STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 31, 2015

Bingwa wa Taifa Wanawake kuzoa Mil.3

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhENRxfiE96-KL4ns71WPE2_XM1rUPglyqgf7sij2rgovmDsZi8fpyZJd_YZoswfB67v51e2xA3AoMNgNjzrK728L5tHgcMEVDmQ1vzukkgCK7lD5lb9wuNnWnoNjKAXtEuumAvIqQElrU/s1600/MUKA.jpg
Waziri Dk Fenella Mukangara atakayekuwa mgeni rasmi katika fainali za Kombe la Taifa la Wanawake
Na Boniface Wambura 
BINGWA wa michuano ya Kombe la Taifa Wanawake, inayodhaminiwa na kampuni ya Proin na atapata Kombe na fedha taslimu Sh. Milioni 3. 
Aidha, katika michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini, mshindi wa pili atapata Sh. Milioni 2, wakati mshindi wa tatu atapata Sh. Milioni 1.
Fainali ya Kombe la Taifa Wanawake itazikutanisha Pwani na Temeke kesho Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam na mashabiki wataingia bure.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mechi hiyo itakayoanza Saa 10.15 jioni, ikichezeshwa na refa wa FIFA, Jonesia Rukyaa na kuonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam.
Marefa wasaidizi wanatarajiwa kuwa Hellen Mduma, Agnes Alphonce, na Mwanahamisi Matiku wakati Kamisaa atakuwa Ingridy Kimario. Timu za Ilala na Kigoma zitacheza mechi ya utangulizi kutafuta mshindi wa tatu kuanzia saa 8.00 mchana.

Bayern Munich waonja kipigo Bundesliga

Bas Dost scores
Bayern walivyokuwa wakiangamizwa na Wolfsburg
Pep Guardiola
Kocha wa Beyern Munich, Pep Guardiola akiwa haamini kama vijana wake wamemuangusha ugenini
MABINGWA watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich jana ilikiona cha moto ugenini baada ya kunyukwa mabao 4-1 na Wolfoburg kikiwa ndicho kipigo cha kwanza kwao kwa msimu huu katika ligi hiyo.
Mabao mawili yaliyofungwa na Bas Dost katika dakika ya nne na 45 na mengine ya Kelvin De Bruyne ya dakika za 53 na 73 yalitosha kuwazima wababe hao wa Ujerumani ambao walipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 55 kupitia kwa Juan Bernat.
Licha ya kipigo hicho Bayern wameendelea kukalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo wakiwa na pointi 45 na wapinzani wao waliowatoa nishai Wolfsburg waking'ang'ania nafasi ya pili wakiwa na pointi 37.
Ligi hiyo inaendelea jioni hii kwa michezo kadha kabla ya kesho kumalizia michezo mingine ya wikiendi hii.












Newcastle Utd yainyuka Hull City, Man Utd waongoza 3-0 HT

Sammy Ameobi (right) is congratulated after scoring for Newcastle
Wachezaji Newcastle waksihangilia moja ya mabao yao
Ahmed Elmohamady of Hull City punches the ball into the Newcastle net
Hekaheka langoni mwa Newcastle
Sammy Ameobi shoots to score for Newcastle
Sammy Ameobi akifunga bao la pili la Newcastle
KLABU ya Newcastle United ikiwa ugenini imetoa kipigo cha mabao 3-0 kwa wenyeji wao Hull City katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya England.
Newcastle walianza kuandika bao la kwanza dakika ya 40 kupitia kwa Remy Cabella kabla ya kuongeza bao la pili dakika tano baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kupitia kwa Sammy Ameobi na katika dakika ya 78 Yoan Gouffran alimaliza udhia kwa kufunga bao la tatu na kuipa ushindi muhimu Newcastle United.
Kwa sasa michezo kadhaa ipo mapumziko huku Spurs wakiongoza mabao 2-0 dhidi ya West Bromwich, Everton ikiwa ugenini wanaongoza bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace, Liverpool dhidi ya West Ham Utd wapo 0-0, Manchester United wanaongoza 3-0 dhidi ya Leiceister City uwanja wa Old Trafford, Stoke City wakiwa nyumbani wanaongoza 2-1 dhidi ya QPR na Sunderland wakiwa mbele kwa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Burnley.

Mnyama 'yaua' Taifa, Mbeya City yalala Moro 1-0

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhQw0Q6Z99EoVWkyx9Yf4-SQu6v6ms0PaPb_sKenOOroi-QKbRnmecjHWsCkMjBGp9Gme9kVSLBI6loRiDVMNpxjyOidGhsx9k3uN8L4NzFcmC9SUT8cQrLUnJwL2a4pbDoK4TypzmK_ig/s1600/_HMB7014.JPG
Simba
JKT Ruvu
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/IMG-20140920-WA005311.jpg
Mbeya City iliyolala Morogoro

BAADA ya kuwaweka roho juu mashabiki wao, Simba jioni ya leo imezinduka mbele ya JKT Ruvu baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 2-1 na kupanda hadi nafasi ya saba.
Mabao mawili ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Dan Sserunkuma yameisaidia Simba kupata ushindi wake wa tatu katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye uwanja wa Taifa na Simba walianza kuandika bao mapema kabla ya JKT Ruvu kurejesha na kwenda mapumziko matokeo yakiwa bao 1-1.
Bao la Simba lililofungwa na Sserunkuma liliwekwa kimiani katika dakika ya pili tu ya pambano hilo akiunganisha krosi pasi ya Emmanuel Okwi.
Hata hivyo JKT Ruvu walikuja kusawazisha bao hilo dakika ya 19 kwa George Minja kuunganisha kwa kichwa mpira wa Jabir Aziz na kufanya timu ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa.
Sserunkuma aliihakikishia Simba ushindi baada ya kufunga bao la pili katika dakika ya tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kewa kichwa akiwahi mpira wa krosi ya Okwi na kusaidia Simba kulipa kisasi kwa maafande hao ambao waliwafunga mabao 3-2 walipokutana mara ya mwisho.
Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 16 na kuchupa kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya saba.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Mtibwa Sugari imejikuta ikichupa hadi nafasi ya pili ya msimamo ikiziengua Yanga na JKT Ruvu baada ya kupata suluhu ya bila kufungana dhidi ya Coastal Union.
Mtibwa Sugar ilipata sare hiyo uwanja wa Mkwakwani Tanga na kufikisha pointi 18 sawa na ilizonazo Yanga waliokuwa wa pili ambao wanashuka hadi nafasi ya tatu japo kesho itashuka dimbani kuumana na Ndanda na kuwa na nafasi ya kukwea kileleni.
Nayo timu ya Polisi Moro imefanikiwa kuinyuka Mbeya City bao 1-0 ikiwa ni sikui chache tangu Mbeya City kutoka  kuilaza Simba 2-1 katikati ya wiki kwenye mechi yao ya kiporo kilichochezwa uwanja wa Taifa.
Mjini Mbeya wenyeji Prisons ililazimishwa sare ya 1-1 na wageni wao Kagera Sugar katika mchezo unaodaiwa ulikuwa mkali na wa kusisimua wenyeji walianza kuzinguliwa kwa bao la Rashid Mandawa kabla ya kuchomoa dakika 15 kabla ya kumalizika kwa pambano hilo kupitia Nurdin Chona..
Katika mfululizo wa ligi hiyo kesho, Yanga itaikaribisha Ndanda kwenye uwanja wa Taifa wakati Ruvu Shooting wataialika Stand United ya Shinyanga kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.

Friday, January 30, 2015

NGOMA MPYA YA MATONYA-HOMA YA JIJ

Ngoma mpya ya Matonya - Homa Ya Jiji.mp3 @Hulkshare:

Chelsea yakaribia kumnasa Cuadrado

http://resources2.news.com.au/images/2015/01/27/1227198/061530-6ca4ddec-a5bb-11e4-a11e-9d15a37a8504.jpg
Juan Cuadrado anayekaribia kutua Chelsea
VINARA wa Ligi Kuu ya England, klabu ya Chelsea ipo katika hatua za mwisho kukamilisha dili la Pauni Mil. 23.3 ili  kumsajili winga wa Fiorentina Juan Cuadrado, 26.
Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia tayari ameshafikia makubaliano kuhusu mambo yake binafsi na Chelsea na kwa sasa klabu ziko katika hatua za mwisho kukamilisha uhamisho huo.
Inakadiriwa kuwa Chelsea watatoa kitita cha Pauni Mil.26.8 kwa ajili ya winga huyo kiasi ambacho ndio kilichowekwa na klabu yake hiyo ya Italia sambamba na kudaiwa kuwa mbioni kumtoa kwa mkopo kinda lake Mohamed Salah, 22 kwa klabu hiyo ya Fiorentina ikiwa ni sehemu ya kukamilisha dili hilo.
Hata hivyo, Salah ambaye ni winga wa kimataifa wa Misri bado hajaamua kama anataka kwenda kucheza Serie A au sehemu gani nyingine.
Aidha imedokezwa kuwawinga nyota wa Chelsea, Andre Schurrle yupo katika mazungumzo ya kutua klabu ya Bundesliga,Wolfsburg.

