![]() |
Williams akilala chini kwa furaha uwanja wa Arthur Ashe Arena baada ya kumshinda Caroline Wozniacki
|
Williams ameshinda katika mchezo
uliofanyika usiku wa kuamkia leo baada ya kumtwanga Caroline Wozniacki
wa Denmark kwa ushindi wa moja kwa moja.
Mpambano huo wa fainali ulipigwa mjini New York ambapo Serena ameshinda kwa seti 6-3, 6-3 na kujinyakulia ubingwa huo kwa mara ya 6.
Kwa sasa Serena ndiye mchezaji nambari 1 duniani kwa mchezo huo na pia bingwa mara 18 wa Grand Slam, amekuwa bingwa wa kombe hilo mara tatu mfululizo tangu mwaka 2012.
Wozniacki ambaye ni rafiki wa karibu wa Serena alimpongeza rafiki yake huyo baada ya mchezo na kusema alistahili ushindi huo kutokana na jinsi alivyocheza.
Serena Williams akishangilia ushindi wa US Open dhidi ya Caroline.

Serena Williams akianguka kwa furaha baada ya kumchapa Caroline Wozniacki katika US Open



Kashindwa kufikia malengo: Wozniacki akijinyoosha msuli dhidi ya Williams dakika ya 75

Wozniacki na Williams wakionyesha tabasamu jijini New York
No comments:
Post a Comment