitamba kwenda kulipa kisasi cha mabao 3-0 ilichopewa na wenyeji wao kwenye mechi ya kirafiki ya kuadhimisha Siku ya Uhuru, ilishindwa kutimiza tambo hizo kwa kukandikwa na wenyeo wao kwenye mechi hiyo ya ugenini.
Mabao yaliyoizamisha Stars yalifungwa katika dakika ya kwanza tu ya mchezo na Saido Ntibazonkiza kabla ya Yusuf Ndikumana kuongeza la pili kwenye dakika ya 29 na kuifanya Stars ipigane kusaka angalau bao la kufutia machozi bila mafanikio yoyote.

Thomas Muller aibeba Ujerumani Euro

Easy does it: Thomas Muller remained composed in the area to side-foot the ball into the roof net to put Germany back in front with twenty minutes remainingMSHAMBULIAJI nyota wa Ujerumani,  Thomas Muller aliendeleza rekodi yake ya mabao wakati alipoisaidia nchi yake kupaa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Scotland katika mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016 (Euro 2016).
Muller alifunga bao la kwanza katika dakika ya 18 ya mchezo, kabla ya  Ikechi Anya akaisawazishia Scotland katika dakika ya 66.
Baada ya matokeo kuwa 1-1, Ujerumani ambao ni mabingwa wa kombe la dunia chini ya kocha Joachim Low walifanya mashambulizi kadhaa langoni kwa Wascotish na katika dakika ya 70, Muller aliandika bao la pili na la ushindi.
Mabao hayo yamemfanya Muller kufikisha jumla ya  25 katika mechi 58 alizoichezea timu ya Taifa ya Ujerumani.
Katika mchezo huo Scotland walipata pigo katika dakika za majeruhi baada ya Charlie Mulgrew kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Polisi Geita wanasa wawili, bunduki 7 mabomu 10

Bunduki 7 na mabomu 10  yaliyokamatwa huko Bukombe

MSAKO mkali unaoendelea Geita kusaka wale wote waliohusika na tukio la kuvamiwa na kisha kuuwawa kwa askari Polisi wawili wa kituo cha Polisi cha Bukombe, umefanikiwa kuwanasa wawili na silaha kadhaa yakiwamo mabomu.
Habari zilizothibitishwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Geita ni kwambawatu wawili walikamatwa na kukutwa na bunduki saba na mabomu 10 eneo la Ushirombo wilaya ya Bukombe.

Inasadikiwa kuwa bunduki hizo ni kati ya bunduki kumi zilizoporwa na majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Bukombe na kufanya mauaji ya askari polisi wawili waliokuwa zamu  usiku wa kuamkia juzi na kujeruhi askari wawili.

Tunaarifiwa kuwa Bunduki zilizokamatwa nne ni SMG na tatu aina ya Shotgun  pamoja na panga zimepatikana  katika tanuru la kuchomea matofali zikiwa zimefichwa pamoja na mabomu hayo.

Habari zinasema kuwa  katika msako huo mkali unaoendelea, Jeshi linaloendelea kufanya kazi nzuri  limekamata watu watatu  pia  na mwalimu mmoja wa shule ya sekondari Ushirombo anayedaiwa kushiriki katika tukio.
Msako huo wa jeshi la polisi bado unaendelea kufanya msako mkali ili kuwakamata wahusika wote na silaha zote zilizoporwa na majambazi.