HII NDIYO TANZANIA BHANA YENYE AMANI NA UTULIVU!


Simba katika mtihani mwingine, kulipa kisasi kwa JKT kesho?

Simba watavuna nini kesho kwa JKT
JKT Ruvu kuendeleza machungu Msimbazi?
WAKATI Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola akiomba kuachia ngazi mwenyewe ndani ya klabu hiyo, timu hiyo kesho itakuwa na kibarua kingine kigumu mbele ya maafande wa JKT Ruvu katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika mechi ya mwisho baina ya timu hizo msimu uliopita, Simba ilicharazwa mabao 3-2 na maafande hao hali inayofanya mechi ya kesho miongoni mwa mechi zitakazochezwa katika viwanja tofauti kuwa ni kama vita ya kisasi.
Simba na JKT wataumana kwenye uwanja wa Taifa, huku timu hizo zikiwa na matokeo tofauti katika mechji zao zilizopita, Simba ikitoka kupokea kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City wakati JKT Ruvu wakilazimishwa sare ya 1-1 na Mgambo JKT.
Mechi nyingine zitakazopigwa kesho ni pamoja na zile za timu za Coastal Union dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo utakaochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga, huku Prisons Mbeya itawalika Kagera Sugar uwanja wa Sokoine Mbeya na Polisi Moro waliotoka kucharazwa bao 1-0 na Yanga wataialika Mbeya City uwanja wa Jamhuri.
Mechi ya Mgambo JKT na Azam yenyewe imeahirishwa kwa kuwa Azam wapo DR Congo wakicheza mechi za kirafiki za michuano maalum.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa michezo miwili Yanga itaikaribisha Ndanda ya Mtwara na Ruvu Shootimng itavaana na Stand United kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi Pwani.
Mpaka sasa katika ligi hiyo Azam wapo kileleni wakiwa na pointi 21 wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 18 sawa na JKT Ruvu.
Katika hatua nyingine uongozi wa Simba umesema umepata taarifa za Kocha Msaidizi wa timu yao Seleman Matola kutokana na kile kinachoelezwa kuwa kuitingwa na majukumu, japo inaelezwa kusakamwa na baadhi ya wanachama na viongozi wa klabu hiyo ni sababu ya Matola kuamua kubwaga manyanga.
Uongozi wa Simba kupitia Rais wake, Evance Aveva umesema kuwa umemtaka kocha huyo kuandika maombi yake kimaandishi ili kuyajadili na kutoa maamuzi, sambamba na kutoa sababu ya timu yao kuwa na matokeo mabaya katika mechi za karibuni kuwa inatokana na uchovu wa wachezaji kucheza mfululizo.
Wakati ligi ikiingia kwenye raundi ya 13 wikiendi hii chini ni msimamo na orodha ya wafungaji mpaka sasa.
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                                P   W    D    L    F    A   GD   Pts
01. Azam                 11  06  03  02  15  08  07   21
02. Yanga                10  05  03  02  12   07  05  18
03. JKT Ruvu           12  05  03  04   12   11  01  18
04. Mtibwa Sugar     10  04  05  01  13  07  06   17
05. Coastal Union    11  04  04   03  10   08  02  16
06. Polisi Moro         12  03  06  03   09  09  00  15
07. Mbeya City         11   04  03  04  08   09  -1   15
08. Ruvu Shooting    12  04  03   05   07   09  -2  15
09. Kagera Sugar     12  03  05  04   09   10   -1  14
10. Mgambo JKT      11  04  02  05   06    10  -4  14
11. Simba                11  02  07   02   11   10  01  13
12. Ndanda Fc          12  04  01   07  12    17  -5  13
13. Stand Utd           12  02  05   05   07   14  -7  11
14. Prisons               11  01  06   04   08   10  -2   09
Wafungaji:

7- Didier Kavumbagu(Azam)
6- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu)
5-Ame Ali (Mtibwa), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Danny Mrwanda (Yanga)
4- Rama Salim (Coastal),  Simon Msuva (Yanga),  Emmanuel Okwi (Simba)
3- Ally Shomari (Mtibwa),  Jacob Massawe (Ndanda), Nassor Kapama (Ndanda)

Gerrard Pique, Shakira wapata mtoto wa pili

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/08/Shakira-Gerard-Pique-Milan.jpg
Shakira na Pique wakiwa na Milan
BEKI wa Barcelona, Gerard Pique na mwanamuziki nyota Shakira wamepata mtoto wao wa pili aliyezaliwa usiku wa jana.
Shakira alijifungua mtoto wa kiume bila matatizo yeyote katika hospitali ya Quiron Tecknon iliyopo jijini Barcelona.
Pique, 27 na mwanamuziki huyo wa Pop kutoka Colombia mwenye umri wa miaka 37, walitoa taarifa hizo muda mfupi kabla ya usiku wa manane.
Jina la mtoto ambaye amezaliwa miaka miwili baada ya wawili hao kupata mtoto wao wa kwanza aitwaye Milan Piqué Mebarak, ni Sasha Piqué Mebarak.
Wawili hao wamekuwa pamoja toka mwaka 2010 walipokutana katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Diego Costa majanga! Afungiwa England

The Spain striker celebrates his goal in the 2-0 Premier League win over West Ham
Diego Costa aliyefungiwa mechi tatu kwa kosa la kumtimba Emre Can
STRIKA mkali wa klabu ya Chelsea, Diego Costa amefungiwa mechi tatu kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Liverpool Emre Can.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu kati ya timu yake na Manchester City utakaochezwa Stamford Bridge kesho pamoja na mechi dhidi ya Aston Villa na Everton. Chama cha Soka cha Uingereza-FA kilimtwanga adhabu hiyo ambayo Costa aliipinga kuhusiana na tukio lake alilofanya katika dakika ya 12 ya mchezo wa nusu fainali ya mkondo ya pili wa Kombe la Ligi uliofanyika Jumanne iliyopita.
Costa aliyesajiliwa kwa kitita cha Pauni Mil. 32, ameshafunga mabao 17 katika mechi 19 za Ligi Kuu alizocheza simu huu.
Tukio hilo halikuonwa na waamuzi lakini lilinaswa katika picha za video na FA kutumia kama ushahidi wa kumtia adabu mshambuliaji huyo ambaye alikuwa akitetewa na kocha wake, Jose Mourinho.

ROBO FAINALI AFCON 2015 NI VITA TUPU!

