STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 10, 2015

Ozil arejea Arsenal, Rojo, Blind waipa furaha Man Utd

Kipa Valdes akiwa na wachezaji wenzake wapya wa Manchester United

Daley Blind akifanya mazoezi hapa akiwa na Dogo Andreas Pereira
Rojo naye alipasha na wenzake
WAKATI Manchester United wakichelekea kurejea tena dimbani kwa nyota wake Marcos Rojo na Daley Blind, Kiungo Mesut Ozil wa Arsenal naye amepona na huenda akarejea uwanjani kesho wakati Arsenal inakipiga dhidi ya Stoke City.
Mashetani Wekundu wanatarajiwa kuwa nyumbani kuwavaa Southampton baada ya kupata sare mbili mfululizo ugenini katika Ligi Kuu ya England, lakini ikiwa na furaha kurejea kwa nyota hao sambamba na kumnasa kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes waliyemsainisha.
Kama ilivyo kwa Manchester, Arsenal wenyewe wanafurahi baada ya Ozil kurejea Ligi Kuu England baada ya kukaa nje miezi mitatu kutokana na maumivu ya goti.
Kocha Arsene Wenger amesema Ozil amekuwa akifanya mazoezi na wenzake na sasa yuko fiti, hata hivyo inaonekana ataanzia benchi.
Mjerumani huyo aliyejiunga na Arsenal akitokea Madrid aliumia katika mechi dhidi ya Chelsea, Oktoba mwaka jana.
Ozil ndiye mchezaji ghali zaidi Arsenal iliyompata kwa kitita cha pauni milioni 42.5.

Real Madrid yazinduka yaipiga Espanol 3-0

Gareth Bale
Bale akishangilia bao lake wakati Real ikiiadhibu Espanyol
Real Madrid v Espanyol
Nacho akishangilia bao lake
LICHA ya kucheza pungufu timu ya Real Madrid imepata ushindi wa mabao 3-0 nyumbani katika  Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Espanyol na kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Fabio Coentrao alilimwa kadi nyekundu kaytika dakika ya 53, lakini mabao ya James Rodriguez katika dakika ya 12 , Gareth Bale dakika ya 28 na  lile na Nacho la dakika ya 70 yalitosha kuwapa ushindi muhimu Real Madrid iliyoshuhudia nahodha wake, Cristiano Ronaldo akitoka uwanjani bila kufunga bao ikiwa ni mara ya kwanza baada ya muda mrefu msimu huu.
Kwa ushindi hio Madrid wamefikisha pointi 42 na kuiacha Barcelona ikiwa nafasi ya pili na pointi 38 sawa na ilizonazo nazo Atletico Madrid ambazo zinatarajiwa kushuka dimbani kesho.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo, Malaga ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 na  Villarreal na hivi sasa Celta Viro ipo dimbani kuumana na Valencia nyumbani kwao na tayari wamekubali bao 1-0.

Haya ndiyo matokeo ya EPL kwa leo

Balotelli akichuana na mchezaji wa Sunderland
City ilipong'ang'aniwa na Everton ugenini leo
Chelsea wakipongezana baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle Utd
Sunderland     0 - 1     Liverpool
Burnley     2 - 1     Queens Park Rangers
Chelsea     2 - 0     Newcastle United
Everton     1 - 1     Manchester City
Leicester City     1 - 0     Aston Villa
Swansea City     1 - 1     West Ham United
West Bromwich …     1 - 0     Hull City    
Crystal Palace     2 - 1     Tottenham Hotspur

Fainali Mapinduzi ni Simba na Mtibwa

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/simba1.jpg
Simba waliowafuata Mtibwa Fainali za Kombe la Mapinduzi
Mtibwa Sugar (jezi za kijani) watakaoumana na Simba siku ya Jumanne
KLABU ya Simba imefanikiwa kutinga Fainali za michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 baada ya kuing'oa Polisi ya Zanzibar na sasa wanatarajiwa kukutana na Mtibwa Sugar siku ya Jumanne.
Mtibwa ilifanikiwa kufuzu hatua hiyo mapema leo jioni baada ya kuiondosha kwa mikwaju ya penati 4-3 'wababe' wa Yanga, JKU baada ya kumaliza dakika 90 wakiwa sare ya 0-0.
Simba iliyoonyesha mabadiliko makubwa tangu ianze kunolewa na kocha Goran Kopunovic, walipata nafasi hiyo muda mchache uliopita baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika Nusu Fainali ya pili iliyochezwa uwanja wa Amaan. Zanzibar.
Bao lililoipelekea Simba kwenye hatua hiyo na kurejesha kumbukumbu ya nusu fainali ya mwaka 2010 ambapo timu hizo zilikutana na Mtibwa kuibuka wababe kabla ya kwenda kutwaa taji kwa kuilaza Ocean View bao 1-0.
Pia fainali hizo zinarejesha pia fainali ya ABC Top 8 iliyocvhezwa mwaka juzi na Simba kuilaza Mtibwa kwa mabao 4-3.
Mechi hiyo ya faionali itachezwa usiku wa Jumanne kwenye uwanja wa Amaan huku kila timu ikiwa na matumaini makubwa ya kutwaa taji hilo lililokosa mwenyewe baada ya KCCA ya Uganda kutemeshwa hatua ya Robo Fainali baada ya kufungwa kwa penati na Polisi.

JKT Ruvu waikamata Mtibwa Sugar,, yailaza Stand Utd Ndanda

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjrGUIMxPw7cdxPgyXtAxRJHOSLFdOsz_Yetg7EBn6y-K7pPB3ToQogwImAjfSZceVrbx9aUL72b0URIua7OK30a6XbaCvr5aiWZXfZNKy95h3Kn2aQ1qmkPYpYSe6mpm7NGtNDBnXSwLZ/s640/DSC_0805.JPG
KIkosi cha JKT Ruvu kilichochupa hadi naasi ya pili ikiziengua Yanga na Azam
MAAFANDE wa JKT Ruvu jioni ya leo wamepata ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Stand United ya Shinyanga na kuikamata Mtibwa Sugar ambao wapo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015.
Samuel Kamuntu na Amos Mgina waliifungia mafaande hao mabao hayo na kuifanya timu hiyo inayonolewa na kocha Fred Felix Minziro katika mchezo uliochezwa uwanja wa Chamazi na kuifanya ifikishe pointi 16 sawa na Mtibwa waliosalia kileleni. Bao la wageni Stand lilifungwa na Mussa Said.
JKT waliotangulia michezo miwili mbele dhidi ya Mtibwa inatoautiana na vinara hao mabao ya kufunga na kufungwa, Mtibwa ikiwa na 11 na kuungwa manne ilihali JKT ikiwa na mabao 10 na kufungwa 9.
Katika mechi nyingine iliyochezwa mjini Mtwara, wenyeji Ndanda Fc ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro.
Wageni walitangulia kupata bao kupitia Said Bahanuzi kabla ya wenyeji kuchomoa kupitia Jacob Massawe na kumanya mshambuliaji huyo wa zamani wa Toto African na African Lyon kuikisha bao la tatu msimu huu.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi moja tu itakayowakutanishja wenyeji Mgambo JKT itakayoikaribisha Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.