*Wakongo kumaliza ubishi kesho, Ghana, Guinea balaa

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/74471000/jpg/_74471882_161377467.jpg
Taji linalosubiri mbebaji wake
http://static.allsports.com.gh/img/incoming/origs3434059/431253271-w1280-h960/DR-Congo-National-team.jpg
DR Congo
http://www.redpepper.co.ug/wp-content/uploads/2015/01/eq.jpg
Wenyeji Guinea ya Ikweta
FAINALI za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON- 2015) yamefikia patamu wakati kesho timu nane zilizofanikiwa kupenya kutoka kwenye makundi zitaanza kutupa karata zao katika mechi za Robo Fainali kuwania kucheza Nusu Fainali baadaye wiki ijayo.
Guinea ambayo ililinagana kila kitu na Mali katika nafasi ya pili ya Kundi D lililoongozwa na Ivory Coast jana ilipenya kwa kupitia turufu ya kura na kurejesha matukio matatu kama hayo kuwahi kushuhudiwa kwenye michuano mikubwa duniani ya Kombe la Dunia 1954 na 1990 pamoja na Kombe la Mataifa mwaka 1988.
Guinea na Mali zilishindwa kutambiana katika mechi yao ya mwisho kwa kutoka sare ya 1-1 ikiwa ni sare zao za tatu baada ya awali kufanya kama hivyo mbele ya Ivory Coast na Cameroon iliyooaga mashindano kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa vinara wa kundi hiyo Tembo wa Ivory.
Ndipo Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likaamua kuzipambanisha timu hizo katika kapu la sadakarawe na Mali kuangusha kuwapisha wenzao kuendelea ambapo sasa Guinea wamepangwa kuumana na Ghana katika mechi ya tatu ya Robo fainali itakayochezwa siku ya Jumapili jioni.
Mechi zitakazochezwa kesho kwa mujibu wa ratiba ni Congo Brazzaville dhidi ya wapinzani wao wa jadi DR Congo pambano litakalochezwa saa 1 jioni kwenye uwnaja wa Bara kabla ya wenyeji Guinea ya Ikweta kupepetana na Tunisia katika mechi isiyotabirika kutokana na timu hizo kumaliza katika uwiano sawa kwenye makundi yao.
Wakongo wameshakutana mara tano katika michezo mbalimbali ya karibuni tangu mwaka 2000 na timu hizo zimeshindw akutambiana kwa kila mmoja kushinda mara mbili na kutoka sare moja.
Kupenya kwa Guinea kwa kutupia turufu ya sadakarawe inakumbusha michuano ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1954 wakati Ugiriki ilipowazidi kete Uholanzi
Katika fainali hizo Ugiriki na Hispania zililingana katika kundi lao na turufu ikawabeba Ugiriki kwenda kwenye fainali na tuykio hilo lilijirudia tena kwenye fainali za mwaka 1990 Ireland iliibwaga Uholanzi katika zoezi kama hilo.
Katika fainali za Afrika za mwaka 1988 Algeria ilipenya mbele ya Ivory Coast baada ya kulingana kila kitu.
Mbali na michezo hiyo ya kesho, Jumapili kutakuwa michezo miwili kubwa linalosubiriwa kwa hamu kubwa ni Ivory Coast dhidi ya Algeria litakalochezwa usiku wa saa 4:30 huku Tembo wakiwa na wasiwasi na hali ya kiafya ya nahodha wao, Yaya Toure.
Timu zitakazofuzu hatua hiyo zitakutana kwenye nusu fainali zitakazochezwa katikati ya wiki kabla ya kufahamika timu mbili zitakazocheza Fainali itakayopigwa Februari 8 na kupatikana kwa bingwa mpya wa michuano hiyo baada ya wlaiokuwa watetezi Nigeria kukwama kwenye kwenye fainali hizo za Guinea ya Ikweta.

VUMBI LA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI HII LIPO HIVI

http://www.footballgate.com/wp-content/uploads/2014/09/barclays-english-premier-league-wallpaper-2014-2015-790x444.jpgKIVUMBI cha Ligi Kuu England kinatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii baada ya wiki iliyopita kusimama kupisha Raundi ya nne ya Kombe la FA na mechi za Nusu Fainali ya Kombe la Ligi (Capital One).
Chelsea ambao wamefanikiwa kufuzu Fainali za Kombe la Ligi kwa kuvaana na Tottenham Hotspur Machi Mosi kwenye uwanja wa Wembley, itashuka dimbani kesho kuvaana na Mabingwa Watetezi, Manchester City.
Kwa mujibu wa ratiba ya mechi hizo za wikiendi hii Kesho kutakuwa na mechi nane zitakazokutanisha timu 16 kabla ya Jumapili kushuhudiwa mechi mbili tu ambazo zitazikutanisha timu nne.
Mechi za kesho zipo hivi:
Hull City15:45 Newcastle United
Crystal Palace  18:00  Everton
Liverpool  18:00 West Ham United
Manchester Utd 18:00 Leicester City
Stoke City    18:00 Queens Park Rangers
Sunderland  18:00  Burnley      
West Bromwich 18:00 Tottenham Hotspur   

Chelsea  20:30 Manchester City
Jumapili:

Arsenal     16 : 30     Aston Villa     
Southampton   19:00 Swansea City

KUMEKUCHA SIMBA! WANACHAMA WATAKA MKUTANO

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi1rzqcYY91IP82IKEyguMFJWPC4hCQgVwYhX3RKM0wUWMMuRH11c_EXojxJd1liCSgl-5xR3eMAFwHxHQxLf1A63zvgEBMnmQv-b_GOPlE8nQo6YIctaW4NKlP7YZhAd43uG-OnVBeNiY/s1600/hans+poppe+na+aveva.jpg
Rais Evance Aveva akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hanspop
KUFUATIA timu yao kupata kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa wageni Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi, wanachama wa klabu ya soka ya Simba wanautaka uongozi wa klabu yao kuitisha mkutano mkuu wa dharura ili kujadili mwenendo mbaya wa kikosi chao kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Simba juzi ilipoteza mechi yake ya pili msimu huu na kuangukia katika nafasi ya 11 kwenye msimamo ligi hiyo ya timu 14 ikiwa imetoka sare mara saba na kushinda mechi mbili tu.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake, Mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa lililoko Magomeni jijini Dar es Salaam, Ustadh Masoud, alisema kwamba wanauomba uongozi kuitisha mapema mkutano ili waweze kupata suluhisho kabla ya 'jahazi' halijazidi kuzama.
Masoud alisema kwamba kupitia mkutano wa wanachama, wanaamini watafahamu kinachosababisha timu yao kufanya vibaya kwenye mechi zake za ligi na kupoteza matumaini ya kutwaa ubingwa.
Alisema pia wamebaini ndani ya uongozi hakuna umoja na baadhi yao wanaingilia majukumu ya watu wengine.
"Mwenendo wa timu hauturidhishi kabisa, ndiyo maana tumeomba viongozi waitishe mkutano wa dharura, tayari tumeshapeleka barua kuwaomba mkutano haraka," alisema mwenyekiti huyo wa kundi maarufu na lenye nguvu ndani ya Simba.
Aliongeza kwamba pia hawana imani na baadhi ya viongozi waliopo kwenye benchi la ufundi na kuutaka uongozi ulifanyie kazi.
Mashabiki wa klabu hiyo na wanachama walisikika wakisema baada ya mechi yao ya juzi kuwa Simba si shule ya soka, ni klabu kubwa inayopaswa kupigania mataji hivyo viongozi wanapaswa kusajili wachezaji walioiva tayari na kwamba vijana waingizwe wachache taratibu kupewa uzoefu tofauti na ilivyo sasa.
Simba juzi iliwatumia yosso saba Manyika Peter, Hassan Isihaka, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Jonas Mkude, Twaha Ibrahim, Ibrahim Hajib na Ramadhani Singano.
Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema kuwa amepata taarifa za wanachama hao kuomba mkutano na kueleza kwamba mkutano utafanyika kwa kufuata programu iliyoandaliwa na si vinginevyo.
Aveva alisema kwamba Kamati ya Utendaji itakutana kupanga siku ya mkutano si kwa kufuata maelekezo ya wanachama.
"Mkutano utafanyika kwa kufuata programu, tutakutana wakati wowote ili kupitisha tarehe ya mkutano, hatuwezi kufanya kitu kilichoko nje ya utaratibu na kalenda ya mwaka," alisema.
Rais huyo alisema pia yeye binafsi hafurahishwi na matokeo hayo na kuwataka wanachama na mashabiki kuwa watulivu kwenye kipindi hiki.
"Tunawapa wachezaji wetu kila kinachotakiwa, ila matokeo yanayopatikana si mazuri, inatuuma na kutuchanganya sisi pia," alisema Aveva.
Baada ya kichapo cha juzi, Simba inaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi yake dhidi ya JKT Ruvu itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini.

Uwanja wa Real Madrid kubadilishwa jina

http://www.larbes.com/photos/2010/1023-1110/large/image045.jpg
Uwanja wa Santiago
KLABU ya Real Madrid inajipanga kubadili jina la Uwanja wake wa Santiago Bernabeu ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya udhamini na Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Petroli-IPIC yenye maskani yake Umoja wa Falme za Kiarabu. Wawili walikubali kushirikiana katika mkataba unaoaminika kuwa na thamani ya euro milioni 500 itakazovuna Madrid katika kipindi cha miaka 20 ijayo kuanzia Octoba mwaka huu. Mkataba huo unajumuisha haki ya kubadili jina la uwanja ambao umekuwa nyumbano kwa timu hiyo toka mwaka 1947. Uwanja huo pia ndio uliochezewa mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1982. Sasa inaaminika uwanja huo utakuwa ukiitwa The Abu Dhabi Santiago Bernabeu. Rais wa klabu hiyo Florentino Perez amesizitiza kuwa urithi wa uwanja huo utaheshimiwa kwa kuendelea kubaki na neno Santiago Bernabeu. Perez amesema dhumuni kubwa la udhamini huo ni pamoja na kuukarabati upya uwanja huo na kuuongeza mpaka kufikia uwezo wa kubeba mashabiki 91,000 kutoka 81,000 wa hivi sasa

Diego Simeone awakingia kifua nyota wake

http://www.fm-base.co.uk/forum/attachments/football-manager-2015-tactics/751628d1421605865-diego-simeone-4-4-1-1-simeone_1968268a.jpg
Kocha Diego Simeone
MENEJA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone amekataa kukosoa nidhamu ya kikosi chake baada ya mchezo wao wa Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona, akisisitiza anajivunia ari iliyoonyeshwa na wachezaji wake.
Atletico walimaliza mchezo huo wa robo fainali ya mkondo wa pili wakiwa wako tisa baada ya Gabi kutolewa nje kwa tukio alilofanya kipindi cha mapumziko kabla ya Mario Suarez naye kulimwa nyekundu katika dakika mwishoni na mchezo.
Naye Arda Turan pia alilimwa kadi ya njano kwa kumtupia mwamuzi wa pembeni kiatu wakati Raul Garcia yeye alipewa kadi ya njano kwa kujibizana na wajumbe walikuwa katika benchi la ufundi la Barcelona wakati wa mapumziko.
Hata hivyo, wakati akiulizwa kuhusiana na tabia za wachezaji wake baada ya kufungwa mabao 3-2 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2, Simeone alijibu kuwa anajivunia wachezaji wake.
Simeone amesema kipindi cha kwanza kilikuwa kizuri kwani walicheza vyema na kukiri kuwa Barcelona walicheza vyema kwani wako katika kiwango cha juu toka Desemba.

Paulista atua Arsenal, Campbell atolewa kwa mkopo

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2015/01/28/252596E800000578-2930164-Gabriel_Paulista_poses_with_an_Arsenal_shirt_as_the_club_unveil_-a-46_1422466068639.jpg
Paulista akiwa na uzi wa The Gunners
KLABU ya Arsenal imefanikiwa kumsajili rasmi beki wa Villarreal, Gabriel Paulista kwa kitita cha Euro Mil. 15 huku wakimtoa mshambuliaji Joel Campbell kujiunga na timu hiyo kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu.
Beki huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Villarreal msimu huu na anaweza kupangwa katika mchezo wa Jumapili hii dhidi ya Aston Villa.
Akihojiwa Paulista amesema alifanya mazungumzo na familia yake na kuwaambia kuwa ilikuwa ni ndoto zake kucheza katika Ligi Kuu hivyo mashabiki wa Arsenal wategemee mtu ambaye atajituma kadri ya uwezo wake ili kuisadia timu kushinda vitu muhimu.
Arsenal walipewa kibali cha kufanyia kazi cha Paulista Jumatatu pamoja na ukweli kuwa nyota huyo hajawahi kuitumikia timu yake ya taifa na pia hatoki katika umoja wan chi za Ulaya.
Paulista alijiunga na Villarreal akitokea klabu ya Vitoria ya nchini kwao Brazil 2003.
kwao Brazil mwaka 2013.

Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin

NGUMI KUPIGWA UWANJA WA NDANI YA TAIFA

Shamsa Ford amsifia Mama Muuza

MWANADADA nyota wa filamu nchini, Shamsa Ford amewataka mashabiki wake kujiandaa kuipokea filamu yake moya iitwayo 'Mama Muuza'.
Shamsa aliyefanya vema mwaka uliopita kupitia filamu za 'Hukumu ya Ndoa Yangu' ya Jacob Stephen 'JB' na 'Chausiku' ambayo ni kazi binafsi alisema filamu hiyo mpya ipo jirani kutoka.
Muigizaji huyo alisema filamu hiyo ni miongoni mwa filamu anazotegemea kufanya vema mwaka 2015 kutokana na simulizi lake lilivyo na jinsi washiriki wake walivyoitendea haki.
Alisema ndani ya filamu hiyo imeshiriki wasanii wakali akiwamo yeye na Baba Haji.
"Mama Muuza ipo jirani kutoka, hivyo mashabiki wajiandae kuipokea kama walicvyoipokea Chausiku," alisema Shamsa Ford ambaye anatamba na kazi nyingine kadhaa zilizomweka katika orodha ya wasanii nyota nchini wa filamu.

Wednesday, January 28, 2015

Mdomo wamponza Jose Mourinho atozwa faini

http://static.guim.co.uk/sys-images/Observer/Columnist/Columnists/2013/6/7/1370621593808/jose-mourinho-010.jpg
Jose Mourinho
KOCHA mwenye maneno mengi anayeinoa Chelsea, Jose Mourinho ametozwa faini ya paundi 25,000 kwa kauli yake aliyodai kuna kampeni za makusudi zinazofanywa na waamuzi kuidhoofisha timu yake.
Mourinho alitoa kauli hiyo baada ya kikosi chake kukataliwa penati katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton Desemba 28 mwaka jana.
Chama cha Soka cha Uingereza-FA kimemtoza faini kwa kauli hiyo ambayo inaweza kuleta mkanganyiko katika soka huku akionywa kutofanya kosa kama hilo katika siku za usoni.
Mbali na hilo Mourinho pia alionywa kwa kauli yake aliyotoa kabla ya mchezo kati ya Chelsea na Stoke City Desemba 22 ambao walikuja kushinda kwa mabao 2-0.
Kikosi cha kocha huyo usiku wa jana kilitinga Fainali ya Kombe la Ligi kwa kuing;oa Liverpool kwa jumla ya mabao 2-1 na Jumamosi inatarajiwa kuvaana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City.

Mbeya City 'yaua' Mnyama Taifa, Chollo akosa penati

mbeyacityfc 1-4 vipers fc_2014_1
Mbeya City
IMG_6078 (2)
Simba
KLABU ya Simba jioni ya leo imewanyima raha mashabiki wake baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mbeya City, huku ikishuhudiwa timu hiyo ikipoteza nafasi ya kuasawazisha bao baada ya beki wake, Masoud Nassoro 'Chollo' kukosa penati sekunde chache kabla ya filimbi ya mwisho.
Simba ambayo ilipata ushindi mfululizo tangu ilipotoka kwenye Kombe la Mapinduzi ambapo walinyakua kwa kuifunga kwa mikwaju ya penati Mtibwa Sugar, walianza kupata bao kupitia kwa Ibrahim Hajibu aliyefunga kwa mkwaju wa adhabu ndogo nje kidogo ya lango la Mbeya City dakika chache kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili katika pambano hilo lililochezwa wenye uwanja wa Taifa, Mbeya walionyesha upinzani mkali zaidi na kufanikiwa kurejesha bao katika dakika ya 77 kupitia Hamad Kibopile kabla ya kupata penati katika muda wa ziada kupitia kwa Yusuph Abdalla baada ya kipa wa Simba Peter Manyika Jr kucheza faulo.
Hata hivyo mfungaji wa bao hilo alifanya kosa la kizembe la kumchezea vibaya Jonas Mkude na kupewa penati ambayo Chollo aliipoteza na pambano hilo kumalizika kwa Simba kulala kwa mabao 2-1.
Kipigo hicho kimewafanya baadhi ya wanachama kjuucharukia uongozi wa juu wa klabu hiyo sambamba na Kamati ya Mashindano wakidai wameshindwa kufanya kazi.
Kwa ushindi huo wa leo Mbeya ambayo ilienda mapumziko Novemba 9 wakiwa mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo, imechupa toka nafasi ya 13 hadi nafasi ya 7 wakiwa na pointi 15 na Simba kusaliwa na pointi  13 na kushuka hadi nafasi yua 11.
Simba itashuka dimbani tena Jumamosi kukabiliana na JKT Ruvu ambao wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 18 sawa na Yanga.

Luis Figo naye ajitosa Urais FIFA

http://static1.purepeople.com/articles/5/66/45/@/23351-luis-figo-au-gala-iwc-637x0-1.jpg
Luis Figo
GWIJI wa zamani wa soka wa Ureno, Luis Figo ametangaza uamuzi wake wa kugombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Mei mwaka huu. 
Figo amechukua uamuzi huo wa kugombea nafasi ya hiyo siku muda kabla ya muda wa mwisho wa kutuma maombi baada ya kukusanya vielelezo vyake vikiwemo vyama vitano vya soka vinayomuunga mkono. Akihojiwa na CNN, Figo amesema anajali mpira hivyo anachikiona sasa katika taswira ya FIFA hakubaliani nacho ndio maana ameamua kugombea nafasi hiyo ili kumng’oa rais wa sasa Sepp Blatter ambaye amepanga kugombea kwa kipindi cha tano.
Gwiji huyo aliendelea kudai kuwa kama utaitafuta FIFA katika mtandao jambo la kwanza litakalokuja ni kashfa mbalimbali zinazoiandama katika miaka ya karibuni jambo ambalo sio zuri kwa ukuaji wa soka. 
Figo amesema amezungumza na watu wengi muhimu katika soka, wachezaji, mameneja, marais wa mashirikisho na wote wanadhani kunatakiwa kufanyika mabadiliko. 
Mshambuliaji huyo wa zamani wa vilabu vya Barcelona, Real Madrid na Inter Milan ameungana na Jerome Champagne, Prince Ali Bin Hussein, David Ginola na Michael van Praag ambao tayari wametangaza nia hiyo ya kupambana na Blatter.

Baby Madaha atambia Saint and Ghost

MUIGIZAJI nyota wa filamu na muimbaji wa muziki wa Bongofleva, Baby Madaha, ametamba kuwa filamu yake mpya anayoianda kwa sasa iitwayo 'Saint and Ghost' ni kati ya kazi zitakazoleta mapinduzi makubwa nchini katika ulimwengu wa filamu.
Madaha, alisema filamu hiyo ambayo inawashirikisha nyota mbalimbali nchini akiwamo yeye mwenyewe (Madaha) ni kati ya filamu za kusisimua ambazo hazijawahi kutengenezwa nchini kutokana na msuko wa simulizi lake.
"Hata aina ya wasanii walioshiriki ni vichwa kwelikweli kitu kinachoifanya filamu hiyo kuwa ya kipekee, alisema Madaha.
Madaha aliwataja wasanii walioshiriki kazi hiyo iliyozalishwa chini ya kampuni yake ya DarkAngel Film Production & Entertainment ni pamoja na Kulwa Kikumba 'Dude', Hidaya Njaidi,  Grace Mapunda 'Mama Kawele', Ramadhani Ally 'Tafu', Ahmed Olotu 'Mzee Chillo' na wengine.
Kabla ya filamu hiyo Madaha, alicheza filamu kama 'Nani', 'Misukosuko3', 'Mpishi', House Na.44' na 'Ray of Hope' iliyompa tuzo kadhaa ikiwamo ya ZIFF na African Movie.

C.P.U kutinga Uganda kufuatilia mkasa wa mtoto aliyeteswa

WARATIBU wa Filamu ya kutetea watoto ya  C.P.U iliyoshirikisha nyota mbalimbali nchini na ambayo itakuwa ikitolewa kwa mtindo wa matoleo (episode) wanatarajiwa kutinga nchini Uganda kwa ajili ya kufuatilia mkasa wa 'hausi gel' aliyefungwa nchini humo kwa sababu ya kumfanyia kitendo cha ukatili mtoto wa bozi wake.
Filamu hiyo iliyotungwa na Stanford Kihore na kuandikwa na Novatus Mgulusi 'ras' imetengenezwa  kwa ushirikiano wa kampuni mbili za kitanzania za Haak Neel Productions na Wegos Works Ltd ilizinduliwa mwaka juzi na kuanza kuonyeshwa kwenye majumba ya sinema kabla ya sasa kuandaliwa katika mtindo wa DVD ili kuonwa na watu mbalimbali ndani na nje ya nchi,.
Wakizungumza na MICHARAZO waratibu wa filamu hiyo walisema kuwa kwa sasa filamu hiyo ina kuendelezo wa sehemu ya kwanza na itakuwa na matoleo 16 yanayohusu namna ya kukabiliana na unyanyasaji na ukatili kwa watoto.
Waratibu hao walisema kuwa, mwandishi wa C.P.U, Ras Mgulusi anatarajiwa kwenda nchini Uganda kuongea na familia ya mtoto aliyefanyiwa tukio baya na msichana wa kazi kupigwa na kutupwa chini kisha kupigwa mateke sambamba na kufanya mahojiano msichana huyo ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka minne kwa kosa hilo ili kutambua kilichomfanya afanye unyama ule.
"Lengo kubwa ni katika kuboresha na kuliweka tukio hilo ndani ya filamu hiyo ya CPU, ambayo ni kitendo maalum cha kutetea watoto ikiwa imeshirikisha nyota mbalimbali nchini," taarifa ya waratibu wa filamu hiyo inasomeka.
“Nilikuwa nafuatilia ripoti ya Unisef kuhusu taarifa za unyanyasaji wa Watoto kitu kilichonigusa na kuamua kuandika filamu ambayo inaweza kuwa ni dira na mwongozo wa jamii kukwepa au kuwasaidia watoto wanaonyanyaswa katika familia zao,”alisema Ras Mgulusi.
Filamu hiyo imeshirikisha zaidi ya wasanii 100 baadhi yao ni; Kulwa Kikumba ‘Dude’ Illuminata Posh 'Dotnata', Richard Mshanga ‘Mzee Masinde’, Hashim Kambi ‘Ramsey’, Sauda Simba, Subira Wahure, Steve Sandhu 'Pride', Nkwabi Juma, Mohamed Fungafunga ‘Mzee Jengua’ Mobby Mpambala ambao ndiyo vinara wake.
Kwa mujibu wa warartibu hao filamu hiyo inatarajiwa kuwa sokoni kuanzia mwezi ujao.

Hammer Q mkewe wajipanga kutoa mpya

MKALI wa miondoko ya mduara, Hussein Mohammed 'Hammer Q' pamoja na mkewe Salha Abdallah 'Salha wa Hammer' wanatarajia kuachia wimbo wao mpya wa 'Safiri Salama' ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya kutoa albamu yao kamili.
Akizungumza na MICHARAZO, Hammer Q alisema kazi hiyo mpya ambayo imesharekodiwa kitambo itaachiwa mara baada ya kumalizika kwa maonyesho ya sherehe za miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT).
Hammer Q, alisema mpaka sasa wamefanikiwa kutoa wimbo mmoja wa 'Wapendanao' ambao umekuwa ukifanya vema kwenye vituo vya redio na kwamba utakaofuata ni 'Safiri Salama' kabla ya kumalizia kurekodi nyimbo nyingine za albamu hiyo inayaokuwa na nyimbo tano.
"Kwa sasa tupo bize na sherehe za miaka 10 ya THT, baada ya hapo tutaachia wimbo wetu wa pili kabla ya kumalizia albamu ambayo tumepanga kuitoa kabla ya Juni mwaka huu," alisema Hammer Q.
Msanii huyo aliwahi kutamba kwenye Bongofleva kupitia wimbo wa 'Lady' kabla ya kuhamia kwenye miondoko ya taarab akipitia makundi kadhaa likiwamo la Dar Modern, Five Star, na TOT taarab.

Ommy Dimpoz akiri kutengeneza video na Avril si mchezo!

Dimpoz akiwa na Avril
Avril
Dimpoz na Avril
MSANII nyota nchini, Omar Nyembo 'Ommy Dimpoz' amesema haikuwa kazi rahisi kwake kutengeneza video na mwanadada Judith Mwangi 'Avril' aliyeimba naye wimbo uitwao 'Hello Baby'.
Dimpoz aliyeshirikishwa katika wimbo huo ambao 'audio' na video yake zinafanya vema hewani Afrika Mashariki kati zilipoachiwa, alinukuliwa na mtandao wa Bongo5 kwamba utengenezaji wa video ya wimbo huo ulikuwa mtihani mgumu kwake.
Msanii huyo alisema Avril ni mrembo ambaye jicho la mwanamme yeyote rijali ni vigumu kuvumilia anapobadilisha nguo mbele yake ili kuinogesha video, lakini yeye alijikaza kiume.
'Ilikuwa mtihani kidogo unajua kufanya kazi na msichana mrembo ushawishi unakuwa mwingi. Kwa hiyo nilikuwa najizuiazuia," alisema kabla ya kuongeza;
"Kwa sababu kwenye video kuna mambo mengi, mtu anaweza akatokea akabadilisha nguo mbele yako, kwa hiyo yote niliyavumilia, ni lazima uvumilie majaribu ili kazi iende," alinukuliwa mkali huyo.
Dimpoz alidokeza pia namna picha zake na Arvil katika utengenezaji video alizotupia kwenye mtandao wa Instagram zilivyotaka kuibua kasheshe kwa mchumba wa mwanadada huyo mrembo

Hofu yatanda AFCON baada ya wenyeji kufuzu robo fainali

Mashabiki wa Guinea ya Ikweta
Mashabiki wa Guinea ya Ikweta wakijiandaa kuingia uwanjani siku ya ufunguzi wa AFCON 2015
MALABO, Guinea ya Ikweta
KUFUZU kwa wenyeji Guinea ya Ikweta katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika kumetengeneza wasiwasi juu ya usalama kwa waandaaji wa michuano hiyo.
Wenyeji waliwashangaza majirani zao Gabon kwa kuwachapa mabao 2-0 Jumapili iliyopita na kumaliza katika nafasi ya pili katika kundi A. Guinea ya Ikweta sasa itachuana na Tunisia katika hatua ya robo fainali Jumamosi hii huko Ebibeyin. Lakini kuna wasiwasi kuwa uwanja huo mpya wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 5,000 pekee utakuwa mdogo kwa ajili ya mashabiki wengi wanaotegemewa katika mchezo huo. Michuano hiyo tayari imeshashuhudia mashabiki wakibomoa na kupita katika uzio katika mchezo wa ufunguzi uliofanyika Bata Januari 17 ambapo uwanja wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 35,000 ulifurika.
Katika viwanja vingine mara kadhaa maeneo ya maalumu na sehemu za wanahabari zimekuwa zikivamiwa mara kadhaa na mashabiki huku polisi wakipambana kurejesha hali ya utulivu.
Waandaaji sasa inabidi waangalie uwezekano wa kuupeleka mchezo huo katika Uwanja wa Bata ambao ndiyo mkubwa katika nchi hiyo ambapo tayari Guinea ya Ikweta wameshacheza mechi zao tatu huku mashabiki wakiwa wamejaa.
Uwanja huo pia ndiyo utakaotumiwa kwa ajili ya mchezo wa fainali Februari 8.

'Bosi' Bayern adai Guardiola ni zaidi ya Wajerumani

Pep Guardiola
MWENYEKITI wa klabu ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Pep Guardiola na kutania kuwa kocha huyo wa zamani wa Barcelona anafanana na Wajerumani kuliko Wajerumani wenyewe.
Rummenigge amesema kutokana na bidii ya kazi aliyokuwa nayo Guardiola anapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa watu wote.
Mwenyekiti huyo aliendelea kudai kuwa wakati wachezaji wote wamerejea nyumbani na kupumzika katika masofa yao, Guardiola yeye huendelea na kazi akipanga mikakati kwa ajili ya mchezo ujao.
Juu ya tetesi za kuwapo kwa mpango wa Guardiola kuondoka na kurejea Barcelona, Rummenigge alipuuza taarifa hizo na kudai kuwa kocha huyo ataendelea kuinoa Bayern hata katika msimu ujao wa Bundesliga
Tangu kocha huyo aliyeipa mataji lukuki Barcelona kutua Bayern ameifanya ibadilishe soka lake lililozoeleka kiasi cha awali kuzua hofu kabla ya mashabiki kutulia kufuatia kufanya vema kwa timu hiyo inayoongoza Bundesliga bila kupoteza mchezo wowote hadi sasa.

Bale asisitiza hana 'bifu' na Ronaldo, achekeea maisha Bernabeu

Ronaldo akiwa na Bale
MCHEZAJI ghali wa Real Madrid, Gareth Bale amesema hana mpango wa kuihama klabu hiyo akisisitiza kuwa ana uhusiano nzuri na nyota wa klabu hiyo, Cristiano Ronaldo na pia anapendwa na mashabiki.
Mshambuliaji huyo kutoka Wales, akihojiwa na kituo kimoja cha redio nchini Hispania, alisema uhusiano wake na Ronaldo ni nzuri na wenye nguvu na kudai hajawahi kuambiwa lolote na Ronaldo juu ya taarifa kwamba alimnyima pasi wakati wakiumana na Espanyol.
Bale alisema uhusiano wake na Ronaldo haujabadilika tofauti na inavyoelezwa, huku akisema anakumbuka kila kitu katika pambano hilo na kukiri kwamba hakumuona Ronaldo kiasi cha kumnyima pasi.
"Nakumbuka kila  kitu wakati nilipochukua mpira na nilikuwa katika kuhakikisha najaribu kufunga bao. Sikumuona, nafikiri ingeweza kuwa pasi ngumu kwake. Sijawahi kuzungumza na Ronaldo kuhusu habari hizo za  kumnyima pasi," alisema Bale.
Bale alisema kwa vyovyote anavyojua yanayotokea uwanjani huishia uwanjani ndiyo maana hawakuweza kujadili suala hilo, licha ya kwamba alijikuta akizomewa na mashabiki wa Santiago Bernabeu.
Nyota huyo mwenye miaka 25, alisema anajisikia furaha kucheza Bernabeu kutokana na sapoti ya mashabiki wa klabu hiyo na kudai hufanya kila linalowezekana ili kuonyesha uwezo wake na kuwapa furaha mashabiki hao.
Bale ameifungia Madrid jumla ya mabao 36 katika mechi 72 alizoichezea tangu ilipomsajili kwa kitita kilichoweka rekodi duniani akitokea Tottenham Hotspur, miongoni mwa mabao hayo 25 ameyafunga katika mechi 43 za La Liga.
Hata hivyo mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na mipango ya kutaka kuihama klabu hiyo ili kujiunga na Mashetani Wekundu kwa kile kilichoelezwa kutokuwa na furaha klabuni hapo, japo mwenyewe amesisitiza anafurahia maisha Madrid pamoja na familia yake.

Chelsea yatinga fainali Capital One, yainyoa Liverpool darajani

Ivanovic akiruka juu kufunga bao pekee la Chelsea dhidi ya Liverpool katika mechi ya marudiano ya Kombe la Ligi
BAO pekee la dakika za nyongeza lililofungwa na beki Branislav Ivanovic limeiwezesha vinara wa Ligi Kuu ya England, Chelsea kufuzu fainali ya michuano ya Kombe la Ligi (Capital One) baada ya kuing'oa Liverpool kwa jumla ya mabao 2-1.
Chelsea walipata ushindi huo kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Stanford Bridge, katika pambano la marudiano la Nusu Fainali ya michuano hiyo baada ya wiki iliyopita timu hizo kushindwa kutambiana uwanja wa Anfield kwa kutoka sare ya goli 1-1.
Katika pambano hilo lililokuwa na ushindani mkubwa baina ya wachezaji wa timu hizo kiasi cha kushuhudiwa wachezaji tisa, watano wa Liverpool na wanne wa Chelsea wakiwamo manahodha Steven Gerrard na John Terry pamoja na Diego Costa wakionyeshwa kadi za njano dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kushindwa kufungana licha ya kosa kosa za hapa na pale.
Costa alinusurika kupewa kadi nyekundu kwa kuwakanyaga kwa nyakati tofauti mabeki wa Liverpool Emre Can na Martin Skrtel, huku pia Chelsea ikanyimwa penati ya wazi baada ya Skrtel kumuangusha Costa langoni mwake.
Dakika nne baada ya kuanza kwa muda wa nyongeza wa dakika 30, beki Ivanovic aliwainua mashabiki wa Chelsea kwa kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Willian na kuiandikia timu yake bao pekee lililowavusha hadi fainali.
Ushindi huo wa Chelsea umekuwa faraja kubwa kwa kocha Jose Mourinho ambaye mwishoni mwa wiki aliishuhudia timu yake iking'olewa kwenye raundi ya tatu na klabu ya daraja la pili ya Bradford City.
Klabu hiyo inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu na ambayo mwishoni mwa wiki itakuwa na kibarua kingine kigumu kwa kuumana na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Manchester City sasa itasubiri kujua itacheza na nani kati ya Tottenham Hotspur na Sheffield United ambazo usiku wa leo zitakuwa dimbani zikirudiana katika mechi nyingine ya nusu fainali.
Spurs ikiwa nyumbani kwake White Hart Lane katika pambano la kwanza lililochezwa wiki iliyopita walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 na kama itakuwa imeulinda ushindi huo itaungana na Chelsea kwenye pambano la fainali litakalochezwa mwezi Machi uwanja wa Wembley.

Ndanda yaipiga mkwara Yanga pambano lao la Jumapili

Ndanda Fc
KLABU ya Ndanda imetamba kuwatoa nishai Yanga watakaoumana nao siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ndanda ambayo tayari wameshatua jijini Dar es Salaam wakitokea Mwanza walipoisambaratisha Kagera Sugar kwa kuilaza mabao 2-1, imesema kuwa lengo lao ni kuvuna pointi tatu ili kujiweka pazuri katika msimamo wa ligi hiyo.
Katika Mkuu wa Ndanda, Edmund Njowoka amesema kuwa kikosi chao kinatambua ugumu wa pambano hilo dhidi ya Yanga, lakini wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi uwanja wa ugenini.
Kikosi cha Ndanda kinachocheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza, kipo nafasi ya 11 kikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi 12 ikishinda michezo minne na kupoteza saba kitavaana na Yanga wanaokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na pointi 18 baada ya mechi 10.
Njowoka alisema kikosi chao kipo tayari kwa vita na amehakikishiwa na benchi lao la ufundi chini ya Kocha Meja Mstaafu Abdul Mingange kwamba vijana wao watapambana kufa na kupona kuhakikisha wanavuna pointi nyingine tatu.
"Tumekuja kwa ajili ya kuvuna pointi, kama tulivyofanya kwa Kagera ndivyo tunavyotaka kufanya kwa Yanga, licha ya kutambua ugumu wa pambano hilo la Jumapili," alisema Njowoka.
Yanga iliyolazimishwa sare mbili mfululizo na Azam na Ruvu Shooting, ilirekebisha makosa yake mwishoni mwa wiki kwa kuinyuka Polisi Moro kwa bao 1-0 na kuwajongelea watetezi wa ligi hiyo, Azam wanaoongoza wakiwa na pointi 21.
Azam kwa sasa ipo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kushiriki michuano maalum kujiandaa na pambano lake la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Marreikh. Michuano hiyo inashirikisha jumla ya timu nne zikiwamo TP Mazembe, Don Bosco na Zesco ya Zambia.
Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm alinukuliwa juzi kwamba kikosi chake kimejiandaa kupata ushindi dhidi ya Ndanda, akiwasisitiza vijana wake kuwa makini uwanjani ili kutopoteza nafasi za wazi kama walivyofanya katika mechi zao zilizopita.

Kumekucha Bungeni, kikao chaahirishwa kisha Prof Lipumba

Prof Lipumba akiwa ndani ya gari la Polisi baada ya kutiwa mbaroni jana
SPIKA wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania, Anna Makinda amelazimika kuahirisha kikao cha Bunge kilichoanza jana, baada ya vuta nikuvute iliyotokea  baada ya kutolewa kwa hoja binafsi kutoka kwa Mbunge na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia kuhusu jeshi la polisi kumshambulia Profesa Ibrahim Lipumba jana akiwa kwenye maandamano .
Akizungumza katika bunge hilo Mbatia amesema kuwa kitendo cha polisi cha kuwapiga raia wasiokuwa na hatia, kuwadhalilisha waandishi wa habari na kupiga mabomu ya machozi kiasi cha kuwafanya watoto wadogo kuhangaika hakikubaliki.
Amesema polisi wakiendelea kuachwa kufanya vitu vya uvunjifu wa Amani Serikali haitatawalika hivyo ili kurejesha amani na imani ya wananchi kwa Serikali yao ni vema shughuli zote za Bunge zikaahirishwa kupisha mjadala wa hoja hiyo binafsi kwa lengo la kuinusuru nchi.
“Mheshimiwa Spika naliomba bunge lako liahirishe shughuli zake ili leo tuweze kujadili suala hili la uvunjifu wa amani uliofanywa na  jeshi letu la polisi jijini Dar es Salam jana, wao wanasema kuwa wamepewa amri kutoka ngazi za juu tunataka serikali ituambie ni nani anayetoa amri hizi za kupiga watu wasiokuwa na hatia yeyote, amesema Mbatia.
Baada ya kuwasilisha hoja hiyo asilimia kubwa ya wabunge walisimama juu ishara ya kuunga mkono hoja hiyo, lakini Spika Makinda akawaomba wakae ili aweze kutoa ufafanuzi kwa mujibu wa kanuni.
Spika Makinda aliwaeleza wabunge hao kuwa suala hilo ni nyeti kwa sababu ni la kiusalama, ili kupata ufafanuzi zaidi anaiagiza Serikali kufikisha bungeni hapo majibu ya hoja hiyo kesho ili wabunge waweze kujadili.
Baada ya maamuzi hayo ya Spika Makinda kelele zikasikika bungeni huku wabunge wakitaka kufanyika kwa mjadala huo leo leo, ndipo Spika alipoamua kuahirisha bunge hadi saa kumi jioni.

Ghana, Algeria watinga robo fainali, vumbi jingine leo

Andre Ayew akichuana na mchezaji wa Bafana Bafana
Wachezaji wa Algeria wakishangilia ushindi wao dhidi ya Senegal
VINARA wa soka Afrika, Algeria na Ghana zimefuzu hatua ya Robo Fainali ya michuani ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), kwa kishindo baada ya kuziondosha patupu timu za Senegal na Afrika Kusini katika mechi zao za mwisho za Kundi C zilizochezwa katika miji ya Malabo na  Mongomo.
Algeria walikuwa wametoka kuduwazwa na Ghana kwa kufungwa bao 1-0 katika mechi yao iliyopita, walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya waliokuwa vinara wa kundi hilo la kifo, Senegal katika pambano tamu lililochezwa kwenye uwanja wa Malabo.
Ikiwa bila nyota wake Islam Slimani, Algeria wanaoongoza orodha ya viwango vya soka barani Afrika waliwashtukiza wapinzani wao kwa bao la mapema la dakika ya 11 lililowekwa kimiani na Riyad  Mahrez lililodumu hadi wakati wa mapumziko.
Senegal walicharuka kusaka kurudisha bao hilo ili angalau waambulie sare na kuwavusha hatua hiyo ya mtoano, lakini walijikuta wakikatishwa tamaa baada ya Algeria kuandika bao la pili dakika nane kabla ya kumalizika kwa pambano hilo baada ya Nabil Bentaleb kumalizia kazi nzuri ya
Sofiane Feghouli.
Kwa kipigo hicho Senegal wameyaaga mashindano hayo sambamba na Afrika Kusini ambayo ilikumbana na kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Ghana waliokuwa nyuma hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Bafana Bafana iliyofuzu fainali hizo kwa kishindo bila ya kupoteza mchezo katika kundi lake lililokuwa na waliokuwa mabingwa Nigeria, ilianza kupata bao katika dakika ya 17 kupitia kwa Mandla Masango, lakini katika kipindi cha pili waliruhusu wapinzani wao kurejesha bao hilo na kuongeza jingine lililowapeleka robo fainali bila kutarajiwa baada ya kuianza michuano hiyo kwa kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Segenal.
Bao la kusawazisha la Ghana liliwekwa kimiani na John Boye katika dakika ya 73 baada ya kuunganisha mpira wa krosi ya Andre Ayew 'Pele' kabla ya mtoto huyo wa nyota wa zamani wa Afrika, Abeid Pele kufunga bao la ushindi kwa kichwa katika dakika ya dakika ya 83 na kuwavusha mabingwa hao manne wa michuano hiyo katika hatua hiyo ya robo fainali.
Ghana imemaliza kileleni mwa kundi hilo wakilingana pointi sita na Algeria waliokamata nafasi ya pili, huku Senegal wameshika nafasi ya tatu wakiwa na pointi nne na Bafana Bafana wameburuza mkia wakivuna pointi moja tu.
Hatua ya robo fainali inatarajiwa kuanza kuchezwa siku ya Jumamosi kwa pambano la kukata na shoka baina ya majirani Congo-Brazzaville dhidi ya DR Congo kabla ya Tunisia kuvaana na wenyeji Guinea ya Ikweta katika pambano jingine la pili.
Ghana na Algeria zenyewe zinatarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumapili kumenyana na washindi wa kundi D ambalo usiku wa leo zibnatarajiwa kuumana kuwania nafasi mbili zilizobaki za kutinga hatua hiyo ya robo fainali.
Wakati Ivory Coast na Cameroon zitaumana kwenye uwanja wa Malabo, wenzao Mali na Guinea watapepetana kwenye uwanja wa Mongomo, huku timu zote zikiwa na nafasi sawa kutokana na kulingana kila kitu wakiwa na pointi mbili baada ya kila moja kucheza mechi mbili.

Saturday, January 24, 2015

Breaking News: Waziri Prof Muhongo atangaza kujiuzulu

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgofvT59YEKqnPi1tct_v_grVGvyKfclYGpMmBYSTtY0gNer1nQKkuaZLVla2I4kKMgccK2BxgsjRwv7R7ir3wuPloEP6HfBp4xKUDUmVr9KDZrWyiYZ23hkBw1IwEi1_jEW1woldsH3oz8/s1600/Prof.+Muhongo.jpg
Prof Muhongo aliyetangaza kuachia ngazi serikali asubuhi hii
HATIMAYE Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo leo ikiwa ni karibu mwezi mmoja tangu kuwepo kwa shinikizo la kumtaka ajiuzulu nafasi hiyo kutokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.
Prof Muhongo ni miongoni mwa waliotajwa katika kashfa hiyo, lakini hakuchukuliwa hatua zozote na Rais Jakaya Kikwete wakati akilihutubia taifa, huku aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka akiondolewa kwenye nafasi yake kutokana na sakata hilo.
Maamuzi ya kuachia ngazi kwa Prof Muhongo yametolewa mbele ya wanahabari aliokutana nao asubuhi jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kueleza mafanikio yake ndani na nje ya nchi kupitia wizara hiyo na kujitaja kama mtu msafi ambaye ana doa lolote, waziri huyo alitangaza kuachia ngazi kwa madai ya kutafakari kwa kina, ingawa kabla ya hapo alishawahi kunukuliwa kwamba asingejiuzulu ng'o.
Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wakubwa wake, ikizangatiwa heshima aliyonayo kama Profesa.
Kujiuzulu kwake kumekuwa wakati Katibu wake, Eliakim Maswi kutimuliwa kazini na Katibu Mkuu Kiongozi kutokana na sakata hilo, huku watendaji kadhaa umma wakiburuzwa mahakamani wakikabiliwa na kesi zinazohusiana na sakata hilo la Tegeta Escrow.

OCODE yawaokoa wanafunzi 651 kukaa chini Chanika

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tungini, Chanika wakiyajaribu mawadati waliokabidhiwa na OCODE
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tungini, wakiyakalia madawati waliyokabidhiwa
Wakiwa haamini kama hawatakaa tena chini baada ya shule yao kupewa madawati 100
Wazazi wa Shule ya Msingi Tungini walikuwa mashuhuda wa makabidhiano hayo
Wanafunzi walishangilia na kupongeza kwa makofi
Afisa Elimu Shule za Msingi, Ilala, Elizabeth Thomas alitoa nasaha zake katika hafla ya makabidhiano ya madawati 217 kwa shule tatu za manisapaa yake toka kwa OCODE
Mratibu Mkuu wa OCODE, Jackson Joseph akisoma risala kuelezea asasi yao na misaada wanayotoa kwa jamii ya Watanzania katika nyanja ya elimu na uchumi
Akaikabidhi risala hiyo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Rogasian Seda aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo aliyekuwa awe mgeni rasmi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya OCODE, Vedasto Ngaiza naye akatoa nasaha zake kwa waalikwa
Mwenyekiti wa Bodi ya OCODE akakabidhi waraka wake kwa Mgeni Rasmi, Mchumi wa Manispaa ya Ilala aliye pia Kaimu Mkurugenzi, Rogasian Seda 
Kaimu Mkurugenzi wa Ilala, Rogasian Seda akimkabidhi cheti Mwalimu Mkuu wa Shule ya Tungini, Peter J Peter kuonyesha ishara ya kukabidhiwa msaada toka OCODE
Jamani madawati yenyewe ndiyo haya hapa kaimu Mkurugenzi wa Ilala (mwenye koti) na Afisa Elimu wakionyeshwa madawati na uongozi wa OCODE
Kaimu Mkurugenzi wa Ilala na Mwenyekiti wa Bodi ya OCODE wakishikana mkono kuonyesha ishara ya kukabidhiana madawati huku wakishuhudiwa na Mwalimu Mkuu wa Tungini, Peter J Peter (shati jeupe), Afisa Elimu (wa pili kushoto) na Mratibu wa OCODE, Jackson Joseph.
Wanafunzi wakayachangamkia kuyakalia kama ishara ya kuyapokea shuleni kwao
Mchumi wa Manispaa ya Ilala na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Rogasian Seda akitoa nasaha zake
Wanafunzi wakifuatilia kila tukio lililokuwa likiendelea katika hafla hiyo iliyofanyika Shule ya Msingi Tungini, Chanika jijini Dar es Salaam
Weweee hatukai tena chini ahsanteni OCODE, ahsanteni wazazi
Na Rahim Junior
WANAFUNZI zaidi ya 651 wa Shule za Msingi tatu za Tungini, Nzasa II na Msongola zilizopo Chanika, wilayani Ilala jiji la Dar es Salaam wameokolewa kukaa chini baada ya Asasi ya Maendeleo ya Jamii iitwayo Organization for Community Devlopment (OCODE) kuzikabidhi shule hizo msaada ya madawati 217 yenye thamani ya Sh. Milioni 21.
Aidha asasi hiyo imezisaidia kukarabati na kujenga majengo matatu ya madarasa yenye thamani ya Sh. Milioni 22 kwa Shule za Msingi Viwege na Msongola ambayo waliyakabidhi katika hafla zilizofanyika juzi na kushuhudiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, ambaye pia ni Mchumi wa Manispaa hiyo, Rogasian Seda aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa aliyekuwa awe mgeni rasmi wa hafla hiyo.
Msaada huo wa madawati na madarasa hayo ulikabidhiwa kwa wakuu wa Shule hizo juzi na kuhudhuria pia na Afisa Elimu wa Shule ya Msingi wilaya ya Ilala, Elizabeth Thomas ambaye aliushukuru uongozi wa OCODE kwa msaada huo na kutoa wito kwa asasi nyingine na wananchi kuendelea kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini na kuwafanya watoto wafurahie kwenda shuleni kwa sababu ya mazingira mazuri.
Kabla ya makabidhiano hayo, Mratibu wa OCODE, Jackson Joseph alifafanua mgawanyo wa madawati hayo kwa kueleza kuwa, Shule ya Msingi Tungini yenyewe imepata madawati 100,  wakati Nzasa II ilipewa madaewati 72 na Msongola ilipewa madawati 45, ambayo kwa jumla yake itawafanya wanafunzi 651 kwa maana ya kila dawati moja wanakaa wanafunzi watatu kuokolewa kukaa chini kutokana na msaada huo.
"Kwa hapa Tungini tunakabidhi madawati 100, lakini tayari tumeshapeleka madawati 72 katika shule ya Nzasa II na 45 Msongola ambapo kwa idadi hiyo ya madawati 217 tutakuwa tumewaokoa wanafunzi 651 kuketi chini kama ilivyokuwa mwanzoni kwa kuwafanya sasa wakae katika madawati na kusoma kwa utulivu," alisema Jackson.
Aliongeza kuwa asasi yao ambayo iliasisiwa mwaka 1992 na kusajiliwa serikali mwaka 2003 ilikabidhi pia madarasa mawili kwa Shule ya Viwege, moja wakilikarabati na jingine likiwa kipya wakishirikiana na wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo na jingine moja wamelikarabati katika Shule ya Msongola ambayo nao pia walikabidhiwa tayari kuwafanya wanafunzi wasome katika mazingira mazuri.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Rogasian Seda, licha ya kuishuruku na kuipongeza asasi ya OCODE pamoja na wazazi walioshiriki kuchangia michango mbalimbali ya shule zao, alisema bado manispaa hiyo ni tatizo sugu la madawati kwa shule zake.
Seda, alisema Ilala ina upungufu ya jumla ya madawati 12,000 na kwa bajeti ya mwaka huu wametenga kiasi cha madawati 2,100 tu hivyo kuwahimiza wazazi kuendelea kushirikiana na serikali na asasi za kijamii kama OCODE ili kupunguza tatizo hilo, huku akiwakumbusha wazazi na Kamati ya Shule za Ilala kulinda na kutunza vema misaada wanayopewa ili kuwaokoa watoto kukaa kwenye vumbi.
"Ni wajibu weenu kutunza misaada mnayopewa, wanafunzi tunzeni madawati yenu ili muendelee kuyakalia, msikubali yaharibike kwani mtataabika, kwa hakika Manispaa imefarijika kwa hili lililofanywa na OCOPDE na kuhimiza wengine kujitokeza," alisema Seda.
Kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Afisa Elimu wa Shule ya Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas, alisema wamefurahishwa na juhudi ambazo zimekuwa zikifanyw ana OCODE na kuahidi kuwa nao bega kwa bega ili kuleta maendeleo ya elimu sawia na yale ya kiuchumi kwa wananchi wa manispaa hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi wa OCODE, Vedasto Ngaiza aliweka bayana kuwa asasi yao haitaondoka Ilala mpaka ihakikishe tatizo la madawati katika shule za Ilala linaisha kama walivyoweza kufanya Temeke kwa kuzisaidia Shule 24 ambayo waliweka kambi kwa zaidi ya miaka 10.
Ngaiza alisema kitu cha muhimu wazazi na kamati za shule kuhakikisha hawageuzi madawati wanaoyopewa kuwa kuni baada ya kuharibika bali wayatunze na kuyakarabati ili yaweze kuwasaidia watoto.
Pia alisema mikakati ya OCODE ambayo tangu Januari mwaka jana imeanza kutekeleza programu mbili za miaka mitano katika manispaa ya Ilala moja ikiwa ni kusaidia kwenye masuala ya Elimu na nyingine kuwainua wananchi kiuchumi kupitia miradi mbalimbali, lakini pia wanafikiria kusaidia kuzijengea shule za manispaa hizo uzio kwa ajili ya kuwafanya wanafunzi wasome sehemu salama wao na vifaa vyao kama madawati.
"Kwa hali kama hii tunayoiona shule ikiwa haina uzio, ni rahisi misaada kama hii kuibwa na madarasa kuanza kutumiwa kwa mikutano ya nguvu za giza, hivyo OCODE tunafikiria pia kusaidia kujengwa kwa uzio ili wanafunzi na mali za shule ziwe salama," alisema Ngaiza na kuamsha vigelegele toka kwa walimu wa shule hiyo na wazazi waliohudhuria sherehe hizo za makabidhiano Tungini.